" Uongozi unaweza ukawa mzuri au mbaya, au usiojali, lakini kama watu wameamka na wanajitambua wenyewe, kutoshirikishwa kwa mawazo na tabia ya jamii hakutaendelea kwa muda mrefu"
Chanzo: kutoka katika kitabu cha kipindi cha ujamaa na kujitegemea yakisemwa na mwal. Julius K. Nyerere.
3 comments:
Tatizo liko kwenye kuamka na KUJITAMBUA hasa ukizingatia kuna uwezekano mtu ukafikiri unajitambua kumbe UNATAMBULISHWA.
Na ukitambulishwa vizuri unaweza usistukie hujitambui.:-(
Wanasema usimwamushe aliyelala, akimuka, huenda ukalala wewe, sasa sijui utalala fofo-fo!
Watawala wengii wenye nia binfsi wanaitahidi kuhakikisha wananchi hawaamuki, hawaui nini kinachoendelea, hawashirikishwi kwenye mambo yanayoadiliwa na `viongozi' Mkiulizwa mtaambiwa `hayawahusu' lakini kumbe yanawahusu!
Sasa huyu mtu akiamuka akajua na kujitambua, wewe mtawala binafsi upo pabaya...kiti kitakuwa hakikaliki!
Ujumbe mzuri kwakweli
Wakuu mmemaliza yoooote.
Mkuu Mtakatifu hakika umelonga, sina jipya ingawaje ninalo wazo kichwani na ruksa kulibishia hilo wazo.
Post a Comment