Monday, January 17, 2011

KWA NINI WATU WANAOANA?

Kama ukimuuliza au ukiwauliza watu wanaooana, kwamba kwa nini wanaoana au ni kwa nini wako kwenye ndoa? Utapata majibu tofauti tofauti kulingana na namna watu hao wanavyotafsiri neno ndoa. Mimi sitajibu swali hilo lakini labda kile ninachokusudia kukiandika hapa huenda kikakusaidia kupata jibu la kwa nini watu wanaoana.

Kuna ukweli kwamba binadamu wamefanya kuoana kama jambo la kimaumbile, na wakilifunganisha na tendo la ndoa. Mtu anajikuta akioa au kuolewa tu. Hana haja ya kujiuliza ni kwa nini anaoa au kuolewa, kwa sababu anaona watu wanoa na kuolewa na akiangalia umri wake anaona kwamba amefikia umri wa kuoa au kuolewa hana haja ya kutaka kujua sababu. Hivi ni nani aliyepanga umri wa kuoa au kuolewa? Na umri wa kuoa au kuolewa umapangwa kwa kuzingatia vigezo gani? Je kupitisha umri huo kuna athari gani?

Ipo sababu nyingine inayotajwa kuwa watu wanoana kwa sababu wamependana, upendo ninaouona hapa ni wa mtu kumtamani mwenzie awe mwanamke au mwanaume, kwani kwetu sisi tunaamini kuwa kutamani ndio kupenda.

Hivi kama watu wanoana kwa sababu ya kupendana kungekuwa na talaka kweli? Naamini kama kungekuwa na talaka basi zingekuwa ni chache sana, na wanaoachana wasingeachana kwa ugomvi na visasi, bali wangeachana kwa upendo na wangeendelea kupendana na kuheshimiana, kwa sababau upendo ni tofauti na kutamani, upendo upo na utaendelea kuwepo na si vinginevyo.

Utakuta wanandoa wanasema “sisi tumeoana kwa sababu tunapendana” lakini baada ya mwaka wanandoa hao hawaelewani na wanakuwa na ugomvi wa mara kwa mara mpaka kufikia mmoja kumuua mwenzie, huu ndio upendo wa aina gani?

Ndoa za namna hii, hazikuwa ni za upendo bali watu kutamaniana au mtu kutamani mwili wa mwenzie, lakini kulikuwa hakuna upendo miongoni mwao.

Wengi wameoana kwa kufuata mnyororo ule ule wa kuoana kwa kufuata dhana iliyowekwa na jamii kuwa ni lazima watu waoana bila kutafuta tafsiri ya kufanya jambo hilo. Na mara waingiapo katika ndoa huona kama wamejitwisha mzigo mzito wasioweza kuubeba. Kuna zile kauli zinazotolewa ambazo wengi huita usia kwa wanandoa kwamba ndoa ni kuvumialiana, lakini watu hawajiulizi ni nini maana ya kuambiwa ndoa ni kuvumiliana, kuvumiliana kwa lipi? Kuna kitu gani katika ndoa kinachohitaji watu kuvumiliana?

Haya maswali inapaswa watu wajiulize kabla hawajaingia katika ndoa maana kuna mambo mengine hayafai kuvumilia, sasa itakuwaje nikishindwa kuvumilia? Na kuvumilia huko ni mpaka wapi?

Kuna watu wengi wanapata shida katika ndoa kwa sababu hawakujua ni kwa nini wanaoa au kuolewa, inawezekana, waliunganishwa na tendo la ndoa zaidi na sio upendo, na hapo ndipo wanpokuja kugundua kuwa walifanya makosa.

Nadhani imefikia wakati sasa ya watu kujiuliza ni kwa nini wanaoa au kuolewa, kwani ni hii itapunguza magomvi na talaka katika ndoa.Inabidi kila mtu awe na sababu yake mwenyewe ya kuamua kufanya hivyo sio kwa kuangalia sababu zilizowekwa na jamii au kusukumwa na matakwa ya jamii bali uwe ni uamuzi wake mwenyewe bila kushurutishwa au kusukumwa na matakwa ya jamii.

Kama hujaoa au kuolewa isikupe shida tulia, na ukitaka kuoa au kuolewa ufanye hivyo ukiwa na sababu yako binafsi

12 comments:

Koero Mkundi said...

Mara nyingi nimekuwa nikijiuliza, hivi kuna ulazima watu kuoana?

Kwa mtazamo wangu mimi kama Koero, nadhani kwa nyakati hizi tulizo nazo hakuna ulazima wowote watu kuona, kwanza ni kufungana minyororo ya utumwa bila sababu.....

Niliwahi kumuuliza shoga yangu mmoja aliyekuwa akilalamika mara kwa mara kuwa umri unakwenda na hatokei wa kumuoa.....

Nikamuuliza kuwa anataka kuolewa ili iweje?
Alinijibu kuwa anataka kuwa na mume wake na watoto pia.....

Je asipotokea wa kukuoa..Nilimsaili.
Sidhani kama nitakuwa na amani maishani mwangu.alinijibu.

Ukichunguza utagundua kuwa shoga yangu huyu, amefungwa na jamii kuwa mwanamke ni ndoa, yaani mwanamke hakamiliki kama atakuwa hajafunga ndoa au kuolewa kwa lugha nyingine.

Lakini siamini kuwa hakuna wanaume wa kuoa...la hasha wanaume wapo tena wengi tu wa kutosha, tatizo la sisi wasichana wa siku hizi ni kuchagua......utakuta binti anaweka viwango vya aina ya mwanaume wa kumuoa utadhani ni bidhaa, kama swala ni kuolewa basi si ujitwalie yeyote anayekuja mbele yako halafu mtakuja kurekebishana mkiwa pamoja (No body is perfect)

Na kama ni watoto si unaweza kujibebe mimba yako na mwanamume yeyote yule kisha ukalea mwanao kivyako...naamini kuwa mwanaume hawezi kujua kama mimba ni yake kama hujamwambia... au labda adai vipimo vya DNA.

Napenda kumalizia kw akusema kuwa.... Sidhani kama hakuna maisha bila ndoa..... na hakuna ulazima wa kuoana kwani ni sawa na kutoa uhuru wako kwa mwingine......

Simon Kitururu said...

Tatizo la kupenda KITU leo ,...
.... hakuji na GUARANTEE utaendelea kupenda hicho kitu kesho.

Na nafikiri sio sahihi kuamini wapeanao talaka mwanzoni hawakupendana kikweli na waliongozwa na kutamaniana tu!


Na kuna waliooana kwa kutamaniana tu na hawajapeana talaka ukichunguza,...
.... kama tu waliochaguliwa MKE au tu MME wasiomjua na WAZAZI na kuishi kwa amani tu na kujifunza ndoa mbele kwa mbele ya safari ya maisha .


Ya binadamu si rahisi sana kuya simplify kirahisi kihivyo kama tu ilivyokuwa si rahisi mtazamo mmoja majibu yake kuwa sahihi kwa kila kitu!:-(


Na ni mstari mwembamba sana tu kati ya kutamaniana na kupendana kama ukiangalia kitu kinamna fulani:-(


Ni mtazamo wangu tu!:-(

Unknown said...

Kwa ufupi sana maana muda wangu hautoshi ajili ya majukumu yanayonikabili.

Mimi nijuavyo ni Mwanamume kupata msaidizi wake katika maisha (Mungu alifanyia Adam msaidizi ambaye ndiye Hawa) Mapadre wapo wanao oa na wasio oa! Ambao hawaoi hawataki msaidizi ktk maisha ila wanamtegemea MUNGU. Ila wanashiriki tendo la ndoa tena ni vipanga hasa, wake za watu, visichana ni fujo tupu! Tuache hilo.

Kuna watu umri ukifika au kupita wana lazimisha kuingia kwenye ndoa ambazo hazi dumu au zina jaa matatizo. Ukiangali uta kuta mtu wa umri fulani akionekana hajaoa au kuolewa anaonekana ana kasoro au ni mhuni na wakati hata kwenye ndoa zenyewe kuna wenye kasoro na wahuni kibao. Mimi nasema ndoa siyo ya kila mtu. Usioe/kuolewa kama haupo tayari. Marriage should be a personal decision influenced by only your desire and will.

Biblia inaeleza kwamba:
" mwanamke mpumbavu huivunja ndoa kwa mikono yake mwenyewe ".

Nimetoka naenda.

chib said...

Nimesoma ya Yasinta, nikatafajkari. NIkaja ya Koero, nikaguna guna.
Nawaachia wenye ndoa kuzungumza, kwani kuna baadhi ya watu husifia ndoa zao na kujivunia maendeleo waliyoyapata hata kuliko walipokuwa waseja au watu wa ma-home, na kuna wanaochukia na kuona ni kama utumwa. Ukubwa wa pua .....
Swali la kizushi, hivi Dada Yasinta hiyo picha ni ya kweli! Au watu wamejipakaa masizi kufurahisha macho ya watazamaji.
Tuhifadhi mipingo na mazingira jamani kama kuna mtu amechonga!
Nasisitiza, ni uzushi tu wa kwangu

emu-three said...

Kwanini watu wanao-ana! Ni swali ambalo unaweza ukalijibu kirahisi, lakini sio rahisi kihivyo. Kwasababu wengi tunatizama `majukunu ya kimaisha' zaidi kuliko `Kiini cha ndoa au kuoana.
Nafikiri kama tungelitaka kujibu kirahisi tungelisema kwasababu `tumeamrishwa ki-imani kufanya hivyo'.
Je watu wanaoana wanavyotaka, yaani umekutana na Anna au john mkasema basi tuoane. Hapana lazima mfuate sheria ambazo nyingi zimekizana na imani au sheria fulani ili mwisho wa siku iitwe ndoa.
Mnaweza mkaoana hata kama hampendani au sio. Labda mnataka mpate chetii tu, wapo waliofanya hivyo, na inaitwa ndoa!
Lakini ukiingia kiundani , nafikiri watu wanao-ana ili kuhalalisha `tendo la ndoa' nikisema hivyo usilenge kwenye maana ya moja kwa moja.
Tendo la ndoa ni majukumu yote ya ndoa, ambayo yanafanywa na mke na mume.Ambayo yakifanywa nje ya ndoa yanatafsiriwa kuwa na upungufu wa maadili.
Mimi naona niishie hapa maana kama nilivyosema awali sio rahisi kihivyo kuelezea kwanini watu wanaoana.
OMBI: Tusikatae ndoa kwasababu ya uzaifu wa kibinadamu. Ndoa ni nzuri kama watu wataielewa vyema ndoa ni misingi yake!

Goodman Manyanya Phiri said...

Mambo ya ndoa yanakuwa magumu ukiwa wewe binafsi ni mgumu kujielewa: usiende ndoani kutaka kuimarishwa bali nenda kuimarisha utakatifu wa ndoa! Fanya subira kama hujawa tayari; na kwa ukweli ndoa haina uzee!

NAAM, UBAVU WAKO UPO! Lakini UHAKIKA (guarantee) wakufiana au kuzikana (TILL DEATH DO US PART)hamna kama penzi lenu hamjengi siku hadi siku kila siku mpaka kifo hicho cha ahadi mlipofunga ndoa yenu!


Zijulikanavyo SENSES za binadamu (yaani ile namna ya kutambua au kwelewa mazingira yake) ziko tano (5):


1. kuona
2, kusikia
3. kupata ladha (ulimi)
4. kugusa (pitia ngozi, kwamfano)
5. kunusa (pua)


Mimi binafsi nina utafiti vilevile na ninayo imani (HYPOTHESIS) kwamba yule wako unaemchagua (hata WAKO UNAYEWACHAGUA, TUKITAKA KUKIMBIA IMANI YA "one-man-one-wife/one-woman-one-husband"), unamchagua (tena bila kuzingatia, yaani WITHOUT CONSCIOUSLY DOING SO) kwakupitia kadri anavyokutosheleza juu ya hizo 5 MAIN SENSES na mara nyingi hizo ndizo zinazosababisha kile kwaVizungu kinachoitwa "LOVE AT FIRST SIGHT" (yaani mnaonana mara ya kwanza huko
Dar kwenye daladala kutoka Posta kwenda Kivukoni, mnatongozana na kukubaliana papo hapo, mnaamua siku hiyohiyo kuoana na kweli mnaoana na ndoa yenu inadumu na kushangaaza ulimwengu).

Penina Simon said...

penina simon till mig
visa information 08:36 (1 timme sedan)

Yasinta kuoa na kuolewa, ukumbuke ni tendo Mungu alibariki tangu wkt anaumba hii dunia, hivyo basi huna jinsi ya kulikwepa,
ukiwa mdogo ndg ni wazazi wako na jamaa zako, lakini ukiwa mkubwa unajisikia kabisa huna haja ya kuwahitaji na unatafuta mwenza, ingawa na wazazi wana nafasi yao.


Kwa hiyo kuolewa ni agizo la Mungu wala sio hiyari yetu, na muda ukifika utaona kuwa si vyema mwanamke/mwanaume kuishi peke yake na kujikuta unahitaji mwenza.
Fanya uchunguzi wanawake/wanaume waliopita kuoa/kuolewa wanavyoishi (kuchanganyikiwa fulani hivi ingawa hujifanya wapo fit)

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

unadhani tukijiuliza kwa nini twaoana itaepusha hayo yote? sidhani

kuna wakati twasema "I can't live without you" kumbe ni kinyume!

hapo linakuja pia suala la kupendana...upendo ni nini? wengi wanadhania hisia (feelings) ndo upendo! pole zao!

Unknown said...

Nimejifunza vyakutosha, mbarikiwe sana.

Vtoret said...

Mbarikiwe kila mmoja KWA kutoa mawazo mazuri sana

Vtoret said...

Mbarikiwe kila mmoja KWA kutoa mawazo mazuri sana

Moses Mgimwa said...

YESU AWABARIKI SANA SANA