Showing posts with label umoja. Show all posts
Showing posts with label umoja. Show all posts

Tuesday, May 5, 2015

ENZI HIZO WATU WOTE WALIKUWA SAWA....

Ni kweli, zamani kulikuwa na Kanisa moja,  hospital moja, chama kimoja, shule moja kila kijiji, watu walikuwa wakitembeleana na walikuwa wajamaa...pia hata chakula tulikuwa tunakula sahani moja ...

Friday, November 22, 2013

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA HAPO KALE UJAMAA, UMOJA, USHIRIKIANO NA UNDUGU !!!

 
Lakini leo /sasa kila mtu na chake. Hakuna tena ule umoja wa kunywa pamoja, kula pamoja na kusali pamoja. Je? kwa nini umoja wetu umepotea?----Nawatakieni wote Ijumaa njema ila usiwe ugimbi/ ulanzi/ pombe...mwingi/nyingi ,,Lol

Saturday, October 18, 2008

JAMHURI YA SAHARA MAGHARIBI


Marocco ilijitoa kwenye Umoja wa Nchi Huru za Afrika Mwezi Novemba 1984 baada ya Umoja huo kuitambua rasmi Jamhuri ya Sahara Magharibi kama Nchi Huru.

UMOJA WA NCHI HURU ZA AFRIKA

Umoja wa Nchi huru za Afrika uliundwa tarehe 25 mei 1963 na Nchi Huru 32 huko Addis Ababa. Malengo ya Umoja huu ni kudumisha Umoja wa Udugu baina ya Wanachama wake, Ukoloni katka Afrika na kukuza ushirikiano wa Kimataifa. Baraza la Wakuu wa nchi hizi hukutana kila mwaka kuratibu masuala mbalimbali ya Kisiasa, Kiutamaduni, Afya, Sayansi na Ulinzi. Mpaka mwaka 1987 Umoja huu ulikuwa na Wanachama 50

BENDERA ZA CHAMA CHA SWAPO+CHAMA CHA ANC+CHAMA CHA PAC


Chama cha SWAPO kinachopigania Uhuru wa Namibia, Vyama vya ANC na PAC vinavyopigania haki na kupinga siasa ya ubaguzi wa rangi huko Afrika ya kusini, vinashiriki katka vikao Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) kama wasikilizaji