Showing posts with label maneno. Show all posts
Showing posts with label maneno. Show all posts

Friday, April 11, 2014

NAPENDA KWATAKIENI MWISHO WA JUMA KWA USEMI HUU KWENYE KANGA HII!!

Muwe na mwisho wa juma mwema sana wote. Pia kama ulimkosea rafiki, jirani, ndugu, au mtu yoyote sasa ndiyo wakati mwafaka wa kumsamehe maana wikiendi ijayo ni PASAKA. IJUMAA NJEMA!!!

Wednesday, July 17, 2013

NIMEUPENDA HUU WIMBO NA LEO NILIKUWA NAWAZA HIVI NA BAHATI NIMEKUTANA NA WIMBO HUU UKIPATA MUDA EBU SIKILIZA ASEMAVYO MUIMBAJI...MANENO MANENO....


Kila siku ninapoamka ninapoinza siku mpya ninamshukuru Mola kwa kunilinda nafasi nyingine nikapewa labda nikijituma kwa siku wataniletea ......haya endelea kusikiliza ujumbe wake..JUMATANO NJEMA SANA.

Tuesday, June 26, 2012

NENO LA LEO!!

Kama vyakula ulavyo sio vizuri kwa mwili wako, basi angalia viwe ni vizuri kwa ajili ya nafsi yako.
SIKU NJEMA KWA WOTE...KAPULYA

Saturday, December 17, 2011

MANENO YA BUSARA AMBAYO NIMEAMBIWA ....

Moja ya furaha si lazima kwa yule ambaye ana kila kitu, lakini anaweza kuwa mmoja ambaye anajua jinsi ya kufanya kwa ubora kila kitu kilicho karibu yake.
.............JUMAMOSI NA JIONI NJEMA KWA WOTE...

Friday, May 6, 2011

TAFAKARI YA IJUMAA HII YA LEO!!!

Kila nikijaribu kusoma maandishi haya "Mpumbavu ni Mpumbavu 2 awe amesoma au hajasoma" nahisi kichwa changu kama kimechoka vile na mwisho nimeona afadhali niweke hapa kwani kila wakati palipo na wengi hapaharibiki neno... Halafu baada ya muda nakutana ....




.....na maneno haya tena "Fisi Akiwa Hakimu Mbuzi Hana Haki" nikaona hapa sasa kaaaazi kwelikweli ...Sijui nami niandike kwenye baiskeli yangu...mmmmhh TUTAFAKARI PAMOJA JAMANI....NA PIA NAWATAKIENI IJUMAA NJEMA PI MWISHO WA JUMA MWEMA PANAPO MAJALIWA TUTAKUTANA TENA!!!!

Monday, September 14, 2009

UJUMBE WA LEO:- JINSI YA KUCHEZA NA MANENO (KISWAHILI)

Dar es Salaam = Lala salama
Afrika nzima = Wazimana
Tanga = Wanatanga tanga
Wakenya = Wanakenyana
Tanzania = Wanazamia
Naiorobi = Wanaibiana
Arusha = Wanarusharushana
Wasukuma = Wanasukumana
Mombasa = Wanatongozana
Uganda = Wanagandana
Kisumu = wanakisiana

Monday, May 18, 2009

MISEMO /ORDSPRÅK

Ngoja leo tuangalia misemo yetu nimeona niandike lugha zote mbili.


Kiswahili: Kwa kila dakika uwepo na hasira, unapoteza sekunde sitini za furaha yako.
Svenska/kiswidi: För varje minut som du är arg, förlorar du sextio sekunde av glädje.

Kiswahili: Ni afadhali kupoteza maneno kwa uzuri kuliko kukusanya.
Svenska/Kiswidi: Det är bättre att slösa med vänliga ord än att samla på dem.

Kiswahi: Kila kitu kinahitaji uamuzi.
Svenska/kiswidi: Mycket handlar om beslutsamhet.

Kiswahili: Watu wengi wanataka kuwabadili wengine kuliko kujibadili wenyewe
Svenska/Kiswidi: Många människor vill hellre förbättra anda än sig själva

Kiswahili: Si muhimu wapi unatoka isipokuwa wapi unakwenda.
Svenska/Kiswidi:Det viktigaste är inte vårifran man kommer, utan var man går.

Kiswahili: Tupa likusumbuala, pokea lichangamshalo
Svenska/Kiswidi: Släng ut det som stör, led in det som stimulerar.

Kiswahili: Anayeacha kuwa bora anaacha kuwa mwema.
Svenska/Kiswidi: Den som slutar att bli bättre slutar att vara bra

Kiswahili: Kama hali inakuwa mbaya rudi nyuma na uangalie vizuri
Svenska/Kiswidi: När allt verkar hopplöst ta då ett steg tillbaka och lift blicken.

Friday, October 10, 2008

BAADHI YA MANENO YA KISWAHILI NA MAANA YAKE

Leo nimeona nijikumbushe kidogo maneno ya kiswahili kisije kikaniacha. Kama si sahihi naomba msaada:-

Muungwana = Mtu mwenye adabu na desturi njema, Mtu anayekaa na binadamu wenzie kwa uzuri, mtu mwenye utu. Pia unaweza kusema mtu asiye mtumwa au jina la heshima analoitwa mtu.

Mvumilivu = Mtu anayestahamili taabu au mambo mazito (mstahamilivu).

Ngangari = Mtu mwenye msimamo.

Fadhila = Wema, ukarimu, hisani, huruma.

Wema = Ni hali ya matendo mazuri.

Ukarimu= Utoaji vitu au mali kwa kukaribisha watu au kuwasaidia wanaohitaji msaada bila ya malipo. Ni kinyume cha ubahili.

Hisani = Moyo wa kutaka kutenda mazuri kwa ajili ya mwingine.

Huruma = Moyo wa wema; imani, rehema na upole.

1. Imani ni mambo anayokubali mtu kuwa ni ya kweli na anayopaswa kuheshimu hasa katika dini: itikadi. Na pia ni maoni ya moyo yanayomfanya mtu awe na mkabala fulani juu ya jambo au kitu.

2. Rehema ni neema anazopata binadamu kutoka kwa mwenyezi Mungu. Na neema ni hali ya kuweko na uwingi wa nafasi; hali ya kutoweko shida au upungufu wa vitu vya kumuendeshea binadamu maisha; baraka na ustawi. Pia ni jambo jema analopata kiumbe kutokana na uwezo wa mwenyezi Mungu; riziki.

3. Upole ni hali ya kutopenda fujo, hali ya mtu mtulivu na mtaratibu.

Thamini = Gharama au ubora wa kitu kutokana na hali na kuhitajika kwake na jamii.

Na mwisho ni Si bitozi = Asiyejisikia.