Wednesday, March 18, 2015

PALE LUGHA ZINAPOPIGA CHENGA...

Nimetumiwa hii na sikuweza kubaki nayo peke yangu nikaona ni iweka hapa ili na wenzangu muone jinsi watu  wanavyoweza kucheza na lugha----haya karibu uvunje mbavu!!!
----------------------------------------------------------------------
Mbena mmoja alifika Dar, nyumba aliyofikia akasikia mke na mume wanaitana Darling.. Jamaa aliporudi Njombe akamwita mkewe hello my Njombeling.. Mke akamuuliza maana yake nn? Mume akacheka tena kwa zarau sana akamwambia ushamba mwingine bwana tembea uyaone ukiwa Dar unaitwa Darling sasa ukiwa Njombe unafikiri utaitwaje kama si Njombeling.
PAMOJA DAIMA! PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA!!

2 comments:

Anonymous said...

Hahahah nimecheka sana. Haya mambo ya njombeling.

Yasinta Ngonyani said...

Usiye na jina wa 1:38! Basi tupo wengi tuliocheka ... sijui aliwaza nini?:-)