Showing posts with label desturi. Show all posts
Showing posts with label desturi. Show all posts

Monday, August 8, 2016

KUANZA KUPOTEA KWA DESTURI YA UKARIBU WA KIFAMILIA KUNAVYOATHIRI MALEZI

Malezi katika mazingira yetu ya ki-Afrika ni suala nyeti. Kwa kutambua umuhimu wa malezi katika kujenga jamii yenye ustawi, wa-Afrika tumekuwa na desturi ya kuelekeza nguvu zetu nyingi katika malezi ya wanetu. Kwa mfano, tangu mtoto anazaliwa, ilikuwa ni lazima alale kitanda kimoja na wazazi wake kwa muda unaozidi miaka miwili. Mtoto mchanga hakuachwa alale kwenye kitanda chake mapema kwa sababu za msingi zilizokubalika katika jamii zetu.


MAMA AKIWA KAMBEBA MWANAE
Aidha, mtoto daima alikulia mikononi mwa watu wazima aliowafahamu vyema. Watu hawa ama aliishi nao kwenye boma la wazazi wake au walitoka miongoni mwa jamaa inayomzunguka. Muda mwingi mtoto alibebwa mgongoni kwa mama yake au dada zake. Desturi ya kubeba watoto mgongoni ilifanya suala la ukuaji wa mtoto kufuatiliwa kwa karibu sana na imethibitika kisayansi kusaidia kujenga muunganiko wa kihisia kati ya mzazi na mtoto. Jambo hili, hata hivyo, halieleweki kwa wageni wa bara hili wanaodhani ni aina nyinine ya udhalilishaji wa mtoto.

Chakula cha pamoja ni kitamu sana

Wakati wa jioni, familia zilikuwa na desturi ya watoto kukaa na wazazi wao kijinsia. Baba aliota moto na watoto wa kiume akiwasimulia mambo mbalimbali ya kimaisha. Kadhalika, mama naye alifanya kazi za jikoni kwa ushirikiano wa karibu na watoto wa kike. Chakula kilipokuwa tayari kililiwa kwa ushirikiano. Muda wa chakula ulifahamika, na kwa kweli, kila mtoto aliwajibika kuwepo kupata chakula. Kwa kuwa chombo kilichotumika kulia chakula mara nyingi kilikuwa kimoja basi kila mmoja katika familia alilamizika kula kwa ushirikiano na wenzake.

Desturi hii ya kukaa karibu na watoto na kufanya mambo mengi kwa pamoja iliwasaidia wazazi kuwafundisha watoto maarifa na ujuzi wa aina mbalimbali. Vile vile, ukaribu huu ulikuza uhusiano wa karibu wa kifamilia. Kadhalika, karibu huu uliwahakikishia watoto usalama wao. Kisaikolojia walijua hawana wasiwasi kwa sababu baba na mama wapo na wangepigana na yeyote anayetishia usalama wao. Watoto waliwategemea wazazi wao.

Upo ushahidi wa kiutafiti kwamba kutegemewa kwa mzazi ni nguzo kuu ya malezi. Kwamba mtoto huiga mengi wa mzazi ikiwa anaamini mzazi huyo ni wa kutegemewa na yuko upande wake. Hali hii ilimfanya mtoto asiwe na wasiwasi na usalama wake pale yalipojitokeza mazingira ya kutengana kimwili na kwa hivyo wazazi kwa kweli hawakulazimika kuwa na watoto muda wote. Kama tutakavyoona katika mfululizo huu, hali hii ya mtoto kumwamini na kujisikia salama mikononi mwa mzazi inategemea sana uwepo endelevu wa mzazi kimwili na kihisia tangu siku za mwanzo za maisha ya mtoto.

Hata hivyo, kadri mwanadamu anavyozidi ‘kuendelea’ na ‘kustaarabika’, ndivyo desturi hii ya kupatikana kwa wazazi nyumbani inavyozidi kukosa umaarufu. Kwa mfano, ipo dhana inajengeka katika jamii kwamba maendeleo halisi ni vitu. Matokeo ya imani hii ni kutufanya tutumie muda mwingi ‘kuhusiana na vitu’ zaidi kwa gharama ya mahusiano na ustawi wa familia zetu.

Kadhalika, zipo changamoto nyingine za kijamii zinazotishia desturi ya familia. Kuna masuala kama kazi/ajira zinazowatenganisha wazazi na familia, misukosuko ya kimahusiano inayozaa talaka na/ama kulazimisha malezi ya mzazi mmoja, ujio wa shule za bweni kwa watoto wadogo pamoja na matatizo kadha wa kadha yanayofanya watoto wadogo wakue katika mazingira magumu yasiyo na uangalizi mzuri. Haya tutayaangalia wakati wake ukifika.

Kwa hiyo, ili kukabiliana na changamoto hizi mpya, upo umuhimu mkubwa wa kujadili tafiti zilizochunguza athari za mazingira haya mapya ya kimalezi ambayo kwa kiasi kikubwa hayakuwepo huko nyuma. Kwa mhutasari, tunaweza kutaja suala kuu linalojitokeza kwa haraka. Kwamba uhusiano kati ya mzazi na mtoto unaathiri mahusiano ya mtoto huyo na watu wengine. 

Wednesday, March 14, 2012

KUVAA SHANGA... NI UREMBO AU?

Ndiyo ndugu zanguni ni JUMATANO TENA na ni kile kipengele chetu cha MARUDIO..katika pita pita nimekutana na mada hii nikaona si mbaya tukirudia kujadili tena . Nimeipata hapa.
watu huvaa shanga kwa maana nyingi naamini, hivi shanga zina maana ngapi? najua maana za nyekundu, nyeusi na nyeupe je nihizo tu ama na rangi nyengine pia zinamaana tofauti? na wanaume hupendelea nini kwenye shanga? na wanawake waova je hujisikiaje kuwa nazo..


kuna wakati nilikuwa navaa shanga kwenye kiuno sio kwamba nilipenda ila mpenzi wangu kipindi hicho ndio alikuwa anapenda nivae akisema anapoziona anasisimuka lakini baada ya kuachana naye nikaachana nazo kwakuwa sikuwa nazipenda kuvaa bali kumridhisha tu..

kitu cha kushangaza ni kwamba kuna rafiki yangu anaolewa karibuni mchumba wake amemletea shanga avae, anasema yeye anapenda kumuona mpenzi wake akiwa amevaa ndipo nilipo mshauri azivae baada ya kumpa story yangu hapo juu..

wanaume kuna raha gani ambayo mnaipata pindi wapenzi wenu wanapo vaa shanga????na je ni wanaume wa makibala fulani ama wote kwa ujumla? maana rafiki yangu huyo mchumba wake mkuria na ndicho kilicho zidi nishangaza...na mwanaume aliyenifanya mimi nivae ni mmakonde ndio inazidi kunichanganya..

sio vibaya nikufahamishana tu ili tujuwe kama tutaendelea kuzivaa ama tuziweke kapuni.....

TUTAONANA TENA JUMATANO IJAYO KATIKA KIPENGELE CHETU CHA MARUDIO!!!

Thursday, March 1, 2012

TAFAKARI YA LEO:-MILA NA DESTURI ZETU!

Nimekuwa nikiwaza jambo hili tangu nilipoanza kupata akili....Ni swali ambalo nimekuwa nimewauliza watu wengi nao hawajaweza kunijibu kwanini. Na leo nimeamka na naliona linazunguka kichwani mwangu na nimeshindwa kuacha kuuliza hapa kibarazani.
Ni hivi:- Hivi kwa nini msichana asimwombe kijana ampendaye kuwa anataka waoane? Najua ni mila na desturi zetu za kale kwamba ni mvulana/kijana /mwanaume afanye hivi. Je msichana/binti /mwanamke akifanya hivi kwa mvulana/kijana/mwanamume anayempenda itakuwa si sawa?

Thursday, June 9, 2011

Swali la leo:- CHANZO CHA UKOO NI NINI?

Swali langu la leo nimeenda hadi Upareni na kurudi...Nikimaanisha litawalenga hasa ndugu zetu WAPARE. Ila nitaanza na mifano miwili ambayo ni zoefu kwangu:-
Nilipokuwa msichana mdogo nakumbuka niliwauliza wazazi wangu kwa nini twaitwa NGONYANI na ni nana alianzisha na pia kwa nini karibu majina mengi ni ya wanyama? Sikumbuki kama nilipata jibu.
Baadaye nikawa msichana mkubwa na nikaanza maisha na nikaanzia maisha yangu kuishi na WABENA. Kwa kweli walibifanya UDADISI/UKAPULYA wangu uzidi. Kwa vile wao U-KOO wao unaanza na M, mfano:- Mwageni, Mgaya, Mbilinyi, Mgina nk.
Lakini hata hivi si WABENA tu ambao wanaanza na M. Na hili ndilo ambalo lilikuwa kiini cha swali langu zaidi ndugu zetu WAPARE... Yaani koo kama za KIPARE:- Kwanini zinaanza na M?. Mfano MSUYA, MMBAGA, MZIRAYI, MFINANGA, MSHANA,MCHOMVU ......NK. Nina uhakika hapa nitasaidiwa. TUKUTANE TENA WAKATI MWINGINE:-

Monday, June 6, 2011

Mungu wa Kimasai adhaniwaye kuwa na nyuso mbili


NI pembezoni mwa jiji la Nairobi, Kenya, watu wa kabila hili wametengeneza duara, mmoja anaimba kwa sauti ya mtetemo mfano wa zeze na wengine wanaitika kwa sauti mchanganyiko nyembamba na nzito, kisha mmoja mmoja anaingia kati na kuruka juu akiwa amenyooka mithili ya nguzo.

Shuka zao zenye mchanganyiko wa rangi zinasalimu amri kwa kupepea kila warukapo juu, hali kadhalika vito vyao miguuni na mikononi hata shingani vinatoa sauti na kutengeneza mapigo kama ya ala za muziki. Hao ni Wamasai, watu wanaosifika ulimwenguni kote kwa kutunza tamaduni zao.
Zimekuwepo dhana na hadithi mbalimbali kuhusu mila na taratibu zao, baadhi zimesifiwa, nyingine zimekuwa zikipigwa vita na baadhi yake zinashtusha na kuacha simulizi la kushangaza.

Lakini, ukweli unabaki palepale kuwa kabila hili ni kivutio kwa wengi na ni miongoni mwa machache yaliyoweza kuhifadhi na kuheshimu mila zao, licha ya maendeleo ya sayansi ya teknolojia.
‘Enkai’ au Mungu wa Kimasai
Wao huabudu, wanamwabudu mungu mmoja, ‘Enkai’ au Engai ambaye si mwanamke wala si mwanaume. Lakini, mungu huyu amegawanyika katika sura mbili tofauti, upande mweusi(engai narok) na mwekundu(engai nanyokie). Upande mweusi ni mwema na wenye upendo na mwekundu ni wa kishetani na usio na chembe ya huruma.

Wanaamini kuwa, sauti ya radi ni dalili ya pande mbili za ‘Enkai’zikigombana, ambapo upande mweusi unataka kutoa mvua kwa ajili ya mifugo na watu, na upande mwekundu unataka mvua isinyeshe na wamasai pamoja na mifugo yao wapoteze maisha.

Wanaume husuka, wanawake hunyoa vipara
Kimila, wanawake kunyoa vipara na wanaume kusuka rasta ni baadhi ya taratibu za kipekee kwa kabila hili, si hivyo tu, bali wanawake ndiyo hujenga nyumba ya familia, tofauti na makabila mengi ya Afrika Mashariki ambapo wanaume wanawajibika katika ujenzi wa nyumba na wanawake wakiwa na jukumu la ulezi na si ujenzi.

Dhana ya kuchomeka mkuki
Imekuwepo hadithi ya kwamba, mwanamke wa Kimasai anamilikiwa na ukoo wote, kwa hilo, kila mwanaume hushiriki kitanda na wanaume wengine.
Anachofanya ni kuchomeka mkuki mbele ya nyumba (boma) na kisha kuendelea na shughuli iliyomfikisha mahali pale.
Hivyo basi, yeyote atakayekuja na kukuta mkuki huo mbele ya nyumba, hatakiwi kuingia ndani, bali kusubiri, na kuwa mvumilivu. Wivu hautakiwi kwao.

Kwa mujibu wa Simeon ole Serere, dhana hiyo ipo mbali na ukweli, kwani, mkuki huo unamaanisha kujisalimisha na hana nia ya kudhuru, hivyo mwenyeji atakaporejea asiwe na shaka kwani silaha ipo nje.

Laana ya kukata misitu
Hadi leo, Wamasai wamezungukwa na mimea katika mazingira yao, kwa mfano kuna msitu karibu na kijiji cha Mau unaoitwa Medung’i, ukimaanisha ‘Maa’ yaani ‘ usikate’. Inaaminika kwamba, ukikata miti katika eneo hilo, damu itatiririka kutoka humo na kukulaani.
“Mila hizi ndizo zilizowezesha uoto asilia kustawi katika mazingira yetu, tumeweza kuhifadhi Masai Mara, Amboseli na hifadhi za wanyama za Serengeti kwa kuwa hatuli wanyama pori,” anasema ole Kulet, mwandishi wa riwaya nane kuhusu mila za Wamasai.

Hakuna kilio, wala hisia za maumivu
Vijana wa Kimasai wanapofikia umri wa kubalehe, hutakiwa kupitia hatua ya tohara, hii huwajumuisha vijana wote wenye umri wa miaka 12 hadi 25. Kitendo hicho hufanyikaa bila ganzi na inasemekana kuwa wakati wa tendo hilo hutakiwi kulia au hata kukunja sura kuonyesha unahisi maumivu, kwani kufanya hivyo kunaonyesha udhaifu na ni aibu kwa ukoo wako.

Lakini pia, kutikisika au kukunja sura kunaweza kusababisha makosa katika ukataji wa ngozi ya uume na kusababisha kovu la kudumu au kilema cha aina yoyote ile.
“kupona kunachukua miezi mitatu hadi minne, kipindi ambacho vijana hupata shida kujisadia haja ndogo huku kukiambatana na maumivu makali. Vijana hao hutakiwa kuvaa mavazi meusi kwa kipindi cha miezi minne hadi minane,” anasema Laizer Selelii, mlinzi katika ghala moja la mazao jijini Nairobi.

Wanawake pia hufanyiwa tohara au emorata tendo hilo limekuwa likipingwa vikali na wanaharakati na wanawake ambao wamefanyiwa, kama Agnes Pareiyo.
“Usipofanyiwa tohara unaweza kukosa mume, ni kitendo kinachochukuliwa kama cha thamani na sifa kwa mwanamke, wakati mwingine, mahari yako huweza kuwa ni ng’ombe wachache kama usipopitia hatua hii,” anasema Pareiyo. “Lakini, madhara yake ni makubwa wakati wa kujifungua.”

Uchumba wa mimba
Inasemekana kuwa, wanaume wa kimasai huchumbia mimba na kuitolea mahari endapo mtoto atazaliwa wa kiume mahari ile hurudishwa.
Mila hii ndiyo inayosababisha mabinti wa kabila hili kuolewa wakiwa na umri mdogo wengine hata miaka kumi hadi kumi na mbili.
Ole Serere, anasema, suala la wao kuchumbia mimba lilikuwepo zamani ingawa sasa halifanyiki sana.Anakiri kuwa, mabinti wa Kimasai huchumbiwa wakiwa na umri mdogo kwa sababu hawaendi shule.

Ung’oaji wa jino la chini
Utafiti uliofanywa mwaka 1991/92 na kuhusisha watoto tisini na tano wenye umri wa kati ya miezi sita na miaka miwili uligundua kuwa wameng’olewa meno ya chini.

Wakati wale wenye umri wa miaka mitatu hadi saba, asilimia 72 ya watoto 111 walionekana hawana jino moja au mawili ya chini.
Utafiti huo uligundua kuwa, meno hayo hutolewa kwa ajili ya kupitisha maziwa endapo mtu amekunywa sumu au anaumwa mahututi.
Baadhi yao wanasema, kitendo hicho hufanywa wakati wa utoto ili kuondoa meno hayo ya plastiki yenye minyoo ambao husababisha watoto kuharisha na kutapika.

Kutowazika maiti
Wamasai wanaamini kuwa kila binadamu ana malaika wake mlinzi ambaye mtu akifariki humbeba na kumpleka sehemu mbili kati ya hizi, aidha jangwani kama mtu huyo alitenda maovu au katika rdhi ya utajiri wa ng’ombe kama alitenda mema.

Hata hivyo, hawatamki hata siku moja kuwa mtu amefariki, kama ni mtoto husema amepotea na kama ni mtu mzima hutajwa kuwa, amelala.
Hawawaziki wafu, bali baada tu ya kifo,mwili hutupwa porini ili uliwe na fisi. Katu hawachimbi kaburi, kwani wanaamini ardhi imebarikiwa kwa ajili yao, endapo wataichimba watalaaniwa.

“wakati mwingine tunahama kabisa makazi ambapo mtu amefariki, kwani nyumba hiyo yote huwa na mizimu,” anaeleza Serere.
Katika miaka ya hivi karibuni, wameanza kubadilika, kwani sasa hivi hulima, hufanya biashara na wapo wasomi, wake kwa waume.
Hata hivyo, hiyo si sababu ya wao kuacha baadhi ya mila zao muhimu na zenye manufaa kwao. Bado wangali wamebeba fimbo na sime, kama alama ya ushujaa wao.
Na Florence Majani wa Gazeti la Mwananchi

Wednesday, September 1, 2010

Sheria, Mila na Desturi pia Tamaduni pale Zinapotofautiana!!

Mama, baba na watoto, maisha ya ndoa!!

Mama na watoto wake peke yake!!
(Ensamstående )

Fuatana nami kwa habari hii fupi kuhusu maisha yalivyo tofauti:- Kwa miaka kadhaa iliyopita nchini Sweden kulikuwa na uhaba wa watoto. Yaani maisha yalikuwa magumu na watu walipunguza "waliacha" kuzaa watoto wengi. Baada ya Serikali kuona hivyo ikaja na sharia kuwa kila mtoto atayezaliwa basi wazazi watalipwa kiasi fulani kila mwezi mpaka mtoto atakapotimiza miaka 18. Pia ni kwamba kiasi cha malipo kitaongezeka mtoto wa pili atapozaliwa kama mtaliwa 2000SEK na sasa mtalipwa 4000SEK na mtoto wa tatu wa tatu mtalipwa 7000SEK huu ni mfano tu

Sasa tatizo jingine limeibuka sasa hivi tu, nilikuwa nasikiliza habari na nikasikia kitu ambacho sikuweza kuamini. Naweza kusema nilishangaa ama kweli TEMBEA UONE YA DUNIA. Ni hivi kama mmefunga ndoa na baadaye mnapata mtoto hapo kuna utaratibu kwamba wazazi mnapewa siku 480 kwa mwaka kuwa nyumbani na mtoto. Ni hiari yenu kama mnataka kugawana hizo siku au mzazi mmoja atabaki nyumbani na mtoto. Inaitwa (föräldraledighet) au kwa lugha ya kitaalamu ni (Maternity live) na hizo siku mnalipwa kwa kuwa nyumbani na mtoto wenu.

Ila sasa kama mnaishi bila kufunga ndoa (Sambo) hizo haki zote zitaenda kwa mama. Na halafu baba atakuwa hana haki hata ya kuwa na mwanae, kwa maana hiyo anakosa kile kipindi cha mtoto awapo mchanga kipindi ambacho kila mzazi/mlezi angependa kukishuhudia.

Mwisho, ni kwamba Sweden mume na mke wakiachana mtoto au watoto watakuwa wanafuatana na mama. Pia ni ruksa kuitwa ubini wa mama. Nimetoa mfano huu kwa vile Tanzania kama wazazi wanaachana watoto wanabaki na baba. Najua Tanzania ni Lazima kuitwa ubini wa baba au NIMEKOSEA tusaidiane .

Thursday, March 25, 2010

MILA NA DESTURI ZA WANGONI:- Upande wa ndoa na kuchumbia

Kwanza uchumba halafu harusi/ndoa.

Katika mila za wangoni, hapo zamani kijana na msichana wakikua kufikia umri wa kuoa walioa. Kwa mila za wangoni, mtoto wa kiume hata kama akikua na kuoa halafu hajaenda vitani ilikuwa haionyeshi maana. Wakati wa kupigana vita kijana ilibidi aonyeshe nguvu zake zilivyo. Kijana ambaye bado hajaenda vitani aliitwa (walimwita) ”lijaha” ikiwa na maana ya kijana/mvulana mdogo. Kijana ambaye ametoka vitani walimwita/aliitwa ”lidoda” ikiwa na maana mkubwa . Mke wa kuoa walimtafuta ambaye ni mwenye ukamilifu, anayejua kufanya kazi za nyumbani. Anatafutwa mwanamke anayeweza kuokota kuni, kuchota maji, kutwanga, kupika chakula, kupika pombe na awe mwanamke anayecheka vizuri na watu wote katika mji.

Ndoa haifungwi katika ukoo. Kwa wangoni hawaoi mke au kuolewa na mume mwenye (kibongo) ubini mmoja. Kama watu wakioana katika ukoo, basi wazee wataulizia kwanza kama ukoo huo ni wa karibu au wa mbali. Kama hawa watu walioana katika ukoo wa karibu, basi watawaapizia. Watu wnaogopa kuoana ndani ya ukoo kwasababu wakifanya hivyo watoto watakaozaliwa watakufa. Na pengine watoto hao watapata kifafa au pengine mababu (mahoka) watakasirika.

Mtenga:-

Kwa kingoni cha zamani mtenga ni mtu anayenunua au kuuza kitu. Mtenga anamuuza mototo wa kike. Yeye ndiye atoaye ”Chiyagabuli” yaani mali ya mwanzo na ”Mawolowolo” ikiwa na maana mali yote kwa wenye mtoto wa kike.

Kulonda mdala=Kutafuta mke:-
Wenye mtoto wa kiume wanapotaka kumwoza kijana wao , wazazi wengine walimtafutia mke. Wazazi wengine walimwacha kijana wao atafute mwenyewe mke. amtakaye. Kama walimwona msichana mrembo watamtafuta ndugu yao ambaye watamtaka na kumwelezea habari za ndoa. Na huyu ndiye atakayekuwa MTENGA wao. Mtenga huyu ataanza kuulizia kwa siri mambo ya wazazi wa msichana yule na wanaukoo wake wote na halafu ataenda kuwaeleza wazazi wa kijana. Kama wazazi wataona ya kuwa ni msichana wa hodari, watenga wale wataenda kwa wazazi wa msichana na kuuliza kama wanaruhusiwa kumwoa? Kama wenye binti watakataa, watenga wataombeleza.

Kujitokeza:- Ni lazima wawe na kiulizio , watenga ndio wataenda kuulizia kumwoa mke. Wanapoenda kule , wanachukua kitu fulani ”lukotelu au luhongelu” ni kiulizio , kitu hicho chaweza kuwa nguo, ushanga au hela nk.

Chiyagabuli= Mahari ya mwanzo

Kama wakwe wa pande zote mbili wanakubaliana watoto wao waoane, watenga watapeleka mahari kidogo kwa mama na baba wa binti ambayo ni mahari ya mwanzo. Baada ya muda yatapelekwa tena mahari ya mwanzo yaani kwa mara ya pili itakuwa jembe moja LUSUKA. Kama aina fulani ya jembe "ngwamba" ni jembe lenye tundu pale pmini unapotumbukizwa. Hii itamaanisha binti yao tayari amekwisha poteza ubikira

Kuchicha= kumtembela mchumba
Kuchicha ni kitendo cha msichana aliyechumbiwa kwenda rasmi kumtembelea mchumbake, kimila huyo msichana aliyechumbiwa anaenda na rafiki yake wa kike. Hivyo basi siku hiyo inakuwa ni kama anaenda kuona mazingira atakayokuja kuishi. Kimsingi katika siku ya kuchicha hairuhusiwi kulala pamoja na kufanya mapenzi ndio maana msichana alipaswa kusindikizwa na msichana mwenzake. Lakini basi mara nyingi imekuwa ngumu kujizuia wengi wamekuwa wakiishia kufanya mapenzi, mbaya zaidi unakuta mvulana anaalika na mvulana mwenzake halafu wanagawana hao wasichana waliofika hapo. Lakini pia hilo neno limekuwa likitumika isivyo rasmi kama vile kitendo cha msichana kutongozwa na mvulana wapo walioita kitendo hicho kuchicha na imezoeleka na wengi.

Au pia inakuwa kinyume:- Kijana wa kiume pamoja na vijana wenzake wanaenda rasmi kumtembea mchumba/msichana. Huko anafanya kazi nyingine nyingi. Kwa kufanya hivyo, wakwe watamwona ni kijana /mume wa uhakika, kuwa anaweza kufanya kazi za kianaume, kama anajua/weza kulima kukata matema(kukata miti shambani kwa ajili ya kuandaa shamba), kama ana kaa/ishi vizuri na watu au kama hana haraka ya kula. Muda wote huo wa aliokuwepo, kijana huyu hajionyeshi kwa wakwe zake. Anapotaka kutoka nje ya nyumba alalayo ni lazima ajifunike nguo usoni gubigubi. Kijana atafanya hivyo atakapotaka kumwona mtarajiwa mkewe, hakuna kujionyesha kwa wakwewe mpaka atakapozaa mtoto. Na mwanamke atafanya hivyo kwa wazazi wa mumewe.

Nimefanya utafiti katika kuon au kulipa mahari inaweza kuwa kama ifuatavyo
Mbuzi 1 dume
Mbuzi 5 dume 1 , majike 4
Sufuria kubwa 1
Mablanket 2
Nguo- kanga doti 2
Nguo vitenge doti 2
Nguo shuka 2
majembe 2
Simulizi/maelezo ni kutoka kwa babangu mzee Ngonyani

Ngoja tusikilize pia ngoma hii ya kitoto/lizombe ambayo ni ngoma ya wangoni karibuni!!

Thursday, January 21, 2010

SWALI:- NI VYAKULA GANI KATIKA KABILA LAKO AMBAVYO UKILA UNAONEKANA WEWE NI MASKINI WA KUTUPWA?

Kila kabila lina mila na desturi zake kuhusu vyakula. Kuna vyakula akina mama na watoto hawatakiwi kula kutokana na mila hizo. kwetu Ruhuwiko,Litumbandyosi, Kingoli ukila MANGATUNGU(aina ya upupu)au ukila ugali wa BUNDURA(mihogo ya kuvundika) ukila ....unaonekana wewe ni maskini sana. Pia nimeishi kule Ubenani na wao walikuwa wanakula sana MAKANDE(ng´nde)na kuna makabila waliona kuwa wao ni maskini sana. Katika utafiti nimegundua/nimekikuta kitu kama hicho Usukumani, kwa wasukuma wa sehemu za Maswa mpaka Mwagala njia ya kulelekea Meatu ambapo mtu akionekana anakula ugali wa MTAMA anaonekana amechacha ile mbaya!

Je? hali ikoje kwa makabila yenu? Je? wasukuma (najua wamegawanyika; wa Bariadi, Malya, kahama, mwanza, tabora nk) wote wana mila hizi?

Wednesday, October 7, 2009

MILA NA DESTURI HIZI KAAAZI KWELI KWELI!!

Ni miaka karibu 15 sasa inakaribia tangu nilipoingia hapa Sweden. Na ni miaka 6 imepita tangu niwe mwanafunzi yaani kukaa darasani na kubukua.

Kuna kitu nataka kuwasimulia ambacho nilikiona miaka sita iliyopita wakati nasoma. Katika darasa letu tulikuwa wanafunzi mchanganyiko, wenyeji na wahamiaji. Kwa hiyo siku hiyo kulikuwa na somo la mila na desturi. Ilikuwa tuangalie filamu inayoonyesha mambo ya hali halisi. Basi tukawa tunaangalia hiyo filamu ambayo ilikuwa inahusu maisha ya mwanadada mmoja (jina linahifadhiwa) ambaye alikuwa akiishi na wazazi wake na alikuwa mtoto pekee katika familia ile.

Mwanadada huyu alikuwa hana maisha ya kawaida. Alikuwa mlevi na mvutaji yaani si sigara tu na madawa ya kulevya alikuwa anatumia. Sasa, kibaya zaidi alikuwa akiwaibia wazazi wake vito vya thamani, na kuuza ili kupata pesa na kwenda kununu hayo mahitaji yake na pengine aliiba pesa pia. Ila alikuwa mwema alikuwa akiwapa rafiki zake pia.


Kwa tabia hiyo ilifikia mahali wazazi walishindwa kumvumilia wakamtimua pale nyumbani na akawa hana sehemu ya kuisha. Akawa analala vibarazani bila hata hata ya kuwa na shuka ya kujifunika, chakula hana na anachovaa hakieleweki…...Siku zikapita.......

Maisha yakazidi kuwa magumu, siku moja akaamua kurudi kwa wazazi wake na kusema ameacha ile tabia. Wazazi wakawa shingo upande ila kwa vile uchungu wa mtoto wanaujua wazazi wakampokea. Siku zikapita lakini ghfla siku moja akabadilika na kuanza tena ila tabia. Kama tusemavyo ukionja asali ni ngumu kuacha. Akawa anaiba vito tena na kuuza ili kupata pesa za pombe na madawa ya kulevya.Wazazi walivumilia, lakini mwisho walishindwa na wakamfukuza tena. Akawa hana kwa kwenda isipokuwa kule mitaani kuungana na marafiki na kuendela kulala vibarazani kama awali.

Mnajua ni jambo ambalo mimi sijaelewa mpaka leo katika kutafakari kwangu. Kwasababu mimi naona hapa sweden kuna misaada mingi ya kuwasaidia watu wa aina hii na nilishangaa kwa nini naye asingetafutiwa msaada? Ukizingatia wazazi wake walikuwa na uwezo na pia alikuwa mtoto pekee wanamwacha na kuwa mlevi tu??

Cha kushangaza zaidi ni kwamba hazikupita siku nyingi wazazi wa mwanadada huyu walijitafutia mbwa. Wakamnunulia mbwa huyo vitu vizuri vya kuchezea, sehemu nzuri ya kulala na chakula kizuri pia alipata. Wakati binti yao yupo hatarini hana chakula, hana mavazi wala sehemu ya kulala.

Hapo ndipo nilipokuja amini sisi binadamu tupo tofauti sana katika kuthaminiana. Mbwa/wanyama wanathaminiwa kuliko binadamu tena mwanao? Kazi kwelikweli!! Ila siku ile nililia sana kwa vile niliguswa sana na nilifoka sana darasani. Mwalimu wangu akanituliza na kuniambia karibu Sweden, Habari ndio hii. Je? Wenzangu mngejisikiaje?

Tuesday, September 1, 2009

KILA MTU ANA MILA+ DESTURI PIA UTAMADUNI WAKE

Hapa ni wanawake wakiwa katika pozi ni huko Papua New Guninea.
Na hapa ni wanaume wa huko huko Papua N ew Guninea nao wakiwa kwenye pozi bila wasiwasi.

Friday, June 19, 2009

HAPA SWEDEN LEO NI MIDSUMMER(MIDSOMMARAFTON)


HISTORIK
Traditionen kam från Tyskland på 1500- 1600 talet.
Seden var först förknippad med förstamajfesten.
Ordet majstång kommer av att man lövade (majade)sina hem
Flyttades från maj till midsommar av klimatskäl.

Nitajaribu kutafsirikwa kiswahili:-

KIHISTORIA KUHUSU HII MIDSUMMER NI HIVI:-

Kihistoria, mila na desturi hii imetokea Ujerumani karne ya 1500 - 1600.
Mila hii inauhusiano na sikukuu ya wafanyakazi
Neno Majstång linatokana na au niseme, watu hapo zamani walikuwa wanapamba majani kwenye nyumba zao.
Kwa hiyo wakaamua kuacha kusema (maj) na kusema (midommar)"midsummer" kutokana na hali ya hewa.

Labda niongezee ni hivi wengi walikuwa wanaamini kuwa kutokana na idadi ya hiyo miviringo inaonyesha watoto wangapi wamezaliwa kwa mwaka.

Tuesday, March 24, 2009

MILA NA DESTURI/JE? KUTAHIRI WASICHANA NI HAKI?

Ni jambo la kutatanisha kidogo kwangu: Labda nianze hivi katika Tanzania tupo makabila tofauti. Na ni mengi na kila moja lina mila na desturi zake. Makabila 129 (130). Kwa hiyo hapa ninachotaka kusema ni kwamba hili jambo la kutahiri wasichana hasa wenzetu wamasai (pia nchi yenzetu jirani Somalia) lina maana gani? Kwa sababu wao wanadai wakishawatahiri ndo wanakuwa wanawake kamili na pia wanakuwa safi. Lakini papo hapo hawajui kama ni hatari sana :-

Tukianza na vyombo wanavyotumia, Je? Ni visafi au je wanabadili kwa kila mtoto hapana. Halafu kubwa zaidi je wanawapa ganzi? Hapana. Kwa sababu baada ya hapo inasemekana wanawashona na kuacha shimo ndogo sana kwa ajili ya kukojoa mkojo tu.

Je? Huyu msichana atapoolewa mnafikiri atapata maumivu kiasi gani wakati anatarajia kufanya tendo la ndoa kama sio mateso makali. Ambayo badala ya kuifurahia ndoa yake inakuwa kuijutia. Na itakuaje atapotarajia kuzaa. Kwa kweli na mateso makubwa sana atayapata. Ambayo atatamani hata asingeishi.

Kwa nini? Na je? ni safi kwa nani?. Kwa sababu msichana wa miaka mitano hawazi kuelewa ni nini kuwa mwanamke.
Na watoto wengi wamepoteza maisha yao wakati wa tendo hili, wengine wanapata tetanus, wengine wanapata mshtuko pia maambukizo mbalimbali. Tukiendelea hivi tutamaliza wasichana!!.

Tuesday, August 5, 2008

AGOSTI 5,2008 AFYA

Mwenzenu nahisi kuchanganyikiwa. Labda kwa sababu nina tamaduni/mila na desturi mbili najua mimi ni mtanzania na najua mila na desturi pia utamaduni wangu. Lakini sasa kichwa/akili yangu imevurugika kabisa:-

Ni hivi najua nyumbani TZ ni kawaida au labda niseme safi kama mtu umenenepa/nawili. Nakumbuka mwaka wa kwanza niliporudi TZ kusalimia watu walishtuka/shangaa sana na kuzani nilikuwa na ngoma au. Na baada ya miaka kadhaa nikarudi tena na wote walifurahi na kusema ya kwamba hivi ndiyo inavyotakiwa, wao walisema ya kwamba nilipendeza yaani niliongoza kilo kidogo nilinenepa. Na niliporudi hapa watu walisema eeh? Mbona unanenepa sana si vizuri inabidi upungue. Sasa nadhani mmegundua kwa nini nimesema nimechanganyikiwa. Ngoja niendelee kidogo kiundani au niseme kiafya nakubaliana na "waswidi" wazungu, lakini hali hii inanipa hofu kidogo kwani sasa hata watoto wadogo wanafuata mwenendo wa wazazi na marafiki pia, wanajinyima kula. Na wengine wanakula kama kawaida na baadaye wanatapika makusudi. Mnajua wanasemaje, eti wanataka kuwa wembamba, ndiyo wanapendeza. Lakini ukiwaangalia wanaonekana kama mti hata matako (wowowo) hawana.
Ndiyo najua kunenepa sana sio safi kwani kuna madara yake kama vile mshtuko wa moyo(heart attack) daibetes nk.

kama nilivyosema hapo juu mara nyingi sijui mimi ni nani na nchi gani ni yangu. ndio maana nimesema nimechanganyikiwa. Watanzania (waafrika) wanaona kunenepa ni safi na wazungu wanasema ni hatari, Na najua hakuna anayesema kweli au uongo. Je wasomaji mnasemaje Nisaidieni kidogo!!!!!!!!!