Tuesday, February 26, 2013

PALE MNAPOKUTANA NA MLIOFANYA NAO KAZI/MLIOSOMA NAO....

 
 
......Furaha inakuwa ni ya ajabu...hapa ni mwalimu mtaafu Eusebius Mlelwa na mwal. Klaesson walikuwa wanafanya kazi pamoja Wilima Secondary hapa walikutana mwaka huu mjini Songea. Hapa ni stendi kuu ya Songea
Sio wao tu walipata bahati ya kuonana ..la hasha Yasinta/kapulya naye alionana na rafiki yake ambaye walisoma chuo pamoja ni Pendo Mapunda. Nilifurahi sana kuonana na Penda miaka mingi tulipoteana. Hapa ni Lizabon Songea.....Raha eeeehhhh....

10 comments:

Shalom said...

Jamani naona ulifurahi sana lkn dada mbona shoga ako kawahi kuzeeka mm nilijua lbd dada ako.

Ester Ulaya said...

huwa ni furaha sanaaaaaaaa kwakweli, ni kukumbushana mlipotoka na kuambiana yanayojiri na kucheka kwa wingi

Yasinta Ngonyani said...

Shalom! hapana si dadangu ni rafiki yangu...maisha ..na wala si mzee ni kama mimi tu..lol

Ester miaka ishirini kupoteana hakika hapo kucheka ni lazima...ilikuwa raha sana

emu-three said...

Inafurahisha na kupendezesha, maana mnatamani siku hizo zirejee tena, lakini haiwezekani.

Mija Shija Sayi said...

Yasinta na ile picha yako ya mkanda wa kipepeo ulipigia wapi vile...

Rachel siwa Isaac said...

Kweli ni Furaha na Raha.....wengine mpaka huwa wanalia!!!!

Anonymous said...

Kwa hizo picha mbili Yasinta na Pendo, unaweza kupata picha au kuona tofauti ya maisha ya Tz na ulaya, kwa sura tu. Jamani Yasinta nje kuzuri mana unazidi kunawiri na kuwa msichana wakati wenzio wanazeeka, usije kujisahau siku moja ukamwamkia Pendo! Kweli ukipitisha miaka mingi tena hujamuona huyo Pendo utampa shikamoo mwenyewe kwa hiari yako.

Shalom said...

Kweli maisha ya kijijini sio mchezo.

Anonymous said...

Embu ona hata huyo mwl. aliyefundisha na baba erick, mh naye anaonekana ni mzee sana! huwezi amini kama ni office mates jamani.Haya tutafute wazungu tuolewe tukaishi ulaya ili tubakie vijana.

Yasinta Ngonyani said...

emu3! Yaani inafurahisha mno mno:-)

Mija nawe na ile picha ya mkanda wa kipepeo naona imekunogea kweli ..haya dada mkuu nilipiga Matetereka/wilima Secondary. Vipi?

Rachel/kachiki! unafikiri hata mie nililia:-(

Usiye na jina wa 1045! kumwamkia Pendo shikamoo HAPANA hata nikiwa usingizini nitamfahamu tu tumetoka mbali...

Shalom:-)
Usiye na jina wa 7.17! huyu mwalimu nakwambia hazeeki wakati huo alipokuwa anafundisha alikuwa hivyo hivyo wengine bwana wana bahati kupata miili isiyozeeka...