Sunday, October 12, 2008

JE? NI VIGUMU KUISHI BILA NGONO?

Wengi tunajua/pia tunajadili ukimwi na ngono, lakini tunahitaji kukumbuka kuwa sio waTanzania wote ama binadamu wote ni hivyo. Cha muhimu ni kuelewa kuwa ugonjwa huu unaua binadamu, na kwamba, hawa binadamu wanatokea katika kila sekta ya maisha, wanadini, wapagani, wasio na elimu, wenye elimu, wamjini, wanavijiji, nk.
Je? kuna ubaya gani kuwaelimisha wengine kuhusiana na matumizi ya ndomu?

Tukumbuke ya kwamba baada ya Hawa na Adam kula lile tunda baya, sote tulizaliwa madhambini, na tunashawishika kirahisi. Yaani, hata Hawa na Adam , ghafla waligundua ya kuwa wako uchi, nadhani mle bustanini kulikuwa kuzuri na kulikuwa na hewa bora yaani jua lilikuwa haliwachomi, majani hayakuwakata ..walipofukuzwa ndio walilazimika kuvaa nguo kwa sababu ya jua kali, mavumbi, miiba nk. Hakuna aliyewaamrisha kuvaa nguo.

Ngono inashawishiwa maishani kwa mbinu nyingi ambazo ni vipofu tu wasioziona. Katika magazeti, mavazi, sinema, hadithi za waliojaribu, umbea nk. Ni kama vile Hawa na Adamu, walivyoshawishika kula lile tunda hata walivyojua Mungu wao aliwakataza, lakini sisi wengine tuanashawishika kirahisi kula hili tunda liitwalo "ngono". Wote tunajua tukishalionja tunda hata yeyote akikuambia "basi acha" wengi tunacheka ana kushangaa? Hii in kama vile mtoto akishaonja pipi, halafu ategemewe kutotamani pipi mbeleni.

Pipi zitakuwepo duniani kwa miaka mingi, vishawishi vya ngono vitakuwepo duniani kwa miaka mingi... Hii ndio sababu tunahitaji kuelimishwa kuwa pipi si nzuri kiafya. Lakini pia tunahitaji kuelimishwa kuwa wale watakao tamani basi wale nyingina wasisahau kupiga mswaki. Naamaanisha, ujembe wa kuacha ngono uambatane na ujumbe wa kupunguza kufanya ngono na watu wengi NA elimu ya kutumia ndomu.

2 comments:

Anonymous said...

utamu ndugu yangu, tupunguze kuogopa ukimwi? mm jamani kweli utamu lakini ukimwi nao .................. kazi kwenu

Yasinta Ngonyani said...

Utamu huo utakupeka kaburini ndugu yangu usiyekuwa na jina