Tuesday, September 28, 2010

HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA KAKA YANGU SHABAN KALUSE


Kaka Shaban Kaluse
Napenda kukutakia HONGERA kwa siku yako ya kuzaliwa, na nakutakia kila la kheri kwa kila jambo utakalotenda liwe jema na pia nakutakia maisha mema, upendo na amani itawale katika familia yako. Na halafu uwe na mafanikio kwa kila utakalo tenda. Halafu najiuliza hivi siku hizi sijui upo wapi wewe kaka wa utambuzi ? HAYA HONGERA SANA KWA SIKU HII MUHIMU KATIKA MAISHA YAKO. HONGERA KAKA SHABAN!!!!!. Kwa kutaka kujua mambo ya mwanautambuzi huyo gonga hapa.

12 comments:

emu-three said...

Twampa hongera sana kwa siku ya kukumbuka uzawa wake. Namuona kaadimika kidogo, lakini najua yupo katika muwajibiko fulani. Ahsante dada Yasinta kwa kulikumbuka hilo!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Hongela kaka! Uishi miaka mingi...

chib said...

Hongera Kaluse, tarehe hii pia ni muhimu sana kwangu, ingawa siyo siku yangu ya kuzaliwa!

John Mwaipopo said...

'ongela' shaban kaluse kwa kuchana kalenda.

chib ni siku ulipofanikiwa jambo gani?

Simon Kitururu said...

Kikore Hongera avae!

Mija Shija Sayi said...

Hongera sana wajameni.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kaluse. Hongera na uzidi kubarikiwa.


Ng'wanambiti - vipi tena? -r- za Wakurya zimeanza kukushinda kwani naona umegonga "hongela" Au umeanza kugeuka kuwa Msukuma??? Bagishage!

EDNA said...

Hongera kaka Kaluse. Nakutakia kila rahel.

Fadhy Mtanga said...

japo nimechelewa, lakini duwa kwa Mwenyezi Mungu huwa haichelewi.. Nami napenda kutumia fursa hii kukutakia kaka Shabani heri ya siku ya kuzaliwa.
nilitamani leo ningekutana nawe walau tunywe kahawa lakini isivyo bahati nimerejea saa moja jioni kutoka Unguja.
kaka, ninamwomba Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu sana, si tu maisha marefu, bali pia akujaalie furaha, amani, upendo na mafanikio daima.
pamoja sana kaka.
upendo daima.

Unknown said...

Ahsanteni sana kwa kunitakia heri katika kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa.
Awali ya yote ningependa kumshukuru dada yangu Yasinta kwa kuniwekea kumbukumbu hii katika kibaraza chake.
Ni kweli nimeadimika sana mtandaoni na hiyo imetokana na chagizo za kimaisha.
Kwa sisi wanaadamu huwa tunakumbwa na mabadiliko ya kimaisha kila uchao, kuna wakati waweza kujikuta ukiwa hapa na wakati mwingine ukiwa kule.
Ni katika mabadiliko hayo nami nimejikuta nikiwa kule katika kuweka sawa mustakabali wa maisha yangu ya mbeleni na familia yangu.
Umri unasonga mbele na Kayumba wangu anayo matarajio makubwa kwangu...sitaki nimuangushe, na ndio maana nimejikuta nikiwa mbali na wanablog wenzangu.

Ingawa sijaonekaan kwa kitambo kidogo, lakini sijawasahau na naamini hata ninyi hamjanisahau pia.

Nawaahidi nitarejea siku si nyingi.

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua nafasi kwa kuwashukuruni wote kwa kumtakia kaka ndugu yetu siku ya kuzaliwa pia mafanikio meme. Ahsanteni sana. UPENDO DAIMA!!!

MARKUS MPANGALA said...

Waaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaoooooooooooooooooooooooooooooooooooo nimecheewaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
KALUSEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE tupo pamojaaaaaaaaaaaaaaaaaa kaka