Thursday, July 17, 2008

JULAI 17, 2008 TUNAWEZA KUBADILI/KUACHA KUPIGA WATOTO

Katika nchi nyingi dunianai wanaona si kitu cha ajabu kuchapi/kupiga watoto. Wanaona ni moja ya malezi.

Lakini tukumbuke kila mtoto ana haki ya malezi yenye usalama. Inabidi tukazane kwani mpaka sasa, yaani leo hii kuna nchi 24 tu ambazo ni marufuku kupiga watoto.

Nadhani karibu kila mtu anakumbuka jinsi tulivyopata viboko, yaani nyumbani pia shuleni. Ndugu zanguni wasomaji tujaribu kusaidiana kuzuia kuchapa/kupiga watoto kwani viboko sio dawa ya malezi. Jinsi mimi ninavyoon/fikiri mtoto akishazoea kupigwa viboko kila siku anakuwa sugu(hasikii) anaona kawaida tu na pia akili yake inadumaa. Najua ni jambo (somo) ambalo wengi hawatakubaliana nalo lakini ni LAZIMA tuanze. Tuache kupiga watoto nyumbani na pia shuleni. Wazazi wawe huru kwa malezi ya watoto wao wakati wote na pia wawe na haki sio kuwapiga piga.
Sio kufuata sheria tu pia wazazi na walimu wanaweza kusema /kuona ni nini na aina gani ya malezi yanatakiwa.

2 comments:

Unknown said...

Kwa mtazamo wangu hapo nakubaliana nusu na kukataa nusu.

Najaribu kupiga hesabu kama mama yangu mzazi aisngekuwa ananichapa kiboko tangu utoto wangu kwa kweli ningemwendesha ile mbaya maana kwa utundu wangu ningegundua hakuna bakora yaani ingekuwa raha sana, asingeniweza, mimi nipo wazi kiboko kilinifanya kuwa mwenye mstari na kuwa mtoto mzuri hadi maisha yangu kwa ujumla. Napinga sana wazazi wanaotandika watoto hadi wanakuwa sugu kweli huo ni utesaji, ila kupata kiboko matakoni kuondoa ujinga kwangu hilo sina shida na naona malezi pia. Nipo hapa Canada naona jinsi ilivyoshida kwa hao watoto ambao huwa hawaguswi kwa kweli sasa ni watoto sugu na matokeo yake wamekuwa na teenagers ovyo kabisa duniani kwa tabia ovyo. Sijui wengine wanaseaje ila kila utamaduni una malezi yake!

Yasinta Ngonyani said...

Sawa kabisa nakubaliana na kaka Mbilinyi kuwa hii inawezekana ni kila sehemu na utamaduni wake pia malezi yake. Lakini hata hivyo sikubaliani kuwa kiboko ni dawa ya malezi