Wednesday, September 1, 2010

Sheria, Mila na Desturi pia Tamaduni pale Zinapotofautiana!!

Mama, baba na watoto, maisha ya ndoa!!

Mama na watoto wake peke yake!!
(Ensamstående )

Fuatana nami kwa habari hii fupi kuhusu maisha yalivyo tofauti:- Kwa miaka kadhaa iliyopita nchini Sweden kulikuwa na uhaba wa watoto. Yaani maisha yalikuwa magumu na watu walipunguza "waliacha" kuzaa watoto wengi. Baada ya Serikali kuona hivyo ikaja na sharia kuwa kila mtoto atayezaliwa basi wazazi watalipwa kiasi fulani kila mwezi mpaka mtoto atakapotimiza miaka 18. Pia ni kwamba kiasi cha malipo kitaongezeka mtoto wa pili atapozaliwa kama mtaliwa 2000SEK na sasa mtalipwa 4000SEK na mtoto wa tatu wa tatu mtalipwa 7000SEK huu ni mfano tu

Sasa tatizo jingine limeibuka sasa hivi tu, nilikuwa nasikiliza habari na nikasikia kitu ambacho sikuweza kuamini. Naweza kusema nilishangaa ama kweli TEMBEA UONE YA DUNIA. Ni hivi kama mmefunga ndoa na baadaye mnapata mtoto hapo kuna utaratibu kwamba wazazi mnapewa siku 480 kwa mwaka kuwa nyumbani na mtoto. Ni hiari yenu kama mnataka kugawana hizo siku au mzazi mmoja atabaki nyumbani na mtoto. Inaitwa (föräldraledighet) au kwa lugha ya kitaalamu ni (Maternity live) na hizo siku mnalipwa kwa kuwa nyumbani na mtoto wenu.

Ila sasa kama mnaishi bila kufunga ndoa (Sambo) hizo haki zote zitaenda kwa mama. Na halafu baba atakuwa hana haki hata ya kuwa na mwanae, kwa maana hiyo anakosa kile kipindi cha mtoto awapo mchanga kipindi ambacho kila mzazi/mlezi angependa kukishuhudia.

Mwisho, ni kwamba Sweden mume na mke wakiachana mtoto au watoto watakuwa wanafuatana na mama. Pia ni ruksa kuitwa ubini wa mama. Nimetoa mfano huu kwa vile Tanzania kama wazazi wanaachana watoto wanabaki na baba. Najua Tanzania ni Lazima kuitwa ubini wa baba au NIMEKOSEA tusaidiane .

9 comments:

Fadhy Mtanga said...

Mie nimezipenda sana hizo pozi za kwenye picha.

Subi Nukta said...

Kweli tembea uone. Sikuwa nayafahamu haya yote uliyoyaandika hapa kuhusu maisha ya Baba, Mama na Mtoto, sasa nimefahamu. Elimu haina mwisho. Asante!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

(Maternity live), sio lugha ya kitaalamu bali ni kiingereza kinachomaanisha likizo ya uzazi

hii ya mtoto na likiizo hata mimi naona ni kwa mama zaidi hata kama wanaachana, watoto ni wamama zaidi,.upendo wa mama ni muhimu sana

ubini wa mama?? hili sijui, mila na desturi ila kama mama hana mume kazalishwa tu, aweza tumia ubini wake kwani hamna noma ila kama ni ndoa, ubini ni wababa kwa tamaduni zetu kumbuka afrika mke akiozwa ni sawa na kauzwa mahali kuubwa hutolewa na ujenga ukoo mpya

Bennet said...

Haya mambo kweli tembe auone, hapa kwetu watu tunazaana tu hata kama hatujui kesho tutakula nini, maana kila mtoto anakuja na baraka zake

Anonymous said...

sasa unaonaje na wewe ukaongeza mtoto mwingine ili ufaidike na hizo pesa za bure?

emu-three said...

Unknwn mmoja hapo kanichekesha anasema wewe hutaki zaidi, yaani uongeze mtoto ili dau lipande...kuzaa na kulea sio mchezo!
Mila ndivyo zilivyo kutegemeana na mahala, wapo ambao hata wakati wa kuoa, mke ndiye anatoa mhari. Na ukiwauliza wanasababu zao za msingi. Na kwa vile wamezizoea mila zao wanaona kama kawaida tu.
Hayo ndio maisha, na maisha imetuwakilishia, ahsante dada yetu

Yasinta Ngonyani said...

Anonymous September 1, 2010 9:30 PM.nanukuu:- "sasa unaonaje na wewe ukaongeza mtoto mwingine ili ufaidike na hizo pesa za bure?" mwisho wa kunukuu. ha ha ha! eti niongeze ili nifaidi hizi pesa za bure, ndugu yangu ondoa hilo wazo la kufaidi kwani ingawa watu wanapata hizo pesa lakini maisha yako juu sana hata hivyo hazitoshi. Kwani si kulima mihogo hapo na inakua tu, na ukizingatia misimu ya mwaka ni totafuti sana na misimu yote inahitaji nguo zake nazo si za bure. Na bado hapo hujaingiza matibbabu kwani hao watoto si mawe ni lazima siku moja wataumwa. Kwa hiyo hapa sio kuzaa tu ili kufaidi pesa, la hasha , ni vipi utawatunza hao watot? kwa hiyo nadhani utakuwa umenielewa.

Sara Chitunda said...

Ni kweli kwa tanzania mtoto huitwa ubini wa baba.

Desderius Ngonyani said...

Nimesoma article yako inayohusu sheria,mila na desturi.miaka kumi na nne iliyopita nilikuwa mkoani mtwara ktk wilaya ya masasi ambako nilipangwa kufanya kazi ya ualimu ktk shule ya sekondari Ndwika.katika ujana wangu wote wa kusoma mpaka kusomea kozi ya ualimu nilikuwa nasoma tu kuhusu watoto wanaozaliwa katika ndoa huwa ni mali ya mama siyo mali ya baba na ukoo wake katika mikoa ya mtwara na lindi na si kama familia nyingi zinavyofanya hapa kwetu Tanzania.basi mikoa ya kusini hapa Tanzania siyo jambo la ajabu kuona mfumo huo wa watoto wanaozaliwa katika ndoa kuwa mali ya mama na hupewa majina ya upande wa mwanamke.Hata kitu kingine ambacho nilikiona ni ajabu kwangu ni kwamba mwanamume ukioa unatakiwa kwenda kuishi pale ukweni siyo kwenda kuishi mbali na wakweze.Ni kweli katika maisha ya ndoa ni vizuri kabla ya kuoa kuzingatia sheria,mila na desturi ili kuepuka mikanganyiko ambayo inaweza kutokea katika familia zetu.