Wednesday, January 5, 2011

LEO NI SIKU YANGU YA KUZALIWA

Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda salama mpaka kufika siku hii ya leo na kuongeza limwaka limoja zaidi. Namshukuru kwa kuniepusha na mambo mabaya, magonjwa na pia vishawishi. Kijana wangu Erik amepata nafasi kuchagua hii picha anasema ameipenda.

kutimiza miaka bila mziki hapana. Haya wote UNGANENI NAMI NA WIMBO WA TUSELEBUKE NI KITOTO/LIZOMBE....


Namshukuru Mungu kwa yote, familia yangu pia ninyi marafiki zangu!!!

39 comments:

Mija Shija Sayi said...

Kudadadadeki siku zinaenda! Si majuzi tu ilikuwa siku yako ya kuzaliwa? Haya rafiki yangu naomba Mungu azidi kukulinda hivi hivi hadi uone vitukuu vyako...

Hongera sana kwa siku hiii...umenishinda vijisiku vidooooogo..Vinginevyo ningekuwa dadako.

Bless you!

Evarist Chahali said...

Hongera dada kwa siku yako ya kuzaliwa.Mungu akuzidishie heri na baraka zake.

Godwin Habib Meghji said...

HAPPY BIRTHDAY DADA YASINTA

Born 2 Suffer said...

Dadi Witu nakuombea maisha mema na marefu mpaka miaka 100 kila la kheri.

Faith S Hilary said...

Hongera kwa siku yako ya kuzaliwa dada Yasinta! Mungu akuzidishie mema katika maisha yako uishi miaka miiiingi sana yaani hata 100 upite kabisa! Hehehe! Baraka kwako dada, Happy Birthday

Mzee wa Changamoto said...

Kumbe "sem dei" na "mai papa"?
Good one. Watu wawili wenye umuhimu ndani ya siku moja iliyo muhimu
UNAPENDWA PIA.
UNASHUKURIWA MNO
NA
UNATHAMINIWA SANA

Happy EARTHDAY

Unknown said...

Happy birthday mamito
whr is a party?

Unknown said...

Hongera dada yangu na Mungu akulinde na kukuzidishia mema!!

http://tanzania-sports.blogspot.com/ said...

Unauhakika au umekosea...kila la kheri binti maringo. Mungu akujalie uishi sana na uwe na watoto wengi kama mwana wa mfalme!

Israel Saria said...

Hiyo picha ya mkonyezo imeniacha hoi..wee haya weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

mumyhery said...

Happy birth day Mama Maisha tunauombea Mafanikio zaidi.
Mungu akubariki

Mwanasosholojia said...

Hakika ni furaha
Iliyochanganyika na raha
Mwaka mwingine kwa Yasinta
Neema zizidi kujikita
Miaka izidi kukatika
Hepi Besidei da' Yasinta!

emu-three said...

Hata mimi siamini dada yetu juzijuzi tu ulikuwa ukisherehekea kulia ng'aa ng'aa...leo tena.
Hongera sana twakutakia maisha mema, yenye baraka na fanaka, mungu akuzidishie uhai uwaone watukuu wako!

EDNA said...

Hongera sana Da Yasinta kwa siku yako ya kuzaliwa,Mungu na akulinde ili ufikishe miaka zaidi ya mia moja.

camilla said...

hongera sana kwakuzaliwa, mama! <3
i hope you'll have a great day :)

Erik said...

Grattis Mamma !
ha en trevlig och rolig dag.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Hongera Yasinta!!!

Simon Kitururu said...

Hongera sana Yasinta!

malkiory said...

Happy birthday.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Hongela sana...ntakuletea ugimbi tugide kidogo bana!

Albert Kissima said...

Heri ya siku ya kuzaliwa mama wa maisha na mafanikio. Mungu akuzidishie miaka mingi mingine yenye amani, upendo, furaha na ,mafanikio tele.

Rachel Siwa said...

Hongera sana dada mpendwa kwa siku yako hii muhimu!Mungu akubariki sana pamoja na familiya yako!

Da Yasinta hako kawimbo kananikumbusha mbali sana nimempenda mwenyewe hihiiii hapo ndiyo!

kamwali cheketua cheketuuu!!! hahahaha nipo hoi kwa kucheza.

John Mwaipopo said...

hongera dada mkuu kwa kuchana kalenda. mungu akulinde uchane kalenda kibao mbeleni

chacha o'wambura usinisahau kwenye idadi ya ugimbi nami nimo. nadhani na simon kitururu tusimsahau

Eric ana jicho kali sana. hapana shaka kama ameweza kuchagua pozi kama hili basi naye atachangua kifaa huko mbeleni

Goodman Manyanya Phiri said...

Was looking for Kiswahili blogs and then, on this auspicious occasion, got myself glued on yours. A very happy birthday indeed from Manyanya

PASSION4FASHION.TZ said...

Hongera sana kwa siku yako ya kuzaliwa.pia ahsante kwa lizombee!!!
God bless you.
xx

Eric Luanda said...

Hongera bibie! Mungu akuzidishie maisha marefu na yenye baraka Tele.

Vovatus Ngonyani said...

Mpendwa Dada Yasinta,

Heri sana kwa Siku yako ya kuzaliwa.
Asante kwa shughuli unayofanya ya kutuelimisha na kutuhabarisha daima.
Ujaliwe maisha marefu na heri na baraka daima.

Nduguyo,

Pd. Novatus Ngonyani - München.

MRS said...

hongera kwa siku yako ya kuzaliwa,mungu akuzidishie.pia ahsante kwa wimbo mzuri umenikumbusha mbali sana.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hayaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

Flora Wanna said...

happy birth day to you sister, may god help u to live a hundred years,

Jacob Malihoja said...

Wakati unazaliwa jana nilikuwa kwenye basi naelekea Musoma, hongera mpendwa, nitakutumia zawadi nzuri itakayoimarisha uzalendo wako kwa Tanzania yako, katika mwaka huu. Happy B.D!

loya Malikenya said...

Basi hongera sana

salehe Msanda said...

Hongera
nilikuwa nje ya Njombe.
Kila la kheri na maisha mema na yenye mafanikio na baraka tele
Kumbuka maisha ni safari na katika asfari hiyo kuna vikwazo na changamoto zote zinatakiwa kuwa somo badala ya kuwa kizuizi na kuwa sehemu y akukufanya kukosa furaha

Yasinta Ngonyani said...

Ahsanteni sana wote kweli hapa ndipo ninapoamini kuwa sisi sote ni ndugu na ni watoto wa baba mmoja. Hakika ni furaha ya pekee kusherekea siku hii pamoja nanyi. Najikuta naandika na machozi yananidondoka kwa furaha. Nina swali moja kwa Mija Kudadadeki ni lugha gani? Ahsante sana saaana na wote mnapendwa sana:-)

John Kanene said...

Happy returns though belated on you birthday!
You are a great woman and we are proud of you and your blog is entertaining, educative and we look forward to reading more from you...........

SIKU YAKO LEO!
SIKU YAKO LEO!
FURAHIA, SHANGILIA, SIKU YAKO LEO!

ADELA KAVISHE said...

hongera kipenzi ijapokuwa nimechelewa love u sanaaaa

Nampangala said...

Mlongo hongera sana kwa kushelekea siku yako ya kuzaliwa. natumaini ulikuwa na siku nnzuri kwako. na asante sana kwa kutukumbusha kunyumba ubarikiwe sana.

Mama Jeremiah said...

Hongera kwa siku yako ya kuzaliwa.

Kwa kweli Blog yako ina nivutia sana. Ni kati ya watu ambao huwa tunazunguka blog mbali mbali.
Nakutakia mafanikio mwaka huu kwako na familia yako.
Hongera sana kwa siku kubwa hii.

MARKUS MPANGALA said...

MWAKA HAUJAISHA,
MAISHA YANAKUJA,
SIKU ZINAPITA,
UPENDO NENO MOJA,
FAMILIA NZIMA,
IWE AMANI DAIMA,

SIJACHELEWA MAMA,
SIKU HII NJEMA,
YEYE MAULANA,
AJUA YA MAANA,

NISAMEHE MAMA,
LEO NAKIRI SANA,
SIKU HIIIWE NJEMA,
MUNGU AKUPE PENDO JEMA,
FAMILIA IWE NA RAHA NA NEEMA.