Friday, May 6, 2011

TAFAKARI YA IJUMAA HII YA LEO!!!

Kila nikijaribu kusoma maandishi haya "Mpumbavu ni Mpumbavu 2 awe amesoma au hajasoma" nahisi kichwa changu kama kimechoka vile na mwisho nimeona afadhali niweke hapa kwani kila wakati palipo na wengi hapaharibiki neno... Halafu baada ya muda nakutana ....




.....na maneno haya tena "Fisi Akiwa Hakimu Mbuzi Hana Haki" nikaona hapa sasa kaaaazi kwelikweli ...Sijui nami niandike kwenye baiskeli yangu...mmmmhh TUTAFAKARI PAMOJA JAMANI....NA PIA NAWATAKIENI IJUMAA NJEMA PI MWISHO WA JUMA MWEMA PANAPO MAJALIWA TUTAKUTANA TENA!!!!

10 comments:

emu-three said...

Dada Yasinta aliyeandika maneno ya mwanzoni, huenda likuwa anamlenga mbaya wake, ...rejea maneno ya khanga yanavyoandikwa, ...ni mipasho. Lakini tukumbuke usemi usemao `nyani haoni nini...?
TUPO PAMOJA DADA YANGU MPENDWA SANA

Mwanasosholojia said...

Siku zote methali,nahau,na misemo ina maana ya ndani zaidi ya yanayosomeka, au kuandikwa, shukrani dada Yasinta kwa kutushirikisha, uwe na weekend njema!

Goodman Manyanya Phiri said...

Na mbuzi akishindwa kesi mbele ya hakimu mbuzi-mwenzie, lazima atamtukana kisirisiri huyo hakimu kwa kudai: "mbona yule hakimu fisi tu!"

Kama wanavyosema wenzetu huko Ulaya: [mbwa huwezi kumnyonga bila kumpachika kajina baya]... GIVING A DOG A BAD NAME BEFORE YOU HANG HIM!

Rachel Siwa said...

Duuhhh Maneno ya leo ni mazito,lakini kila mtu anamaana yake mpaka akandika hivyo au kutuma ujumbe huo!

Asante dada uwe na wakati mzuri na familiya pia!.

Simon Kitururu said...

Katika posti hii ya YASINTA natafakarishwa na ....:

``...palipo na wengi hapaharibiki neno...´´


Hivi kwenye wengi si ndio neno huharibika?

Nawaza tu!:-(

Yasinta Ngonyani said...

Ahsanteni wote kwa kuchangia mawazo yenu.
Ni kweli haya maneno, methali, nahau na misemo kila mtu anatafsiri anavyojua yeye.....na kila msemo una maana yake.

SIMON! Niliposema ``...palipo na wengi hapaharibiki neno...´´ nilikuwa na maana kuwa huwa na michango mingi na kila mtu ana uhuru wa kusema akifikiriacho na ndipo wengi hujifunza.... Sikatai ya kwamba ina wezekana pia kama ulivyowaza kuwa panaweza pakaharibika neno.....

Simon Kitururu said...

@Nangonyani: Nilikuelewa kama hivyo uelezavyo na ndio maana ukinisoma nairudia komenti yangu:


``Katika posti hii ya YASINTA natafakarishwa na ....:

``...palipo na wengi hapaharibiki neno...´´


Hivi kwenye wengi si ndio neno huharibika?

Nawaza tu!:-(´´ mwisho.

Misingi ya komenti hii yangu ni maneno ``Natafakarishwa `` na sentensi``Nawaza tu!´´


Na ndicho nilichomaanisha kuwa katika ulichoandika kiini cha kutafakarishwa kwangu ilikuwa hapo!

NI hilo tu na samahani kwa kujielezea !

Yasinta Ngonyani said...

Simon katika maisha ni kuulizana na kuelezana na hapo ndipo tunaelimika...huna haja ya kuomba smahani:-) Na Ahsante kwa ufafanuzi!

Penina Simon said...

1. Ha! ha! ha! dada yasinta hapo mimi, sifahamu kiswahili vizuri lkn nahsi huyo mpumbavu basi huzaliwa akiwa mpumbavu, (tabia ya asili) ina maana kwanza atakuwa hajielewi kama ni mpumbavu, anajiona yeye ndio yeye, kwa hiyo hata akielemika vipi hawezi kuacha huo upumbavu wake sababu hajijui kama yupo mpumbavu.

2. Huo msemo wa pili ni rahisi kidogo, unamaanisha kuwa kama adui yako mkubwa akiwa ndio boss basi wewe sauti tena huna, hata kama huna kosa akipenda anakugandamiza tu atakavyo yeye.

Ahsante sana kwa changamoto hizi.

Goodman Manyanya Phiri said...

@Penina

Mawazo yako ni mazito sana; tena nayapenda kwasababu ni ukweli mtupu.

Lakini huoni kwamba maisha ni mepesi sana ukiwa kila siku unaposhuka ngazi za nyumba yako kwenda kazini unajuwa tayari waziwazi (kutokana na misemo ya Wahenga) ni aina gani ya binadamu utakaekabilana nayo?

Safi sana, aiseee!