Showing posts with label UJUMBE WA WIKI. Show all posts
Showing posts with label UJUMBE WA WIKI. Show all posts
Saturday, August 20, 2022
TUMAZE WIKI NA UJUMBE HUU!
NIMETUMIWA HUU UJUMBE NIMEONA NISIWE MCHOYO WA ELIMU:-
Nyoka uliyembeba kwenye mzigo wa kuni kutoka shambani anaweza kukuumia nyumbani wakati unatua mzigo. Siyo kila unayemsaidia lazima akusaidie, wengine inabidi wakuumize ili ujifunze. Kuna watu wanajifunza vizuri baada ya kuumizwa. Kwa hiyo katika maisha tunahitaji watu wote; wazuri na wabaya. Wazuri watakupa furaha, wabaya watakupa uzoefu ndiyo maana imeandikwa mpende adui yako, ila angalia asikuue, maana ukifa hutojifunza kitu!
Imeandikwa na Mwl. Denis Mpagaze.
Monday, October 23, 2017
JUMATATU HII TUANZE NA UJUMBE HUU....
NI VIZURI KUSAHAU JAMBO LILILO UMIZA MOYO WAKO. LAKINI NI VIZURI KUKUMBUKA ULICHOJIFUNZA KATIKA JAMBO HILO.
NAWATAKIENI JUMA JEMA
NAWATAKIENI JUMA JEMA
Wednesday, May 24, 2017
UJUMBE WA WIKI HII: MAISHA HAYAMTAMBULISHI MTU KWA WATU....
Maisha hayamtambulishi mtu kwa watu atakaokukutana nao. Kuna wakati, maisha yaweza kukukutanisha na watu ambao uliwahitaji/unawahitaji kukutana nao ili wakupe msaada, ili wakuumize, ili wakuongoze, ili wakuache mpweke, ili wakupende na ili wakupe/wakutie nguvu katika hatua ya kukuimarisha ili uwe mtu imara katika maisha yako.....TUPO PAMOJA!
Subscribe to:
Posts (Atom)