Najuvunia sana sanaa zetu, utamaduni wetu, ebu angalia hapo ni kazi za mikono ya watu hizo. Mti umeguuka na kuwa umbo fulani la kupendeza, matete yamegeuka kiwa vikapu na udongo umegeuka kuwa chungu.....mmmhhh maji ya kwenye chungu,,,oh kuna kitu sina hapo ni kata sijui mnanielewa ile ya knywea maji. Weeee maji yanavyonoga kwenye kata. Tusisahau kwetu, vyetu na kuhusudu vya wengine.
9 comments:
Wacha wee,kata mimi naijua maji yake yananoga balaa.
Dada Yasinta inaelekea ukiendaga BOMBI NYUMBI huwa unafungasha kwelikweli...hongera sana.
Basi hiyo kata itakuwa mzigo wa safari ijayo. Edna funga Safari uje utasema ni TZ ndogo..lol. Na Edna Ahsante...
kweli utamaduni wetu ni muhimu sana, kwani mkataa utamaduni wao ni mtumwa!
Hongera da Yasinta kwa kuenzi nyumbani!hivyo vikapu,vijamandana mtungi na maji yake huwa baridi!umekula ugali wa muhogo kwa mboga ya maboga na dagaa za chukuchuku pembeni ukimaliza unashushia na maji ya mtungini kwa kata weweeeeeeeeeee!!!!.
sanaa na utamaduni viko pamoja. Tudumishe sanaa zetu ili tuutunze utamaduni wetu. Tuache kuiga kwa sana yale ya China na Ulaya kwani Ruhuwiko ni kwetu!! Edna Ahsante sana kwa kunikumbusha zile kata pale juu ya mtungi kijijini kwa binti Ndembo!!
yoote tisa, kumi ni maharage ama kisamvu vilivyopikiwa katika chungu. hasa kisamvu kilichopikwa jana na kulala
emu-3 umenena haswaaa!
Swahili na waswahili! Tabia hii ya kukumbushana vyakula tulivyozaliwa navyo inadondosha mate. Ugali wa mihogo, mboga ya mabogo ile ya kuchemsha tu maji na chumvi au matembele na hao dagaa uliwasema...mm basi naacha umenikumbusha Lundo kwangu mweh!!
kaka Mrope mimi sikubaliani kabisa na vitakavyo sijui china nk nakwambia nitatumia utamaduni wangu mpaka chanio...utamaduni.
Kaka John! Sikujua kama tupo wengi tunaojisikia hivyo yaani umenikumbusha ugali na kisamvu kilichopikwa jana halafu kula inyeshapo mvua....najua mtaniona mimi ...lakini habari ndio hiyo:-)
dada Yasinta sikuwezi,kwa kupekuwa pekuwa wee kiboko,umenimaliza na ulivyosema eti huku mvua ina nyesha,na mim namalizia kusema huku unakota moto na umekinga masufuria na vibakuli,mimi mwenyewe natamani chungu lakini kukisafirisha kuja nacho ughaibuni ndio kasheshe.nilijaribu kikavunjika.
Kazi nzuri dada Yasinta, japo nimepata shida kidogo uliposema "matete yanageuka kuwa vikapu", nilidhani ni mianzi (milahi).
Post a Comment