Sunday, March 31, 2013

NAPENDA KUWATAKIENI PASAKA NJEMA NA YENYE AMANI NA BARAKA TELE....!!!!

Ni PASAKA LEO..Je unajua pasaka ni nini? angalia hapa chini:-
P-Pokea
A-Amani
S- Sasa
A- Ambayo
K- Kristo
A- Ametupa-
Mungu awatangulie katika PASAKA HII. AMANI IWE NANYI. AMINA- PASAKA NJEMA KWA WOTE.

Friday, March 29, 2013

JENGO LA GHOROFA 12 LAPOROMOKA TANZANIA ..

Inaarifiwa takriban watu zaidi ya kumi wamefarriki na wengine bado wamenaswa kwa vifusi
 
Takriban watu watatu wamethibitishwa kufariki baada ya jengo lenye ghorofa zaidi ya kumi kuporomoka mjini Dar es Salaam, Tanzania.
Waokozi wanaendelea na shughuli ya kuwatafuta na kuwaokoa manusura na wanasema kuwa hadi sasa watu kumi na watatu waliokuwa wamenaswa wameokolewa.
Zaidi ya wengine arobaini wangali wamenaswa chini ya vifusi.
Shughuli ya ujenzi ilikuwa inaendelea kwenye jengo hilo wakati lilipoporomoka katikati mwa mji wa Dar es Salaam.
Miongoni mwa watu ambao wangali kupatikana ni wafanyakazi wa mjengo na watoto kutoka shule jirani ya mafunzo ya dini ya kiisilamu.
Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo, watu walisikika wakipiga mayowe kutaka msaada.
"nilidhani lilikuwa tetemeko la ardhi, na kisha nikasikia mayowe,'' alisema shahidi mmoja.
Jengo hilo liko katikati mwa Dar es Salaam na liliporomoka saa tatu kasorobo asubuhi kwa saa za Afrika mashariki.
Mamia ya watu wanaaminika kuwa ndani ya jengo hilo huku wengine wakiwa nje wakati wa ajali hiyo . Hata hivyo idadi kamili ya watu hao bado haujulikani.
Habari na picha BBC

NATAMANI SIKUKU HII YA PASAKA NINGEKUWA RUHUWIKO TENA KAMA X-MAS HII 2012 NYUMBANI RUHUWIKO..!!!IJUMAA KUU IWE NJEMA KWA WOTE!!!

Hapa ni nje ya kanisa la Ruhuwiko mwaka jana mwishoni siku ya x-mas. Hakika nilijisikia RAHA sana angalia mwenyewe jinsi umati wa watu ulivyokuwa. Nimekaa hapa na naota/natamani pia pasaka hii ningekuwa hapa. IJUMAA KUU IWE NJEMA KWA WOTE NA MSISAHAU HAKUNA KULA NYAMA LEO...

Thursday, March 28, 2013

SWALI NILILOULIZWA NA NIKASHINDWA KUJIBU....

Leo nimeulizwa swali hili ..ilianza  hivi:- Kuna swali linanisumbua katika kichwa changu ngoja niulize ili tusaidiane...haha hivyo nikashindwa lakini nikakukumba kwenye wengi hakiharibiki kitu. Na swali lenyewe likawa kama ifuatavyo:- Laiti jana ingekuwa kesho, leo ingekuwa Ijumaa. Je? mwalimu aliyasema haya siku gani?

Wednesday, March 27, 2013

MVUA JIJINI DAR ZAZUA MAFURIKO.....PICHA JUMAPILI 24/3

 Hapa hata kutoka nje tu huwezi labda kuwe na mtumbwi ila maji yameingia hadi ndani....
Hapa picha zote mbioli ni Tandale kwa Mtogole. Picha nimetumiwa na mdogo wangu ...

Monday, March 25, 2013

KAPULYA HAKUSANYI SCALF TU HAPANA MAWE NA BIRIKA PIA..

 Hapa ni aina mbalimbali za rangi za mkusanyiko wa SCALF(HALSDUKAR) zake..hapa ziko zaidi ya 30....katika mwezi kila siku natumia moja :-)
 Halafu ana mtindo wa kukusanya MAWE kila sehemu anayokwenda/nchi anayokwenda anaporudi anarudi na jiwe...halafu..
 
....kwa vile kapulya ni mnywaji sana wa chai basi anapenda sana BIRIKA hapa ameanza tu kukusanya birika...je na wewe msomaji kuna kitu ambacho unakusanya?


TUANZE JUMATATU HII NA UJUMBE HUU-: PALE MTU ANAPOUMIA KWA AJILI YA KUPENDA /PENZI!!!!

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMATATU NJEMA SANA...

Sunday, March 24, 2013

LEO NI JUMAPILI YA MATAWI...IWE JUMAPILI YA AMANI NA BARAKA KWA WOTE...


Napemda kuwatakieni wote jumapili ya matawi iwe njema sana kwa wote pia iwe yenye amani, bara ka upendo..JUMAPILI NJEMA SANA WOTE.

Saturday, March 23, 2013

KUMBUKUMBU...LEO NI MIAKA MIWILI TANGU MPENDWA WETU ASIFIWE NGONYANI ATUTOKE

ASIFIWE KATIKA UHAI WAKE NYUMBANI RUHUWIKO
Ni vigumu kuisahau tarehe 23/3/ 2011.Imetimia  miaka miwili leo tangu ndugu yetu mpendwa Asifiwe atutoke.MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA. AMINA.....TUTAKUKUMBUKA MILELE....

Friday, March 22, 2013

Wednesday, March 20, 2013

MSIBA..DADA MARIANA HATUNAYA TENA...

 
 
 

 
Kama mnawakumbuka picha hii na tukio lake basi ni kwamba Dada mkubwa Mariana Kutoka nchini Angalo katika picha kushoto mwenye miwani katuacha ghafla leo . Ni masikitiko makubwa sana kwa familia yake marafiki na jamaa. Da Mariana alikuwa mtu mmoja ambaye ni mcheshi, makarimu na mwenye kupenda sana watu. Kwangu ni pigo kubwa sana, kwani yeye alikuwa mtu muhimu sana kwangu, zaidi ya rafiki...alikuwa hakosi kunifariji pale nilipokuwa na matatizo.. nimepatwa na mshtuko wa ajabu kwa kweli...hebu soma hapa. MWENYEZI MUNGU NA AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI...AMINA

TANZANIA NCHI YANGU ...NAKUPENDA TANZANIA

Nitakutangaza nchi yangu tanzania,nakupenda Tanzania nchi yangu Tanzani na najivuna kuwa mTanzania.JUMATANO NJEMA KWA WOTE...

Monday, March 18, 2013

MSONGAMANO WA MAGARI/FOLENI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM!!!

Nimekuwa nikijiuliza muda mrefu sasa kuhusu foleni katika Jiji letu la Dar es salaam. Nianze hivi hivi kwanini watu wanaishi nyumba moja na kila mtu anakuwa na gari lake? Kwanini wasitumie gari moja?
Kwanini tusiwekeane zamu kutumia gari moja kwa wiki na hata mwezi..kwa mfano mfanyakazi mwenzako au jirani..hii ingepunguza sana gharama za mafuta pia foleni zingepungua kwa kiasi fulani. Haya ni mawazo yangu..karibuni sana tujadili kwa pamoja...Kapulya

KUTANA NA YASINTA, MJASIRIAMALI ALIYESEMA HAPANA KWA WANAUME WAKWARE

Leo nimemkumbuka sana mdogo wangu wa hiari KOERO MKUNDI..sijui yupo wapi. nimemiss sana uandishi wako ambao ninauhusudu sana na ndio maana nimeona niweka moja ya makala azilizoandika na iliyonigusa sana. Kumsoma zaidi mdada huyu ingia hapaNusura niwe mtoto wa mitaani
Juzi ijumaa nikiwa ofisini kwangu alipita binti mmoja akiwa na begi lake dogo kama yale yanayotumiwa na wanaume kubebea Lap Top.
Alinisalimia kwa uchangamfu na kujitambulisha kwangu kuwa anitwa Yasinta. Alionekana kuwa mchangamfu utadhani tunafahamiana siku nyingi, hata hivyo na mimi nilimchangamkia pia. Kumbe Yasinta ni mfanyabiashara wa kuuza viungo mbalimbali kama vile vya Pilau, viungo vya Chai, kwa kweli sikujua kama chai nayo ina viungo, pia alikuwa na viungo vya kupikia nyama , samaki au hata kuku na hasa kuku wa kienyeji na alitumia muda huo kunifundisha namna ya kutumia. Kwangu mimi hayo yalikuwa ni mapinduzi makubwa katika mapishi ya vyakula vya kiswahili
Yasinta Alionekana kuwa ni mdogo kiumri yaani ukimuangalia kwa haraka haraka anaonekana kuwa na umri wa kama miaka 18, hata hivyo sikukosea sana kwani nilipoomuliza umri wake aliniambi kuwa ana umri wa miaka 19 na mwishoni mwa mwaka huu ndio atatimiza umri wa miaka 20. Mara akaja jirani yangu mmoja ambaye ofisi zetu zinafuatana, alipomuona Yasinta alimshangilia sana na kuwaita wenzake na kuwajulisha ujio wa Yasinta, nilibaki nimeduwaa.
Baadae niliambiwa kuwa Yasinta alikuwa ni maarufu sana pale kwani alikuwa akiwauzia viungo vya mbalimbali na hivyo kufurahia mlo wao wa siku. Waliniambia kuwa walimfahamu Yasinta takribani miaka mitano iliyopita tangu alipoanza kuwapitishia ile biashara, wakati huo akiwa ni binti mdogo sana kwa umbo na umri.
Ni mwaka jana mwishoni alipowaaga kuwa anatarajia kufunga ndoa, na walimchangia fedha na zawadi nyingine. Tangu wakati huo Yasinta hakuonekana mpaka wakadhani labda ameamua kuachana na biashara hiyo, au mumewe amemkataza kuendele nayo.
Nilinunua viungo mbali mbali na niliamua kutumia fursa hiyo kufanya mazungumzo nae.
Yasinta alianza biashara hiyo mnamo mwaka 2005 Mara baada ya kumaliza darasa la saba mkoani Mbeya.
Je alifikaje mjini?
Yasinta alikuja mjini mwaka 2004 akiwa ndio amemaliza darasa la saba, baada ya kuwa hakufaulu na mama yake kutokuwa na uwezo wa kumuendeleza kielimu alichukuliwa na mama mmoja aliyekuwa akiishi maeneo ya Ilala hapa jijini Dar es salaam mwenyeji wa huko huko Mbeya ili kuja kufanya kazi za ndani.
Baba yake alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu wakati alipokuwa darasa la nne na kuanzia hapo majukumu ya kutunza familia aliyabeba mama yake pekee. Akiwa ni wa kwanza kuzaliwa na binti pekee kwa wazazi wake huku akifuatiwa na na wadogo zake wawili wa kiume, hakuwa na jinsi ilibidi aje mjini kufanya kazi za ndani ili aweze kumsaidia mama yake kuwatunza wadogo zake.
Alidumu na yule mama kwa mwaka mmoja. Lakini kutokana na mateso ilibidi atoroke na kujikuta akishia mtaani. Siku moja katika mizunguko yake ya kutafuta kazi alikutana na mabinti wa umri wake ambao walikuwa wakijiuza maeneo ya Buguruni na walimtaka ajiunge nao ili kujitafutia kipato, na walimuhakikishia kuwa shughuli ile ya kujiuza ina kipato kushinda hata ya kuajiriwa, hata hivyo Yasinta alikataa kata kata kujiunga nao, akamua kujichanganya na wale mama ntilie pale Buguruni CCM kwa kuwasaidia ili kujipatia kipato, hata hivyo mama mmoja allijitolea kumpa hifadhi.
Siku moja akiwa katika shughuli zake kama kawaida, alipita mama mmoja na kuagiza chakula, wakati akimuhudumia na kwa kuwa alikuwa ndie mteja pekee kwa wakati huo alianza kuzungumza nae. Katika mazungumzo yao yule mama alimjulisha juu ya biashara ya Viungo, mbalimbali vya mapishi ambayo ndio aliyokuwa akiifanya. Yasinta alivutiwa sana na ile biashara na kwa kuamini kuwa ule ulikuwa ndio wakati wa kuondokana na kazi za kutumwa, alimuomba yule mama amfundishe namna ya kufanya ile biashara.
Kwa bahati nzuri yule mama alimkubalia na na kuahidi kumpitia kesho ili wafuatane nae ili akamuoneshe mahali anaponunulia na kumuonesha namna ya kutayarisha.
Na kweli yule mama alimpitia kesho yake. Yasinta alimuaga yule mama aliyempokea pale Buguruni na kuondoka na yule mama kuelekea Kariakoo kufanya manunuzi.
Yule mama alijitolea kumpa hifadhi ya muda nyumbani kwake maeneo ya Vingunguti na kumfundisha namna ya kutengeneza viungo mbali mbali, Kutokakna na bidii aliyonayo ilimchukua Kiasi cha mwezi mmoja Yasinta kufudhu mafunzo hayo.
Yule mama alimkopesha Yasinta mtaji wa shilingi elfu kumi wa kuanzia.
Yasinta anakiri kuwa awali alikuwa na wakati mgumu sana kutokana na biashara kuwa ngumu lakini yule mama alimpa moyo wa subira.
Haikuchukuwa muda mrefu hali ilibadilika na biashara kumnyookea na kuweza kulipa mkopo aliokopeshwa na yule mama yake mlezi ambaye alimfanya kama mama yake mzazi kutokana na kumlea. Ilimchukuwa mwaka mmoja Yasinta kuhama na kupangisha chumba chake maeneo ya Buguruni na kuanza kujitegemea huku akiendelea na biashara yake hiyo ya viungo. Kuanzia hapo akawa anatuma hela kwa mama yake huko mbeya ili ziweze kumsaidia.
Mwaka mmoja baadae Yasinta alifanikiwa kununua kiwanja chenye ukubwa wa nusu eka maeneo ya Kinyerezi na ili iwe rahisi kwake kujenga. Ikabidi ahamie Segerea ili awe karibu na kiwanja chake. Taratibu alianza kujenga nyumba yake ya vyumba viwili. Ilimchukua mwaka mmoja na nusu kukamilisha nyumba yake ya vyumba viwili na kufanikiwa kuweka umeme na kuhamia nyumbani kwake. Lengo lake la kwanza likafanikiwa.
Yasinta alijiwekea malengo makuu matatu, wakati alipoanza biashara ya viungo.
Aliyataja malengo hayo kuwa ni kujenga nyumba yake mwenyewe, kukarabati nyumba ya mama yake kule Mbeya na kuwasomesha wadogo zake mpaka chuo kikuu.
Baada ya mdogo wake anayemfuatia kumaliza darasa la saba mwaka juzi akamleta na kumuandikisha katika shule ya sekondari ya binafsi iliyoko maeneo ya Ubungo na gharama za masomo analipa yeye kutokana na biashara yake ya viungo anayofanya.
Je Yasinta amemudu vipi kufikia hapo alipofikia na nini matarajio yake? Nilimuuliza.
Yasinta alikiri kuwa subira na uvumilivu ndio umemfikisha pale alipo sasa, kwani kuna wakati biashara ilikuwa haitoki kabisa mpaka anashindwa kulipa kodi ya nyumba, lakini kwa kuwa alikuwa amejiwekea malengo alihisi kuwa alikuwa na deni kubwa mbele yake na hiyo ilimpa hamasa ya kutokata tamaa na aliamini kuwa atafanikiwa.
Anasema aliponunua kiwanja alianza kuishi kwenye nyumayake kabla hata hajaijenga, kwani alikuwa akijiona kabisa kuwa amejenga na alikuwa akiiona nyumba yake ikiwa imekamilika kabisa, hakudhani kama atashindwa, aliamini tu kuwa ataweza.
Vipi kuhusu wanaume?
Nilimuuliza kwa kuwa yeye ni binti ambaye bado ni mbichi, kabla hajaolewa aliwezaje kukabiliana na vishawishi vya wanaume hasa ikizingatiwa kuwa alikuwa akiishi peke yake na shughuli zake ni za kuzunguka maofisini?
Yasinta alikiri kuwa alikuwa akipata sana mitihani ya kutakwa na wanaume, wengine wakiwa ni wababa wazima wakuweza hata kumzaa mara tano lakini alikuwa amejiwekea nadhiri ya kutofanya mapenzi kabla ya ndoa, pia alikuwa amepanga kuwa hataolewa mpaka awe amejenga nyumba yake mwanyewe, kitu ambacho amefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Je alimpataje Mwezi wake?
Yasinta alicheka kidogo, huku akiongea kwa aibu kidogo, alisema, “ Huyu mume niliyekuwa nae nilijuana nae miaka miwili iliyopita wakati akisoma sekondari wakti huo, tulikuwa tukikutana mara kwa mara kituoni tukisubiri usafiri wa daladala wa kwenda mjini. Kutokana na usafiri wa daladala Segerea kuwa ni mgumu tulikuwa tukigombea mabasi pamoja, siku moja akanilipia nauli, nilikataa kwa kuwa niliona kuwa yeye ni mwanafunzi, kwa hiyo haikuwa ni vyema anilipie nauli, lakini alisisitiza kunilipia na akakataa kupokea hela yake aliyomlipa kondakta wa daladala, na huo ukawa ndio mwanzo wa kufahamiana kwetu.
Baada ya kumaliza masomo alijunga na chuo kimoja mjini na kusomea mambo ya information Technology, na sasa ameajiriwa na kampuni moja binafsi akiwa ni mtaalamu wa kompyuta”.
Je mumeo anayo mikakati gani ya kukuendeleza kielimu, au ndio umeridhika na kiwango cha elimu ya darasa la saba ulicho nacho? Nilimuuliza.
Yasinta alisema kuwa ameanza kusoma masomo ya sekondari ya jioni katika shule moja ya binafsi iliyoko Tabata na ndio ameanza kidato cha kwanza ambapo itamchukua miaka miwili kumaliza kidato cha nne.
Ukweli ni kwamba nilifurahishwa sana na mazungmzo yangu na Yasinta, kwani ni miongoni mwa mabinti wachache hapa nchini wenye mtazamo chanya kuhusiana na maisha, na ameonesha kuwa, ukiamua unaweza, kwani hakuna kisichowezekana chini ya jua, kinachotakiwa ni kujiwekea malengo na kuwa na nia na dhamira ya kufikia malengo uliojiwekea. Kingine ni nidhamu katika kila jambo unalolifanya, kwani bila nidhamu hakuna kufanikiwa.
Hivi ni wasichana wangapi ambao wameshindwa kuendelea na masomo, na badala ya kujitafutia maendeleo kwa njia ya halali wamejikuta wakijiuza ili waweze kujikumu?
Ni wangapi wamekufa kwa ukumwi au wanaugua ukimwi sasa hivi baada ya kujiingiza katika vitendo vichafu vya kujiuza mwili?
Yasinta katuonesha njia kuwa tukiamua tunaweza.
Namtakia kila la heri katika ndoa yake, idumu na iwe na amani na upendo

Sunday, March 17, 2013

JUMAPILI YA LEO TUSALI SALA HII:- SALA YA MUME NA MKE PAMOJA....

Ee Bwana, tuko sote wawili
Tumepiga magoti mbele yako,
Mara nyingi kila mmoja huongea nawe peke yake,
Lakini sasa tumekuja pamoja, kama mume na mke.
Tunataka kukushukuru, Bwana,
Kwani umekuwa mwema kwetu. Umetupatia zawadi na baraka nyingi sana-
Tangu baraka ile ya kwanza siku ile ya ndoa yetu.

Maisha hayakuwa matamu siku zote, wewe wajua
Kumekuwepo magonjwa na matatizo, magumu na kuto elewana kati yetu. Lakini umetusaidia.
na kuyashinda hayo yote.

Kwa njia ya kila mmoja wetu, umetupatia moyo mkuu, nguvu, faraja na furaha. kwa ajili ya raha hiyi yote, Bwana Tunasema, AHSANTE.

Na tukiangalia sasa siku za usoni, tunaomba msaada wako.
Utuwezeshe kukua katika upendo wako, na katika upendano kati yetu.
Utusaidie ili tuelewane na kupokeaana zaidi na zaidi-

Utufanye tuyajali mahitaji ya kila mmoja wetu,
Na tuwe tayari kutafuta njia mpya za kupendezana.

Na tunakuomba, Ee Bwana,
Uwe nasi, hapa nyumbani petu,
Na utujalie tuwezekukaa nawe Daima.
NAWATAKIENI WOTE DOMINIKA YA 5 YA KWARESIMA C..Na watakatifu wa juma lijalo ni
Jt. Siril wa yerusalem
Jn Yosefu, Baba mlishi
Jo Gisbert, Irmgard
Al Serapion
Ij Lea, Deograsias
Js Turibio, Rebeka
DOMINIKA IJAYO NI DOMIKA YA MATAWI C

Friday, March 15, 2013

NIMEPENDA WIMBO/NYIMBO HII/UJUMBE HUU KUHUSU KUPENDA..UNAWEZA KUSIKILIZA UKIPATA WASAA!!!

NACHUKUA NAFASI HII NA KUWATAKIENI WAOTE MCHANA, JIONI,ASUBUHI AU USIKU NJEMA YA IJUMAA HII..NA IWE YA UPENDO NA AMANI.TUPO PAMOJA DAIMA!!!

Thursday, March 14, 2013

TUSISAHAU HADITHI ZETU TULIZOSIMULIWA PIA TULIZOSOMA:- LEO...MWANAMKE MWIZI!!!

Palikuwa na kijana moja aliyekuwa analala kwenye bwaru, hakuwa na mke. Siku moja aliondoka kwenda kutafuta mwanamke. Alifika katika mji wa watu, na katika mji ule palikuwepo wasichana watatu. Msichana moja mchawi, msichana mwingine mwongo na msichana mwingine mwizi. Basi, yule kijana akafikiri afadhali aoea nayeiba. Aliogopa mwanamke mchawi ataenda kumwua. Kadhalika, alifikiri Moyoni mwake: Kama nikioa mwanamke mwongo kutakuwa na mashauri kila siku. Akasema , afadhali nioe ayeiba nitaweza kumlimia.

Kweli akaoa mwanamke anayeiba, akaja naye nyumbani kwake. Akakaa naye. Siku moja mwanamume yule akachinja mbuzi, akakatakata maini na utumbo akampa mkewe apike. Basi, mwanamke yule akachukua ulezi akaanza kusaga kwenye jiwe. Mwanamume akaondoka akaenda kuoga maji mtoni. Mwanamke yule akaacha kusaga, akaingia nyumbani mwake pale alipokuwa amepika kitoweo, akachukua mwiko akaipua finyango moja akatoka nacho akazunguka nyuma ya nyumba akaanza kula. Mume wake alipotoka mtoni, baada ya kuona mke wake hayupo, naye akachukua finyango moja akazunguka upande wa pili akaanza kula. Mke wake alipomwona akasema :- Wa kukasirika hayupo , sote tunaiba.
MUWE NA  SIKU NJEMA SANA WOTE MTAKAOPITA HAPA. HADITHI NYINGINE ITAKUJA WIKI IJAYO PANAPO MAJALIWA....

Wednesday, March 13, 2013

ZILIPENDWA KWELI NI NZURI HAPA ILIKUWA MWAKA 1993 WILIMA/MATETEREKA...MWANAMKE KANGA!!!

Macho ya huruma hufurahisha moyo, habari huburudisha mwili. Kuchukiana huendekeza fitina, kupendana husitiri makosa yote. Nilikuwa mgonjwa ukaja kuniona .Nilikuwa na njaa ukanilisha. Kumhudumia mgonjwa ni wito. JUMATANO NJEMA KWA WOTE . NA KUMBUKENI WOTE MNAPENDWA!!! NA PANAPO MAJALIWA BASI TUONANE TENA WAKATI MWINGINE.

Tuesday, March 12, 2013

NAPENDA NGUO NDEFU MWENZENU..NA HII NI KAZI YA DADA SUBIRA WAHURE...

 Hili gauni limenivutia mpaka basi ..yaani ningependa nilimiliki kabisaaaa..ebu angalia lipo rahisi rahisi kweli lakini ni bonge la kitu ...mavazi ya heshima hayaa ...
Na hapa hii sketi imenimaliza kabisa ndefu, pana, rangi zake zinavutia yaani kama nipenzavyo...Nakutakia kazi njema sana dada Subira ...kwa kuona kazi zake nyingine inga hapa. NAWATAKIENI JUMANNE NJEMA SANA WOTE.

Monday, March 11, 2013

KAZI YA MIKONO YANGU:- MLO WA JIONI YA LEO LASAGNE...

 Hapa ni maandalizi :- kwanza ni aina ya mchuzi mweupe ambao nimetengeneza kwa unga wa ngano,maziwa,chumvi pilipili manga na baadaye chizi..halafu unaweka kwenye hicho chumbo kwanza mchuzi huo mweupe, halafu aina ya pasta bapa kidogo na halafu nyama ya kusaga iliyokaangwa na kuungwa na nyanya ya kusaga,kitunguu na kitunguu saumu..unafanya hivyo mara tatu au nne....
 Baada ya hapo naweka ndani ya oven 200°, dakika 30 baada ya hapo tayari kwa kuliwa

Na hapa unaona jinsi sahani ya Kapulya ilikuwa pembeni kuna spenchi, nyanya,na aina ya tango kinywaji machi ambayo yana limao kwa mbali...Chakula hili ni maalum zaidi Italia..Samahani kwa wala waiokula nyama msiogope kuja huwa kuna chakula aina nyingine kwa akiba..kama vile Kamala na Chacha ndio ninaowajua ambao hawali nyama.....JIONI YENU IWE NJEMA NA YENYE AMANI...TWIWONAGE CHILAWO BE..SIJUI NIMEPETIA...:-)

ONE DAY I DECIDED TO QUIT.....!!!

HABARI HII NIMEKUTANA NAYO MTANDAONI...NIMEIPENDA KARIBUNI....

One day I decided to quit...I quit my job, my relationship, my spirituality... I wanted to quit my life. I went to the woods to have one last talk with God.
"God", I said. "Can you give me one good reason not to quit?" His answer surprised me...
"Look around", He said. "Do you see the fern and the bamboo?" "Yes", I replied.
When I planted the fern and the bamboo seeds, I took very good care of them.
I gave them light. I gave them water. The fern quickly grew from the earth.
Its brilliant green covered the floor. Yet nothing came from the bamboo seed.
But I did not quit on the bamboo. In the second year the Fern grew more vibrant and plentiful.
And again, nothing came from the bamboo seed. But I did not quit on the bamboo. He said.
"In the third year, there was still nothing from the bamboo seed. But I would not quit. In the fourth year, again, there was nothing from the bamboo seed. "I would not quit." He said.
"Then in the fifth year a tiny sprout emerged from the earth. Compared to the fern it was seemingly small and insignificant... But just 6 months later the bamboo rose to over 100 feet tall.
It had spent the five years growing roots. Those roots made it strong and gave it what it needed to survive. I would not give any of my creations a challenge it could not handle. "He said to me."
Did you know, my child, that all this time you have been struggling, you have actually been growing roots." "I would not quit on the bamboo. I will never quit on you.
"Don't compare yourself to others .." He said.

"The bamboo had a different purpose than the fern... Yet, they both make the forest beautiful." Your time will come, "God said to me." You will rise high! "How high should I rise?" I asked. How high will the bamboo rise? "He asked in return."
As high as it can? "I questioned." Yes. "He said," Give me glory by rising as high as you can.
I left the forest and bring back this story. I hope these words can help you see that God will never give up on you. He will never give up on you.
Never regret a day in your life.
Good days give you happiness.
Bad days give you experiences;
Both are essential to life.
A happy and meaningful life requires our continuous input and creativity. It does not happen by chance. It happens because of our choices and actions. And each day we are given new opportunities to choose and act and, in doing so, we create our own unique journey.
Keep going...
Happiness keeps you Sweet, Trials keep you Strong, Sorrows keep you Human,
Failures keep you humble, Success keeps You Glowing, but Only God keeps You Going!
JIONI NJEMA KWA WOTE PANAPO MAJALIWA TUTAONANA HUMUHUMU....

LUNDO SEKONDARI INA HALI MBAYA SANA KIELIMU

Tuanza na historia fupi ya shule ya Lundo: Shule ya Lundo ilianza kama shule ya msingi ya wakimbizi ..na ilikuwa inaitwa shule ya msingi wa wakimbizi Lundo. Na kama nakumbuka vizuri ilianza miaka ile ya sabini(1970) na baba yangu alikuwa moja wa walimu waanzilishi. Nami nilipofikia umri wa kuanza shule nilianzia shule hii, ila sikumalizia Lundo baba alipata uhamisho. Kwa hiyo ikaenda weee mpaka ....miaka ya tisini tisini (1990 ikawa Sekondari...sasa niliposoma makala hii hapa chini nimeguswa sana ...haya karibuni msome nanyi wenzangu.
..................................................................................................................................................................

Tangu kutanagazwa matokeo ya kidato cha nne shule mbalimbali zimekuwa na matokeo mabaya sana. Miongoni mwa shule hizo ni Lundo sekondari ambayo ilikuwa ikisifika kwa ubora wa wahitimu na matokeo mazuri.
Lundo sekondari iliwahi kuweka rekodi ya kufaulu wanafunzi wa kidato cha pili, hivyo hakuna aliyefeli kwa mwaka 1999. Sifa nyingi za shule hii ilikuwa nidhamu na wanafunzi kupenda masomo huku wakikabiliana na hali ya maisha na kuyazoea.
Wengi waliohitimu hapo wamefanikiwa kuwa watumishi imara na kuzalisha wanamapinduzi wazuri kifikra ambao wanaendelea kusukumu gurudumu la maendeleo ya wilaya ya Nyasa, na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla pamoja taifaletu la Tanzania.
Lakini kwa sasa hali ni tofauti. Licha ya kusifika wakati wa uongozi wa mkuu wa shule Bwan Ndunguru, sasa hali imekuwa mbaya sana. Maskini Lundo Sekondari.......masikini wilaya yetu Nyasa....
Inasikitisha kuona shule ile tuliyosoma, shule ile iliyokuwa kinara kwa ufaulu wa kidato cha nne tangu miaka ile ya 90's hadi mwanzoni mwa 2003.... Leo hii shule ni ya division 4 na 0 tuu.... Kwa mtazamo Wangu kutokana na vile nilivyokuwa nikifuatilia matokeo ya shule hii kwa miaka kadhaa,nimegundua shule imekosa Uongozi....
Samahani kwani huenda nitakuwa nimewagusa wengine moja kwa moja,lakini kwa nini wakati ule wa mzee Ndunguru mambo hayakuwa hivi.... Imeniuma kwa ujumla wa matokeo Kitaifa,lakini nimeumizwa zaidi na matokeo ya shule zetu wilayani Nyasa.... Sitaki kuamini kama Sisi ni Vilaza; Hapana
Na Richard Mwanja, Dar es Salaam

Sunday, March 10, 2013

BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO INAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAPILI NJEMA SANA !!!


Jumapili njema sana kwa wote..kwa kuifanya jumapili iwe njama zaidi basi mtembelee mtu yeyote yule kama vile wagonjwa, mayatima au hata rafiki...

Friday, March 8, 2013

WIKI HII NI YA WANAWAKE DUNIANI NA HAPA NI HII TAREHE NANE NDO YENYEWE...NAMI NIMEONA TUISHEREKEE KIHIVI:- BILA WANAWAKE ULIMWENGU UNGESIMAMA

MAMA ANALIMA 

Bila wanawake ulimwengu huu utasimama, yaani hakuna kitu kingeenda/fanikiwa..Ukiangalia kila mahali wanawake wapo, hasa katika shughuli kama kuchota maji, kutafuta kuni, kulea watoto na hata kazi ya kulima mazao /bustani(mbogamboga ...pia hata kazi ya kutafuta madini ghafi na kazi ngingine ngingi, nying zaidi. Anatumia masaa mengi kufanya shughuli hizi. Mara nyingi inakuwa siku nyingi kuliko mwanaume afanyavyo kazi. Na hii ndiyo sababu kubwa hasa ya kupigania USAWA ulimwenguni kote.
Tuzidi kuupigania USAWA sehemu zote :- Majumbani, mashuleni, makazini, kwa watu walio jirani yetu, kwenye siasa na kiutamaduni- ULIMWENGUNI kwote. WANAWAKE OYEEEEEEEEEE..NA KUMBUKENI WANAWAKE TUNAWEZA... Lakini pia tusiwasahau akina baba kwani bila wao tusingekuwepo akina mama....IJUMAA NJEMA SANA.

Wednesday, March 6, 2013

NENO LA JIONI YA LEO :- JE WEWE UNASAMEHE?......JE, UNAPASWA KUONA KWAMBA UMEKOSEWA KIMAKUSUDI?

Kuna hali nyingi maishani zinazomfanya mtu akasirike. Tuseme kwamba unaendesha gari, na karibu ligongwe na gari lingine. Utatendaje? Umesoma kuhusu visa vingi vya madereva wenye hasira waliowashambulia madereva wengine. Hata hivyo, ukiwa Mkristo, bila shaka hungependa kufanya jambo kama hilo. Itakuwa bora zaidi kutua kidogo ili kuchanganua mambo. Labda wewe pia una makosa kwa sababu ulikengeushwa na jambo fulani. Au huenda gari la yule dereva mwingine lilikuwa na tatizo. Somo ni kwamba tunaweza kupunguza hasira, hisia za kukata tamaa, na hisia nyingine zisizofaa tukitumia uelewaji, tukiona mambo kwa njia tofauti, na kuwa tayari kusamehe. Andiko la Mhubiri 7:9linasema hivi: “Usiwe na haraka kuudhika katika roho yako, kwa maana kuudhika hukaa katika kifua cha wajinga.” Usione kwamba umekosewa kimakusudi. Mara nyingi, huenda tukafikiri kwamba mtu fulani ametukosea kimakusudi lakini huenda sivyo ilivyo; labda ni kwa sababu tu ya kutokamilika au kutoelewana. Jitahidi kuwa na maoni yenye usawaziko kuelekea matendo unayoona kuwa si ya fadhili, na uwe tayari kusamehe kwa upendo. Utakuwa mwenye furaha zaidi ukisamehe.—Soma 1 Petro 4:8 NA JIONI IWE NJEMA SANA KWA WOTE

LEO EBU TUMSIKILIZE HUYU KAKA BINAFSI NIMEPENDA SANA MAZUNGUMZO YAKE ...NA DA SALAMA...EBU SIKILIZA UKIPATA MUDA

Nimependa sana mazungumzo haya ..nawatakieni wote JUMATANO NJEMA SANA....

Tuesday, March 5, 2013

PICHA YA/ZA WIKI MAZOEZI NI MUHIMU KATIKA AFYA ZETU TUZINGATIE!!!!

 Mchaka mchaka chinja....aaah ebu tuchukue wimbo huu Idi amini akifa mimi siwezi kulia nitamtupa Kagera awe chakula cha mamba....
Dada mkuu msaidizi naye hayuko nyuma kabisa ..Haya dada mkuu msaidizi msimu wa kuanza mazoezi unakaribia ,,wewe endelea  usitazame nyuma ..haya alisema, alisema, alisema Nyerere alisema vijana wangu wote mwalegea sharti tuanze mchakamchaka....mmmmhhh ngoja niwaachie na wengine waanzishe kuimba maaana mapumzi hapa  yanasumbua kweli....Sijui mnawafahau wadada hawa?:-) JUMANNE IWE NJEMA SANA KWA KILA MMOJA!!!!!

Monday, March 4, 2013

Mtoto Wako Ni Mwalimu Wako!!!!

Ninimesoma habari  hii kwa makini sana na napenda kusema nakubaliana na kaka Mjengwa...na ndio sababu katika malezi yangu sijakuwa mbali na wanangu . Hata hawajawa na mlezi mwingine zaidi yetu na labda walimu. Wazazi tujitahidi sana kuwa karibu na watoto wetu ni mambo mengi sana tutapata kutoka kwa watoto, ni watoto lakini wana mambo mazuri sana ....haya endelea kusoma hapo chini ili nawe ujifunze kitu kama nilivyojifunza mimi...karibu....
Ndugu zangu,

Moja ya maamuzi mazuri niliyopata kuyafanya ni hili la kutojihusisha na siasa za majukwaani ili kuwa na muda zaidi na watoto wangu.
Hakika, miaka kumi ya mwanzo ya makuzi ya mtoto ni muda muhimu sana katika makuzi ya mtoto. Hapo ndipo unajengwa msingi wa mtoto maishani.
Mzazi unatakiwa kuwa karibu na mtoto katika miaka yake kumi ya mwanzo, lakini, hata baada ya hapo, kabla mtoto hajatimiza miaka kumi na minane, bado mzazi unatakiwa kuwa karibu na mtoto wako. Kujenga misingi ya mahusiano ya mtoto na mzazi, awe mzazi wa kike au kiume.
Mara nyingi tumefanya makosa kudhani kuwa mahusiano yanayopaswa kujengwa ni kati ya watu wazima. Kati ya mke na mume, na kati ya mzazi na wazazi wengine. Tunayasahau mahusiano kati ya mtoto na mzazi.
Tunafanya makosa kuwaachia mayaya wa nyumbani jukumu la kulea watoto wetu. Tunafanya makosa pia, kuwaachia walimu tu, jukumu la kufuatilia mienendo ya elimu ya watoto wetu.
Na wazazi wa kiume tumekuwa mfano mbaya sana wa kuliacha jukumu la kulea kwa mzazi wa kike.
Hakika, mtoto, awe wa kike au kiume, anahitaji sana kuwa karibu na mzazi wa kiume pia. Kuwa na mahusiano ya kirafiki pia. Kazi ya mzazi haipaswi kuwa ni ya kukaripia watoto tu, bali kuwa rafiki nao, kuwa na muda wa kucheka nao. Na kubwa zaidi, uwa tayari kujifunza kutoka kwa watoto.
Na mtoto anaweza kuwa Mwalimu mzuri kwa mzazi, kama mzazi atamwandalia mtoto mazingira ya kuifanya kazi ya ualimu kwa mzazi wake.

Niwe mkweli, kuwa nimejifunza mengi kutoka kwa watoto wangu kama wao wanavyojifunza kutoka kwangu.
Mathalan, leo asubuhi nilimkuta mwana wangu akisoma kitabu (hicho pichani). Nikamwomba anisimulie kidogo juu ya anachosoma. Alipoanza kunisimulia, basi, nilijikuta nataka kumsikiliza zaidi. Kinahusu mtoto ambaye wazazi wake walitengana. Mzazi mmoja anaishi Marekani na mwingine Canada.
Mtoto huyu aliondoka kwa mama yake Marekani ili aende kumwona baba yake Canada. Alipanda ndege ndogo. Alikuwa yeye na rubani tu.
Huko angani rubani akapatwa na mshtuko wa moyo. Mtoto huyu akalazamika kuongoza ndogo hiyo. Aliongoza huku ndege ikipotea angani. Mwisho ndege ikaishiwa mafuta, maana hakujua haswa namna ya kuongoza ndege.
Ndege ikaanguka ziwani. Bahati njema mtoto aliweza kuogelea na kunusurika. Akalikuta pango, hapo akaanza kutafuta mbinu za kuishi akisubiri msaada wa kuokolewa... Kisa kinaendelea...!
Tunajifunza nini?
Umuhimu wa wazazi kuwajengea watoto wetu utamaduni wa kujisomea. Mimi niliwasomea vitabu watoto wangu tangu wangali wadogo sana. Hivyo, nikawajengea hamu ya kusoma.
Si ajabu, kuwa leo wanasoma vitabu kiasi cha hata kuweza kunisimulia ya kwenye vitabu ambavyo nisingeweza kuviona maishani mwangu. Na kuna ninayojifunza. Hivyo, watoto wangu wanakuwa walimu wangu pia.
Naam, mtoto wako ni mwalimu wako.
Na hilo ni Neno la Leo.
Maggid Mjengwa,
Iringa
0788 111 765
JIONI NJEMA KWA WOTE!!!!


JUMATATU YA LEO TUIANZE KWA KUANGALIA VIPI JUMAPILI YA JANA ILIKUWA KWA KAPULYA...MLO WA JUMAPILI JIONI ULIKUWA KAMA IFUATAVYO:- WALI, SAMAKI AINA YA COD NA SLAMON, MCHUZI WA NAZI NA NJEGERE!!!

 Hapa mishikaki ipo tayariinasubiri kuchomwa ni mishikaki ya samaki ya aina mbili:- cod na salmon anayejua kwa kiswahili anisaidie tafadhali nimetafuta sijapata jibu.
 ---na hapa tayari mishkaki imeiva ..nimechoma kwenye oveni kwa vile huko nje bado kuna baridi na theruji nyingi sana ....
Na hapa mlo mzima ndivyo ulivyokuwa wali, njegere, salmon,cod na mchuzi ulioungwa kwa nazi  jioni ya jana ilikwisha safiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii sana...
 
Na baada ya kula chakula kilibaki basi Kapulya akapata kutengeneza la kwa ajili ya kula leo jumatatu awapo kazini.Huwa sipendi kununua chakula kazini---kama unavyona hapo ndo mlo umekamilika nitakula leo jioni niwapo kazini ...JUMATATU NJEMA KWA WOTE.

Sunday, March 3, 2013

NI JUMAPILI YA KWANZA YA MWEZI MACHI:- NAMI NAPENDA KUWATAKIA IWE NJEMA SANA!!!

Mbali na kuhimiza kulinda na kutunza mazingira, tuwatunze na kuwalinda pia wanyama walio katika mbuga zetu za Tanzania na po pote. Tazama, jinsi twiga huyu anavyovutia na kuipamba nchi yetu. Mungu akaona kitu alichokifanya, na tazama ni chema sana. JUMAPILI NJEMA SANA KWA WOTE NA KWARESMA NJEMA PIA...KAPULYA

Friday, March 1, 2013

Inuka Twende Ni Kwa Walioagana​- MAGGID MJENGWA

Ndugu zangu,
Hakuna wawili watembeao pamoja pasi na maelewano.
Ukiwaona wanadamu wawili wanatembea pamoja, basi, wana makubaliano. Ni watu waliopatana.
Kwenye kundi la watu wa mataifa tofauti ukimsikia Mtanzania anamtamkia Mtanzania mwenzake, tena kwa Kiswahili; " E bwana inuka twende zetu!", na Mtanzania huyo mwingine akabaki amekaa bila kushtuka, basi, utilie mashaka UTanzania wake.
Ndio, " Inuka twende ni kwa waliogana". Ni watu wenye kufahamiana. Ni ndugu.
Nimeanza kuingiwa na hofu kuwa Watanzania tumeanza kupoteana kama ndugu. " Inuka twende' yetu imeanza kuangaliwa kwa sura ya udini, ukabila na itikadi.
Hatujafika pabaya sana, lakini, tunakoelekea ni kubaya. Tumeshaziona ishara. Miongoni mwetu Watanzania tumeanza kuzisikia kaauli za ; " Umewasikia jamaa zetu Wakrito? Umewasikia jamaa zetu Waislamu? Umewasikia jamaa zetu WaZanzibar? Umewasikia jamaa zetu wa Bara?......"
Hizi ni ishara za undugu unaosambaratika. Zamani sisi sote tulikuwa ni ndugu. Tulitembea pamoja, ishara ya watu tuliopatana.
Leo kuna Watanzania wanaoambiwa; " E bwana wee, siku hizi nakuona unatembea na kuongea na wale jamaa zetu wa upande mwingine!"
Ndio, Watanzania tumeacha kuwa ndugu. Tunagawanyika kwenye mapande. Ni kwa kuzitazama tofauti za dini, kabila na itikadi.
Hatujafikia pabaya, lakini, tunakoelekea ni kubaya. Tukumbuke; " Inuka twende ni kwa waliogana". Watanzania tulishaagana. Tulishakubaliana. Tulijua tunakokwenda kama Taifa. Kama ndugu. Tumeanza sasa kusambaratika.
Tuinuke sasa twende kupambana na yote yenye kutugawa kama ndugu wa taifa moja. Tuna kila sababu, nia na uwezo wa kushinda mapambano haya dhidi ya ubaguzi wa aina zote.
Na hilo ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
mjengwablog.co.tz

CHAGUO LA MAISHA NA MAFANIKIO KATIKA KUUANZA MWEZI HUU WA MACHI/TATU NA IJUMAA YA KWANZA YA MWEZI HUU NI:- WIMBO HUU WA DADA RAY-C UPO WAPI...


Tuanza mwezi huu kwa kujiulizani lini nimewasiliana na baba, mama, babu, bibi, shangazi, mjomba, kaka, dada, mama mdogo, baba mdogo, mtoto, rafiki, mpenzi wangu  au hata jirani yako. Kwa hiyo chukua nafasi na mtafute yule mliopoteana na mpeana mawili matatu....NAWATAKIENI IJUMAA NJEMA NA MWISHO MWEMA WA WIKI...