Showing posts with label amini. Show all posts
Showing posts with label amini. Show all posts

Sunday, June 6, 2010

JUMAPILI NJEMA KWA WOTE NA UJUMBE NI HUU UPITIOA KWA WIMBO HUU WA ZAKAYO!!!



Wimbo huu nadhani unaimbwa kwa kimasai nimeusikiliza mara nyingi na nikaona ni vema kulinukuu hili neno:-
Mtakatifu Luka 19: 1-10
”Naye alipoingia Yeriko alipita katikati yake. Na tazama, palikuwa na mtu, jina lake Zakayo, mkubwa mmoja katika watoza ushuru, naye ni tajiri. Huyu alikuwa akitafuta kumwona Yesu ni mtu wa namna gani, asiweze kwa sababu ya umati wa watu, maana ni mfupi wa kimo. Akatangulia mbio, akapanda juu ya mbuyu apate kumwona , kwa kuwa atakuja kuipitia njia ile. Na Yesu, alipofika mahali pale, alitazama juu akamwambia, Zakayo, shuka upesi, kwa kuwa leo imenipasa kushinda nyumbani mwako. Akafanya hharaka, akashuka, akamkaribisha kwa furaha. Hata watu walipoona, walinungúnika wote, wakisema, Ameingia kukaa kwa mtu mwenye dhambi. Zakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang´nya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne. Yesu akamwambia, Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu. Kwa kuwa mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.”
TUMSIFU YESU KRISTO MILELE AMINA. JUMAPILI NJEMA WANDUGU!!!

Sunday, October 19, 2008

MAISHA BAADA YA KIFO

Baada ya kifo kinatokea nini?
Kuhusu kifo kuna mitazamo mbalimbali inayotofautiana kadiri ya imani ya mtu. Katika maisha ya binadamu kwa kipindi chote cha maisha yake, amakuea akipambana vikali sana na swali hili: “Baada ya kifo changu kitaendelea nini?” Jibu la swali hili lina maana sana katika maisha yetu hapa duniani, ingawa watu wengi wanaogopa kuongea juu ya jambo hilo. Madhehebu mbalimbali ya dini yamekuwa yakitoa majibu ya swalihili kadiri ya imani ya mapokeo yao.
Wakristo wanaamini nini?
Lakini katika imani hizo zote, tumaini la wakristo ni la uhakika kwa sababu kuu mbili. Moja, Ufufuko wa Kristo na Pili ni ushuhuda wa Maandiko Matakatifu. Biblia inatupatia picha ya kweli na kamili kuhusu kitakachoendelea baada ya kufa. Hata hivyo, wakristo wengi wameelewa vibaya juu ya maisha baada ya kufa. Wengene wanaamini kwamba watakuwa miongoni mwa malaika, wengine wanaamini wataingia katika hali ya usingizi wa roho, wakati wengine wanaamini kwamba watakuwa wanaelea katikati ya mawingu.
Wakristo wanaamini kwamba Kifo sio kitu cha kuogopa, baada yake katika kufa ndipo tutafikia kilele cha maisha yetu yaani kurudi kwa Baba Mbinguni. Kuishi maana yake tunadumu katka nchi ya kigeni. Kifo kimepoteza maumivu yake na sasa kifo ni ushindi kupitia Ufufuko wa Yesu Kristo Bwana wetu.
Wakana Mungu(Atheists)
Wakana mungu(Atheists) wanaamini kwamba mtu akifa ndio mwisho wake. Hakuna maisha baada ya kifa wala kwamba kuna roho ambayo inakwenda Mbinguni na itaendelea kuishi milele. Tunachotakiwa kutegemea maishani ni kwamba kifo hakiepukiki, binadamu lazima afe na maisha ya ulimwengu huu yana mwisho.
Wale wanaoabudu miungu(Pantheistics) wanafundisha kwamba mtu yumo katika mzunguko usio na mwisho na umwisho mpaka mzunguko huo unapovunjika ndipo mtu anakuwa kitu kimoja na mwumba wake. Namna mtu atakavyokuwa katika maisha ya baadaye inategemea namna gani aliyaishi maisha ya awali. Pale mtu anapounganika na muumba wake, palepale anakoma kuwa kuishi kama mtu, ila anakuwa sehemu ya nguvu za maisha matakatifu kama vile tone la maji linalotua Baharini.
Wale wanaoshikilia dini za makabila yanayosema kwamba vitu vyote vina roho(animistic) wanaamini kwamba baada ya kifo roho ya binadamu inabaki ardhini au inasafiri kwenda kuungana na roho zilizotangulia za mababu (wahenga) zilizoko duniani. Kwa milele wanatembea na wanatangatanga katika giza wakikumbana na furaha na huzuni. Baadhi ya roho hizo zilizotangulia zinaweza kuitwa tena kuja kusaidia na kuwatesa wale wanaoishi duniani.
Waislamu wanaamini nini?
Waislamu wanafundisha kwamba, mwisho wa dunia, Mungu atahukumu maisha na kazi za bainadamu. Wale ambao matendo yao mema yanazidi matendo yao mabaya wataingia paradizini. Wanaobaki wataingia ahera. Korani inafundisha kwamba paradizini watu watakuwa wanakunywa divai na kuhudumiwa na wasichana wa mbinguni na baadhi ya wasichana hao watakuwa wake zao.