Sunday, October 19, 2008

MAISHA BAADA YA KIFO

Baada ya kifo kinatokea nini?
Kuhusu kifo kuna mitazamo mbalimbali inayotofautiana kadiri ya imani ya mtu. Katika maisha ya binadamu kwa kipindi chote cha maisha yake, amakuea akipambana vikali sana na swali hili: “Baada ya kifo changu kitaendelea nini?” Jibu la swali hili lina maana sana katika maisha yetu hapa duniani, ingawa watu wengi wanaogopa kuongea juu ya jambo hilo. Madhehebu mbalimbali ya dini yamekuwa yakitoa majibu ya swalihili kadiri ya imani ya mapokeo yao.
Wakristo wanaamini nini?
Lakini katika imani hizo zote, tumaini la wakristo ni la uhakika kwa sababu kuu mbili. Moja, Ufufuko wa Kristo na Pili ni ushuhuda wa Maandiko Matakatifu. Biblia inatupatia picha ya kweli na kamili kuhusu kitakachoendelea baada ya kufa. Hata hivyo, wakristo wengi wameelewa vibaya juu ya maisha baada ya kufa. Wengene wanaamini kwamba watakuwa miongoni mwa malaika, wengine wanaamini wataingia katika hali ya usingizi wa roho, wakati wengine wanaamini kwamba watakuwa wanaelea katikati ya mawingu.
Wakristo wanaamini kwamba Kifo sio kitu cha kuogopa, baada yake katika kufa ndipo tutafikia kilele cha maisha yetu yaani kurudi kwa Baba Mbinguni. Kuishi maana yake tunadumu katka nchi ya kigeni. Kifo kimepoteza maumivu yake na sasa kifo ni ushindi kupitia Ufufuko wa Yesu Kristo Bwana wetu.
Wakana Mungu(Atheists)
Wakana mungu(Atheists) wanaamini kwamba mtu akifa ndio mwisho wake. Hakuna maisha baada ya kifa wala kwamba kuna roho ambayo inakwenda Mbinguni na itaendelea kuishi milele. Tunachotakiwa kutegemea maishani ni kwamba kifo hakiepukiki, binadamu lazima afe na maisha ya ulimwengu huu yana mwisho.
Wale wanaoabudu miungu(Pantheistics) wanafundisha kwamba mtu yumo katika mzunguko usio na mwisho na umwisho mpaka mzunguko huo unapovunjika ndipo mtu anakuwa kitu kimoja na mwumba wake. Namna mtu atakavyokuwa katika maisha ya baadaye inategemea namna gani aliyaishi maisha ya awali. Pale mtu anapounganika na muumba wake, palepale anakoma kuwa kuishi kama mtu, ila anakuwa sehemu ya nguvu za maisha matakatifu kama vile tone la maji linalotua Baharini.
Wale wanaoshikilia dini za makabila yanayosema kwamba vitu vyote vina roho(animistic) wanaamini kwamba baada ya kifo roho ya binadamu inabaki ardhini au inasafiri kwenda kuungana na roho zilizotangulia za mababu (wahenga) zilizoko duniani. Kwa milele wanatembea na wanatangatanga katika giza wakikumbana na furaha na huzuni. Baadhi ya roho hizo zilizotangulia zinaweza kuitwa tena kuja kusaidia na kuwatesa wale wanaoishi duniani.
Waislamu wanaamini nini?
Waislamu wanafundisha kwamba, mwisho wa dunia, Mungu atahukumu maisha na kazi za bainadamu. Wale ambao matendo yao mema yanazidi matendo yao mabaya wataingia paradizini. Wanaobaki wataingia ahera. Korani inafundisha kwamba paradizini watu watakuwa wanakunywa divai na kuhudumiwa na wasichana wa mbinguni na baadhi ya wasichana hao watakuwa wake zao.

4 comments:

EDWIN NDAKI (EDO) said...

nimependa tafakari nzuri uliyoleta leo.

hakika wote tu wasafirina lazima tujipande jinsi ya kuis

EDWIN NDAKI (EDO) said...

nimependa tafakari nzuri uliyoleta leo.

hakika wote tu wasafirina lazima tujipangea na kuishi vema na wenzetu ili siku mmoja tuweze kufia huko pema

Unknown said...

Dada umegusa sehemu ambayo inabidi tukae tuitafakari kwa makini sana
dada uwe na wakati mzuri.

Christian Bwaya said...

Tafakari nzuri Yasinta.

Binafsi, naona bila kurejea mafundisho ya dini zetu zinazopingana, naona maisha baada ya kifo yapo.

Kwa nini?

Ukifikiria maana ya maisha haya ya sasa, kwa kujiuliza swali kwa nini tunaishi, huoni maana ya wazi. Maana yake ni kwamba ionekanavyo tunaishi kujiandaa kwa maisha yajayo!

Nasubiri kusoma mawazo ya wachangiaji wengine.