Showing posts with label usawa. Show all posts
Showing posts with label usawa. Show all posts

Tuesday, September 18, 2012

UJUMBE WANGU WA LEO:- WASICHANA NA WANAWAKE WANA HAKI!!

Watu wote ni sawa, watu wote wana thamani sawa. Hii ina maana kuwa wanawake na wanaume, wasichana na wavulana, wana haki sawa. Lakini katika jamii zetu wanawake na wasichana wananyimwa haki zao.
Hatua ya kwanza kuleta usawa ni kuielewa na kutokuukubali unyanyasaji wa wanawake na wasichana
JUMANNE NJEMA NDUGU ZANGUNI!!!

Wednesday, December 3, 2008

KWA NINI WANAUME/AKINA BABA WENGI WANAFIKIRI WAO NDIO WAAMUZI/WAFALME WA NYUMBA?

Suala hili limekuwa likinikera sana akilini mwangu kwa miaka mingi. Ya kwamba akina baba/wanaume wao wanafikiri kazi yao kubwa katika nyumba ni kuwa MUME/BABA basi. Mara nyingi utasikia wanasema mimi ndio mkubwa wa nyumba. Na kama wanafanya kazi za ofisini basi ndo itakuwa kero mno. Kwani hapa atataka anaporudi toka kazini akute chakula mezani, maji ya kuoga bafuni tena ya moto, nguo zmepigwa pasi n.k. Na kinyume kama hana kazi basi atakuwa anashinda kilabuni(UGIMBI) na akirudi toka huko basi ni kelele tu, hakuna amani wala maelewano

Bado naendelea, kuna wengine wanaona kupika, kulea watoto, kutafuta chakula ni kazi ya wanawake. Yaani hawawezi hata kujipikia chai kwa vile wao ni wanaume au hata kumbadili mtoto nepi, Mtoto amabaye ni wake. Kikubwa wanachofanya ni kukaa kitini/sofani na kuletewa kile wanachotaka. Wanasahau kabisha jambo la USAWA.

Bado wanaishi dunia ya mababu, mababu na mababuzi. Tuache UBINAFSI tuishi kwa kushirikiana/kusaidiana kwani wote ni SAWA. Nasema tena tuishi kwa kusaidiana hapo wote tutafurahia maisha. Tuache mambo ya UTUMWA.