Thursday, July 31, 2008

31 JULAI 2008 MJI MKUU AU?

mwenzeni leo nimekuwa bungeni. Nawaona jinsi mnavyoona wivu

JULAI 31,2008 USAFIRI


Mimi sisemi nawaachieni wasomaji

JULAI 31, 2008 KWAYA TENA


Mwenzenu leo nimefurahi sana nimeiimba kwa kiswahili nyimba za kumsifu mungu. Yaani raha kweli nimejikuta nipo nyumbani nimesahau kutamani nyumbani. Mmmm najua wengi mnaona wivu mtajiju.

JULAI 31,2008 KWAYA




Monday, July 28, 2008

JULAI 28,2008 UPENDO KWA NCHI YANGU

sijui kama wenzangu mmewahi kujisikia hivi, mwenzenu leo nimeamuaka na kujiona ya kwamba:- Ninaringa kwa kuwa mtanzania nchi yangu yenye sifa zote za ustaarabu.

Ninaringia rangi yangu nyeusi, macho meupe, ngozi yangu nyororo, ninapendeza na nywele zangu nyeusi na kiswahili ni lugha yangu.

Ninajivunia nchi yangu ya Tanzania yenye miji ya kuvutia iliyojengeka. Angalia Dar es salaam, Mwanza nayo Dodoma bila kusahau kwenye marashi mji wetu Zanzibar. Halafu ukienda Arusha, Tanga, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa na Songea.

Mnajua kuna vivutio vingi ndani ya Tanzania vinavyotufanya sote tujivunie kwa mfano kuna bahari fahari ya Taifa, Ziwa nyasa, viktoria, Tanganyika pia mlima mkubwa barani afrika Kilimanjaro. Bila kusahau mbuga za wanyama Serengeti, Ngorongoro, Tarangire, Mikumi n.k

Sunday, July 27, 2008

JULAI 27,2008 MATETEREKA


Miaka 17 iliyopita niliishi Matetereka na hapa katika picha ni majirani zangu "babu na bibi yangu" Lakini sasa nasikitika babu ameniacha nimepata habari.

JULAI 27,2008 KANGA


nadhani mnajua ni nini nafanya. kununua nguo mmhhh napenda mno

Saturday, July 26, 2008

JULAI 26, 2008 TANZANIA NDOGO

Leo nimefikiwa na wageni/marafiki ambao tuliishi pamoja TZ. Yaani raha sana, kama mnanielewa yaani ule urafiki umepita sasa ni ndugu. Nimeptwa na furaha ya pekee kuongea mambo ya zamani pia kuongea kiswahili lugha yangu. Sijui kama mtu unaweza kuona /jisikia raha japo kukumbuka nyumbani tu. kwani mara nyingi nakumukapo huwa natamani sana nyumbani.

Najua wengu mtashangaa na kuona nimechanganyikiwa. Sawa lakini kama mnavyoelewa utamaduni wa waafrika na wazungu basi mtaelewa naongoa nini. Nina maana kuishi pamoja, kushirikiana, kuishi pamoja kusaidiana hii napenda mimi kwani huondoa upweke. Hii yote nataka kusema leo nimejisikia nipo nyumbani TZ kweli nyumbani ni nyumbani.

Monday, July 21, 2008

JULAI 21, 2008 JIMBONI


Angalieni wenyewe halafu niambieni ni wapi hapa.

Sunday, July 20, 2008

JULAI 20, 2008 ZANZIBAR


Tusisahau kuwa Zanzibar na Tanzania ni nchi moja.

JULAI 20, 2008 KUMBIKUMBI


Leo nimefurahi sana kula chakula hiki yaani siku hizi naweza kula kila chakula

Saturday, July 19, 2008

JULAI 19, 2008 SONGEA


Huyu ni mmoja wa washiriki wa vita vya majimaji. Waliofika Songea mjini pale makumbusho majimaji nadhani wameona. sisemi sana semeni ninyi.

Thursday, July 17, 2008

JULAI 17, 2008 TUNAWEZA KUBADILI/KUACHA KUPIGA WATOTO

Katika nchi nyingi dunianai wanaona si kitu cha ajabu kuchapi/kupiga watoto. Wanaona ni moja ya malezi.

Lakini tukumbuke kila mtoto ana haki ya malezi yenye usalama. Inabidi tukazane kwani mpaka sasa, yaani leo hii kuna nchi 24 tu ambazo ni marufuku kupiga watoto.

Nadhani karibu kila mtu anakumbuka jinsi tulivyopata viboko, yaani nyumbani pia shuleni. Ndugu zanguni wasomaji tujaribu kusaidiana kuzuia kuchapa/kupiga watoto kwani viboko sio dawa ya malezi. Jinsi mimi ninavyoon/fikiri mtoto akishazoea kupigwa viboko kila siku anakuwa sugu(hasikii) anaona kawaida tu na pia akili yake inadumaa. Najua ni jambo (somo) ambalo wengi hawatakubaliana nalo lakini ni LAZIMA tuanze. Tuache kupiga watoto nyumbani na pia shuleni. Wazazi wawe huru kwa malezi ya watoto wao wakati wote na pia wawe na haki sio kuwapiga piga.
Sio kufuata sheria tu pia wazazi na walimu wanaweza kusema /kuona ni nini na aina gani ya malezi yanatakiwa.

Wednesday, July 16, 2008

JULAI 16,2008 WASICHANA NA TAHADHARI

Ngoja niachane na picha na niandike kidogo kwani kila siku nilikuwa nawaza nianza vipi sasa nimejua. Ni kwamba nataka kuandika kuhusu maisha ya wasichana:


NI hivi kila kitu hapa duniani kina upande wake mwema na mbaya. Hali kadhalika mawazo na matendo ya msichana/wasichana nayo. Mara nyingi mawazoni mwake/mwao msichana/wasichan hujishughulisha na mambo madogomadogo sana. Kwa ajili ya kujihusisha kwake na hayo mambo madogomadogo hushindwa kuyatekeleza makubwa, mapaswa yake halisi, yenye kuhitaji juhudi kubwa. Hapo hufanana na mtu ambaye anayehangaika kuwaandalia wageni vyakula hali hajawaalika, wala hata hafahamu kama watakuwa watu wa aina gani?

Msichana/wasichana huchukizwa upesi hata kama jambo ni dogo kabisa. Matokeo yake ni manungúniko, kutokuwa na furaha, kujaa uchungu moyoni, kujiona ameachwa na jamaa, ndugu, marafiki zake wote. Atajisikia kuwa katika dibwi kubwa la giza. Na hapo inawezekana ni jambo dogo tu. Ikiwa aliyemchukiza ni mama yake, hapo kuna hatari ya kupoteza imani yake kwa mama huyo katika mambo yote. Atasahau upendo wa mamake jinsi alivyomhangaikia na jinsi anavyozidi kumhangaikia hata leo hii. Hii yote ni ajili ya chuki. Kwa hiyo mwisho wake unakuwa msichana huyo anaanza kutafuta kitulizo nacho ni mvulana. Kutokana na hasira msichana huyo anaweza kumpokea mvulana yeyote bila hata kumchunguza dhahiri.

Kwa sababu hiyo ni hatari kwa msichana huyo kujihusisha na mvulana kwa ajili ya fadhila moja tu aliyoiona. Ndani ya fadhila kuna huruma,ukarimu na wema. Anasahau kabisa kudadisi na pia kuzungumza lengo halisi la urafiki huo. Anakuwa hajali tena kuchunguza ya kuwa urafiki huo ni wa kumhatarisha ama la.
Yawezekana upendo huo umesukumwa na tamaa za kimwili tu, hivyo kwamba hata watafunga ndoa itavunjika ila sasa kwa vile hakupima kwa uzito wa mambo, msichana anakuwa anajiingiza katika ndoa kipofu ni kama kipofu mwenyewe aingiapo hatarini. Kutokana na msukumo huo na kwa ajili ya maumbile yake kuna hatari msichana huyo asikubali ushauri wa wazazi wake, jamaa, marafiki au hata wakubwa wa kanisa. Uamuzi wa aina hiyo huhatarisha sio tu ujana wake bali hata maisha yake yote ya siku za mbele

Sunday, July 13, 2008

JULAI 13,2008 KINYWAJI


Zote hizo nimezitwanga leo, nakuambia zinapatikana hadi huku.

JULAI 13, 2008 KAHAWA


Ukitembelea Mbinga usisahau kunywa kahawa wanalima sana kule.

Friday, July 11, 2008

JULAI 11, 2008 GAZANIA JINA LA UA

Mimi ni mpenzi sana wa maua. Leo katika kutembelea maduka ya maua nikaona ua hili nzuri kwa kweli sikuweza kuacha kulinunua kwa uzuri wake. Na zaidi Jina la ua lenyewe. Kwa kweli ni nzuri au wenzangu mnasemaje?








JULAI 11, 2008 NYOKA


Sijui kama wasomaji mtanielewa. Hawa nyoka anatunzwa ndani ya nyumba analishwa na kutunzwa kama mtu. Wakati ni adui mkubwa wa binadamu. Na pia ni nyoka aliwadanganya Adamu na Eva. Nyoka analala safi wakati kuna watu wengine hawana sehemu ya kulala. Wanateseka na njaa pia baridi. Ila bahati mbaya sijui jina lake je? mnaweza kunisaidia halafu wapo wawili hapo. Haya kazi kwenu.

Wednesday, July 9, 2008

JULAI 9, 2008 KWA NINI

Nimekuwa najiuliza kila siku kwa nini binadamu tumezaliwa tofauti. Labda kwa namna nyingine ni afadhali. Angalia kama wote tungezaliwa na hasira, chuki, haraka n.k dunia ingekuwaje? Na je? kama wote tungezaliwa wenye furaha, upendo, huruma n.k ingekuwa si vizuri. Kwani katika maisha ni muhimu sana kupendana, sisemi ni lazima kupendana hapana kwani hili linakuja lenyewe( ni nature kumpenda mtu)

Pia jambo jingine kuwezakusameheana ni muhimu sana hata kama si jambo nzuri inabidi kujaribu. Kwani tusipofanya hivyo tutaishi maisha yetu yote tukiwa hatuna raha. bad feeling) na hii si nzuri kwa maisha ya binadamu.

Chuki na hasira ni muhimu kuviepuka kwani vinaweza kusabisha kifo. Nadhani wote tunajua tukiwa na chuki au hasira matokeo yake ni kuua au kufa. Tumeona watu wakiwa na hasira wanatuma kama pipa la pombe na mwisho wake kifo.

Kuomba radhi na kusameheana sio kitu rahisi na sio wengi wanaoweza ni kipaji. Sijui kama wasomaji mnakubaliana nami????????????????????????????????????

Tuesday, July 8, 2008

JULAI 8, 2008 SAMAKI



Mwenzenu leo nimeenda mpaka nyasa kuvua samaki bahati mbaya kulikuwa na zoruba kwa hiyo nimepata samaki moja tu na huyu amekuwa mlo wa jioni hii. Halafu tena nimekosa unga wa muhogo kwa hiyo nimekula na viazi vya kuchemsha (matosani) najua wengine wanaona wivu sana kazi kwenu. Mmmmmm utamu mpaka kwenye kidole gumba. Nakuomba Mr Mpangala watajie jina la samaki huyu kwani nimesahau kidogo.

Monday, July 7, 2008

JULAI 7, 2008 MTI WA LIMAU



Bustani imejaa/ ardhi imekwisha kwa hiyo nimeamua kupanda kwenye makopo mnaona yanavyostawi. nilikuwa mjinga miaka yote kununu kwa bei kubwaaaaaaaaa

JULAI 7, 2008 MABIBO


Kuna watu wameniambia wanapenda mabibo haya nawaletea sasa karibu.
Na: Yasinta Ngonyani

JULAI 7,2008 KILIMANJARO


Nimechoka kulima, nimeenda nyumbani kwanza likizo na bila kusahau nimetembelea mlima wetu mrefu. Sisemi sana kwani leo hali yangu si nzuri!!!!!!!
Na: Yasinta Ngonyani

JULAI 7, 2008 MAHINDI


Pia hata shamba la mahindi ninalo nitawatumia kadi wakati wa mavuno kama sitamaliza yote kula, kuchoma.
Na; Yasinta Ngonyani

JULAI 7, 2008 PAPAI


Mapapai ni moja ya chakula bora. Naona kuna wengine wananionea wivu shauri yenu lakini wote mnakaribishwa kuja kula.
Na; Yasinta Ngonyani

Sunday, July 6, 2008

JULAI 6,2008 BUSTANI YA NDIZI


Nilifikiri labda ndizi zinastawi kule Madaba (Matetereka) pia Mbeya. Kumbe ni uongo tu hata hapa Sweden zinastawi safi sana. Haha haha, mtajiju sasa sina taabu tena ya kutamani matunda ya nyumbani (kunyumba) kilugha. Wivu eeehh!! tutaonana
Na; Yasinta Ngonyani

JULAI 6, 2008 MJI WA KARLSTAD


Hapa ni nyumba ya kulala wageni msije mkafikiri ni meli ile ya mv Songea inaende Mbamba by na Itungu.
Na ; Yasinta Ngonyani

JULAI 6, 2008 BUSTANI YANGU

Nimeona afadhali niadhishe bustani ya matunda ya nyumbani kuliko kununua kila siku yanayosafirishwa kutoka mbali au ya kopo. Natumaini wote mnajua hili ni tunda gani. Karibuni tule.




Na; Yasinta Ngonyani

Thursday, July 3, 2008

JULAI 3,2008 KOROSHO















Korosho ni zao mojawapo Tanzania. Wakati nilikuwa mdogo nilikuwa nachezea korosho yaani zilikuwa nyingi sana. Nilikuwa naokota na kuchoma pia kupasua na kupata ile korosho. lakini sasa hapa ni ghali mno kununua korosho kilo moja ni shilingi 28000. Nimeacha kula sasa.




Na; Yasinta Ngonyani
Posted by Picasa