Tuesday, March 31, 2015

TUMALIZE MWEZI HUU WA TATU NA PICHA HII:- NIMEPENDEZA EEHH!!

Ubonifu huo..hahaaa si unaona nilivyopendeza eeehh! Watoto ni wabunifu sana ..Mwisho wa mwezi uwe mwema kwa wote na kumbuka kesho usidanganywe..

Monday, March 30, 2015

TUANZE JUMATATU HIII/WIKI HII NA UJUMBE HUU!!

"Mafanikio makubwa katika maisha sio kutoa anguka bali ni kuinika kila unapoanguka"
- Nelson Mandela

Saturday, March 28, 2015

HUKIFIKA FORODHANI HUJAFIKA ZANZIBAR...

Kama uonavyo hapo nilifika zanzibar mwaka huu na nikatembelea Forodhani ni sehemu nzuri sana sana..usikose kupitia ukiwa Zanzibar
Angalia panavyoonekana... haya tutaonana tena mwaka mwingine Zanzibar Forodhani...Kapulya!

Friday, March 27, 2015

FUATANA NAMI MPAKA MTO RUAHA / MBUGA YA WANYAMA

TUMALIZE WIKI HAPA RUAHA..PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA ...KAPULYA

Wednesday, March 25, 2015

UTANI KIDOGO- MLEVI NA MCHUNGAJI WAMEKUTANA!!

Ungana nami na utani huu nimeona si vizuri kupata elimu hii peke yangu ...nimetumiwa na msomaji wa Maisha na Mafanikio. KARIBU.....


MCHUNGAJI; "Unakunywa bia!?      
MLEVI; "Ndio.
MCHUNGAJI; "Kwa siku unakunywa bia ngapi!?
MLEVI; "Nakunywa bia tano!
MCHUNGAJI; "Bia moja bei gani!?
MLEVU; "2500/
MCHUNGAJI; "Ulianza lini kunywa bia!?
MLEVI; "Miaka 18 iliyopita!
MCHUNGAJI; "Kwa hiyo kwa siku unatumia zaidi ya 10,000??
MLEVI; "Ndio!
MCHUNGAJI; "Kama u gekuwa unatunza hiyo pesa 10,000 kwa siku leo hii si ungekuwa na Range Rover!?
MLEVI; "Samahani, naweza kukuuliza swali!?
MCHUNGAJI; "Uliza!
MLEVI; "Unakunywa bia!?
MCHUNGAJI; "Hapana!
MLEVI; "Nionyeshe Range Rover yako!
MCHUNGAJI; "Akakimbia.....

Monday, March 23, 2015

KUMBUKUMBU.....LEO NI MIAKA MINNE TANGU MPENDWA WETU ASIFIWE NGONYANI ATUTOKE!!

 
 ASIFIWE WAKATI WA UHAI WAKE 
 Ni vigumu kuisahau tarehe 23/3/ 2011, siku hii ndiyo tuliyompoteza mpendwa wetu Asifiwe Ngonyani. Na leo imetimia miaka minne tangu ndugu yetu mpendwa Asifiwe atutoke. MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA. AMINA.....TUTAKUKUMBUKA MILELE....

Saturday, March 21, 2015

PICHA YA WIKI...NIMEYAPENDA MAZINGIRA YAKE

Mazingira ya picha hii nimeyapenda sana yananikumbusha hapo kele kule kwetu Kingole na Litumbandyosi. NAWATAKIENI JUMAMOSI NJEMA SANA. UJUMBE:- TUPENDANE!!

Friday, March 20, 2015

CHEKA UNENEPE: KUTANA NA MUUZA SAMAKI MKOROFI NA MTEJA MWENYE MASWALI!!

MTEJA; Samaki bei gan?
MUUZAJI; 5000!
MTEJA; Mwisho?
MUUZAJI; Mkiani!
MTEJA; Mbona samaki mwenyewe kalegea hivyo?
MUUZAJI; Muulize labda alikuwa shoga baharini!  
MTEJA;M bona una majibu ya shombo lakini?  
MUUZAJI; Kwasababu nauza samaki ingekua nauza sukari majibu yangekua matamuu.
NAWATAKIENI WOTE IJUMAA NJEMA!!

Wednesday, March 18, 2015

PALE LUGHA ZINAPOPIGA CHENGA...

Nimetumiwa hii na sikuweza kubaki nayo peke yangu nikaona ni iweka hapa ili na wenzangu muone jinsi watu  wanavyoweza kucheza na lugha----haya karibu uvunje mbavu!!!
----------------------------------------------------------------------
Mbena mmoja alifika Dar, nyumba aliyofikia akasikia mke na mume wanaitana Darling.. Jamaa aliporudi Njombe akamwita mkewe hello my Njombeling.. Mke akamuuliza maana yake nn? Mume akacheka tena kwa zarau sana akamwambia ushamba mwingine bwana tembea uyaone ukiwa Dar unaitwa Darling sasa ukiwa Njombe unafikiri utaitwaje kama si Njombeling.
PAMOJA DAIMA! PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA!!

Tuesday, March 17, 2015

NAJIVUNIA MALIASILI YETU

Angalia jinsi wanavyopendeza lakini inasikitisha kuona/kusikia asilimia kubwa ya wanyama pori imeteketea hakuna Tembo au wanyama wengu wa kutosha katika Mbuga kama hapo kale.

Sunday, March 15, 2015

SALA YA LEO...AMBAYO IMETUNGWA NA KAPULYA WENU.

Mwenyezi Mungu ! Sikuombi uyafanya maisha yangu yawe rahisi, isipokuwa nakuomba unipe nguvu za kukutana na shida zote.Amina

Saturday, March 14, 2015

JUMAMOSI NJEMA KWA WOTE UKIPATA MUDA SIKILIZA UJUMBE HUU!

UJUMBE WAA LEO: SISI SOTE NI NDUGU NA NI WATOTO WA BABA MMOJA!!

Friday, March 13, 2015

Thursday, March 12, 2015

TUSAIDIANE KUDUMISHA NYIMBO/MIZIKI YETU YA ASILI ...LEO TUPO UHEHENI NA KAKA RIZIKI MSOLA...

Leo twende UHEHENI tumsikilize kaka Riziki Msola wimbo huu uitwao TWILUMBA na nyingine nyingi utazikuta YOUTUBE haya karibuni..... Riziki Msola ni mwanamuziki mwenyeji wa Iringa anayechipukia katika tasnia ya muziki wa asili nchini Tanzania.Amekuja hewani na nyimbo za Kihehe ijapokuwa hajaweza kukamilisha video yake kutokana na ukosefu wa fedha. Tafadhali sana wapenzi na wafadhili wa utamaduni wa mtanzania jitokezeni ili ubunifu wa Rikizi ukamilike. Wasiliana naye kwa namba hii hapa chini. +255 759 523785 KILA LA KHERI PANAPO MAJARIWA TUTAONANA TENA !

Tuesday, March 10, 2015

MWANAMKE UNATAKIWA KUJITAMBUA!

Leo au niseme wiki hii katika pita pita zangu nimekutana na hii mada kwa dada Adela Kavishe nikaona si mbaya isambae haya karibu uungane nami.... Kila mtu anaweza kuwa na majibu tofauti pale anapoulizwa uzuri wa mwanamke ni nini? kuna atakayesema uzuri wa mwanamke ni muonekano wake, yaani umbo lake zuri la kuvutia, sura yake, miguu nk, lakini pia yupo atakayesema uzuri wa mwanamke ni kuwa na tabia nzuri ama uzuri wa mwanamke ni kujituma na kufanya kazi kwa bidii. Majibu yote yanaweza kuwa na mtazamo tofauti, lakini ukimfikiria mwanamke mzuri ni yule ambaye anajitambua na kufahamu umuhimu wake katika jamii, mwanamke mzuri ni zaidi ya urembo wa sura yake, ama muonekano wake kumbuka sura nzuri haiwezi kudumu milele, kwani kuna siku itachoka na kuzeeka, muonekano wa mwili na wenyewe hubadilika siku zinavyozidi kwenda hata kama ufanye nini lakini mabadiliko katika mwili ni sehemu ya maisha ya binadamu, ila mwanamke ambaye ni mzuri kutokana na tabia yake, yaani mzuri kutoka moyoni siku zote atabaki kuwa mzuri haijalishi mabadiliko ya muonekano wake. Mwanamke mzuri ni mwanamke anayemjua Mungu na anaishi akiwa na hofu ya Mungu, vilevile ni mvumilivu, mpole, na anayejua kuishi na watu mbalimbali wanaomzunguka katika maisha yake. Mwanamke mzuri sikuzote anajikubali katika hali yoyote iwe ni katika shida au raha, siyo muongo ni mkweli katika maisha yake na wakati wote anasimamia ukweli bila kuwa na hofu. Mwanamke mzuri hatakiwi kuwa na hasira ijapokuwa ni kitu ambaocho kipo katika maisha yetu. Inapotokea unajiona umekereka na una hasira sana ni vyema ukajua namna ya kuzuia hisia zako ili usikurupuke kuchukua maamuzi ambayo yataleta madhara katika maisha yako, kumbuka kutafakari kila jambo kabla ya kuchukua maamuzi, Katika maisha ya mahusiano unaambiwa mwanamke mzuri sikuzote huijenga familia yake, na vilevile mwanaume yeyote ambaye unamuona anamafanikio katika maisha yake basi ujue kuna mwanamke mzuri ambaye amechangia kuwepo maendeleo hayo. Mwanamke mzuri akipenda basi atakupenda kutoka moyoni lakini mwanamke mwenye tabia mbaya akikupenda utaona matokeo yake kwani migogoro itakuwa haishi hususani kama akiwa amekupenda kwasababu ya mali zako siku zikiiisha hawezi kuvumilia ila mwanamke mzuri atakuvumilia katika shida na raha. Mwanamke mzuri anamvutia mwanaume mzuri, ijapokuwa wakati mwingine mwanamke mzuri anaweza kukutana na mwanaume mwenye tabia mbaya, na akavumilia, ila inapofikia wakati mwanaume huyo akazidisha manyanyaso kwa mwanamke huyu basi inampelekea kukakata tamaa na mwisho kulivua pendo, ukipata mwanamke mzuri katika maisha yako usichezee bahati muheshimu sana, na maisha yenu yatakuwa na furaha milele. Mwanamke mzuri sikuzote anatafutwa na mwanaume aliye mzuri, na siyo yeye anamtafuta mwanaume.Mwanamke mzuri sikuzote anawaza mambo mazuri, ikiwa ni pamoja na mafanikio katika maisha kwa njia ya kujituma na kuwa mbunifu huku akifanya kazi kwa bidii kufikia malengo yake, Mwanamke mzuri siyo mbinafsi, atawasaidia na kuwashauri wanaohitaji msaada kutoka kwake kulingana na uwezo alionao mwanamke mzuri ana huruma na anafurahia mafanikio ya wenzake. Ili kuwa mwanamke mzuri unahitaji kujitambua na kuwa na hofu ya Mungu atakusaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali ambazo unaweza kukutana nazo katika safari ya maisha. Unaambiwa hakuna binadamu aliyekamilika lakini hakuna linaloshindikana kwa Mungu hata pale tunapokosea tunapiga magoti nakuomba msamaha na Mungu anatusamehe mara saba sabini, kisha maisha yanaendelea jambo la msingi ni kutambua kosa na kuwa makini usirudie kosa. katika maisha furaha ni jambo la msingi sana na ili kuwa mzuri sikuzote ni vyema ukaitafuta furaha kwa kuishi vizuri na watu wanaokuzunguka, usiwe mtu mwenye visasi, hasira,majungu, ubinafsi, chuki, choyo na mambo mengine kama hayo Mwanamke mzuri unatakiwa kuwa na upendo kwa watu wote.UJUMBE NA ADELA KAVISHE.... HAPPY WOMEN'S DAY Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani huadhimishwa kila mwaka nchini tarehe nane mwezi wa tatu. Mwaka huu kitaifa yanafanyika mkoani Morogoro yakiwa na Kauli Mbiu “Uwezashaji Wanawake, Tekeleza Sasa.” KILA LA KHERI!!

Monday, March 9, 2015

TUANZE JUMATATU NA PICHA HII...

Harusi si lazima iwe kuuuubwa hata kwa baiskeli inawezekana. JUMATATU NJEMA!

Saturday, March 7, 2015

NIMETUMIWA ZAWADI KUTOKA NYUMBANI ....

 
 Nimewahi kuona hizi soda na majina lakini sikuwahi kuona jina langu na pia ubini/jina la ukoo wangu. Nimeipenda sana hii zawadi ingawa si mpenzi wa soda. AHSANTE SANA  KWA ZAWADI. JUMAMOSI NJEMA KWA WOTE!!!

Friday, March 6, 2015

UKIPATA WASAA EBU WASIKILIZENI HAWA VIJANA NA WIMBO WAO SHUKURANI.....


Nimeusikiliza  hawa vijana maneno yao nimeyapenda sana. Kwa kweli inabidi kumshukuru Mungu kwa lolote ufanyalo ana pia kumshukuru kwa wewe kuwa wewe. Binafsi nawatakieni Dogo Muu ft. Aslay waifikie ndoto yao.

Wednesday, March 4, 2015

LEO TUANGALIA ZAO LA KARANGA

 Mmea wa karanga punde utakapo kuvunwa
 Karanga baada ya mavuno zimekauka  tayari
Ulijua ya kuwa nchi ilimayo karanga  ni CHINA? Basi Chini huta asilima 41,5%  Na inayofuatia ni India na asilimia 18,2%. Kwa mabara ya Ulaya ni Ugiriki ambayo hutoa  kwa wastani tani  2000 za karanga kwa mwaka. 
Na inasemekana karanga chanzo chake ni Amerika kusini katika nchi ya Peru. Na kwamba karanga  ambazo zipo leo sio za pori 
Mmmmhh! mimi katika mawazo yangu nilifikiri karanga asili yake Afrika na zinalimwa zaidi Afrika. Ama kweli kujua kusoma naona furaha/kuperuzi peruzi...ni muhimu nikaona sio mbaya nikiwajuza na mwenzangu. 
Chanzo:-ILLUSTRERAL VETENSKAP

Monday, March 2, 2015

JUMATATU HII YA KWANZA TUANZE NA KUKARIBISHANA CHAKULA CHA MCHANA ...

Ni chakaula ambacho akipendacho sana Kapulya/dada mkuu...ni ugali samaki, maharagwe, na mbogamboga...KARIBUNI TUJUMUIKE:-