Wednesday, October 1, 2008

TABIA TA NCHI ( Yaani joto upepo mvua n.k) CLIMATE

Hali ya hewa inabadilika nchi anzazo miaka ya zamani kulikuwa na baridi (theruji) nyingi sasa ni joto. Kiasi kwamba mimea ya afrika inastawi ughaibuni wakati wa baridi kali.
Jambo jingine ambalo ni muhimu sana ni kwamba watu wanakata miti juu ya mlima kilimanjaro na halafu hawapandi mingine.Hii inasababisha kuyeyuka kwa ile theruji iliyopo pale kileleni. Labda niseme kwa ujumla si vizuri kukata miti sehemu yoyote na kuacha bila kupanda mipya. Tusisahau ya kwamba ni muhimu tukate na tupande miti tena.

The Gulf Stream hii ina nguvu sana na inahakikisha hali ya hewa iwe joto kiasi. Inasemekana katika bara la Ulaya kama barafu itayeyuka basi maji yote ya baharini The Gulf Stream itazuia. Kwa hiyo The Gulf Stream inasaidia kwa bara la Ulaya kuwa na joto.

Inasemekana mwaka 2010 Ughaibuni itakuwa na baridi kama Sibiria na Afrika Mashariki kutakuwa na ukama. Kwa hiyo itabidi tuhamie katika Sayari nyingine au tupunguze dioksidi ya kabon (CO2) . Na hii ni haraka inabidi tuanze sasa.

4 comments:

Unknown said...

Mambo vp niaje?nikweli hapa cpati picha baada ya miaka kumi hali ya hewa itakuwaje,watu watatafutana.

Christian Bwaya said...

Mlima Kilimanjaro ukiuuona sasa hivi hutaamini zile picha zilizopigwa miaka mitano iliyopita. Tunakokwenda siko.

Ipo haja ya kuchukua hatua. Kila mmoja kwa nafasi yake.

MARKUS MPANGALA said...

kwa hii serikali ya walemavu wa akili hii,hakuna noma utaona watazungumza na kuweka semina kibao halafu makabrasha wanayafungia kabatini mpka yawe navumbi. habari inakwisha hapo huku tukingojea majanga. amani kwao watu hawa

Yasinta Ngonyani said...

Kwa hiyo ni sasa ndio wakati wa kuchukua hatua kaka zangu tukichelewa basi itatubidi tuhamie katika Sayari nyingine je tupo tayari?