Thursday, February 21, 2013

HONGERA KWA KUTIMIZA MIAKA KUMI NA TANO(15) DADA /BINTI CAMILLA!!!

Dada Camilla ndani ya kitenge akiwa nyumbani Ruhuwiko mwaka huu..naenda kusakasaka picha pia...Mdada huyu ni fundi sana wa kupiga picha....
.....Na sio kupiga picha tu binti Camilla anapenda pia kusaidia kazi za jikoni kama mnavyoona . Hapa anatengeneza kachumbali...HONGERA SANA KWA SIKU YAKO YA KUZALIWA CAMILLA. Duh! siku zinakimbia kweli twamshukuru Mungu kwa kututakia kila jema na kumlinda binti yetu mpaka leo anatimiza miaka 15. AHSANTE KWA MEMA YAKO MWENYEZI MUNGU NA TWAKUOMBE UMPE NAFUU KWANI HII SIKU KAAMKA NA HOMA......

14 comments:

Ester Ulaya said...

Hongera sana Camila kutimiza miaka 15, pia hongera kwa wazazi kumlea vema na kutimiza umri huo..... Mungu azidi kumbariki na kumlinda daima, mimi penda sana wewe Camila

ray njau said...

MAMBO UNAYOWEZA KUFANYA
===========================
Kwanza, tambua kwamba matineja wanahitaji—na hata wanataka sana—kuwekewa mipaka. Kwa hiyo weka sheria, na uhakikishe kwamba kijana wako anazielewa. Kitabu Letting Go With Love and Confidence kinasema hivi, “Vijana wanaobalehe wanapowekewa mipaka iliyo wazi na kutazamia wazazi wawape mwongozo fulani, ni vigumu kwao kujiingiza katika tabia zisizofaa.” Kinyume cha hilo, wazazi ambao huhisi kwamba hakuna uhitaji wa kuweka sheria huwafanya vijana wao wafikiri kwamba wazazi wao hawajali. Na kwa hakika jambo hilo huwafanya waasi.—Kanuni ya Biblia: Methali 29:15.

Unawezaje kuonyesha usawaziko? Acha kijana wako aeleze anavyohisi kuhusu sheria za familia. Kwa mfano, ikiwa anaomba muda aliyowekewa wa kurudi nyumbani urekebishwe, msikilize anapoeleza sababu zake. Huenda ikawa rahisi zaidi kwa tineja kuheshimu na kufuata maamuzi unayofanya—hata kama hakubaliani nayo—ikiwa anahisi kwamba umemsikiliza kwa makini.— Kanuni ya Biblia: Yakobo 1:19.

Hata hivyo, kabla ya kufanya maamuzi kumbuka jambo hili: Matineja huwa na mwelekeo wa kutaka uhuru zaidi kuliko wanavyostahili, na wakati huohuo wazazi huenda wakawa na mwelekeo wa kuwapa matineja uhuru kidogo kuliko wanavyopaswa kuwapa. Kwa hiyo, fikiria kwa uzito ombi la kijana wako. Je, ameonyesha kuwa anaweza kutegemeka? Je, sheria inaweza kubadilishwa kwa sababu ya hali? Inapofaa, uwe tayari kubadilikana kulingana na hali.—Kanuni ya Biblia: Mwanzo 19:17-22.

Mbali na kusikiliza hisia za kijana wako, hakikisha pia yeye anajua mahangaiko yako kumhusu. Kwa kufanya hivyo, unamfundisha kutofikiria mapendezi yake tu bali pia afikirie hisia za wengine.—Kanuni ya Biblia: 1 Wakorintho 10:24.

Mwishowe, fanya uamuzi na ueleze sababu za uamuzi huo. Hata kama hapendezwi na uamuzi huo, yaelekea atafurahi kuwa na wazazi wanaomsikiliza na kutaka kujua maoni yake. Kumbuka, unamfundisha kijana wako anayebalehe kutenda kama mtu mzima. Kwa kumwekea kijana wako sheria zinazofaa na kuzizungumzia pamoja naye, utamsaidia awe mtu mzima mwenye kutegemeka.—Kanuni ya Biblia: Methali 22:6.MAANDIKO MUHIMU
-----------------------

“Usawaziko wenu na ujulikane.” —Wafilipi 4:5.

“Msiwe mkiwakasirisha watoto wenu, ili wasivunjike moyo.”—Wakolosai 3:21.

KWA MATINEJA
--------------------
“Wazia mtu amechukua mkopo katika benki. Akiwa na mazoea ya kulipa kwa wakati, benki itamwamini na inaweza kumpa mkopo mkubwa zaidi siku za usoni. Ndivyo ilivyo na nyumbani. Unapaswa kuwatii wazazi wako. Ukifanya hivyo hata katika mambo madogo, wazazi wako watakuamini hata zaidi wakati ujao. Lakini, ukiwatamausha wazazi wako mara kwa mara, usishangae wakikaza kamba au hata kukuzuilia kabisa.”—Kutoka Kitabu Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2, kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.

Anonymous said...

Hongera sana Camilla, Mungu azidi kukutunza, kukupa afya njema na kukubariki katika maisha yako. Hongera pia wazazi mmaomlea Camilla.

Anonymous said...

Happy birthday Camilla and wish you prosperous future. By Salumu.

Rachel siwa Isaac said...

Hongera sana Camilla...MUNGU azidi kukubariki na kukulinda kila iitwapo Leo..Uwebaraka kwa wazazi na Jamii pia...Akupe Maisha marefu na ufanikishe malengo yako.

Hongereni sana Wazazi/walezi,MUNGU azidi kuwapa Hekima,Busara na Maarifa katika Malezi Yenu.

Mija Shija Sayi said...

Miaka kumi na tano...??? Siku zinaenda sana. Hongera sana Kamila kwa siku yako ya kuzaliwa...

Nataka nifanye uchunguzi nione kama watu waliozaliwa tarehe hii wanafanana tabia, nami wangu kazaliwa mwezi na siku hii..

Hongera tena na tena...Shalo said...

Hongera totoo

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua nafasi hii kwa niaba ya binti Camilla na kuwashuru wote mliojumuika nasi kuisherekea siku ya jana na Mwenyezi Mungu awajalie/awazidishie upendo ili tuweze kuwa pamoja kila litokeapo jema na baya..Upendo Daima...kapulya

John Fisher Kanene said...

Happy Birthday to Camilla as you celebrate 15 years!

Mimi said...

Asante

Sam mbogo said...

safi sana ukiona mwanao anakuwa nakufikisha miaka kama hiyo.mungu azidi kumlinda,nakumuongoza njia sahihi katika maisha yake. nakemea kwa jinaa la aliye ju kwa wale wote wanaoji fanya MAFATAKI WASHINDWE NA WALEGEE. KAKA S

Sam mbogo said...

safi sana ukiona mwanao anakuwa nakufikisha miaka kama hiyo.mungu azidi kumlinda,nakumuongoza njia sahihi katika maisha yake. nakemea kwa jinaa la aliye ju kwa wale wote wanaoji fanya MAFATAKI WASHINDWE NA WALEGEE. KAKA S

Rachel siwa Isaac said...

Ameen. .kaka.S

Mbele said...

Hongera sana, binti. Mungu akujalie maisha ya mafanikio tele.