Friday, May 30, 2008

Mei 30, 2008 Haraka Haraka Haina Baraka (Stress)

Kwa muda mrefu nimekuwa ninajiuliza kwa nini watu Ughaibuni wanakuwa na haraka. Maana utakuta mtu ana kitabu napia kalamu, humu ndani ya kitabu ameandika kila kitu nani atakutana naye leo au atafanya nini siku hii, yaani kuanzia asubuhi mpaka jioni. Nimejaribu kuwauliza kwa nini wanafanya hivi? wengine wanasema bila kufanya hivi basi hawawezi kuishi. Pia nimejaribu kuwaambia nitakako mie hakuna mambo haya yaani kwa mfano, naenda kumsalimia mtu/jamaa au rafiki ni kwenda tu na pia wakati huu nakwenda naweza nikakutana na rafiki /mtu mwingine na hapo gumzo litaanza. Lakini hapa haiwezekani kwani safari imepangwa kwenda kwa (Anna). basi ni kwa "Anna". Kwa hiyo sasa utakuta hata watoto wadogo wanasema hawana hali nzuri kwa vile wana mambo mengi. Mambo mengi kiasi kwamba wengine wanashindwa kuendelea na masomo vizuri. Kwa ajili ya (Stress) KILA KITU NI MUDA HATA KULA CHAKULA. Pia hata kutembea. Ammmh kwa kweli naipenda Afrika yangu hakuna haraka afrika au mie mwongo semeni mwenyewe basi kama kweli au vipi.

Na ; Yasinta Ngonyani

Sunday, May 18, 2008

Mei 18, 2008 Litumbandyosi

Haya sasa wasomaji leo nimekumbuka Geografia kidogo.

Litumbandyosi ni kijiji ambacho kipo katika kata ya Litumbandyosi. Tarafa ya Namswea. Wilaya ya Mbinga na mkoa wa Ruvuma. Kijiji hiki kipo kusini magharibi mwa Tanzania. Mashariki kinapakana na kijiji cha Mgazini ,Magharibi kinapakana na kijiji cha Rwanda, Kaskazini kimepakana na kijiji kiitwacho Kingoli na kusini kimepakana na kijiji cha Luhagala. Litumbandyosi ni maarufu kwa kilimo cha mpunga, karanga na mihogo. Kijiji cha Litumbandyosi kina jumla ya watu 7,318 na idadi ya kaya ni 1,449 na kila kaya kwa wastani wanaishi watu watano.
Kijiji hiki ndipo alipozaliwa baba yangu.

Na; Yasinta Ngonyani

Saturday, May 17, 2008

Mei 17,2008 GETO ZA AFRIKA KUSINI ZINAUNGUA

Gazeti la mwananchi hapa sweden limeandika hivi:.
Johannesburg: Siku chache zilizopita mageto mengi ya huko Johannesburg yameongua moto kwa fujo kali, kwa sababu ya kufukuza wakimbizi, hasa wakimbizi wa kutoka Zimbabwe. Ma mia ya mapolisi wameitwa huko getoni Alexandra, ili kujaribu kuwatuliza watu ambao wanatoka nyumba hadi nyumba. Wanafanya hivyo kwa ajili ya kuwasaka wakimbizi. Majambazi wanapowakuta waamiaji hao wanawaibia mali zao, wanaunguza nyumba zao na kuwapiga wananchi. Kesi nyingi za vifo na ubakaji (mzito) mbaya umeripotiwa lakini hata hivyo haijulikani wangapi wamekufa.
Wanazimbabwe mamia kwa mamia wamekimbia na kutafuta njia ya kwenda katika vituo vya polisi ili kuepuka uwingi wa watu.

Na; Yasinta Ngonyani

Friday, May 16, 2008

Mei, 16,2008 BABA

Naona hapo http://www.lundnyasa.blogspot.com/ ananilaumu kwa nini sijampa baba sifa. Hapana kwani bila baba basi basi tusingezaliwa. Kwani lazima tukumbuke Mungu alimuumba Eva lakini baadaye aliona si haki Eva awe peke yake alimletea mume Adam. Nadhani wote mmenielewa. Kwa maana hiyo baba naye ana sifa zake, ambazo hazifanani na mama kwani, Kama mmewahi kumsikiliza Dr Remmy Ongala anavyoimba kwa kweli unaweza kulia. (baba amepata mke mwingine na wangoni kwa ugimbi). Hii ndio sababu niliandika kwanza mama na ukizingatia kwa sasa mama yangu mpendwa hayupo nami. Pia mama ana majukumu makubwa zaidi yaani ana kazi ya kuzaa, kulea, na kazi za aina mbalimbali za nyumbani. Inawezekana labda nilikuwa namtamani mama. Kwa hiyo msidhani ya kwamba simthamini/ sina upendo na baba HAPANA. Si unajua father and dotter. natumai nimewapa wasomaji jibu la kuwapendeza.

Na; Yasinta Ngonyani

Monday, May 12, 2008

Mei, 12, 2008 Dini/wakoloni

Hii habari nimetaka muda mrefu kuieleza lakini nilikuwa nashindwa vipi nitawaeleza watu sasa nimepata njia ya kuelezea kwa kifupi. Ni hivi;. Hapo kale Waafrika tulikuwa na nchi pia dini zetu yaani tulikuwa tunajitawala pia tulikuwa na dini zetu. Lakini baadaye wazungu wakaja na kutawala afrika, kwa unyonge wetu tukakubali kutawaliwa. Pia walipokuja wakaja na dini zao. Wakatuambia tuache dini zetu za kuamini mizimu na wakaanza kujenga makanisa na kuanza kuhubiri. Hapo ilikuwa mwaka 1898-1998 kama umesoma (UJIO WA WAMISIONARI WABENEDIKTINI TANZANIA - UNGONI) Na sisi kwa unyonge na upole wetu tukawaamini. Nadhani tangu hapo akili zetu zinaamini wazungu wanaweza kufanya kila kitu tunawaheshimu wao kama mungu. Jambo ambalo si kweli. Ninachotaka kusema ni kwamba wazungu /wamisionari walipoingia afrika waliingia kwa kasi na kuanza aina ya vita yaani kuonyesha wao ndio wenye nchi. Pia wao waliona ni jukumu lao kutusaidia waafrika. Hii ndio sababu mpaka leo tuna kaa tu na kusubiri kupewa ( asante baba) yaani kupata miasaada. Bado inanitatanisha sana, Kwani waafrika bado tunaamini yote tuliyofunzwa na wazungu. Hususani dini, wakati wao wenyewe wameacha kabisa kuamini kuwa kuna MUNGU wanaamini miungu wengine kama miti n.k. Je? kwa nini wao walitukataza sisi tusiamini miungu/mizimu wetu?

Na; Yasinta Ngonyani

Sunday, May 11, 2008

Mei 11, 2008 Hali ya hewa inaendelea..........

Kama ulisoma blogg ya hali ya hewa ya kwamba kulikuwa na baridi kiasi kwamba mtu hukuweza kutoka nje. Sasa ni kinyume kabisa watu wamefufuka. Kiasi kwamba unashikwa na butwaa kuona watu jinsi wanavyojianika kama mihogo. Kwa kweli mila na desturi ni kitu muhimu sana. Siku ya kwanza nilishikwa na butwaa kuona baba, mama, mtoto, mamamkwe, babamkwe wote wamejianika kama mihogo au mamba. utakuta wtu wanatembea na hizi nguo za kuogelea siku nzima. Kisa wanataka kupata rangi yaani sisi binadamu hakuna anayeridhika na kile mungu alichompa. Mwafrika anataka kuwa mzungu na mzungu anataka kuwa mwafrika.

Na; Yasinta Ngonyani

Saturday, May 10, 2008

Mei 10, 2008 kazi bila mshahara

Hakuna mtu apendaye kufanya kazi bila kulipwa,kama si utumwa. Kwani nimesoma na pia nimesikia hapa na pale ya kuwa kwa sasa kuna utata wa walimu Afrika(tanzania) kuna shule moja ipo hapo Songea inaitwa Taifa foundation sec. school. wao hawana walimu. Inawezekana wakawa siku nzima bila kupata hata kipindi kimoja. Walimu wamekula mgomo hawapati mshahara. Ni vizuri kwa wao na ni hasara kwa wanafunzi. Kwani ukizingatia kuna wanafunzi ambao wanahitimu yaani kidato cha nne . Inaonekana watu wanadharau sana kazi ya ualimu na wanasahau ya kwamba hatuwezi kupata elimu bila ya walimu na walimu hawawezi kufanya kazi bila kupata ridhiki yao. Cha kushangaza zaidi ni kwamba wanafunzi wakifanya maandamano/kulalamika, hakuna anayewasikiliza isipokuwa wanapigwa marungu na wengine hata kuwekwa ndani je? Wanafunzi hao hawana haki? Na ukizingatia hiyo elimu si bule, kwa hiyo sio walimu tu ambao inabidi walipwe. Kwani hata wazazi wanaumia wanatoa ada ili watoto wao wapete elimu. Kama itaendelea hivi basi hakutakuwa na taifa la kesho. Je? wasomaji mnasemaje labda inawezekana Waziri wa Elimu halifahamu suala hili au vipi. wani inabidi lichukuliwa majukumu haraka sana tunapoteza maraisi, mawaziri na maprofesa wa baadaye.

Na; Yasinta Ngonyani

Tuesday, May 6, 2008

Mei 6, 2008 Furaha ni kitu adimu

Mara nyingi napatwa na hasira sana na pia uchungu.Yaani ninaposikia watu wanasema, fulani yule anaishi maisha mazuri mwenzetu. Yaani watu wanafikiri kuwa ma gari nzuri, nyumba nzuri nguo nzuri basi akili zao zinawatuma ya kuwa huyu mtu/mwenzetu sio mwenzetu ana furaha na pia raha sana. Kwa kweli sio hivi:- unaweza ukawa na vitu vyote hivyo na ikawezekana maisha yako hayana furaha. Kwani FURAHA sio vitu.
1. Furaha ni kuwa na marafiki/rafiki wenye/mwenye furaha.
2. kuwa na furaha unaweza ukawa na furaha hata kama huna mali yaani vitu vizuri. Nina maana FURAHA NI MUHIMU KOLIKO PESA.
3. Pia furaha ni kuamka kila asubuhi na kujua kuwa ni mzima wa afya pia kuwa na familia ambayo inakujali na kukupenda wewe kama wewe.

Mtu /watu mwenye/wenye furaha huishi maisha marefu.

Na; Yasinta Ngonyani

Thursday, May 1, 2008

Mei 1, 2008 Elimu

Hili jambo limekuwa likinikereketa sana akilini mwangu. ELIMU je? ni nani ana haki ya kupata elimu hapa duniani. Kwa mfano afrika yetu,wazazi wengi wanasema hakuna haja ya kusomesha watoto/mtoto wa kike kwani wanaogopa watapoteza bure pesa kumsomesha mtoto wakati wanajua baada ya muda atarudi nyumbani tu. Lakini kitu ambach mimi bado sijaelewa kwa nini hao wasichana wanaokatishwa masomo baada ya kulea mtoto wake asiendelee na masomo? kwani kwa akili yangu sioni kama kuna tatizo wao wasiendelee na masomo yaani yote ya shule ya msingi na pia sekondary. Au kwa nini basi kusiwe na shule maalum kwa wale wasichana waliopata watoto. Kwani inasemekana kuwa Elimu ni ufunguo wa maisha , Sasa je? kama sisi wasichana hatupati elimu tutakuaje na ufunguo wa maisha?

Na; Yasinta Ngonyani