sijui kama wenzangu mmewahi kujisikia hivi, mwenzenu leo nimeamuaka na kujiona ya kwamba:- Ninaringa kwa kuwa mtanzania nchi yangu yenye sifa zote za ustaarabu.
Ninaringia rangi yangu nyeusi, macho meupe, ngozi yangu nyororo, ninapendeza na nywele zangu nyeusi na kiswahili ni lugha yangu.
Ninajivunia nchi yangu ya Tanzania yenye miji ya kuvutia iliyojengeka. Angalia Dar es salaam, Mwanza nayo Dodoma bila kusahau kwenye marashi mji wetu Zanzibar. Halafu ukienda Arusha, Tanga, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa na Songea.
Mnajua kuna vivutio vingi ndani ya Tanzania vinavyotufanya sote tujivunie kwa mfano kuna bahari fahari ya Taifa, Ziwa nyasa, viktoria, Tanganyika pia mlima mkubwa barani afrika Kilimanjaro. Bila kusahau mbuga za wanyama Serengeti, Ngorongoro, Tarangire, Mikumi n.k
2 comments:
kila ninapo kumbuka wimbo wa marehemu Tupac wa 'To live and Die in Los angeles' huwa naikumbuka Tanzania.Hakika sina mahali patamu kama hapa,ingawa nakumbuka sana asili ya watu hawa waitwao 'Mpangala' ambao asili yao ni Malawi lakini kwa Tanzania nimefika nami nitaishi na kufa hapa
Unajua mimi nimepanga nitakapokufa nitazikwa Tanzania
Post a Comment