Monday, December 21, 2020

UJUMBE WA LEO

ISHI NA WATU VIZURI SIKU HIZI DAMU SIO NZITO TENA! Nawatakieni siku njema!

Thursday, November 26, 2020

Sunday, November 8, 2020

MWENZENU LEO NIMETAMANI MNO MLO HUU VITUMBUA....NIWATAKIENI JUMAPILI NJEMA!

JUMAPILI NJEMA SANA NDUGU ZANGU KUMBUKENI SISI SOTE NI WATOTO WA BABA MMOJA.

Monday, October 26, 2020

TUFANYA HII IWE PICHA YA WIKI HII...SEHEMU FULANI TANZANIA

Nimeipenda hii mandhari nzuri ..kuingalia tu yavutia. Kwa hiyo nafikiria je nikiwa/ukiwa hapo iitakuwaje...mmhh nawaza tu kwa sauti! TUPO PAMOJA DAIMA!
 

Friday, October 2, 2020

NAPENDA KUWATAKIENI MWISHO MWEMA WA JUMA NA MWANZO MWEMA WA MWEZI HUU WA KUMI KWA BURUDANI HII

 <iframe width="560" height="315" src="https://www.youtube.com/embed/amL_MTCsOms" frameborder="0" allow="accelerometer; autoplay; clipboard-write; encrypted-media; gyroscope; picture-in-picture" allowfullscreen></iframe>

MWISHO WA JUMA UWE MWENYE AMANI NA FURAHA KWETU WOTE. TUSISAHAU KUWAOMBEA WAGONJWA  WETU...

Friday, September 4, 2020

HII NI PICHA YA WIKI :- HAPA NIPO NA MARAFIKI TUPO SHAMBANI KWA WAKULIMA KUNUNUA MBOGAMBOGA BILA KUSAHAU MAHINDI

 

Nadhani hapo mwamuona kapulya wenu ... msione tumevaa makoto baridi imeanza 
Hapa kapulya anashangaa mmea fulani ni raha sana kuwenda shambani na kuchuma mbogamboga na mkulima kazi yake ni kupanga bei tu...:-)

Saturday, August 29, 2020

JUMAMOSI YA LEO NIMETAMANI SANA UGALI NA KISAMVU...

Tatizo sijui wapi kupata kisamvu ...ila unga ninao. Mhhhh 
 

Sunday, August 16, 2020

ZILIPENDWA...MIAKA HIYOOOO HUKO MATETEREKA /WILIMA

 AMA KWELI LEO NIMEKUMBUKA MBALI SANA ...WATU TUMETOKA MBALI

Sunday, July 12, 2020

PALE UNAOKOSA SEHEMU YA KULIMA MBOGA MBOGA/BUSTANI USIKATE TAMAA TUMIA NDOO AU MAKOPO KAMA NILIVYOFANYA MIMI HAPA

Hapa ni Nyanya, mchicha, Tangawizi  Malimao, parachichi nk. Karibu tutaanza kula nyana mchicha nishakula mara nyingi tu

Friday, July 3, 2020

MWAMKUMBUKA HUY?


MWAMFAHA MU HYUYU DAAD
  • ZILIENDWA

Saturday, June 20, 2020

JIONI YA JUMAMOSI YALEONIMEONA SI MBAYA KAMA TUKITEMBELEA KWETU MBAMBA BAY

Angalia mandhari ilivyo nadhani ukiwa hapa hutataka kutoka maana ni fukwe nzuri sana. Niwatakieni JIONI YA JUMAMOSI HII IWE YENYE UTULIVU MWANANA. Wenu Kapulya!

Sunday, June 14, 2020

FAMILIA MBILI ZINAPOKUTANA KWA CHAKULA CHA USIKU

Ilikuwa jana 13 /6 kijana Erik kamaliza kozi yake ya jeshi .....

Wednesday, June 3, 2020

NAPENDA MAUA....NA SASA NDIO MSIMU WAKE

Nawatakieni  Jumatano hii iwe yenye furaha na amani

Monday, May 25, 2020

USAFIRI WETU...AKINA MAMA TUNAWEZA

Nimeona tuanza wiki hii kinamna hii  maana nadhani leo hap ni siku ya akina mama...kwa hiyo napenda pia kuwapa shukrani akina mama wote. Tuzidishe uaminifu maana ndiyo nguzo ya mafanikio.

Friday, May 8, 2020

LEO NIMESHINDA NATAMANI HIVV VYAKULA MAANA NDIVYO VILIVYONIKUZA

Hapa ni mahindi ya kuchoma eeeh bwana weee acha tu 
Dagaa  na mboga maboga ni mboga tamu sana...
.....na bila kusahau ugali yaani natamani khali ya hewa iwe joto ili nianza kulima mbogamboga zangu

Thursday, April 16, 2020

NIMETUMIWA ZAWADI KUTOKA KWA KAKA YANGU ...KUTOKA MBINGA

Yaani mpaka raha .....utakula ulivyopanda... hii ni kazi ya mikono ya kakangu Philo huko Mbinga ni ndizi kama muuonavyo kwenye picha
pia kuna matunda ya passion
Karibuni sana kwetu Mbinga chakula kwa kwingi ...au sisi wangoni twasema chakula bwelele...

Monday, April 13, 2020

LEO TUTEMBELEE MBAMBA BAY......

Hapa ni ukumbi wa starehe hapa Mbamba bay kwetu...karibuni 

Tuesday, April 7, 2020

Saturday, March 28, 2020

TUMALIZE NA HII WIKI TUKIWA TUKITEMBELEA MAZINGIRA YA MAKAZI YANGU/YETU HAPO BAADAYE


HAPA NI BAADHI YA MINAZI  YASEMEKANA NI MINAZI YA KISASA KWA HIYO KARIBUNI TUTAKULA NAZI:-) 
HAPA NI NDIZI ...SI MWAJUA TENA BILA NDIZI SIJIWEZI KABISA

Na hapa ni baadhi ya miti ya  MiPARACHICHI ...picha nyingine zaja karibuni....

Monday, March 16, 2020

TUANZE WIKI HII NA PICHA HII:- IWE PICHA YA WIKI

Nimepemda haya mazingira imenikumbusha niliokuwa msichana mdogo kule kwetu KINGOLE/LITUMBANDYÒS  wakati nilipokuwa naenda kisimani kuteka maji. Je? wewe una kumbukumbu kama hii? 

Friday, March 6, 2020

PICHA: MDADA YUPO KATIKA POZI LA KUSHUKA NGAZI!


Wiki moja iliyopita nilikuwa nimejificha sehemu fulani ili kupumzisha akili na hii ni moja ya picha nilizopiga. Napenda kuwatakieni mwisho mwema wa wiki:-) kapulya wenu.

Wednesday, March 4, 2020

VYAKULA NIPENDAVYO KULA NIWAPO HASA SEHEMU ZA BAHARI YA CHUMVI

SAMAKI NA VIAZI VYA KUPONDA
KAMBA KWA MKATE
CHAKULA CHA KIKUU CHA UISPANIA PAELLA NI WALI WA BINZARI NA KARIBU AINA ZOTE ZA SAMAKI
SAMAKI WA KUCHOMA NA AINA YA KACHUMBALI
KAMBA
SAMAKI WA KUCHOMA TENA NA VIAZI MAALUMU VYA  KILE KISIWA PIA SALADI KIDOGO.

Friday, February 21, 2020

LEO NIMEONA TUTEMBELEE MBEYA YETU

Nimependa hii mandhari ..Hapa ni Mbeya . Basi mimi niwatakieni mwisho mwema wa juma kwa picha hii kwa yeyote atakayepita hapa na pia hata kama utasikia . Tupo pamoja Daima. Kapulya wenu!

Thursday, February 13, 2020

PICHA;.- HII ITAKUWA NI MPAPAI AU MATTIKITI MAJI?

Hii picha na iwe picha ya wiki maana nimeshindwa kabisa kujua kama ni matikiti maji au papai! naomba msaada wenu ndugu zangu

Thursday, January 30, 2020

PICHA ZA SIKU...NAWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA SIKU NJEMA


Nawatakieni wote furaha na amani kwa siku ya leo . Tupo pamoja daima Kapyula wenu!

Tuesday, January 28, 2020

NI MANDHARI NILITOKEA KUIPENDA SANA:- NA NDIO MAANA NIMEONA IWE NI PICHA YA WIKI

Kama nilivyosema ni mandhari nzuri sana ambayo nimetokea  kuipenda mno. Je? wewe ndugu yangu wasemaje?. Pamoja Daima!

Tuesday, January 21, 2020

HISTORIA:- VITA KATI YA WANGONI NA WAMATENGO.....

Kabila la Wamatengo ni Kabila la Asili, halijaundwa kwa kutokana na makabila mengi yaliyochanganyika kama ilivyokuwa kwa kabila la Wangoni, ndio maana hata lugha yake haijaathiriwa na lugha zingine kwa kiasi kikubwa.

Ni makabila machache tu yaliyotoka katika koo nyingine ukoo wa akina KAPINGA, KOMBA (Hanze), MAPUNDA na LUANDA; ni koo ambazo ziliingia kutoka upangwa. Vile vile koo kama akina NDIMBO na NCHIMBI zilitoka Magharibi ya pwani ya ZIWA NYASA. Koo hizi ambazo zilitoka nje hazikuleta athari katika lugha ya kimatengo, ukizingatia kuwa koo hizo zilikuwa chache kiidadi kuliko wenyeji wa asili ya nchi ya UMATENGO.

MAKITA KAYUNI wa ukoo wa akina NDUNGURU ambaye ni Babu kati ya watawala waliokuwa machifu katika nchi ya Umatengo mwishoni inasadikika kuwa, kwa asili alitoka kabila la WANINDi, aliishi chini ya mlima Matogoro karibu na Songea.

Alipoingia MPUTA MASEKO katika nchi ya Ungoni. MAKITA KAYUNI alishindwa kupigana naye akasalimisha jeshi lake kisha akajiunga naye na akapata fursa ya kujifunza mbinu za kivita.

Kayuni alijipatia uhuru wa kufanya chochote na kwenda kokote alikotaka baada ya Mputa Maseko kufukuzwa katika Wilaya ya Songea, akaamua kuhamia katika nchi ya umatengo huko LITEMBO ambako alipokelewa kwa ukarimu mkubwa mno na KAWANILA HYERA pamoja na LIHUHU KINUNDA.

Kayuni alikuwa na ufundi katika masuala vita pamoja na akili ya maisha, watu wa Litembo (Wamatengo) waliona anafaa kuwa kiongozi; alipokufa Kawamila bwana Makita alichaguliwa kuwa mrithi wake.

Baba wa Kayuni Mzee Kapitingana alifika Litembo na kuweka makazi yake; licha ya kwamba Kayuni hakuishi Litembo maisha yake yote lakini alizaliwa katika ardhi ya Litembo kwa Ndenya Ndunguru. Kayuni alipewa jina la ukoo wa Mama yake kwa kuwa Baba yake Mzee Kapitingana hakulipa Mahari.

Familia ya Makita kipindi cha Mputa Maseko (1864 -1865)
Ukoo wa Babu, Baba, Makita na Familia yake waliishi Litembo, familia ya Makita ilifika Litembo baada ya Mputa Maseko kuikimbia Songea mwaka 1864s.

Inaelezwa mwaka 1866s Kayuni alipata bahati ya kuzaliwa; hivyo kuna uhakika kwamba Makita Kayuni aliuawa akiwa na umri mkubwa kwenye vita ya mwisho kati ya Wangoni na Wamatengo ambayo ilikuwa miaka minne kabla ya kifo cha Nkosi Mharule kilichotokea mwaka 1885.

MAKAZI YA WAMATENGO NA TAKWIMU ZAO KABLA YA WANGONI KUJA SONGEA

Kabla ya Wangoni kuja Songea na kujenga Makazi yao, Wamatengo waliishi katika vijiji ambavyo vilitengana tengana au kutawanyika (Musi musi) kama vile Litembo, Mapera, Ungima (Ngima), Hanga, Kitogota, Kimati, Nkuka, Ungwindi, Baruma, Matiri (karibu na Milima ya Lilengalenga).

Wamatengo walipata shida sana kulinda Miji yao dhidi ya vita ya Wangoni walipoelekea umatengoni ili kufanya makazi yao. Kundi kubwa la watu wailishi katika Bonde la Litembo.

Mwandishi Fullborn amefafanua kwamba, kijiji cha Makita kilikuwa na watu 5,000 kwa mujibu wa Sensa iliyofanywa na Wajerumani mwaka 1904 huku idadi kubwa ya watu ikitoka katika bonde la Litembo katika eneo la Makita, suala ambalo lilipelekea ulinzi kuwa mdogo wakati wa vita.

Wageni waliobahati kutembelea katika kijiji cha Makita wanafafanua kwamba mitetemeko yote inayohusiana na milima ya Litembo ilijengwa vibanda, mapango katika milima ya Litembo yalitumika kwa ajili ya kujificha wakati wa vita. Bro. Laurentius Brenner aliyapima baadhi ya mapango mwaka 1906 na akaandika mambo muhimu aliyoyabaini.

“Wamatengo wengi wanaishi katika mapango. Sehemu zingine katika hivi vibanda havionyeshi kama wanaishi watu, lakini wanaishi pale, inaonekana miamba mikubwa ndio nyumba zao.
Inavyotokea wazungu wanajitokeza kwao hujificha kwenye miamba hiyo; katika baadhi ya mapango hakuna anayeweza kuingia akiwa wima, nililiona pango mojawapo liliokandikwa kwa udongo ambalo lilijazwa kuni pande zote”
“Ni jambo la kushangaza pango hilo lilikuwa na kina cha mita mbili hadi tatu, hadi kukifikia chumba kulikuwa na ngazi zilizoelekea katika eneo la kuchota maji. Hata hivyo palikuwepo na mapango mengine ambayo haikuwa rahisi kuona mlango wa kuingilia, ila shimo dogo la kutokea moshi lilionekana”
“Mapango mengine yana kina lakini hayaruhusu mwanga wa jua kuingia wala kupenya, inaonekana watu huyatumia wakati wa usiku tu! kuna baadhi ya mapango yana mlango wa pili ambao ni ngumu mno kuuona kwa macho, uenda unatumika wakati wa hatari tu!” alisema Brenner.

Kama si Mapango Wamatengo wangeteketezwa na Wangoni
Hata katika kipindi cha Mputa Maseko na hawaya Wangoni walifanya mashambulizi ya kivita dhidi ya kabila la Wamatengo na kuteka mali za Wamatengo na mifugo yao.

Wamatengo walipoamua kuishi katika bonde la Litembo jeshi la Wangoni lilipata shida mno wakati wa mapambano mara nyingi walirudi ungonini bila kutekeleza mipango yao ya kuwasambaratisha Wamatengo.

Vita ya maana yenye kukumbukwa ni ile iliyotokea mwaka 1885 ambayo ilikuwa ni vita ya mwisho kati yao. Makita alishauriwa na baadhi ya watu kwamba amdharau Nkosi Mharule na kutuma baadhi ya watu wakachukue aina ya nyasi ziitwazo ‘Sekela” ili kuzungushia wigo kwenye vibanda vyake.

Kitendo ambacho kilimfanya chifu Mharule achukie kwa kudharauliwa na Makita na hivyo akaenda umatengoni kupambana nao. Inaelezwa kwamba Mfanyabiashara Litunu alitumwa umatengoni, alipita katika ardhi ya wamatengo kuelekea Ziwa Nyasa, inasadikia njiani alishambuliwa na watu ambao iliilezwa walikuwa ni Wamatengo.

Kutokana na kupea kwa urafiki kati ya Litunu pamoja na Mharule hivyo hata biashara zake zilikuwa chini ya utawala wa Nkosi Mharule, hivyo Mharule alipata sababu za kuwapiga Wamatengo na wakati huo alikuwa amehamia sehemu iitwayo karibu na Matomondo kwenye barabara inayoelekea Mbambabay.

Kuuawa kwa Makita katika vita baina ya Wangoni na Wamatengo
Manduna wa Kingoni walioshiriki kwenda kupiga vita hiyo katika nchi ya Wamatengo ni pamoja na Nduna Songea, Sanangula, Mpangile, Chikuse na wengine. Wakati wa vita hiyo Makita mwenyewe alisimama juu ya mwamba mkubwa ili kuwapa moyo Askari wa Kimatengo.

Wakati vita ilipokuwa imepamba moto katika vijiji mbali mbali mke wa Makita alikuwa na mume wake muda wote juu ya mwamba huku akimwaga dawa ya vita toka kwenye kikapu chake na kumtia moyo ili Wamatengo waweze kushinda katika vita ambayo ilidumu kwa muda mrefu bila kufikia ukomo.

Askari wa kingoni kwa kutumia bunduki yake alimtungua Makita akiwa juu ya Mwambo huo kisha akadongoka na kupoteza maisha pale pale, tukio hilo lilipelekea Askari wa makita kujisalimisha mikononi mwa Askari wa Kingoni na wakajitangazia ushindi na wakafanya sherehe.

Wangoni walirudi katika ardhi yao huku wakiwa na Mateka mengi pamoja na mali zao, baadhi ya waliotekwa ni Makita Ndunguru ndugu yake Makita Kayuni ambaye alitekwa na watu wa Sanangula; lakini baada ya kuwasili huko Sanangula aliteuliwa kuwa kiongozi wa Wamatengo wa Sanangula.

Mtoto mkubwa wa Makita Kayuni alirithi kiti cha Baba yake na akatawala nchi ya Wamatengo kwa mika mingi, mwaka 1897 wakati wa utawala wa Mandawa Wajerumani walifika Songea.

Machi 1902 Wamatengo waliwaasi Wajerumani na wakakataa kulipa kodi kwenye serikali ya Kijerumani na wakachoma moto shule ya msingi Litembo ambayo ilianzishwa na Padre Yohannes Hafliger wa Kigonsera tarehe 11-9-1901.

Kitendo hicho kiliisha mara moja wakati wa utawala wa Mandawa na baadaye alimwachia madaraka mdogo wake Mtwara ili kumpa heshima ambaye naye aliitawala umatengo yote. Vita ya Maji Maji ilipoingia umatengoni hawakupenda kushirikiana na Wangoni ambao ni maadui zao wa zamani ili kuwapiga wajerumani.

Kufuatia kifo cha Mtwara, cheo chake kilichukuliwa na Tekambwani mtoto mwingine wa Makita Kayuni, ambaye alifariki baada ya kutawala kwa kipindi kifupi. Watoto wengine wa Makita Kayuni waliikosa fursa ya kuitawala nchi ya umatengo kwa kuwa walikuwa wadogo mno hivyo wazee wa kimatengo wakamchagua Kapungu na akawa chifu wao.

Mwaka 1916, Waingereza walipoichukua Tanganyika na kuitawala kwa mabavu, Kapungu aliondolewa madarakani kisha akawekwa Makita Kipwele Kayuni mtoto wa mtoto wa Makita Kayuni wa I.

Baadaye alilithiwa na Magnus b. Bunungu na baadaye Mrithi wake akawa Yohannes Christomus Makita Kayuni, jina la Makita kutoka Makita Kayuni II Kipwele.

Sunday, January 19, 2020

KUMBUKUMBU:- JUMAPILI HII YA TATU TANGU MWAKA UANZE NIMETAMANI SANA CHAKULA NINACHOKIPENDA NA KILICHONIKUZA


Chakula nikipendacho chaitwa likungu hupatikana hasa kando kando ya ziwa  nimekula sana wakati naishi ziwa nyasa 

na hapa ni kumbikumbi  kama hujaonja basi jitahidi uonje ni watamu sana

Friday, January 10, 2020

HIZI PICHA NIMETUMIWA NA KAKA YANGU AISHIYE ZANZIBAR HAPA NI MAKAZI YAKE MAPYA YAANI MPAKA RAHA

Angalia mapapai yalivyojipanga.....  
...na muda si mrefu ndizi zitakuwa tayari kwa kuliwa ...ukiangalia kwa mbali hapo ardhini utaona aina za ambogamboga...aahhh mate yanachuruzika
na  hapa ni baadhi ya mahindi na mbogamboga tena
ooohh hapa nimekumbuka Matetereka.....Magimbi...hii ndo mtu unaweza ukaiita kazi ya mikono binafsi ila walaji tupo wengu. Tupo njiani;.)

Monday, January 6, 2020

JANA JUMAPILI 5/1 ILIKUWA KUMBUKUMBU YANGU YA KUZALIWA...NAMSHUKURU MUNGU KWA KUNILINDA NA KUUONA MWAKA MWINGINE TENA!

 Jana tarehe 5/1/2020 mdada huyu ilikuwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.
Na hapa ni zawadi alizozawadiwa na famili pia marafiki zake. Bila kusahau kikombe cha chai 
Kwa vile ni msimu wa baridi nimepata zawadi ya kofia pia...
Muda wa chakula ulipofika...kwanza ni  LOBSTER  ambayo ina viungu vya asili na kitunguu saumu



Na mlo mkuu ulikuwa ni chakula kikuu cha KAPULYA ni SAMAKI ...kwa viazi  maalumu.
NAPENDA KUMSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWA YOTE .