Monday, May 31, 2010

BLOG YA WASIOONA YAANZISHWA:- TANZANIA LEAGUE OF THR BLIND TEMEKE DISTRICT

Umoja ni nguvu


Ulimwengu wa Bloggers sasa unazidi kupanuka, kwani wasioona Wilaya ya
Temeke “Tanzania League of the Blind Temeke District nao wameamua
kufungua Blog yao.

Akiongelea Blog hiyo Mwenyekiti wa Chama hicho ndugu Abdala Ally
Nyangalio alisema kufunguliwa kwa tovuti hiyo ndogo kumekuja baada ya
chama hicho kupata mafunzo ya Utawala bora ambapo moja ya masomo
waliyojifunza ni matumizi ya TEHAMA (ICT) katika maendeleo.

Katika mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Foundation for Civil Society,
Washiriki wa semina hiyo walivutiwa sana na somo hilo na kuomba
ushauri na msaada zaidi kutoka kwa mwezeshaji Ndugu. Jacob Malihoja
ambaye hakusita kuwasaidia kufungua tovuti ndogo (Blog) hiyo.

Akielezea zaidi Bw. Nyangalio alisema kuwa madhumuni ya kufungua
tovuti hiyo ni kuweza kupata mawasiliano na watu ama taasisi mbali
mbali wenye moyo wa ubinadamu, moyo wa huruma kwa walemavu ili waweze
kutoa mchango wao kuwasaidia walemavu wasioona wilaya ya Temeke kila
mmoja kwa kadiri ya nafsi aliyonayo.

Ndugu Nyangalio pia alisema kupitia Blog hiyo wataweza kupata mawazo
na maoni mbali mbali kutoka kwa watu wenye moyo na nia njema katika
kufanikisha harakati zao mbali mbali walizonazo na watakazokuwanazo.

Mwezeshaji huyo waliyemtaja ambaye ni Blogger mwenzetu Ndugu Jacob
Malihoja, alisema kuwa ndugu hawa wanahitaji kusaidiwa kila mmoja kwa
kadiri ya uwezo na nafasi aliyonayo ya kuwasaidia.

Aidha ndugu. Malihoja alisema anawashauri watu mbali mbali
watakaotembelea blog hiyo wawasiliane na viongozi wa Chama hicho
ikiwezekana kwa simu na kuwatia moyo katika juhudi walizonazo kwani
alichojifunza ni kuwa wanahitaji sana kutiwa moyo jambo ambalo
linawaongezea moyo na kasi ya kujiinua na kushiriki katika maendeleo
ya Taifa.

Sambamba na hilo Ndugu Malihoja alisema yeyote mwenye uwezo wa
kujitolea kuwasaidia katika harakati zao, yeye mwenyewe au
kuwaunganisha na watu wanaoweza kuwasaidia litakuwa ni jambo bora sana
kufanya hivyo.

Bw. Nyangalio pia alisema blog hiyo itakapokuwa kanmilika kwa kuwekwa
taarifa zote muhimu wanazohitaji watafanya sherehe ya uzinduzi katika
tukio litakalohusisha wasioona wote Wilaya ya Temeke, Viongozi wa
Serikali na kisiasa, wafanyabiashara na wadau wengine mbali mbali
wataalikwa.

Zaiai ingia hapa kuwasoma http://www.tlbtemeked.blogspot.com/

Sunday, May 30, 2010

LEO HAPA NI SIKU YA AKINA MAMA/MORS DAG!!!


mama na bintiye 1997 Mahumbato/Mbinga

Ok, basi nami nimepata nafasi ya kusema machache ni kwamba. Najua sehemu nyingine siku hii imeshapita ila hapa Sweden ni leo. nami napenda kuwapa pongezi akina mama wote duniani bila kumsaau mamangu.Ingawa hayupo nasi kiwili lakini kiroho yupo nasi Ahsante mama. Pia napenda kuwapongeza akina bibi, shangazi, mama wakwe na mabinti woote katika dunia hii


Hapa ni binti mwingine na mama yake jana 29/5 /2010 Sweden

Hapa Sweden leo ni siku ya akina mama duniani. Nasi leo tumeamua kumpongeza mametu mpendwa ktk blog yake ni sisi Camilla na Erik. Tunampenda sana mametu hasa akiwa na hasira, huwa tunapata kila kitu tutakachotaka.( kwa niaba ya mama) Pia pongezi nyingi kwenu akina kaka babu, baba, mjomba na vijana wote kwani bila uweopo wenu basi tusingekuwepo hapa duniani.

Hakuna sherehe bila mziki nami nimeona mziki huu utafaa siku hii ya leo Haya karibuni tumsikilize dada Emmy Kosgei akiuliza nani kama mama? katika wimbo wake huu!!







NA PIA NATAKA KUWATAKIENI WOTE JUMAPILI HII YA MWISHO WA MWEZI HUU WA TANO MUWE NA WAKATI MZURI SANA WOOOTE JUMAPILI NJEMA SANA!!

Friday, May 28, 2010

Lucia: Uyatima umenifanya nisome kwa shida !!

Lucia, mwenye kitambaa chekundu kichwani akiwa na wadogo zake Jacqline na Elias nyumbani kwao katika kijiji cha Nyambiti Wilayani Kwimba mkoani hapa.


“Wakati baba anafariki aliniacha nikiwa darasa la tano katika shule ya Msingi Nyambiti mwaka 2003 na mwaka mmoja baadaye mama naye alifariki hapo ndipo hali ya maisha katika familia yetu ilipoanza kuwa ngumu,” anasema Lucia Juma (20).

Anasema kuwa kifo cha baba na mama yake kilimfanya aishi maisha magumu, kwani wakati akiwa na matumaini ya kupata elimu alilazimika pia kuwahudumia wadogo zake.

“Nilikuwa nimezoea kutegemea wazazi wangu lakini ilinibidi nianze kutegemewa na wadogo zangu licha ya kuwa sina uwezo na mimi nikiwa bado mwanafunzi tena wa shule ya msingi,” anasema Lucia.

Lucia ambaye ni mmoja kati ya wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka jana katika shule ya Sekondari ya Taro iliyopo katika kijiji cha Nyambiti wilayani Kwimba mkoani Mwanza anasema baada ya wazazi wake kufariki amesoma kwa shida sana na hali hiyo imesababisha hata matokeo yake ya kidato cha nne kutokuwa mazuri na hivyo kujikuta akipata daraja la nne hivyo kushindwa kuendelea na masomo.

“Mazingira ninayoishi yalinifanya hata nisiweze kwenda shule mara kwa mara kwa kuwa muda mwingi nilikuwa nikifukuzwa shule kwa kukosa ada,” anasema.

Lucia anasema mbali na kukosa ada pia alitumia muda wake mwingi akiwa hospitalini badala ya shuleni kutokana na hali ya afya ya mdogo wake kutokuwa nzuri.

“Mmoja kati ya wadogo zangu anasumbuliwa na ugonjwa wa kuishiwa damu, hivyo alipokuwa akiugua nililazimika kutokwenda shule ili nibaki naye na kumuuguza, hata alipokuwa akilazwa hospitali, nililazimika kulazwa naye…,” anasema Lucia na kuongeza kuwa;
‘Sikuishia kulazwa naye tu wakati mwingine nililazimika kutoa damu kwa ajili ya kuokoa maisha yake anapokuwa amepungukiwa damu na kutakiwa kuongezwa,” anasema Lucia.

Anasema kuwa analazimika kubeba jukumu hilo kutokana na ukweli kuwa hakuna mtu wa karibu ambaye anaweza kuwasaidia pindi wanapopata matatizo na hata kujitolea damu kwa ajili ya mdogo wake.

Ninapotoka hospitali ninakuta wenzangu wameishafundishwa sana, hivyo kwangu inakuwa ni vigumu sana kwenda nao sambamba, lakini sikuwa na namna ya kufanya kwa sababu mimi ndiye ninayegemewa na wadogo zangu, wanapopata shida nalazimika kubeba jukumu la kuwasaidia wadogo zangu,” anasema Lucia huku akitokwa na machozi.

Anaongeza kuwa mbali na kutumia muda mwingi hospitalini lakini pia hakuwa na uwezo wa kununua vitabu vya kiada wala ziada kwa ajili ya kujisomea hali ambayo ilikuwa ikimpa ugumu sana pindi anapohitaji kujisomea.

“Tangu nianze kidato cha kwanza hadi namaliza sikuweza kununua kitabu chochote wala mitihani iliyopita (Past papers) kwa ajili ya kujifunzia kama wanavyofanya wenzangu, kwa kuwa sikuwa na fedha ya kumudu kununua vitu hivyo,” anasema
Akizungumzia juu ya ulipaji wa ada anasema kuwa suala la ada na michango mingine ya shule hakuweza kulipa kwa wakati na hivyo alifukuzwa mara kwa mara.

Anasema hatua ya kufukuzwa shule ilikuja baada ya kushindwa kulipiwa ada na Serikali wala halmashauri kwa kuwa hakuwa miongoni mwa wanafunzi ambao majina yao yalipelekwa kwa ajili ya kulipiwa ada.

“Mwaka 2006 nilipoanza kidato cha kwanza nilikwenda kwa Mtendaji wa kata ili na mimi niingizwe kwenye utaratibu wa kulipiwa ada na serikali lakini Mtendaji alidai majina yetu yalicheleshwa kupelekwa Halmashauri na hivyo hatuwezi kulipiwa ada na serikali wala Halmashauri,” Lucia anaeleza.

Anasema kutokana na hali hiyo alilazimika kujilipia ada na kutokana na kutokuwa na uwezo ulipaji wa ada ulikuwa ni mgumu sana kwani hakukuwa na mtu wa kumsaidia.

“Hapa nyumbani tupo na mjomba ambaye anasimamia Saloon iliyoachwa na baba nilipokuwa namwambia juu ya suala la ada alidai hana uwezo wa kunilipia, kwangu ilikuwa ni vigumu sana na wakati mwingi nilifukuzwa shule na hivyo kulazimika kukaa nyumbani hata wiki nzima hadi niende tena kwa mtendaji wa kata aende kuniombea shuleni ndipo niruhusiwe kusoma,” anasema

Anasema kuwa malipo ya fedha ya mtihani wa mwisho wa kidato cha nne alilazimika kwenda kukodisha mashamba yaliyoachwa na wazazi wake ili kupata fedha za mtihani baada ya mjomba wake kukataa kumlipia Sh35,000 za kulipia mtihani.

“Hadi sasa ninavyokwambia nadaiwa shilingi 85,000 shuleni ambazo ni madai ya michango mbali mbali pamoja na ada ambazo nilikuwa silipi kwa kuwa sikuwa na uwezo,” anasema.

“Kwa mazingira ambayo nimesomea naiomba Serikali iweke utaratibu wa kuwasaidia watoto yatima, kwa kweli watoto waliofiwa na baba na mama wanaishi na kusoma kwenye mazingira magumu kwani hata kama kuna ndugu, wazazi wanapokufa ndugu hawawathamini wale watoto,” anasema Lucia huku akilia.

Anasema kuwa maisha ambayo walikuwa wakiishi na wazazi wao na ya sasa ni tofauti kabisa, kwani hata ndugu wamekuwa mbali nao tofauti na walivyokuwapo wazazi wao, hivyo Serikali iangalie watoto yatima na kuwasaidia kwa hali na mali ili waweze kupata elimu kama ilivyo kwa wanafunzi wengine.

Akiwazungumzia wadogo zake anasema kuwa hivi sasa mdogo wake Elias ameanza kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari ya Taro baada ya kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka jana na kufaulu hivyo naye bado anahitaji msaada wa hali na mali ili aweze kusoma na pia anahitaji uangalizi zaidi kwa kuwa ana tatizo la kupungukiwa na damu.

Anasema kwa upande wa mdogo wake Jacqline, yeye hivi sasa yupo darasa la saba na kudai kuwa kulingana na uwezo wake darasani ana matumaini makubwa hata yeye anaweza kufanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba mwaka huu.

Akizungumzia jinsi jamii inavyochukua jukumu la watoto yatima, Lucia anasema kuwa jamii bado haijaona umuhimu wa kuwasaidia watoto yatima licha ya kuwa inafahamu kuwa watoto hao hawana uwezo wowote wa kuweza kuendesha maisha yao.

Akizungumzia matarajio ya maisha yake ya baadaye anasema kama angepata mtu wa kumsaidia kupata nafasi ya kurudia shule angerudia ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuaminika na hatimaye kuweza kupata kazi itakayomuwezesha kujikimu yeye pamoja na wadogo zake.

Naye Mtendaji wa Kata ya Nyambiti, Mathias Mayala, anasema kuwa tatizo kubwa ambalo lilikuwa likiikumba kata hiyo ni kutowatambua watoto yatima na maeneo ambayo wanaishi lakini hivi sasa wameanzisha utaratibu wa kuzunguka kwenye jamii na kuanza kuwatambua watoto hao.

Anasema kuwa hatua hiyo itasaidia hata kuweza kuwahudumia na zinapotokea nafasi za kusomeshwa basi inakuwa ni rahisi kuwafikia kwa kuwa watafahamika sehemu walipo na matatizo yao yatajulikana.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyambiti Joseph Stephen, anasema kuwa hivi sasa wanajipanga kubuni vyanzo vya mapato kupitia kamati za mipango na fedha ili angalau kupata fedha kwa ajili ya kusaidia watoto yatima.

Anasema kuwa suala hilo litafanyika kuanzia kila kitongoji katika kijiji hicho na kuwashirikisha wananchi kwa hali na mali ili waweze kuwasaidia watoto yatima ambao wanazidi kuongezeka kila siku.

Anaongeza kuwa hivi sasa wanaihamasisha jamii kuona namna ya kuweza kuwasaidia watoto yatima angalau kwa kuwachangia chochote ili waweze kuendelea na masomo kwani tatizo la watoto kufiwa na wazazi wao na kubaki peke yao limeonekana kuwa ni kubwa katika wilaya ya kata ya Nyambiti.

Akizungumzia suala la kusaidia watoto yatima diwani wa kata ya Nyambiti Peter Nyanda anasema kuwa ingawa kumekuwa na utaratibu wa halmashauri kuwalipia ada wanafunzi yatima lakini bado wanafunzi wanaolipiwa ni wachache.

Anasema kuwa hali hiyo inatokana na ufinyu wa bajeti kwenye halmashauri na hivyo halmashauri kujikuta zikichukua wanafunzi wachache kutoka kila eneo.

Afisa elimu wa Sekondari wilayani Kwimba Pancras Binamungu anasema baada ya Serikali kuu kurudisha shule kusimamiwa na halmashauri na kutaka halmashauri kuwalipia ada, baadhi ya watoto waliathirika na maamuzi hayo kwa kuwa Serikali kuu ilikuwa ikitoa fedha za ada ya shule na gharama mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya mtoto.

Hata hivyo Afisa Elimu huyo aliitaka jamii kuanzia ngazi ya kitongoji, kijiji na kata kuwasaidia watoto yatima kupata mahitaji yao ya msingi kwani tatizo hilo ni la kijamii na siyo la serikali pekee yake.
“Kuna watoto yatima ambao ndugu zao wa karibu wana uwezo lakini wanashindwa kuwasaidia watoto hao na kuisukumia Serikali,” anasema Afisa Elimu huyo.
“Kuna watoto yatima ambao ndugu zao wa karibu wana uwezo lakini wanashindwa kuwasaidia watoto hao na kuisukumia Serikali,” anasema Afisa Elimu huyo

Na Paulina David, Mwanza (Gazeti la Mwananchi) la alhamis 20/4/2010

Wednesday, May 26, 2010

Maji safi na salama ya kunywa kwa kutumia jua!!

Maji ni muhimu kwa kila binadamu, maji bila wadudu ni muhimu zaidi. Wengi kwa kuatapa Kupata maji salama tunahitaji kuchemsha. Lakini sasa unaweza kupata maji bila kutumia kuni au mkaa sio ndoto, kama unatumia "Solvatten". soma hapa

MAKULILO, Jr. ALA NONDOZI


Mzee wa Nondozi – MAKULILO, Jr. Jumamosi May 22, 2010 amekula NONDOZI – Masters of Arts in Peace and Justice at the University of San Diego (USD) huko California. Hii ni katika kuelekea katika Ph.D in Conflict Analysis and Resolution katika mwaka mpya wa masomo ujao.

Mdau MAKULILO, Jr. ana mpango wa kwenda likizo nyumbani Tanzania akiambatana na mke wake. Katikalikizo hiyo atafanya semina na midahalo kwa watu kuhusu ni jinsi gani mtu unaweza kupata vyuo na SCHOLARSHIPS Ughaibuni. MAKULILO, Jr. yeye mwenyewe amefaidika kwa kupata scholarships zaidi ya nne kwa ndani ya miaka miwili. Na anapenda kuhakikisha wadau wengi wanafaidika na nafasi hizi zilizopo Ughaibuni. Ratiba ya semina na special talks itatangazwa baadaye mara maandalizi yakiwa sawa.

PICHA ZA MAHAFALI

Mdau MAKULILO mara baada ya kula nondozi yake Jumamosi May 22, 2010



MAKULILO Akishangilia kula nondozi



Makulilo akiwa na wanadarasa wenzake waliokula nondozi pamoja


MAKULILO akipongezwa na mke wake Bi. Marie Makulilo


Makulilo na mwalimu wake, Dr. Ami Carpenter

MAKULILO akiwa na Dean of School of Peace, Fr. Bill Headley, PhD

MAKULILO na rafiki zake, Fr. Daniel (Kenya), Ghulam (Afghanstan) wakiwa nje ya School of Peace and Justice


KWA WANAOTAFUTA NONDOZI UGHAIBUNI NA SCHOLARSHIPS,

Tembelea

1. SCHOLARSHIP FORUM http://www.scholarshipnetwork.ning.com/

2. MAKULILO BLOG http://www.makulilo.blogspot.com/

MDAU

MAKULILO, Jr.

San Diego, CA

Tuesday, May 25, 2010

HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA MDOGO WANGU KOERO MKUNDI!!!

Hongera Mdogo wangu Koero mkundi

Terehe hii ya leo 25/5- mwaka jaza wewe mwenyewe ilikuwa ni siku ya furaha na baraka kubwa ndani ya familia ya mzee Japhet Mkundi na Mama Namsifu. Hii yote ni kutokana na kuzaliwa kwako Koero. Napenda kutoa SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA WAZAZI kwa jinsi walivyokulea na kuwa kama ulivyo.
Binafsi najivuna sana kukufahamu, tumekuwa tunawasiliana, tunatakiana hali kila leo, tunashauriana na pia dogo au kwangu ni kubwa zaidi umekuwa MDOGO WANGU WA HIARI.
Mimi na familia yangu tunakupenda, tunakuheshimu,tunakuthamini na pia tunakutakia kila ufanyalo liwe na mafanikio mema.
HONGERA SANA KWA SIKU YAKO YA KUZALIWA MDOGO WANGU KOERO MKUNDI!!!
NIMESHINDWA KUJA NA KUWA NAWE LEO NA KUKUIMBIA KWA HIYO NAWEKA WIMBO HUU AMBAO UMEIMBWA NA STEVIE WONDER. KARIBUNI TUJUMUIKE...







Monday, May 24, 2010

VISA VYA HUYU KIUMBE MWANAUME!

'Kwenye swala la mapenzi wanaume hawana mzaha'

Katika Gazeti la Mwananchi la hivi karibuni la May 18, 2010, kuna habari iliyoandikwa na mwandishi Anthony Kayanda wa Kigoma ambayo ilinisikitisha sana. Habari yenyewe ni ile iliyohusu mtu mmoja kuuwawa kwa kuchomwa kisu kifuani kwa tuhuma za kutembea na mke wa mtu.

Kwa mujibu wa Gazeti hilo, tukio hilo limetokea katika kijiji cha Kitagata kilichopo katika tarafa ya Makere, Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma. Marehemu ametajwa kuwa ni Ally Bwisigwa ambaye ni mkazi wa kijiji hicho.

Ilidaiwa kwamba Marehemu alikuwa akitembea na mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Perusi ambaye aliwahi kuolewa na Hassan Rashid mkazi wa Kasulu Mjini na waliishi pamoja kwa muda mrefu kabla ya mume huyo kufungwa gerezani.

Baada ya mumewe kufungwa, Perusi alirudi kijijini kwao huko Kitagata na ndipo alipoanza mahusiano ya kimapenzi na marehemu.

Inadaiwa kuwa baada ya Mume huyo kutoka Gerezani alimuonya mtuhumiwa mara kadhaa kuacha kutembea na mkewe lakini marehemu aliendelea na mchezo wake huo mchafu.

Inadaiwa kuwa Hassan alifanya majaribio mawili ya kutaka kumuua marehemu kwanza kwa kutaka kumgonga na pikipiki na tukio la pili lilikuwa ni lile la kumchoma kisu ambapo hata hivyo kisu hicho hakikumpata.

Nimesema kuwa tukio hilo limenisikitisha sana kwa sababu bado nashindwa kuelewa hivi inakuwaje mpaka mtu unapoteza maisha kwa sababu ya mwanamke, tena kibaya zaidi mke wa mtu!

Ingawa inasemwa kwamba wanawake ni viumbe wa ajabu lakini naamini wanaume ndio viumbe wa ajabu kupindukia. Kwa nini ninasema hivyo? Ninasema hivyo kwa sababu, wanawake kwa ujumla wao wanavyo vibweka vyao katika swala zima la mapenzi, lakini ukija kwa wanaume naamini nao wanavyo vibwekwa vyao tena vya hatari ukilinganisha na vile vya wanawake.

Kwa mfano, hivi ni mara ngapi tumeshawahi kusikia baadhi ya wanaume wakiamua kujinyonga kwa sababu ya kushindwa kuwashawishi wanawake wanaowapenda?

Namini kuwa matukio ya aina hiyo yapo sana na sio kwa huko nyumbani tu bali pia hata katika nchi zilizoendelea. Linapokuja swala la mapenzi kuna baadhi ya wanaume wanakuwa kama Nyati waliojeruhiwa, na ndio sababu unaweza kukuta baadhi ya wanaume wanajiingiza kwenye vitendo viovu kama vile vya wizi au ujambazi kwa lengo la kuwashawishi wanawake wanaowapenda ili wawakubali. Wakati mwingine hujiingiza kwenye matumizi ya Pombe kupita kiasi au hata matumizi ya Bangi na madawa ya kulevya kutokana na kuachwa na wanawake wanaowapenda.


Tabia hii ya wanaume kuhatarisha maisha au hata kupoteza maisha kama tulivyoona katika tukio hilo la Kigoma ni la tangu enzi za kale. Kuna simulizi nyingi tulikuwa tukisimuliwa enzi za utoto wangu huko nyumbani kwamba kuna wakati wanaume walikuwa wakipigana ili kumgombea mwanamke na shujaa anayeshinda katika ugomvi ndiye anayemchukuwa mwanamke anayegombewa.

Inaonekana wazi kwamba uwezekano wa mwanaume kufa mapema au kuhatarisha maisha yake ni mkubwa ukilinganisha na ule wa wanawake. Na hiyo inatokana na wanaume kupenda sifa na kutaka kuwamiliki wanawake wawapendeo. Kuna matukio mengi ya kusikitisha ambayo huwa tunayasoma katika vyombo vyetu vya habari ambapo matukio kama yale ya mwanaume kumuua mwanaume mwenzie ili kumpata mwanamke ampendae ni vya kawaida kabisa.

Kwa mfano katika tukio hilo la Kigoma, licha na kukoswa koswa kuuwawa mara mbili lakini marehemu hakukoma kutembea na mke wa mwenzie, mpaka akasababisha kupoteza maisha.
Hivi kumekuwa na uhaba wa wanawake kiasi cha kupelekea baadhi ya wanaume kuhatarisha maisha yao au kupoteza maisha kutokana na kumgombea huyu kiumbe mwanamke au kuna kitu kingine kinachotafutwa hapo?

Ni aghalabu sana kusikia mwanamke kamuua mume baada ya kumfumania au kumuua mgoni wake tofauti na wanaume. Kama ukipima jambo hilo kitakwimu basi utapata idadi ya wanaume ya kutosha ukilinganisha na ile ya wanawake.
Kimsingi wanaume wamewageuza wanawake kama mali zao wanazozimiliki na hiyo ndio sababu inapotokea kumfumania mkewe au mchumba wake akiwa na mwanaume mwingine mambo mawili yanaweza kutokea, kwanza atamuadhibu mgoni wake au hata kumuua kisha mke naye atasulubiwa au hata kuuawa.

Lakini, pale anapofumaniwa mwanaume mambo huwa ni tofauti sana. Kuna uwezekano mkubwa wa mke huyo kusulubiwa kwa sababu amemfumania mume na wakati mwingine hata huyo mgoni anaweza kushirikiana na mume huyu kumuadhibu huyo mwanamke aliyefumania.
Nadhani kuna haja ya wanaume kujikagua upya na kubadili mwenendo wao mzima juu ya matendo yao ili kuepuka kupoteza maisha kwa jambo ambalo wangeweza kuliepuka.

Sunday, May 23, 2010

TUMKARIBISHE DADA MAISTARA NA BLOG YAKE TEGELEZENI KARIBU SANAAA!!


Napenda kumkaribisha dada Maistara Wastara na blog yake iitwayo Tegelezeni zaidi ingia hapa http://maisarawastara.blogspot.com/

Wikiend njema na pia Nawatakieni jumapili njema:- kwa sala hii ya nasadiki!!!!!

Haya ndugu zanguni unganeni nami na tusali sala hii
Nasadiki kwa Mungu baba mwenye enzi, muumba Mbingu na dunia. Na kwa Yesu kristu, mwanae wa pekee bwana wetu, aliyeumbwa kwa roho mtakatifu , akazaliwa na bikira Maria, akateswa kwa mamlaka ya Ponsio Pilato, akasurubiwa, akafa, siku ya tatu akafufuka katika wafu,akapaa Mbinguni, amekaa kuume kwa Mungu baba Mwenye enzi. Toka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu. Nasadiki kwa roho Mtakatifu kanisa moja takatifu katoliki la kitume. Maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili na uzima wa milele. Amina.

Jumapili njema kwa watu wote wa dunia hii.


Saturday, May 22, 2010

Swali:- Mmmea huu una sumu au ni uzushi?

Nimeletewa ujumbe huu jana na dada Penina kwa kuwa hili ua ni hatari na nimeona niweke hapa ili kufikisha ujumbe huu na kwa wenzangu.

Upo ujumbe unaozunguka katika barua Pepe ukifahamisha Rangi kuwatahadharisha Watu kuhusiana Rangi mmea ambao wengi wetu tunaufahamu kama Ua ama pambo la nyumbani. Ujumbe umeandikwa Kwa lugha ya Kiingereza lakini mdau Ray Njau ameutafsiri Kwa lugha ya Kiswahili mama ambao unasomeka hivi:

Unaoonekana pichani mmea unapatikana Kwa wingi nchini Cameroon (Hata hapa Tanzania), ofisini, majumbani Rangi kwenye bustani, Ni sumu hasa Kwa Watoto, unaweza kumuua Mtoto ndani ya dakika 15 baada ya kuweka Tu kinywani. Ukigusa huweza kusababisha upofu macho "Wa kudumu.

Swali: Je Habari Hii INA UKWELI WOWOTE AU Ni ya UDANGANYAFU Tu?

Friday, May 21, 2010

Maoni ya Bi Mkora kutoka kwenye mada yenye kichwa cha habari:-KUAMINI KUWA WAMEKAMILIKA Ni Bure KUJIDANGANYA!

Wahaya Nimeyapenda maoni ambayo yamerolewa Rangi Bi Mkora Rangi nimeona Kwa pamoja tujaribu kutafakari. Kama ukitaka kujikumbusha mada nzima bonyeza hapa. Asante sana Bi Mkora.
Hivi ndivyo alivyoanza Bi Mkora: -

Yasinta Wee! mbona umefungua sanduku la Pandora? Maana nyuki watakaotoka humo ndani sipati kusema. Hii mada Mara nyingi huzua mtafaruku mkubwa Kwa sababu Watu wengi wanaamini kuwa wanakoishi Watu wenye ngozi nyeupe Ni peponi Warangi wenyewe Ni Malaika, Ndio maana mtu Mmoja akakujibu kuwa unataka wenzio kuwazibia safari hiyo ya peponi Kwa kuwa wewe umeishafika huko, unataka kufaidi pepo hiyo peke Yako . Mara nyingi Warangi Ni vigumu kufuta AU kubadili kile ambacho wanakiamini Watu Rangi upandaji Kwa siku hizi Ni vigumu kutokana Zaidi Warangi kuwa vyombo vya Warangi kunaswa kimagharibi pamoja Warangi Sinema zao zinazoonyesha kuwa Ulaya Amerika ya Ununuzi Ni Afrika Warangi peponi Ni motoni.

Nimesema Afrika motoni Ni kutokana Warangi potrayal ya picha ya Afrika inayofanywa Warangi wamagharibi, kuonyesha Tabu, mashaka, Shida, maradhi ya Ununuzi matatizo ya Afrika wakati upande mwingine unaona Mambo mazuri Tu hasa kwenye channel zao zinazoonekana ulimwenguni. Mambo Yao yote yenye utata ya Ununuzi matatizo, ulezi, mauaji, ubakaji utakaji Warangi uuwaji Watoto Wa Warangi mengineyo mabaya yanaonekana kwenye channel za mtaa Tu NA SI zao kwingineko, Sasa Ni lini wapi wandengereko Warangi Ununuzi Wa kwetu wamatumbi wataona ukweli kuhusu Amerika ya Ununuzi Ulaya ? Kwa hiyo sie wengine tukisema kuwa SI Kila king'aacho dhahabu, Maisha magumu nako huku tunaonekana wachoyo, wabinafsi waongo NA Kwa sababu tayari tuko peponi. Mbaya Zaidi Kwa mtu kama wewe uliolewa Warangi mzungu, Kwa sisi waafrika wenzetu tulioolewa Warangi tunaonekana kuwa tunasema hivyo Kwa sababu tumekosa Tu kama Sungura "sizitaki mbichi hizi".

Kwa hiyo Kila tutakalosema litaingia sikio Moja ya Ununuzi kutokea sikio la pili. Hata rangi Hao wadogo zetu Warangi Dada zetu wakipata matatizo hawako tayari kusema AU kutafuta Msaada, wako tayari kufa Warangi Tai zao shingoni. Kisa wameolewa NA NA wazungu wanaona aibu kusema yanayowasibu. Huko Afrika Kusini katika Moja ya lugha zao anaitwa Mzungu MULUNGU Warangi sie tumewaguza milungu Kweli Kweli Kila wakifanyacho Warangi wakisemacho kwetu sisi Ni kizuri Hata kama hakina manufaa kwetu.

Pamoja Warangi sababu za umasikini lakini kuna wengine masikini NA SI nyumbani wana Tu Maisha mazuri lakini kuolewa kwao Warangi Mulungu Ni sifa Warangi sababu mojawapo ya kuwakoga marafiki mashoga Warangi. Hivi Ununuzi nafikiri wengine wanamshangaa Warangi kumlaani Yasinta Kila sikU kuweka mapicha ya Ruhuwiko, Kila siku kukumbuka kwao, kuongea kiswahili, hafai VICHUPI kama wazungu, Kwa wao kwao Ni kujidhalilisha lakini wanasahau kuwa "mdharau kwao mtumwa Ni". Kuna Watu wengi tena Tu Watoto Wala wao hawajui kiswahili Hata kidogo cha cha Yale Hata maamkuzi yanawashinda. Hawajui MiLa Warangi desturi zetu za makabila wacha Hata zile za majumui Tu kama kusalimia wakubwa, kuheshimu wakubwa Warangi mengineyo Warangi Wala Wala Hao hawajao kuolewa Warangi wazungu lakini wanaishi Kwa wazungu. Kuna mtu aliwahi tena kunitamkia Bado wakati huo nikiwa naishi Dar, ETI "mimi ningelikuwa msomi kama wewe tena kwenu Warangi ninaishi huku Watoto wangu ningewapiga marufuku kuongea kiswahili". Unafikiri mtu kama huyo akifika ulaya azae tena mzungu amka Warangi Hata Watoto watajua Asili ya mama Kwa Yao?

HAPO NDIPO UKOLONI MAMBOLEO ULIPOTUFIKISHA

Bi Mkora

Thursday, May 20, 2010

Ujumbe/kichekesho au sijui kucheza na lugha

Mmasai kaingia hotelini akaagiza chai na mkate. Alipomaliza kunywa akataka ankara (bill) yake. Alipopewa akakuta imeandikwa, Chai shilingi 300 na mkate shiling 200 jumla ikawa shilingi 500. Mmasai akalipa shiling 200, alipoambiwa hela haitoshi, akajibu...ero mimi nalipa mukate na mukate italipa shai. Kwa sababu mimi nakula mukate na mukate nakunywa shai. Akiwa na maana kwamba alikuwa akichovyo mkate kwenye chai na kula kwa hiyo hakunywa chai bali mkate ndio uliokunywa chai......Hii nimetumiwa na rafiki nimecheka sana nikaona tucheke pamoja

Tuesday, May 18, 2010

KUAMINI KUWA WAMEKAMILIKA NI KUJIDANGANYA BURE!


Tunayo mengi ya kujivunia!!

Jana tarehe 17/5 nimekumbuka sana nyumbani, nadhani ni kwa sababu jana ilikuwa ni tarehe na mwezi ambao mama yangu alifariki. Kwa kweli nam-miss sana mama yangu.

Nakumbuka ilikuwa kila nikienda likizo, nilikuwa natumia muda mwingi kuwa jikoni na mama yangu nikizungumza naye simulizi za kale za enzi ya utoto wangu.
Ni simulizi ambazo kwa kweli kila nizikumbukapo huwa natamani yale maisha yajirudie kwani kuna mengi ya kufurahisha na ya kuhuzunisha ambayo kwangu mimi nimejifunza mengi kwako.

Lakini lipo jambo moja ambalo nimelikumbuka, ambalo kwa kweli huwa linanifikirisha sana. Jambo lenyewe ni kuhusiana na baadhi ya marafiki zangu kule nyumbani.
Kusema kweli ule ukaribu niliokuwa nao na baadhi ya marafiki zangu umepungua kiasi cha kukatisha tamaa.

Sababu kubwa ni kutokana na kile walichodai kuwa nimewatupa kutokana na kutowasaidia kupata wachumba wa Kizungu. Yupo rafiki yangu mmoja mbaye yeye aliwahi kunitamkia wazi kuwa mimi ni mbinafsi kwa kuwa ni mara nyingi ameniomba nimtafutie mchumba wa Kizungu kwa kuwa ninaishi huku ughaibuni lakini nimeshindwa kumtafutia.

Nakumbuka nilimweleza ukweli kuwa siwezi kumsaidia juu ya jambo hilo kwa sababu liko nje ya uwezo wangu, lakini kutokana na labda tuite ufinyu wa kufikiri, nilimpoteza rafiki huyu kwa sababu ya kushindwa kumtafutia mchumba wa kizungu……..yaani kaaaazi kweli kweli.

Hata hivyo nilijiuliza swali moja, kuwa hivi hakuna wanaume huko nyumbani mpaka mtu aamue kutafuta mchumba wa Kizungu? Je ni mapenzi au ni Uzungu unaotafutwa hapo?

Lakini kwa upande mwingine sikumshangaa sana kwa sababu kwa huko nyumbani ipo silka ya baadhi ya watu ambao wanaamini kwamba kuoa au kuolewa na Mzungu ni jambo la kujivunia sana. Huwa nimezoea kauli za baadhi ya watu kule nymbani kila niendapo likizo wakisema, ‘siyo mwenzako yule, kaolewa na Mzungu’ .

Yaani mpaka leo hii bado kuna baadhi ya watu wanaamini kuwa kuoa au kuolewa na mzungu ni jambo la kifahari na la kujivunia. Kinachotafutwa sio mapenzi tena ni huo uzungu..
Kuna baadhi ya watu wamefikia hatua ya kuamini kuwa sisi waafrika ni duni na wenzetu weupe ni bora na waliokamilika.
Lakini nadhani makosa hayo hayakuanza leo, yameanzia mbali sana. Kwani kizazi na kizazi tumekuwa tukiaminishwa kuwa wazungu ni bora zaidi yetu sisi.

Kwa mfano, mtu kufanya mambo yake kwa umakini na anayefuata muda huyo ataitwa ni mzungu, au mtu asiyependa majungu, uzinzi, uasherati na umbeya naye ataitwa kuwa ni mzungu. Nakumbuka wakati nikisoma kule nyumbani, ilikuwa kama kuna mwalimu ambaye ni mwadilifu kwa wanafunzi na anayewajali, utawasikia wanafunzi wakisema, ‘yule mwalimu ni mzungu’

Yaani kipimo cha kufanya mambo kwa uadilifu na kuwajali wengine kimekuwa kikihusishwa na uzungu, mpaka imefikia mahali kila mtu anatamani kuolewa au kuoa mzungu wakiamini kuwa hao wamekamilika.

Hata huko makazini napo watu wanaochapa kazi kwa uadilifu wanafananishwa na wazungu. Wakati mwingine huwa nacheka kwa sababu naamini hao wanaoamini kwamba mtu kuwa mzungu anakuwa amekamilika ni wazi kwamba hawawafahamu watu hao.

Kwamba kuwa mzungu ni kutokuwa na tabia mbaya, kama uvivu, udokozi, kutojali muda, kusengenya, umbeya, wivu, au kijicho, uzinzi, uasherati, ushoga na tabia zote mbaya tunazozijua hapa duniani, nikujidanganya bure.
Nasema kuamini hivyo ni kujidanganya, kwa sababu kwa wale wanaoishi huku ughaibuni au wale wanaofanya kazi na hawa wenzetu huko nyumbani, watakuwa ni mashahidi wangu.

Kama mlikuwa hamjui ni kwamba hawa wenzetu nakubali kuwa wapo waadilifu na wenye tabia nzuri, lakini pia wapo wenye tabia za ajabu kama uvivu, udokozi, kutojali muda, kusengenya, umbeya, wivu, au kijicho, kutojiamini, uzinzi, uasherati, ushoga na tabia zote mbaya tunazozijua hapa duniani.
Ule udhaifu tulio nao pia wenzetu hawa wanao tena wenzetu hawa wamepitiliza. Ila kutokana na kudanganywa na TV na hizo kauli za wazee wetu tumejikuta tukiamini kitu ambacho hakipo.

Mie wakati mwingine huwa nashangaa pale ninapokutana na baaadhi ya Watanzania wenzangu ambao wanaishi au wamewahi kuishi huku ughaibuni wanapozungumza kwa kubana pua kama hawa wenzetu. Wanashindwa kujua kwamba ile ni lafudhi ambayo inatokana na lugha yao. Ni kama pale unapokutana na Mmakonde, Mngoni au Msukuma au Mpare anapoongea Kiswahili kwa lafudhi ya lugha yao.

Mbona wenzetu kwa mfano Wanaijeria au Wakenya wanaongea kwa lafudhi ya lugha zao. Ni rahisi sana kumtambua Mkenya au Mnaijeria kutokana na lafudhi yake pale anapoongea Kiingereza, tofauti na sisi ambapo Tunajitahidi kubana pua mpaka tunajisahau hata pale tunapoongea Kiswahili.
Na ndio maana kuna baadhi ya wanawake huko nyumbani na hata huku ughaibuni wamefikia hatua sasa wanaukataa uafrika na kuanza kujichubua kwa mikorogo ili kuutafuta weupe.

Kuna wakati nilipokuwa huko nyumbani nilishangaa kuwaona baadhi ya wasichana ambao nawajua kabisa rangi zao kuwa ni weusi kama mimi lakini wamekuwa weupe mpaka wanatisha! Taabu yote hiyo ni ya nini?
Tumefikia hatua sasa kila jambo linalofanywa na hawa wezetu tunaiga, na ndio sababu siku hizi tabia kama za ushoga, usagaji na tabia nyingine chafu tunazozishuhudia huku zimetamalaki huko nyumbani.

Sisi kama Watanzania tunazo tabia nzuri ambazo hawa wenzetu wanazitamani sana tofauti na tunavyodhani. Kwa mfano, sisi ni kawaida mtu kuamka na kupita nyumba mbili tatu na kuwajulia majirani zake hali, au kuingia nyumba yoyote na kama akikuta chakula akala bila wasiwasi.

Kwa upande wa Misiba au harusi watu wamekuwa wakichangiana na kusaidiana kwa hali na mali, yaani tumekuwa na ushirikiano wa hali ya juu tofauti na wenzetu hawa.
Kuwa mzungu haimaanishai kuwa mwadilifu wala kuwa na tabia nzuri, bali tabia nzuri inatokana na tabia ya mtu na malezi kwa ujumla wake, hakuna mahusiano yaliyopo kati ya uadilifu, tabia nzuri na uzungu. Nasisitiza kuwa hakuna kitu kama hicho, ni kujidanganya bure.

Inashangaza kuona kwamba, badala ya kujivunia tabia hizi nzuri tulizo nazo ambazo hata hivyo wenzetu wanazitamani, tunatamani za kwao ambazo nyingi ni mbaya na zenye kuumiza.

Tubadilike………………

Swali la leo:- Hivi kwanini kanga mnyama anaitwa kanga na Kanga vazi ni kanga zina uhusiano gani?

Kanga kama mnyama
Kanga kama vazi hasa kwa wanawake!!
Nimekuwa nikijiuliza miaka yote hii leo nimeona niwailize ndugu zangu kwani umoja ni nguvu utengano ni udhifu. Na anayeuliza sana basi anajua mengi...a.k.a KAPULYA MDADISI.

Monday, May 17, 2010

Tatizo la mimba kwa wanafunzi bado ni kubwa

TATIZO la mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari bado ni kubwa kwa wilaya ya Songea hali ambayo imewafanya wadau wa elimu pamoja na viongozi wa ngazi za juu serikalini akiwemo mkuu wa wilaya ya Songea Thomas Sabaya kuwachukulia hatua kali za kisheria wazazi na wanafunzi waliopatiwa ujauzito kwa kulazimishwa kuwataja watu walio wapatia ujauzito ili waweze kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Hali hiyo imechangiwa na tabia ya baadhi ya wazazi kupatana na watu ambao wamewapatia mimba watoto wao kwa kupatiwa fedha na kumalizana nao kinyume na sheria hali ambayo imechangia tatizo la wanafunzi wengi kupewa ujauzito.

Hivi karibuni Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein alipofanya ziara mkoani Ruvuma alionyeshwa kuchukizwa na vitendo vya baadhi ya watu ambao wanapita na kuwarubuni wanafunzi na kuwapatia mimba na hivyo kuwafanya washindwe kuendelea na masomo kutokana na ujauzito.

Akiwa wilayani Songea Dk Shein alifanikiwa kuzungumza na wananchi wa kata ya Matogoro Manispaa ya Songea na kuwaeleza jinsi anavyochukizwa na baadhi ya watu ambao wanapita na kuwarubuni wanafunzi na kuwapatia mimba na kuwaonya waache tabia hiyo mara moja kwani serikali haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Dk Shein anasema bado tatizo la mimba ni kubwa katika baadhi ya mikoa na kuwataka viongozi kuwachukulia hatua za kisheria watu ambao wanawakatisha masomo wanafunzi kwa kuwadanganya na kuwapatia ujauzito, hivyo kuwafanya washindwe kuendelea na masomo yao.

"Bado kuna baadhi ya watu wanaendelea kuwarubuni wanafunzi na kuwapatia ujauzito hivyo naomba muendelee kuwashugulikia watu hao na muwafikishe katika vyombo vya sheria ili waweze kuchukuliwa hatua zaidi," anasema Dk Shein.

Pamoja na hayo Makamu wa Rais amevutiwa na jitihada mbali mbali zinazofanywa mkoani Ruvuma hususan wilaya ya Songea ili kuinua kiwango cha elimu katika mkoa wa Ruvuma kwani, wilaya hiyo imefanya vizuri kwa kufanikiwa kutekeleza mpango wa Serikali kwa kata zote kuwa na shule za sekondari ambazo zitachukua wanafunzi na kuna baadhi ya kata zimekuwa na shule zaidi ya mbili.

"Napenda kuwapongeza wabunge Dk Emmanuel Nchimbi na mwenziwe Jenista Mhagama kwa jitihada kubwa walizofanya katika kushughulikia kuinua elimu katika wilaya hii , wamefanya kazi kubwa na wanastahili pongezi ambapo Dk Nchimbi pekee amechangia Bati 5,096,kofia za bati 2,050,fedha taslimu milioni 13 na misumari kilo 87 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 103," anasema Dk Shein.

Dk Shein amewataka wanafunzi kuwaheshimu wazazi wao na kujali masomo kwa kusoma kwa bidii na kufata yale mema ambayo wanaelekezwa na wazazi wao ili waweze kufikia ndoto zao za baadaye badala ya kukubali kurubuniwa na wanaume ambao wanania mbaya ya kuwakatisha masomo.

Aidha ameahidi kuwa serikali itaendelea kuzisaidia shule hizo kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili ikiwemo ya upungufu wa nyumba za walimu, madawati, maabara, pamoja na walimu.



Akitoa taarifa ya Wilaya ya Songea kwa Makamu wa Rais, Mkuu wa Wilaya ya Songea Thomas Sabaya alisema katika kipindi cha mwaka 2008 wanafunzi 128 wa shule za sekondari walipata mimba na mwaka 2009 wanafunzi 73 walipata ujauzito na kukatisha masomo yao. ambapo katika kipindi hicho hicho wanafunzi 45 wa shule ya msingi nao walipata ujauzito ingawa tatizo hilo limepungua ambapo mwaka 2009 wanafunzi waliopata mimba ni 16 wilaya nzima.

Amesema, tayari mikakati mbali mbali ya kuthibiti mimba kwa wanafunzi imefanywa ambapo wilaya imewapeleka wanafunzi na wazazi mahakamani ili wawataje watuhumiwa hatua ambayo imesaidia baada ya watuhumiwa 25 kuadhibiwa.

Aidha, wilaya imeanzisha utaratibu wa upimaji mimba kwa wanafunzi kila baada ya miezi mitatu hali ambayo imesaidia kupunguza mimba mashuleni.

Na Joyce Joliga wa Gazeti la Mwananchi

Sunday, May 16, 2010

WHATEVER YOU GIVE WOMAN!!!


UJUMBE HUU NIMEUPATA KWA DADA SUBI ZAIDI SOMA HAPA NIMEUPENDA NA NIKAONA SI VIBAYA NAMI NIKIWEKA HAPA. ASANTE DA SUBI.

Saturday, May 15, 2010

JUMAPILI NJEMA KWA WOTE NA UJUMBE NI HUU WA DADA EMMY:-KIBENDI JERUSALEM,TUJYE IYERUSALEMU BY EMMY KOSGEI

NAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA WOOOOTEEE!!!

HONGERA KWA SIKU YAKO YA KUZALIWA MZEE WA LUNDU NYASA

Ni furaha kuwa na rafiki kama wewe na leo ni siku tukufu kwako. Ni siku ambayo ulitokea hapa duniani . Napenda kukutakia yote mema, uishi miaka mingi uwe babu kizee na wajukuu wengi uwe nao. HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA MARKUS MPANGALA!!!!!

Friday, May 14, 2010

Ujumbe wa Ijumaa ya leo!!

Hata kama ukiamua kutoka kwenye
ndoa ngumu huna haja ya kujilaumu.

Maishani ukiwa mtu mwenye kukubali kwamba chanzo cha tatizo ni wewe hutapata shida na tena utazidi kujiimarisha kwani hakuna apendaye kulaumiwa duniani na kumbuka kwamba jamii yetu imefunzwa kwamba kukosea ni ujinga. Kumbe pia inapaswa kufunzwa kwamba kukosea -ni elimu kama unayatumia makosa vizuri. Na zaidi ya yote tukumbuke ya kwamba lawama si mzigo. Kama unapenda usawa, upendo na haki usiogope lawama haitakuumiza popote. ...........Huu ndio ujumbe wangu wa IJUMAA YA leo......IJUMAA NJEMA KWA WOTEEEEEEEEEEEE

Thursday, May 13, 2010

Picha ya wiki hii!! Je Unajua mwanamtindo huyu ni nani?

Nimeipenda hii picha na nimeona iwe picha ya wiki hii. Rangi za mavazi ni rangi ambazo nazipendaaaaaaaa sana. Hakika ukijipenda mwenyewe basi na wengine watakupenda!!

Na sasa ngoja tusikiliza kibao hiki ambacho kinawakilisha ujumbe murwaaaaaaaaaaaaaaaaa.

Wednesday, May 12, 2010

UKIKUTA MANYOYA, UJUE KESHALIWA!!!

Utotoni kuna michezo mingi ya kukumbukwa
Wakati wa utoto wetu yapo mambo mengi ambayo tumeyapitia, ambayo huwa wakati mwingine ukiyakumbuka unatamani sana kurejea utotoni.

Hivi karibuni mdogo wangu Koero aliweka mada yake aliyoipa kichwa cha habari kisemacho, ‘anaposema mwendawazima’.
Katika makala yake hiyo kuna kipengele alizungumzia kuhusu kuteka maji kisimani na jinsi yeye na bibi yake walivyowakuta mabinti wa pale kijijini kwa bibi yake walivyokuwa wakicheza na wavulana pale kisimani badala ya kuchota maji na kupeleka nyumbani.

Pamoja na kukemewa na Bibi Koero, lakini walimdharau ma kuendelea kucheza michezo yao na wavulana wale, bila kujali onyo la Bibi Koero, isipokuwa binti mmoja ambaye alimsikiliza bibi Koero na kuondoka kurejea nyumbani akiwaacha wenzie wakiendelea kucheza pale kisimani. Kama ungependa kujikumbusha makala hiyo unaweza kubofya hapa.

Kipengele hicho kilinikumbusha wakati wa utoto wangu kule kijijini Litumbandyosi/Kingoli wakati ule nikiwa darasa la nne.
Wakati huo tulikuwa tukienda kisimani kuteka maji na huko tulikuwa tukicheza michezo mingi ya kitoto.

Nakumbuka nilipokuwa likizo nyumbani mwaka jana, nilipokuwa naelekea sokoni, njiani nilikutana na kijana mmoja ambaye ningependa kumwita Mpetamanga (Sio Jina lake) kwa kweli nilikuwa nimemsahau, sijui ndio uzee unaninyemelea, maana nilishangaa alinikumbuka vizuri sana tofauti na mimi ambaye nilikuwa nimemsahau.

Mpetamanga nilisoma naye darasa moja na nakumbuka baadae familia yao ilihama pale kijijini na kuhamia kijiji cha jirani na huo ukawa ndio mwisho wa kuonana na kijana huyu.
Kukutana kwetu pale njiani kulitukumbusha mambo mengi sana ya utotoni ikiwemo ile michezo tuliyokuwa tukicheza kule kisimani tulikokuwa tukichota maji.
Mpetamanga alitumia muda huo kunikumbusha mambo mengi ya utotoni ikiwemo hiyo michezo tuliyokuwa tukicheza kule kisimani.

Kwa kuwa nilikuwa na haraka nilimuaga, lakini nilimkaribisha nyumbani, kisha tukaagana na nikaondoka kuelekea sokoni kununua mahitaji yangu.
Siku iliyofuata nikiwa nyumbani na mwanangu Erik, kwani Camilla alikuwa ametoka na baba yake kwenda mjini kununua mahitaji mengine ya pale nyumbani, nilisikia mtu akibisha hodi, nilipokwenda kufungua mlango alikuwa ni Mpetamanga.

Nilimkaribisha ndani kwa bashasha na kisha tukakaa sebuleni kwa mazungumzo.
Nilimwita mwanangu Erik na kumtambulisha kwa mgeni.
Mpetamanga alishtuka sana, na kuniuliza kwa hamaki, ‘Yasinta umeolewa?’
Nilimjibu kuwa nimeolewa na nina watoto wawili. Nilimjulisha kuwa ninaishi nchini Sweden na familia yangu, na pale nyumbani niko likizo tu.

Alishtuka sana na nilimuona dhahiri akiwa amenyong’onyea kabisa. Alinijulisha kuwa alipomaliza shule alikwenda nchini Malawi kundelea na masomo na amekuwa akiishi huko tangu alipoondoka nchini.
Na yeye kama ilivyo mimi aliamua kurudi nchini kuwasalimia ndugu zake na safari hiyo ilimlazimu kufika Ruhuwiko kumuona mjomba wake, lakini pia akiwa na hamu ya kuniona kwani aliambiwa kuwa familia yetu ilihamia Ruhuwiko siku nyingi.

Na pale tulipokutana ndio alikuwa amefika Ruhuwiko.
Aliniambia kuwa, nilipomkaribisha nyumbani alifurahi sana na alijua huo ndio wakati muafaka wa kuzungumza nami kwani ni muda mrefu alikuwa akiniwaza, na lengo lake ilikuwa kama akinikuta sijaolewa basi azungumze nami ili alete posa.

Nilicheka sana na kumwambia kuwa amechelewa kwani mie niliolewa na kuondoka nchini na kuhamia Sweden.
Nilimchekesha pale nilipomwambia, ‘Ukikuta manyoya basi ujue ndio keshaliwa’
Alicheka sana na kuniuliza kama nina maana gani, na ndipo nilipomfafanulia kuwa mpaka amekuta watoto basi ajue kuwa ndio nishaolewa hivyo……..

Lakini kitu kingine kilichomshangaza zaidi ni kuona jinsi ninavyozungumza kingoni na Kiswahili kwa ufasaha pamoja na kuishi nje ya nchi kwa muda mrefu, kwani hata nilipomweleza kuwa nimeolewa na ninaishi nchini Sweden alidhani namtania, hadi nilipomuonesha picha za familia yangu.


Hata hivyo Mpetamanga alikubali matokeo, na kuridhika na maelezo yangu.
Kusema kweli kila niwapo likizo nyumbani nakutana na visa na vituko vingi vya aina hii na haviishii hapo, hata mtandaoni nako kuna visa vyake, hili sitalizungumza kwa undani maana mdogo wangu Koero amelizungumza hili kwa kirefu katika makala yake aliyoipa kichwa cha habari kisemacho, ‘Dalili hizi sio za kweli’ unaweza kubofya hapa kumsoma.

Kuna wanaume wakware ambao hawakubali kushindwa. Hata wakute manyoya lakini bado watapekuwa weeeee! wakiamini kukuta minofu. Jamani mmeshachelewa ndio keshaliwa huyoo…….LOL

Tuesday, May 11, 2010

Wanafunzi Songea waomba elimu zaidi ya Ukimwi madarasani

Wanafunzi mkoani Ruvuma wakiimba wimbo wa pamoja kwa vitendo

TATIZO la wazazi pamoja na walezi kutokuwa wawazi kwa watoto wao hasa wakati wanapotakiwa kuwaeleza kuhusu maswala ya afya ya uzazi na ujinsia ni moja ya tatizo kubwa chanzo linalonachangia kuongezeka kwa wanafunzi wanao ambukizwa virusi vya ukimwi katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.

Kutokana na hali hiyo baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Tuliani iliyopo kijiji cha Lilondo kata ya Wino wameona ni bora wawaombe walimu wao kuwasaidia kutoa elimu ya ugonjwa huo kwa undani zaidi madarasani ikiwa ni pamoja na kuongeza vipindi hivyo ambavyo vitasaidia kuzungumza kwa kina ili wanafunzi hao waweze kutambua na kujilinda wasiambukizwe na maradhi hayo ingawa wapo ambao tayari wameshapata maambukizi hayo.

Wanafunzi hao walisema , ingawa wanafundishwa somo la ukimwi lakini bado kuna vitu vingi hawajui kama njia mbali mbali zinazochangia kuambukizwa virusi vya ukimwi na namna ya kuishi na ugonjwa huo kwa watu ambao wameshambukizwa.

Mwanafunzi Joseph Mwenda (12) wa Darasa la nne shule hiyoamesema, bado wanafunzi wanahitaji elimu zaidi ya ukimwi kwani wamekuwa wakifundishwa juu juu bila kuelezwa namna ugonjwa huo unavyoambukizwa hivyo kuwaacha njia panda.

“Najua ukimwi ni ugonjwa hatari mwalimu mgina ametufundisha ila hajatueleza unavyoambukizwa unavyoenezwa hatujafundishwa darasani ila nimeona mtu anaumwa mama akaniambia anaumwa ukimwi alikuwa anakohoa sana na hawezi kutembea kabisa,”alisema Mwenda.

Kwa upande wake Notigeo Mlowe Mwanafunzi wa darasa la tano anasema si vibaya iwapo walimu watawasaidia kuwaelewesha wanafunzi kwa undani zaidi lakini wafanye hivyo kwa wanafunzi wenye umri mkubwa kidogo kwani wakiwaelekeza wote wengine ni wadogo hawajui chochote.

Anasema,kuna mwanafunzi mwenzao anaishi na virusi vya ukimwi lakini wamekuwa wakimsaidia kumfundisha maswali na kumfundisha michezo mbali mbali ili asijisikie vibaya ingawa kuna wanafunzi wengine wanamwogopa kutokana na kutopata elimu ya kuishi na wagonjwa wa ukimwi.

"Tuna mwenzetu anaumwa ugonjwa wa ukimwi mtoto huyo anateseka kwani mama yake hamtunzi bali anaishi na kaka zake tu uwa anaumwa hadi tunamwonea huruma hata afya yake siyo nzuri na ana furaha kabisa,"anasema

Mwanafunzi huyo kuwa , iwapo wazazi wataendeleea kuwa waoga basi kuna uwezekano watoto wao wakaambukizwa ugonjwa wa ukimwi bila wao kujua kwani watoto wengi wanapenda kuishi maisha mazuri na wanadanganywa kwa kununuliwa vitu vidogo vidogo.

Anasema,Kuna wanafunzi wengi wanadanganywa na kufanya ngono na watu wakubwa ila wazazi wao hawajui sasa wakielezwa watajua na kuogopa kufanya hivyo ,kwani watajua ni hatari katika maisha yao.

Aidha Notigeo anawaomba watu wenye mapenzi mema kuendelea kuwatunza watoto na kuacha kuwaambukiza magonjwa ya zinaa, kuwapatia mimba na kuwaaambukiza virusi vya ukimwi kwanihata wanaofanya hivyo nao wanawatoto ipo siku Mungu hatawaadhibu kwa matendo yao.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Songea Rajab Mtiula amewataka wanafunzi hao kufanya bidii zaidi katika masomo yao na kuacha kujiingiza katika matendo ya ngono kwani yatawaharibia maisha yao.

Aidha ameshauri kuwa walimu waendelee kutoa elimu hiyo madarasani ili wanafunzi wapate elimu hiyo kwa undani zaidi na kuweza kujilinda wasipate maambukizi ya ukimwi.kwani hali ya maambukizi katika wilaya hiyo ni ya kutisha na imekuwa ikiongezeka siku hadi siku.

ni vema wananchi wakawa wawazi na kutoa taarifa sahihi iwapo ndugu au jamaa zao watabainika kuwa wameambukizwa ugonjwa wa ukimwi watoe taarifa za kifo chake ili kupunguza kuendelea kuenea kwa maambukizi.

“Nawaomba ndugu zangu tujenge tabia ya kuwa wawazi , ni vizuri sasa tuwe tunaambiana ukweli iwapo kuna watu watapoteza ndugu zao kwa ugonjwa wa ukimwi basi wawa wawazi ili kusaidia watu wengine wasiambukizwe zaidi pia kusaidia kupatikana takwimu sahihi za watu waliokufa kwa ugonjwa huo hapa kwetu,”alisema Mtiula

Mtiula ,anasema hadi sasa idadi ya wagonjwa 5281 wanaoishi katika halmashauri hiyo wamesajiliwa na kuanza kutunia dawa za kupunguza makali ya ya virusi vya ukimwi.

Amesema,takwimu zilizopatikana katika vituo vya afya zinaonyesha kuwa wagonjwa hao wamesajiliwa katika kipindi cha januari hadi octoba 2009 ambapo kati yao wanawake ni na wanaume ni 2357 ambapo 158 walifariki katika kipindi cha mwaka 2008-2009 ambapo wengi wa wagonjwa hao ufia nyumbani hivyo takwimu zao kutopatikana .

Joyce Joliga,Songea wa Gazeti la Mwananchi

Monday, May 10, 2010

MFALME MROPE: HAYA NI MAJIBU KUHUSU UONGO WAKO.

Inadawa kuwa wanafunzi wa vyuo ndio wadanganyaji wazuri.


Hivi karibuni dada yangu Yasinta aliweka makala hapa ambayo aliitoa katika Gazeti la Jitambua, makala hiyo ilikuwa na kichwa cha habari kisemacho ‘Kuna wale wanaojikuta wanadanganya bila hiyari’ ukitaka kujikumbusha juu ya makala hiyo unaweza kubofya hapa.
Katika makala hayo kulitolewa maoni tofauti tofauti na wasomaji wa kibaraza hiki, lakini Mfalme Mrope ndiye aliyenisukuma kujibu swali lake ambalo aliliita la kizushi kuwa, ni upi ni uongo mzuri na upi ni uongo mbaya?

Ukweli ni kwamba, kila mmoja wetu husema uongo. kuna majaribio mengi ambayo yamefanywa, ya watu kujitahidi kutosema uongo, lakini wote walishindwa jambo hilo.

Uongo huvunja uhusiano na kuondoa kuaminiana miongoni mwa watu. lakini, kuna ukweli kwamba, uongo utaendelea kusemwa. Hata hivyo, wataalamu wanakiri kwamba, kuna uongo ambao ni muhimu katika kumfanya mtu kutimiza mambo yake muhimu ya kijamii, kukabiliana na hali zisizopendeza na kujilinda na udhaifu wa kinafsi.

Pengine ukijua ni kwa kiwango gani watu wanasema uongo unaweza kuwa kwenye nafasi ya kulielewa vema zaidi jambo hili. Mtaalamu mmoja wa saikolojia aliwahi kufanya utafiti kuhusu kiwango cha uongo kwa watu. Huyu bwana alibaini kwamba wanfunzi na hasa wanavyuo, husema uongo kwa wastani wa mara mbili kwa siku.

Ukikutana na mwanafunzi wa chuo ujue kama hatakudanganya wewe, basi kuna watu wawili au mazingira ya aina mbili tofauti ambapo amedanganya au atadanganya kwa siku hiyo.

Kwa ujumla kama mtu akikagua tafiti nyingi zilizowahi kufanywa kuhusu kusema uongo, atabaini kwamba, katika kila mambo matano anayosema mtu mzima, moja linakuwa ni la uongo.

Wanafunzi nao husema uongo zaidi, kwani inaonesha katika kila matukio au mambo matatu, husema uongo mara moja.

Watafiti wamebaini kwamba, uongo husemwa zaidi kwenye simu kuliko watu wanapokuwa uso kwa uso.

Kwa hiyo, watu wanapowasiliana kwa simu uwezekano wa kusema uongo ni mkubwa sana kuliko wakiwa wanazungumza uso kwa uso. maana yake ni kwamba mazungumzo ya kwenye simu hayaaminiki sana.

Imebainika pia kwamba uongo unaposemwa, ni lazima uongo mmoja kati ya kila saba ufahamike. Hii ina maana kwamba, uongo mwingi hupita bila kufahamika, lakini ina maana kwamba, mtu akisema uongo ni lazima kuna mahali atanaswa tu.

Katika kila mara kumi za uongo unaosemwa, uongo mmoja unakuwa ni wa kuongeza chumvi.

Yaani jambo ni la kweli, lakini kunakuwa na kuongezea chumvi kwingi sana. Kati ya kila uongo kumi unaosemwa, uongo sita ni uongo kabisa, usio na chembe ya ukweli. Kumbuka, kuna uongo mwingine hauna hata chembe ya kaukweli fulani ndani.

Uongo uliobaki yaani asilimia 30 ya uongo wote unaosemwa, una viraka vya ukweli na viraka vya uongo wao.

Hii ina maana kwamba akidanganya kuhusu jambo fulani sasa hivi, atarudia kudanganya kuhusu jambo hili kwa mara nyingine.

Ndio pale mtu anaposhtukiwa kwa sababu maelezo yake kwa jambo hilohilo hugongana.

Watu wanaosema sana uongo wanaelezewa kuwa ni watu wanaohisi kupungukiwa, yaani ndani mwao kihisia kuna kutokukamilika au wanahisi kuwepo pengo ndani mwao.

Kwa kutumia uongo hujipandisha au kuhisi nafuu. Watu wanaojiamini hawawezi kuwa na uongo, labda ule uongo, ambao inaelezwa kwamba ni wa lazima kwa sababu ya mazingira.

Huu ni uongo wa aina gani?

Niliwahi kusoma habari fulani ya kidini. Mtu mmoja aliyekuwa akitafutwa na maharamia alikimbilia kwenye nyumba ya watawa.

Huko alionesha uadilifu wake mkubwa hadi watawa wale wakampenda sana.

Siku kadhaa baadae, wale waliokuwa wakimtafuta waliivamia nyumba hiyo na kufanya fujo wakisema wamtafutaye yumo ndani.

Ilibidi watu hao wapelekwa kwa mkuu wa nyumba ile ya watawa.

Ni kwamba, kwa mujibu wa mazoea na ufahamu wa eneo lile, watu walikuwa wanaamini kwamba, mtawa hawezi kusema uongo, na kubwa kabisa, kiongozi wao ndiye ambaye hata iweje hawezi kudanganya.

Wale watu wakorofi walipofika kwa mkuu wa watawa wale walimuuliza, kama mtu wanaye mtafuta yumo mle hekeluni.

Mkuu wa watawa alifikiri na kusema, 'hakuna mgeni humu ndani,vinginevyo tusingemficha' Kwa kuamini kwamba, mkuu wa watawa hawezi kudanganya, wale maharamia waliondoka wakiamini kuwa wamtafutaye hayumo mle.

Baada ya maharamia kuondoka , mkuu wa watawa alimwambia yule mgeni, 'kwa mara ya kwanza nimesema uongo kwa sababu yako. Lakini unastahili kuokolewa kwa mtu kusema uongo, ni uongo wa haki na wa lazima.'

Huo ndio uongo ninaouzungumzia. Na hapo ndipo unapogundua kwamba hakuna mtu asiyesema uongo.

Uongo mwingine ni ule unaotumiwa na madaktari, maarufu kama Placebo. Uongo huu unatumiwa na madaktari pale inapotokea kuwa dawa inayoweza kutibu tatizo hilo haipo au mgonjwa ameonekana kutokuwa na tatizo lolote hata baada ya vipimo vya kitaalamu, pamoja na kwamba ameonekana kuwa na matatizo ya kiafya.

Kinachofanyika ni kumpa mgonjwa dawa ambayo haina madhara na mara nyingi ni vidonge maalum ambavyo vinakuwa havina kemikali yoyote, pamoja na ushauri nasaha imeonekana kuleta mafanikio makubwa.

Huu nao ni uongo mzuri, kwani umeonekana kuponya watu wengi sana na kutokana na tafiti mbalimbali imethibitika kuwa uongo huu uitwao Placebo ni moja ya tiba zilizoonyesha mafanikio makubwa

Makala haya nimetumiwa na kaka Shabani Kaluse wa kibaraza cha Utambuzi na Kujitambua yakiwa ni majibu kwa Mfalme Mrope.

Sunday, May 9, 2010

Jumapili ya leo na tusali sala hizi na pia tusikilize wimbo huu uitwao Neema yake!!!

SALA YA ASUBUHI

Siku mpya inaanza, Nimuabudu Mungu kwanza: Mungu wangu baba yangu, Upokee shukrani yangu. Wewe kwa usiku mzima, ulikuwa kwangu daima: kunilinda kwa amani na mitego ya shetani. Kwako baba wa milele, Ninaomba neema tele: Niepuke dhambi zote, Nikutumikie pote. Ubariki kazi yangu, Shida na furaha Zangu. Mama safi ee Maria, Nipe msaada wako pia. Ee malaika kiongozi, Nipeleke kwa Mwokozi. Yesu nijalie neema, Niwe daima mkristo mwema. Amina.

NIA NJEMA

Nia na kusudi langu, Kumheshimu Mungu wangu. Najiunga kwa imani Na mkombozi msalabani. Roho, mwili chote changu Pendo na uzima wangu, Wazo neno tendo lote, Namtolea Mungu yote. Mungu wangu nakupenda, Wala dhambi sitatenda. Iwe kazi, nipumzike, Amri zako tu nishike. Utakalo nitimize. Kila kazi nimalize. Litukuzwe jina lako, Siku nzima iwe yako. Kwa utii navumilia Shida na matata pia. Nipe, Bwana neema zako, Niongeze sifa yako. Amina.

SALA YA JIONI
Sasa siku inakwisha. Kwako, Mungu, napandisha. Moyo wangu kwa shukrani, Nipumzike kwa amani. Mema mengi umenipa, Ninashindwa kukulipa. Baba mwema, ondolea Yote niliyokosea. Yesu mpenzi, Unijie, Ombi langu usikie: Unifiche mtoto wako Ndani ya jeraha zako. Ewe mama, nipe neema, Raha na usiku mwema. Roho mlinzi, ukakeshe, Pepo asinikoseshe. Naiweka roho yangu Mikononi mwa Babangu. Bila hofu napumzika, Mwisho kwako nitafika. Amina.




NA NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAPILI/DOMINIKA NJEMA. NI JUMAPILI YA 19 YA MWAKA HUU NA YA PILI YA MWEZI HUU WA TANO!!!!

Friday, May 7, 2010

Ijumaa ya tusikilize wimbo huu:- siku ya kifo!!



IJUMAA NJEMA KWA WOTE NA MUWE NA WAKATI MZURI IJUMAA YA LEO. NA PIA WIKIENDI NA TUONANE TENA WAKATI MWINGINE!!

Thursday, May 6, 2010

LEO NIMETAMANI KWELI HIKI CHAKULA KITAMUCHA NYUMBANI!!!!

Dagaa,ugali, samaki na ndizi,
mlo huu sijala muda mrefuuuu!!

Jamani mwenzenu niko katika msimu mbaya sana, mwaka jana nilichukua UNGA wa mahindi lakini sasa umeniishia. Na nimepita kila duka, nimepata unga lakini ni wa njano PALENTA kwa aliyezoea ugali kama mimi haunogi kabisa. Kwa hiyo nilipoiona picha hii mate wacha yanidondoke. Hali hii inanifanya niimbe wimbo huu NARUDI NYUMBANI EEEH, NARUDI PERAMIHO, NARUDI SONGEA NAKWENDA KULA LIKOLO LA NANYUNGU.....

Wednesday, May 5, 2010

KUPENDA NI NINI? KUMBUKUMBU YA MUNGA TEHENAN SEHEMU YA PILI!!

Ilipoishia…….
Bila shaka huwa unakutana na vitukovya karne kila siku kuhusu jambo hili. Mtu anaambiwa na mwingine kwamba hampendi. Inawezekana kuwa ni wapenzi wa muda mrefu-mke na mume au hata wa muda mfupi. Badala ya huyu anayeambiwa huapendwa kukubali jambo hilo kwa sababu hawezi kulibadili, kupinga. Wengine huenda hata mahakamani au kuwauwa wapenzi waliowakataa. Inaendele…..


Vituko hivi viko hata katika mazingira ambapo hakuna ugomvi au kutoelewana. Inawezekana ni katika mazingira ya kawaida kabisa, ambapo mpenzi anamuuliza mwenzake , ”hivi, unanipenda kweli, hebu nithibitishie”
Shabashi! Ni kitu gani hiki! Tangu lini kupendwa limekuwa ni jukumu lako? Jukumu lako ni kupenda, basi. Hili jukumu la kupendwa muachie mwingine.
Kupenda ni hisia na ndiyo maana imekuwa vigumu sana kwa watu kumudu kusema mapenzi ni nini. Jambo loloto la kihisi ni gumu kuelezewa kwa maneno. Kupenda kunapoelezeka kwamba ni kitu fulani, ni lazima kuna mushkeli.
Watu wengi ambao huwa ninazungumza nao katika kushauriana au kufundishana kuhusu kupenda, huwa ninawauliza swali hili ”Umempendae kitu gani mwenzako?” Wengi huwa wanatoa maelezo kama vile, ”nimempendea upole wake” au ”nimempenddea ukarimu wake” ama ”nimempendea tabia yzake”.

Lakini hakuna kabisa ambao wamewahi kusema wamempenda mwingine kwa sababu ya sura au maumbile yao au kwa sababu ya utajiri ama umaarufu wao . Kwa nini?
Ni kwa sababu, ndani ya nafsi zetu tunajua kwamba kupenda sifa za nje ni jambo linalopingwa na kila mtu n ani aibu kulitamka, labda tu miongoni mwa watu waliozoeana sana na kuaminiana.
Hata hivyo, miongoni mwa wapenzi, jambo hilo huwa linasemwa sana bila wenyewe kungámua. ”Unaniacha hoi kwa macho yako,” ni kauli za kawaida kwa wapenzi. Kusikia mpenzi akimwambia mwingine ”nimekupenda kwa kweli, guu unalo,” ni jambo la kawaida.
Mwanamke na kuita hali hiyo kuwa ni kupenda. Hutamani sana sura, miguu, matiti, makalio, macho na hata midomo n apua. Hili ni jambo la kimaumbile zaidi. Ndiyo maana wanawake wanajipamba na kujikwatua. Hufanya hivyo ili kuwavuta wanaume, kwani wanaume hujali muonekano wa nje zaidi.

Kuna wakati hapa nchini suala la wanawake kubabua ngozi au kupaka dawa nywele zao lilikuwa ni suala la mjadala mkubwa. Baadhi ya wanawake ambao walitakiwa kutoa maoni yao kuhusu jambo hili walisema, wao hawapendi sana kufanya hivyo, bali wanaume ndiyo wanaowalazimisha kufanya hivyo.
”mwanaume anaweza kukuacha kwa sababu tu kaona mwingine mwenye ngozi nyeupe na nyororo au nywele laini zilizoangukia mabegeni. Inabidi ujitahidi kumlinda.” walisema , baadhi ya wanawake. Pamoja na kuwa ni kauli zenye kuonyesha unyonge, lakini zina ukweli. Wanaume hukimbilia sifa za nje zaidi.

Wanawake kwa upande wao, huvutwa zaidi na wanaume ambao wanaweza kuwalinda au kuwapa uhakika fulani wa kimaisha. Hata hivyo, unapowauliza kwa nini wamempenda fulani, nao hawawezi kusema ni kwa sababu an fedha au kwa sababu ana jina, hapana. Ni aibu kukiri hivyo au pia kwa sehemu kubwa huwa hawajui kwamba wamevutwa na sifa hizo.
Ni wachache sana ambao hutokea wakajibu kwamba wamempenda mwingine kwa kumpenda tu, bila kutoa maelezo. Kwa nini ni wachache? Ni kwa sababu, wanaopensa siyo wengi. Mtu anayesema nimempenda fulani bila kujua ni kwa nini hasa, huyu ndiye ambaye amependa. Huku ndiko tunakoita kupenda tunapopenda, kwa kawaida kuwa hatuju sababu za kumpenda huyo fulani, bali tunampenda tu. Mtu anapotoa sababu ya kumpenda mwingine, huyo hajapenda bado. Huu ndiyo ukweli!

Kwa bahati mbaya, kuna wengine wamependa na hawajui ni kwa nini wamependa. Lakini unapowauliza, wanaanza kujaribu kutafuta sababu za huko kupenda kwako. Kwa hiyo, mtu ataanza kusema, `nampendea upole`au `nampendea huruma zake` ama `nampenda kwa sabu ametulia.” Anasema haya kwa sababu anaamini kwamba, kupenda ni lazima kutolewe sababu, wakati kinyume chake ndiyo ukweli.

Unapovutwa na mtu na ukajikuta huna sababu unazoweza kuzitoa za kwa nini umevutwa naye, kuna uwezekano mkubwa kwamba uko kwenye upendo wa kweli na mtu huyo. Lakini pale ambapo unaziona sababu waziwazi za kumpenda kwako, hapo hakuna upendo wa kweli.
Kumbuka kuwa sababu zote unazoziona ni za muda, zinaweza kuondoka. Zinapoondoka, ina maana pia kwamba, upendo haupo. Kama ulimpenda kwa sababu ya tabia ya upole na ukarimu, anapokuja kubadilika na kuiacha tabia hio, itakuwa na maana pia kwamba, mapenzi hayatakuwepo kwani ulichokipenda kitakuwa hakipo.

Lakini ukiona mwingine mwenye upole na ukarimu kuliko huyo, utampenda zaidi pia. Je, utaacha kumpenda yule wa kwanza au utawapanga kwa madaraja kiupendo?
Kama ulimpendea sura, mguu au jicho, ni wazi upendo wenu utakuwa ni wa muda kwani kwa kadiri siku zinavyopita, vitu hivyo havyo hupoteza nuru na mvuto. Mazoea nayo huingiza ukinaifu wa hisia. Lakini kuna wengine ambao wana miguu na macho mazuri zaidi ya hayo ya huyo. Hii ina maana kwamba, utahama kutoka mtu mmoja hadi mwingine ukifuata uzuri.

Kumpenda mtu bila kujua ni kwa nini umempenda, kuna maana ya kumkubali mtu huyo kama alivyo, kumpokea bila masharti. Kuna maelezo na nadharia nyingi zenye kuonyesha ni kwa nini siyo kila mtu anaweza kumpenda mwingine kwa njia hii.
Lakini bila shaka, nadharia na maelezo hayo hayana nafasi kubwa sana kwetu katika kujadili jambo hili. Chenye nafasi, ni kujua namna mtu anavyoweza kupima aina ya mapenzi aliyomo. ….tutaendelea wiki ijayo.

Habari hii ni kutoka kitabu cha MAPENZI kuchipua na kuchanua kilichoandikwa na MUNGA TEHENAN



Sio mbaya kama tukimsikiliza dada Saida Karoli na wimbo wake wa Mpenzi nakupenda

KUPENDA NI NINI? KUMBUKUMBU YA MUNGA TEHENAN!!!

Ni miaka miwili leo tangu mwalimu wa utambuzi MUNGA TEHENAN atuache. Nami ninapenda kumkumbuka/tumkumbuke kwa makala hii aliyoiandika kwenye kitabu chake cha MAPENZI kuchipua na kunyauka. Haya tujumuike na kuisoma makala hii:-


Msichana mdogo wa miaka 18 aliwahi kuja kwangu na kuniomba msaada. Hakuhitaji msaada mkubwa sana kama mwenyewe alivyosema, kwani alitaka kusaidiwa kupata jibu la swali ambalo lilikuwa likimtatiza kwa muda mrefu.
”Nataka kujua maana ya kupenda.” ilikuwa ndiyo kauli yake, fupi na inayoeleweka. Sikujibu swali lake moja kwa moja bali nilimwambia, ”umesema unahitaji msaada mdogo, lakini unayemwomba hana uwezo wa kukusaidia.” Nilizidi kumwambia kwamba, hata mimi nimekuwa kwa muda mrefu nikitafuta jibu la swali hilohilo.

Hivyo, sikuweza kumsaidia na niliona jambo lile lilinipa changamoto nami kuanza kusaka jibu la swali lile. Lakini, bahati nzuri ni kwamba, kabla yule msichana hajaondoka kwangu nilimuuliza nami swali moja. ”Ni kwa nini unataka kujua maana ya kupenda”? Alinijibu bila kufikiri mara mbili kwamba, ni kwa sababu gani anataka kujua kama mpenzi wake anampenda. Pengine jibu lake lilinizindua na nilihisi kama vile ndani ya jibu hilo kungeweza kupatikana pia jibu la lile swali lake. ”Ukishajua kama anakupenda ndiyo itakuwa nini baada ya hapo?” Nilimuuliza, pengine nikiwa sitegemei jibu.
Alikuwa ni msichana ambaye majibu yake yameandaliwa tayari kutolewa. ”si ndiyo nijue hanidanganyi, sasa nitampenda vipi kama yeye hanipendi!” alipomaliza kunijibu, nami nikawa nimepata jibu la swali lake.

Wengi husubiri kupendwa kwanza:
Siyo msichana yule tu, bali wengi miongoni mwetu tunasubiri kupendwa au huwa tunataka kwanza kuwa na uhakika kuwa tunapendwa, ndipo nasi tupende. Ukimfuata mtu na kumwambia kuwa unampenda, ungependa awe mpenzi wako au mwezi wa baadaye maishani na mtu huyu akawa mkweli na kukuambia kwamba, yeye hakupendi, utaumia sana. Utaanza hapohapo kumchukia au hata kumfanyia visa.

Unakuwa katika hali hiyo kwa sababu kuu mbili. Kwanza, ni kwa sababu hujui kwamb, kinyume cha kupenda siyo kuchukia. Unapomtaka mtu uhusiano na akasema hapana, unamchukulia kuwa anakuchukia kwa sababu, kwako kama hakuna kupenda, basi ni lazima kuwe na kuchukia.
Tumelelewa na kukulia katika mazingira ambayo yametufundisha kukitazama kila kitu katika uwili. Kwa hiyo, `sikupendi`masikioni mwetu inasikika kama, `nakuchukia`.
Pili, ambavyo ni kubwa, ni kwa sababu kila binadamu anahitaji kupendwa. Wataalamu wengi wa saikolojia wanabainisha kupendwa kama moja ya mahitaji muhimu kwenye ngazi ya mahitaji ya binadamu.
Tangu tukiwa na umri wa siku moja, tunataka kukubaliwa kupokelewa na kulindwa. Haya ya kupendwa ni kama jambo la kimaumbile kwa binadamu. Unapogundua kuwa watu wote hawakupendi ni lazima utababaika, utachanganyikiwa na kwako maisha yanaweza kupoteza maana.
Wengi tunafanya tuyofanya au kuacha kufanya katika kutafuta kupendwa. Kwa hiyo, kila mmoja wetu ana kiu kubwa ya kupendwa. Hapa ndipo linapochipuka tatizo kubwa linalofanya wengi kushindwa kujibu swali la , `kupenda ni nini?` Hushindwa kwa sababu, hakuna anayejali kupenda, karibu wote tunajali kupendwa, tuna kiu ya kupendwa, siyo kupenda Kama nguvu zetu zote tumeziweka kwenye kupendwa, kupenda kunakuwa na nafasi gani kwetu? Ndiyo maana wengi hatuju kupenda ni nini?
Ni kitu gani kinatokea? Ni kwamba, badala ya kuwekeza kwenye kupenda, tunawekeza kwenye kupendwa ambako hakutuhusu. Ni sawa na mtu kuchukua fedha zake na kuziingiza kwenye akaunti ya mwingine akiamini kwamba anaziingiza kwanye akaunti yake. Siku anapokuja kutaka kutoa fedha na kukuta hazipo atazusha zogo kubwa na balaa lisilowezekana. Atadai kwamba benki hazifai na hazina ukweli.

Unaposubiri au kutarajia na mbaya zaidi kudai kupendwa, unapoteza muda wako bure, kwa sababu hilo ni jambo lisilokuhusu. Ni jambo ambalo huwezi kulipanga wala kulidhibiti kwa sababu linamhusu mtu wa upande wa pili. Inawezeakana vipi wewe umalazimishe mtu akupende? Haiwezekani, lakini tunafanya. Tunafanya lisilowezekana.
Lakini unaweza kupenda, kwani ni jambo linalotoka kwako , lililo ndani ya uwezo wako. Kwa hiyo, unapokutana na mtu, kama amekuvutia, wewe ndiye unayetakiwa kumpa upendo, bila kujali kama naye anakufanyia hivyo. Huna haja ya kujali kama naye anakufanyia hivyo kwa sababu, wewe umeamua kumpenda, lakini huna haki na huwezi kumfanya akupende kama yeye hataki.

Bila shaka huwa unakutana na vitukovya karne kila siku kuhusu jambo hili. Mtu anaambiwa na mwingine kwamba hampendi. Inawezekana kuwa ni wapenzi wa muda mrefu-mke na mume au hata wa muda mfupi. Badala ya huyu anayeambiwa huapendwa kukubali jambo hilo kwa sababu hawezi kulibadili, kupinga. Wengine huenda hata mahakamani au kuwauwa wapenzi waliowakataa. ITAENDELEA…….

HABARI HII NIMEITOA KATIKA KITABU CHA MAPENZI KUCHIPUA NA KUNYAUKA KILICHOANDIKWA NA MAREHEMU MUNGA TEHENAN.

Tuesday, May 4, 2010

WATOTO NA MATATIZO YA MTINDIO WA UBONGO

Wapo watoto wengi wanaozaliwa wakiwa na matatizo mbali mbali, lakini mojawapo nitatizo la mtindio ya ubongo ambalo leo nimeona nilizungumzie kwa undani zaidi.

Matatizo ya mtindio wa ubongo yanatokana au kusababishwa na vinasaba (Genetic), dawa alizotumia mama wakati wa ujauzito, matumizi ya madawa ya kulevya, pombe, hali ya hewa, au hata ajali. Mojawapo ya sababu hizo nilizozitaja zinaweza kusababisha kuzaliwa kwa mtoto mwenye mtindio wa ubongo au mtu kupata mtindio wa ubongo.

Nikianza na tatizo la pombe, ni kwamba pombe ina athari kubwa na mbaya kwa akina mama wajawazito. Lipo tatizo linalofahamika kitaalamu kama Fetal Alcoholic Syndrome (FAS) ambalo huwapata watoto ambao wazazi wao walikuwa wanatumia kiwango kikubwa cha pombe wakati wa ujauzito.

Watoto wanaozaliwa na tatizo hili wanakuwa na nyuso ambazo sio za kawaida (Facial Deformities), kwa mfano watoto hawa wanaweza kuwa na pua bapa na macho yaliyoingia ndani au kuwa na mtindio wa ubongo (Mental Retardations), matatizo ya kusikia na kutokuwa na uwezo wa kusoma.

Kwa hiyo unywaji wa pombe hata kwa kiwango kidogo katika kipindi cha mwezi mmoja hadi mitatu ya mwanzo kwa mama mjamzito huchangia kwa kiasi kikubwa kuzaliwa kwa watoto wenye matatizo haya.

Watoto wote wenye matatizo haya ya mtindio wa ubongo wanaweza pia kujifunza kusoma iwapo watapewa msaada maalum na kuandaliwa mazingira mazuri yatakayowashawishi kujifunza kusoma. Malezi kwa watoto wenye matatizo haya, yanatakiwa yawe tofauti na yale ya watoto wa kawaida.

Watoto hawa wanahitaji kuoneshwa upendo, kusikilizwa na mengineyo ya aina hiyo. Hata hivyo swali la msingi tunalopaswa kujiuliza ni kwamba, tutawatambuaje watoto wenye tatizo hili la mtindio wa ubongo wakingali wadogo?

Ukweli ni kwamba ni vigumu sana kwa wazazi kuwatambua watoto wao wenye tatizo hili, kabla watoto hao hawajatimiza umri wa miaka mitatu au minne. Kwa kawaida inashauriwa kwamba mtoto yeyote ambaye anafanya mambo yake pole pole ukilinganisha na watoto wengine wa umri wake, inapaswa kupelekwa haraka hospitalini kwa daktari bingwa wa watoto ili afanyiwe uchunguzi wa kina.

Hata hivyo dalili zifuatazo zinaashiria kuwa mtoto ana tatizo hili Kwanza haoneshi dalili yoyote ya kulia au anaweza kulia kidogo sana. Pili huchelewa sana kutembea na hata kuongea. Tatu haoneshi kuvutiwa nna mazingira yanayomzunguka, kwa maana kwamba hata kama kuna vitu vya kuchezea hawezi kujishughulisha navyo. Nne ni vigumu sana kufundishika na hata kujifunza kusoma huwa ni kazi ngumu ukilinganisha na watoto wa rika lake.

Tano hawezi kula mwenyewe, kuvaa mwenyewe au kujifunza kutumia choo. Hata hivyo zipo dalili nyingi zinazoweza kujitokeza na mara nyingi zinatambuliwa na madaktari maalum wa watoto.

Jinsi wazazi wanavyoweza kuwasaidia watoto wenye tatizo hili:

Watoto wenye mtindio wa ubongo wanafundishika, iwapo tu watafundishwa kwa makini, utulivu na uvumilivu mkubwa, yaani mtu anayemfundisha mtoto wa aina hii hatakiwi kamwe kuwa na hasira, na pia inashauriwa sana kuwapongeza wanapofanya vizuri japo kidogo.

Mwalimu anatakiwa awe mpole na ufundishaji wake usiwe wa haraka haraka, aoneshe mapenzi kwa mtoto, hapaswi kumkemea hata kama anakaosea .

Watoto wa aina hii inashauriwa wapewe nafasi ya kujenga urafiki na watoto wenzao warika lao. Huko nyuma watoto wenye matatizo ya akili walikuwa wantengwa na watoto wenzao katika madarasa, kwa kuwekwa kwenye madarasa maalum.

Lakini siku hizi inashauriwa wachanganywe na wanfunzi wenzao wasio na matatizo ya akili, japo hata kwa nusu siku. Utaratibu huu hujulikana kitaalamu, kama mainstreaming. Itaendelea.....

Monday, May 3, 2010

KUTANA NA YASINTA, MJASIRIAMALI ALIYESEMA HAPANA KWA WANAUME WAKWARE



Nusura niwe mtoto wa mitaani




Juzi ijumaa nikiwa ofisini kwangu alipita binti mmoja akiwa na begi lake dogo kama yale yanayotumiwa na wanaume kubebea Lap Top.

Alinisalimia kwa uchangamfu na kujitambulisha kwangu kuwa anitwa Yasinta. Alionekana kuwa mchangamfu utadhani tunafahamiana siku nyingi, hata hivyo na mimi nilimchangamkia pia. Kumbe Yasinta ni mfanyabiashara wa kuuza viungo mbalimbali kama vile vya Pilau, viungo vya Chai, kwa kweli sikujua kama chai nayo ina viungo, pia alikuwa na viungo vya kupikia nyama , samaki au hata kuku na hasa kuku wa kienyeji na alitumia muda huo kunifundisha namna ya kutumia. Kwangu mimi hayo yalikuwa ni mapinduzi makubwa katika mapishi ya vyakula vya kiswahili

Yasinta Alionekana kuwa ni mdogo kiumri yaani ukimuangalia kwa haraka haraka anaonekana kuwa na umri wa kama miaka 18, hata hivyo sikukosea sana kwani nilipoomuliza umri wake aliniambi kuwa ana umri wa miaka 19 na mwishoni mwa mwaka huu ndio atatimiza umri wa miaka 20. Mara akaja jirani yangu mmoja ambaye ofisi zetu zinafuatana, alipomuona Yasinta alimshangilia sana na kuwaita wenzake na kuwajulisha ujio wa Yasinta, nilibaki nimeduwaa.

Baadae niliambiwa kuwa Yasinta alikuwa ni maarufu sana pale kwani alikuwa akiwauzia viungo vya mbalimbali na hivyo kufurahia mlo wao wa siku. Waliniambia kuwa walimfahamu Yasinta takribani miaka mitano iliyopita tangu alipoanza kuwapitishia ile biashara, wakati huo akiwa ni binti mdogo sana kwa umbo na umri.

Ni mwaka jana mwishoni alipowaaga kuwa anatarajia kufunga ndoa, na walimchangia fedha na zawadi nyingine. Tangu wakati huo Yasinta hakuonekana mpaka wakadhani labda ameamua kuachana na biashara hiyo, au mumewe amemkataza kuendele nayo.
Nilinunua viungo mbali mbali na niliamua kutumia fursa hiyo kufanya mazungumzo nae.
Yasinta alianza biashara hiyo mnamo mwaka 2005 Mara baada ya kumaliza darasa la saba mkoani Mbeya.

Je alifikaje mjini?

Yasinta alikuja mjini mwaka 2004 akiwa ndio amemaliza darasa la saba, baada ya kuwa hakufaulu na mama yake kutokuwa na uwezo wa kumuendeleza kielimu alichukuliwa na mama mmoja aliyekuwa akiishi maeneo ya Ilala hapa jijini Dar es salaam mwenyeji wa huko huko Mbeya ili kuja kufanya kazi za ndani.

Baba yake alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu wakati alipokuwa darasa la nne na kuanzia hapo majukumu ya kutunza familia aliyabeba mama yake pekee. Akiwa ni wa kwanza kuzaliwa na binti pekee kwa wazazi wake huku akifuatiwa na na wadogo zake wawili wa kiume, hakuwa na jinsi ilibidi aje mjini kufanya kazi za ndani ili aweze kumsaidia mama yake kuwatunza wadogo zake.

Alidumu na yule mama kwa mwaka mmoja. Lakini kutokana na mateso ilibidi atoroke na kujikuta akishia mtaani. Siku moja katika mizunguko yake ya kutafuta kazi alikutana na mabinti wa umri wake ambao walikuwa wakijiuza maeneo ya Buguruni na walimtaka ajiunge nao ili kujitafutia kipato, na walimuhakikishia kuwa shughuli ile ya kujiuza ina kipato kushinda hata ya kuajiriwa, hata hivyo Yasinta alikataa kata kata kujiunga nao, akamua kujichanganya na wale mama ntilie pale Buguruni CCM kwa kuwasaidia ili kujipatia kipato, hata hivyo mama mmoja allijitolea kumpa hifadhi.

Siku moja akiwa katika shughuli zake kama kawaida, alipita mama mmoja na kuagiza chakula, wakati akimuhudumia na kwa kuwa alikuwa ndie mteja pekee kwa wakati huo alianza kuzungumza nae. Katika mazungumzo yao yule mama alimjulisha juu ya biashara ya Viungo, mbalimbali vya mapishi ambayo ndio aliyokuwa akiifanya. Yasinta alivutiwa sana na ile biashara na kwa kuamini kuwa ule ulikuwa ndio wakati wa kuondokana na kazi za kutumwa, alimuomba yule mama amfundishe namna ya kufanya ile biashara.

Kwa bahati nzuri yule mama alimkubalia na na kuahidi kumpitia kesho ili wafuatane nae ili akamuoneshe mahali anaponunulia na kumuonesha namna ya kutayarisha.
Na kweli yule mama alimpitia kesho yake. Yasinta alimuaga yule mama aliyempokea pale Buguruni na kuondoka na yule mama kuelekea Kariakoo kufanya manunuzi.
Yule mama alijitolea kumpa hifadhi ya muda nyumbani kwake maeneo ya Vingunguti na kumfundisha namna ya kutengeneza viungo mbali mbali, Kutokakna na bidii aliyonayo ilimchukua Kiasi cha mwezi mmoja Yasinta kufudhu mafunzo hayo.

Yule mama alimkopesha Yasinta mtaji wa shilingi elfu kumi wa kuanzia.

Yasinta anakiri kuwa awali alikuwa na wakati mgumu sana kutokana na biashara kuwa ngumu lakini yule mama alimpa moyo wa subira.
Haikuchukuwa muda mrefu hali ilibadilika na biashara kumnyookea na kuweza kulipa mkopo aliokopeshwa na yule mama yake mlezi ambaye alimfanya kama mama yake mzazi kutokana na kumlea. Ilimchukuwa mwaka mmoja Yasinta kuhama na kupangisha chumba chake maeneo ya Buguruni na kuanza kujitegemea huku akiendelea na biashara yake hiyo ya viungo. Kuanzia hapo akawa anatuma hela kwa mama yake huko mbeya ili ziweze kumsaidia.

Mwaka mmoja baadae Yasinta alifanikiwa kununua kiwanja chenye ukubwa wa nusu eka maeneo ya Kinyerezi na ili iwe rahisi kwake kujenga. Ikabidi ahamie Segerea ili awe karibu na kiwanja chake. Taratibu alianza kujenga nyumba yake ya vyumba viwili. Ilimchukua mwaka mmoja na nusu kukamilisha nyumba yake ya vyumba viwili na kufanikiwa kuweka umeme na kuhamia nyumbani kwake. Lengo lake la kwanza likafanikiwa.

Yasinta alijiwekea malengo makuu matatu, wakati alipoanza biashara ya viungo.
Aliyataja malengo hayo kuwa ni kujenga nyumba yake mwenyewe, kukarabati nyumba ya mama yake kule Mbeya na kuwasomesha wadogo zake mpaka chuo kikuu.
Baada ya mdogo wake anayemfuatia kumaliza darasa la saba mwaka juzi akamleta na kumuandikisha katika shule ya sekondari ya binafsi iliyoko maeneo ya Ubungo na gharama za masomo analipa yeye kutokana na biashara yake ya viungo anayofanya.

Je Yasinta amemudu vipi kufikia hapo alipofikia na nini matarajio yake? Nilimuuliza.

Yasinta alikiri kuwa subira na uvumilivu ndio umemfikisha pale alipo sasa, kwani kuna wakati biashara ilikuwa haitoki kabisa mpaka anashindwa kulipa kodi ya nyumba, lakini kwa kuwa alikuwa amejiwekea malengo alihisi kuwa alikuwa na deni kubwa mbele yake na hiyo ilimpa hamasa ya kutokata tamaa na aliamini kuwa atafanikiwa.
Anasema aliponunua kiwanja alianza kuishi kwenye nyumayake kabla hata hajaijenga, kwani alikuwa akijiona kabisa kuwa amejenga na alikuwa akiiona nyumba yake ikiwa imekamilika kabisa, hakudhani kama atashindwa, aliamini tu kuwa ataweza.

Vipi kuhusu wanaume?
Nilimuuliza kwa kuwa yeye ni binti ambaye bado ni mbichi, kabla hajaolewa aliwezaje kukabiliana na vishawishi vya wanaume hasa ikizingatiwa kuwa alikuwa akiishi peke yake na shughuli zake ni za kuzunguka maofisini?

Yasinta alikiri kuwa alikuwa akipata sana mitihani ya kutakwa na wanaume, wengine wakiwa ni wababa wazima wakuweza hata kumzaa mara tano lakini alikuwa amejiwekea nadhiri ya kutofanya mapenzi kabla ya ndoa, pia alikuwa amepanga kuwa hataolewa mpaka awe amejenga nyumba yake mwanyewe, kitu ambacho amefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Je alimpataje Mwezi wake?
Yasinta alicheka kidogo, huku akiongea kwa aibu kidogo, alisema, “ Huyu mume niliyekuwa nae nilijuana nae miaka miwili iliyopita wakati akisoma sekondari wakti huo, tulikuwa tukikutana mara kwa mara kituoni tukisubiri usafiri wa daladala wa kwenda mjini. Kutokana na usafiri wa daladala Segerea kuwa ni mgumu tulikuwa tukigombea mabasi pamoja, siku moja akanilipia nauli, nilikataa kwa kuwa niliona kuwa yeye ni mwanafunzi, kwa hiyo haikuwa ni vyema anilipie nauli, lakini alisisitiza kunilipia na akakataa kupokea hela yake aliyomlipa kondakta wa daladala, na huo ukawa ndio mwanzo wa kufahamiana kwetu.
Baada ya kumaliza masomo alijunga na chuo kimoja mjini na kusomea mambo ya information Technology, na sasa ameajiriwa na kampuni moja binafsi akiwa ni mtaalamu wa kompyuta”.

Je mumeo anayo mikakati gani ya kukuendeleza kielimu, au ndio umeridhika na kiwango cha elimu ya darasa la saba ulicho nacho? Nilimuuliza.

Yasinta alisema kuwa ameanza kusoma masomo ya sekondari ya jioni katika shule moja ya binafsi iliyoko Tabata na ndio ameanza kidato cha kwanza ambapo itamchukua miaka miwili kumaliza kidato cha nne.

Ukweli ni kwamba nilifurahishwa sana na mazungmzo yangu na Yasinta, kwani ni miongoni mwa mabinti wachache hapa nchini wenye mtazamo chanya kuhusiana na maisha, na ameonesha kuwa, ukiamua unaweza, kwani hakuna kisichowezekana chini ya jua, kinachotakiwa ni kujiwekea malengo na kuwa na nia na dhamira ya kufikia malengo uliojiwekea. Kingine ni nidhamu katika kila jambo unalolifanya, kwani bila nidhamu hakuna kufanikiwa.

Hivi ni wasichana wangapi ambao wameshindwa kuendelea na masomo, na badala ya kujitafutia maendeleo kwa njia ya halali wamejikuta wakijiuza ili waweze kujikumu?
Ni wangapi wamekufa kwa ukumwi au wanaugua ukimwi sasa hivi baada ya kujiingiza katika vitendo vichafu vya kujiuza mwili?

Yasinta katuonesha njia kuwa tukiamua tunaweza.
Namtakia kila la heri katika ndoa yake, idumu na iwe na amani na upendo.
Habari hii imenivutia sana nimeichukua kwa mdogo wangu Koero Mkundi
http://koeromkundi.blogspot.com/ nimeona sio mbaya kama tukujikumbusha na kujadili kwa pamoja.

Sunday, May 2, 2010

Ujumbe wa Jumapili ya leo:- Mwanangu!!

mama na mwana (Yasinta na mwanae)

Shairi hililimenigusa sana na ndio maana nimeamua kuwaka hapa kibarazani kwangu kama huamini soma na utaona utamu wake.
Mwanangu uketi chini, mambo haya nikwambie,
Nisikie kwa makini, kichwani yazingatie,
Usiyaweke pembeni, kazi ukayafanyie,
Mwanangu hii dunia, yahitaji umakini.

Mwanangu wajuwe watu, uishi nao vizuri,
Jifunze kuwa na utu, utende kwa kufikiri,
Usiwadhulumu katu, wemawo uwe hiyari,
Mwanangu katende wema, usingoje shukrani.

Mwanangu wacha papara, wende mwendo taratibu,
Itangulize busara, hata panapo majibu,
Jisafishe yako sura, uepuke majaribu,
Nawe wonekane vema, uwe na yako staha.

Mwanangu wewe ukuwe, ili uje kuyaona,
Siyo majumba ya Kawe, ama jiji kubwa sana,
Bali ukayaelewe, maisha kila aina,
Yenye watu ndani yake, wenye vitu ndani yao.

Mwanangu si lelemama, maisha ni kupambana,
Kuna watu waso wema, kwa macho hutowaona,
Ikuze yako hekima, nayo ikuchunge sana,
Maana ndiyo silaha, dunia yajaa hila.

Mwanangu kuza imani, umtegemee Mungu,
Sidhulumu masikini, ukavunja chake chungu,
Uzidishe umakini, kwao hao walimwengu,
Dunia wala si mbaya, wabaya ni walimwengu.

Mwanangu ujihadhari, na vicheko midomoni,
Mioyoni si wazuri, wala usiwaamini,
Wajichimbia kaburi, wewe kufukiwa chini,
Marafiki wasaliti, ndivyo iwavyo daima.

Mwanangu hii dunia, imejaa uhadaa,
Mambo yakikunyokea, marafiki wanajaa,
Siku yakikuchachia, wote wanakukataa,
Kwao urafiki vitu, bilavyo hakuna pendo.

Mwanangu chunga kauli, pindi unapoongea,
Penda kusema ukweli, mema ukayatetea,
Uepuke ubatili, ubaya sije endea,
Mdomo ndio ubao, watu ndipo hukusoma.

Mwanangu nakushukuru, najua umesikia,
Ninakuombea nuru, Mola kukuangazia,
Mola atakunusuru, na mabaya ya dunia,
Mwanangu uishi vema, maisha kufurahia.



Kila mzazi anapenda mwanawe awe na wakati mzuri maishani. Bado sina mtoto, lakini nimejaribu kuvaa uzazi na kuandika tungo hii. Naamini kila mzazi huwa anamfundisha mtoto wake namna bora ya kuishi na watu duniani. Shairi hili ni zawadi kwa wale wote ambao ni wazazi.



Shairi limetungwa na Fadhy Mtanga ukitaka kusoma mashairi yake zaidi soma hapa nami nimevutiwa nikaona niweka hapa ili tujifunze kwa pamoja. NA NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAPILI/DOMINIKA NJEMA. NI JUMAPILI YA 18 YA MWAKA HUU NA YA KWANZA YA MWEZI HUU WA TANO!!!!

Saturday, May 1, 2010

WANASIASA WASIO NA HURUMA NA NIA YA KUSAIDIA WALEMAVU HAWAFAI KUCHAGULIWA

WATANZANIA wametakiwa kutowachagua wanasiasa wasioonyesha utashi wa wazi katika kuwasaidia na kuwatetea walemavu wa aina mbali mbali nchini.

Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na ndugu Jacob Malihoja Mwezeshaji katika mafunzo ya siku nne juu ya Uongozi na Utawala Bora yaliyoandaliwa kwajili ya viongozi wa chama cha wasioona nchini Tanzania League of the Blind (TLB) Wilaya ya Temeke.

Ndugu Malihoja alitoa kauli hiyo kwa masikitiko baada ya wafanyabiashara, wanasiasa na viongozi kadhaa waliolikwa kwenye hafla ya kufunga mafunzo hayo ya wasioona kutotokea kwenye shughuli hiyo jambo ambalo liliwafanya Walemavu hao kujikuta wako peke yao kwa ufariji wa wajumbe wa Serikali ya Mtaa waliyejitokeza na kumua kumwakilisha Mgeni rasmi Mbunge wa jimbo la Temeke Mhe. Abasi Mtemvu ambaye alipata dharula ya kutembelea wananchi wake walioathirika na mafuriko.

Aidha ndugu Malihoja amesema Watanzania wanapaswa kuelewa kuwa sisi sote hatuoni, alitolea mfano Mhe. Mudhihiri alikuwa salama na viungo vyake vyote lakini alikuwa haoni, kwani laiti angekuwa anaona asingefanya safari ambayo ilisababisha na yeye sasa awe mmoja wa walemavu nchini.

Kwa kutambua hilo amesema Watanzania na wote tunawajibu wa msingi sana kuwasaidia walemavu kwani hakuna anayeona kesho atakuwaje.

Aidha amesema mbali na hilo walemavu wana akili na uwezo mkubwa sana katika kuchangia maendeleo yao wenyewe na maendeleo ya Taifa na kwamba kinachohitajika ni kuwawezesha washiriki maendeleo yao na maendeleo ya taifa kimamilifu kwama watu wengine..

Zaidi unaweza kusoma hapa.