Tuesday, September 21, 2010

CHAKULA CHA USIKU: WAHANGA SASA NI WANAWAKE!

Mwambie, usione haya
Zamani ilikuwa ni wanaume waliokuwa wakilalamika, kwamba wake zao hawataki kuwapa chakula cha usiku kama wanavyotaka. Lakini baadae yaani siku hizi ni zamu ya wanawake kulalamika.

Katika nyumba nyingi siku hizi hasa mijini wanawake ndio wanolalamika zaidi kukosa chakula cha usiku kama wanavyotaka kutoka kwa waume zao.

Kwa nini hali hii?

Ukweli ni kwamba maisha yamebadilika sana na kila mtu anajitahidi sana kutaka kuhahakisha kwamba anafanya kazi hadi anaishiwa nguvu kabisa, akili na mwili vinachoka. Wanaume wengi wanaolalamikiwa na wake zao kuhusu kupata uhaba wa chakula cha usiku ni wale wanaofanya kazi sana.

Ningependa kuwashauri wanaume kwamba wakati wanafanya kazi zao mchana wakumbuke kwamba kuna wake zao wapendwa ambao wanawasubiri jioni kuzungumza nao na zaidi ya hapo. Wakumbuke hawajaoa kazi bali wameoa wake. Pamoja na kwamba ni muhimu kwao kufanya kazi, lakini wakumbuke kwamba kazi hazina mwisho.

Kuna jambo ambalo wanaume na hata wanawake hawalijui vizuri, hili ni lile linalohusu mazoezi. Mtu anapofanya mazoezi anawezesha damu kuzunguka na kufikia sehemu zote za mwili kwa kiwango kinachotakiwa. Kukaa ofisini kutwa na kurudi nyumbani na kukaa kwenye kochi na kuangalia TV siyo aina ya maisha inayoshauriwa tuishi. Mwili unapochangamka kwa damu kufika kila mahali kwa kiwango kinachotakiwa hamu ya kutoa chakula cha usiku na kukipokea huwa kubwa.

Lakini mbaya zaidi ni kwa wanawake wenyewe pia. Kuna wanawake ambao bado wanaishi kwa miiko ya karne moja nyuma. Hawa wanangoja wanaume zao wawachokoze, wasipofanya hivyo, basi hata mwaka watakaa wakilalamika kwamba hawapati chakula cha usiku. Tukumbuke kwamba hata wanaume nao ni binadamu pia, huhitaji wakati mwingine kushtuliwa, kwani wakishtua wao tu kila siku, kuna wakati hukinai.
Habari hii nimeipata toka blog ya kaka Shaban Kalus fungua hapa kumsoma zaidi. Naamini kila mara kurudia kusoam jambo/somo ndo tunazidi kujifunza maishani.

13 comments:

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

mmh!

Luisa said...

Wewe vipi unamshituaje?mimi naogopa siku mojamoja kumshitua,,tupe njia yakumshitua basii,,wengine ukimshitua vibaya atakudhania umeanza umalaya pengine labda.

MARKUS MPANGALA said...

SWALI: binadamu bwana? au unabisha kama siyo kweli tunaogopa nafsi zetu kuwa tunajiogopahata kusema kuwa nanogea ubani wakati umezoea kujifariji na udi???

CHAUKULA CHA USIKU?? duh! watu nwana? unabisha? kwakuwa ipo CHAI, CHAKULA CHA MCHANA na CHAKULA CHA USIKU.... na kwa vile vyakula hivi huiingia tumboni kupitia mdomoni... je CHAKULA CHA USIKU NI KIPI? na kama wahanga ni wanawake ni CHAKULA GANI WASICHOSHIBA?

NDIYO;;;; tunajua kila mtu akishiba anasema AMETOSHEKA.... na asiposhiba anasema hajatosheka.... je yote haya ni kula chakula kipi kimwngonezeacho utamu ajue kuwa CHAKULA CHA USIKU ni kitamu kinamtia hamu USIKU?

natafuta CHAKULA CHA MCHANA, NA ALFAJIRI ya wikiendi ya mama kisabengo akijipumzisha na baba mwajuma wakati mwishoni mwa juma ile anaposema mama kisabengo ile sindano iko wapi siioni hapa chumbani njoo unionyesheeeeee, akifika ni CHKULA CHA......(1). USIKU? (2) MCHANA? (3) MWANGAZA?...
utamu wa CHAKULA CHA USIKU haufanani na ule wa CHAKULA CHA MCHANA chenye vitunguu na nyanya pamoja na pilipili adoado??? nawaza tu hapa mheshimiwa nafikiri kula na kushiba CHAKULA cha usiku nami nikitafute maana sikijui vema...

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kwani ni lazima? ni muhimu?? achana navvyo ni dhambi kwanza

Anonymous said...

chakula cha usiku, muhimu kwa afya na kinapumzisha akili na mtu anaamka vizuri, japokuwa wanaume wengi wanashindwa kuhudumia wake zao kwa kuwapa chakula cha usiku kwani mchana kutwa wanahangaika na wanawake wa nje hivyo ifikapo usiku wako hoi bin taaban....

Baraka Chibiriti said...

Kuambizana ni mhimu...ukitolewa nje basi unalala mzungu wa nne!

emu-three said...

Hilii ni tatizo kubwa sana, na watu wanalipuuzia wakisema `haya ni maswala ya faraghani. Ni sawa ni ya faraghani, basi tuyazungumze kifaragha, watu hawazungumzi, mwisho wa siku wanakuja kulalamika,
'ooh, mbona wangu ananipa mgongo, oooh, mbona hivi mbona vile...'
Kaeni mzungumze, jadilianeni maswali yenu, na hili lipewe kipa-umbele kwa wanandoa!
Nashukuru dada Yasinta umeliweka hadharani, kwani kesi nyingi zinatujia, na ni rahisi kumshawishi mwanamke, kuliko mwanaume...eti mkuu Chacha hebu niunge mkono kwa hili. Mwanaume ashauriwe kuhusu ndoa yake...mmmmh! Lakini wakati umefika kwani kununua `viagra' nk sio suluhisho, suluhisho ni kujifunza `nini na ni vipi' mahusiano yanajengwa! Wapo wataalamu, vipi vijarida na hata kanda zilizoizinishwa kitaalamu!

malkiory said...

Yasinta, hapa majuu wanawake wanalalamika kuwa wakati mwingine wiki moja au hata mbili zinapita bila hata chakula cha usiku japo wanashare meza moja! Lakini sidhani kama hilo ni tatizo kwa sisi waafrika,wanaume wa kiafrika hushambulia dinner bila hiyana, ndiyo maana hapa ulaya mwanaumewa kiafrika ni dili! hahahaaa

Simon Kitururu said...

Chakula hiki hunoga tu sana tu asubuhi pia.

Kama umechoka usiku breakfast basi utoe. AU?

Gerge Olloo said...

kwa kweli waume wanajitihidi kufanya kazi zaidi mchana ili mke wake
aweze kupata maitaji yake lakini anaopofika home mke naye kawa mbogo
kwa hiyo hata kama alikuwa ajachoka sana anakata tamaahatimaye anaamua
kulala kwa hiyo wanawake waqnatakiwa kuwa wamechoka ajue jinsi gani ya
kumrudisha katika hali ya kufanya tendo hilo

Anonymous said...

Estоs mensaϳes dеl depredaԁοr
thе usаge poweг enԁ up еxhаusting the ρartnегѕ
pгеemіnent to intelligent nаp.

I learnt as а kid that уou had to holԁ ωrath phуsicаlly in the tгunk thrοat, аnd is crеditeԁ with communication and increase through aspect.
To smell youг salts use theгapeutical gгad in head, let those who wish try tantric maѕsаgе.

Τherе arе more oг less 2,000 to look to her for way but ωould κind of he
follow his own management.

My blog post; site

Gerd Ulrich said...

Maisha yangu Maajabu yanashangaza ushuhuda, Jinsi nimepata kisanduku chenye nguvu sana ambacho sasa ni pesa yangu mara mbili kutoka mia hadi elfu ya pesa ndani ya masaa 24, na pia jinsi nimerudisha mpenzi wangu wa zamani, sababu kuu niliwasiliana na Dk Lomi kwa msaada mimi kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, basi ananisaidia ni nguvu kubwa ya kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, na ananipenda na ananithamini sasa, basi mimi na Dr Lomi tukawa marafiki, baada ya mazungumzo kadhaa namuuliza ikiwa kuna njia anaweza kuniganga ili nipate pesa, hapo ndipo aliponiambia juu ya sanduku hili la uchawi, akaniambia kuna aina na saizi tofauti ya sanduku, aliniambia aina zote za sanduku, ningeweza kumudu ndogo tu ya sanduku, baada ya maombi muhimu anayofanya kwenye sanduku, ananipeleka kupitia huduma ya kujifungua, aliniambia niweke pesa ndani, niliweka ndani ya sanduku 100 euro baada ya masaa 24 nikagundua ilikuwa elfu 10 euro ndani, na nimekuwa nikitumia sanduku kwa miezi 7 sasa, mimi na mchumba wangu tunaishi maisha bora, ikiwa unahitaji b ack mpenzi wako au pesa spell wasiliana na Dr Lomi kwa barua pepe: lomiultimatetemple@gmail.com au WhatsApp namba +2349034287285 unaweza pia kumwandikia kupitia Jina la Mtumiaji la Snapchat: drlomi20 atakusaidia nje, asante kwa kusoma,

Kwaheri Gerd Ulrich

Anonymous said...

Sikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe nikiwa nimesimama peke yangu bila mwili kusimama na mimi na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na mchawi huyu wa hodari Dk. ASUBUHI, baada ya kumueleza hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi akiniomba kuwa hatawahi. niache tena, miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa pia una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
*penda uchawi
* kama unataka ex wako nyuma
* Acha talaka
*kuvunja mawazo
* huponya viharusi na magonjwa yote
* uchawi wa ulinzi
*Ugumba na matatizo ya ujauzito
Wasiliana na Dk DAWN kwa barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
Whatsapp: +2349046229159