Swali la leo:- Hivi kwanini kanga mnyama anaitwa kanga na Kanga vazi ni kanga zina uhusiano gani?
Kanga kama mnyama
Kanga kama vazi hasa kwa wanawake!!
Nimekuwa nikijiuliza miaka yote hii leo nimeona niwailize ndugu zangu kwani umoja ni nguvu utengano ni udhifu. Na anayeuliza sana basi anajua mengi...a.k.a KAPULYA MDADISI.
Duh! Mi nadhani kufanana ni kule kule kwa mnyama kuitwa komba na binadamu kuitwa komba...ama ukitoa Ngo.....silabi zinazobakia na mnyama kuitwa vivyo hivyo.....ha ha haaaaaa!
Niliwahi kusimuliwa na bibi Koero kuwa kipande cha shuka za kujifunga wanawake cha kwanza kilitengenezwa kwa mfano wa madoa doa kama ya huyu ndege Kanga...na huo ndio ukawa ni mwanzo wa kipande hicho kuitwa kanga mapka leo.
lakini kumetokea mabadiliko makubwa katika kipande hicho mpaka kufikia kuwekwa ujumbe mbalimbali wa kuelimisha hadi kufikia wa matusi tena ya wazi wazi.
Badala ya kanga kununuliwa kutokana na nakshi ilizo nazo, siku hizi hununuliwa kutokana na ujumbe uliopo katika kanga hiyo na ndio maan hata jina wamebadilisha badala ya kuandikwa kanga huandikwa khanga, ili kutofautisha na kanga ndege.......sio mimi bali ni hekaya za bibi koero
wacha na mimi nichangie kanga na kanga hakuna uhusiano hata kidogo na sio kanga tuu kuna majina mengi yanafanana lakini hakuna uhusiano kama mbuzi,myama na mbuzi ya kukuna nazi,kaa au Mkaa kuna mnyama na kuna kaa la kupikia ,sikio ni la kusikia na lile la mkoba wa ukindu.
9 comments:
Nahisi ni kufanana kwa urembo na nakshi zilizopo kwa ndege huyu ukifananisha na vazi lenyewe kuna kitu kinafanana hapa
Sina uhakika, lakini nafikiri kutakuwa na uhusiano.
Duh! Mi nadhani kufanana ni kule kule kwa mnyama kuitwa komba na binadamu kuitwa komba...ama ukitoa Ngo.....silabi zinazobakia na mnyama kuitwa vivyo hivyo.....ha ha haaaaaa!
Mtani bwana kwani we hujui kwa nini?
Niliwahi kusimuliwa na bibi Koero kuwa kipande cha shuka za kujifunga wanawake cha kwanza kilitengenezwa kwa mfano wa madoa doa kama ya huyu ndege Kanga...na huo ndio ukawa ni mwanzo wa kipande hicho kuitwa kanga mapka leo.
lakini kumetokea mabadiliko makubwa katika kipande hicho mpaka kufikia kuwekwa ujumbe mbalimbali wa kuelimisha hadi kufikia wa matusi tena ya wazi wazi.
Badala ya kanga kununuliwa kutokana na nakshi ilizo nazo, siku hizi hununuliwa kutokana na ujumbe uliopo katika kanga hiyo na ndio maan hata jina wamebadilisha badala ya kuandikwa kanga huandikwa khanga, ili kutofautisha na kanga ndege.......sio mimi bali ni hekaya za bibi koero
wate ni wanawake.
kanga wanyama wana tabia za kike kike zaidi hasa kulia kwa kukpana pua, wana urembo na wanajisandia haja ndogo kwa kuchuchumaa!!
wacha na mimi nichangie kanga na kanga hakuna uhusiano hata kidogo na sio kanga tuu kuna majina mengi yanafanana lakini hakuna uhusiano
kama mbuzi,myama na mbuzi ya kukuna nazi,kaa au Mkaa kuna mnyama na kuna kaa la kupikia ,sikio ni la kusikia na lile la mkoba wa ukindu.
dah
hakuna uhusiano hata kidogo
kanga na kanga myama
mbuzi ya kukuna nazi na mbuzi myama
kaa wa baharini na kaa kitako chini
sikio la mkoba na sikia la kusikia
Ahsanteni sana kwa darasa hili Duh kiswahili jamni kazi kwelikweli. Natumaini tutaendelea kufunzani humu humu ktk blogg!!UPENDO DAIMA!!!
Post a Comment