Wednesday, May 26, 2010

MAKULILO, Jr. ALA NONDOZI


Mzee wa Nondozi – MAKULILO, Jr. Jumamosi May 22, 2010 amekula NONDOZI – Masters of Arts in Peace and Justice at the University of San Diego (USD) huko California. Hii ni katika kuelekea katika Ph.D in Conflict Analysis and Resolution katika mwaka mpya wa masomo ujao.

Mdau MAKULILO, Jr. ana mpango wa kwenda likizo nyumbani Tanzania akiambatana na mke wake. Katikalikizo hiyo atafanya semina na midahalo kwa watu kuhusu ni jinsi gani mtu unaweza kupata vyuo na SCHOLARSHIPS Ughaibuni. MAKULILO, Jr. yeye mwenyewe amefaidika kwa kupata scholarships zaidi ya nne kwa ndani ya miaka miwili. Na anapenda kuhakikisha wadau wengi wanafaidika na nafasi hizi zilizopo Ughaibuni. Ratiba ya semina na special talks itatangazwa baadaye mara maandalizi yakiwa sawa.

PICHA ZA MAHAFALI

Mdau MAKULILO mara baada ya kula nondozi yake Jumamosi May 22, 2010



MAKULILO Akishangilia kula nondozi



Makulilo akiwa na wanadarasa wenzake waliokula nondozi pamoja


MAKULILO akipongezwa na mke wake Bi. Marie Makulilo


Makulilo na mwalimu wake, Dr. Ami Carpenter

MAKULILO akiwa na Dean of School of Peace, Fr. Bill Headley, PhD

MAKULILO na rafiki zake, Fr. Daniel (Kenya), Ghulam (Afghanstan) wakiwa nje ya School of Peace and Justice


KWA WANAOTAFUTA NONDOZI UGHAIBUNI NA SCHOLARSHIPS,

Tembelea

1. SCHOLARSHIP FORUM http://www.scholarshipnetwork.ning.com/

2. MAKULILO BLOG http://www.makulilo.blogspot.com/

MDAU

MAKULILO, Jr.

San Diego, CA

7 comments:

ERNEST B. MAKULILO said...

Da Yasinta,

Asante, na ninafurahi kuweka habari hii hapa.

MAKULILO, Jr.
www.makulilo.blogspot.com
www.scholarshipnetwork.ning.com
San Diego, CA

EDNA said...

Yeeeees you made it,Hongera sana kaka Makulilo.

Simon Kitururu said...

Hongera Mkuu!

Mija Shija Sayi said...

Raha sana.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

hongera mkuu kwa kula nondoz!

Unknown said...

Mkuu hongera sana. Hakika umefanya kweli. Nakutakia kila la kheri na fanaka katika kuyatumia yale yote uliyojifunza kwa faida ya jamii yetu...

Yasinta Ngonyani said...

Napenda kuwashukuruni wote kwa kutochoka kupita hapa Maisha na Mafanikio . Nami napenda kusema HONGERA sana kaka Ernest ni mfano mzuri wa kuiga kama ulivyosema wewe mwenyewe " kama nimeweza mimi basi hayta nanyi mtaweza" ni kweli kabsa. Upendo Daima!!