Sijui ninyi wenzangu mmewahi kufikiria kuwa:- Kuna/ni hisia za pekee kujua kuwa kuna mtu anakupenda, kuwa kuna mtu anakutamani, kuwa kuna mtu anakuhitaji. LAKINI kati ya vyote ni hisia za pekee kujua kuwa kuna mtu KAMWE hatakusahau. Huu ni ujumbe wangu wa leo mnapendwa wote , ahsanteni wote kwa uwepo wenu. UPENDO DAIMA.
6 comments:
Ujumbe poa sana!
Na unapendwa Da Yasinta!
nami nakupenda na nawapenda wote pia!
Upendo hutoka moyoni, na unaweza ukajua kuwa unapendwa kwa viendo au kwa hisia, na hili pia hutofautiana kati ya mtu na amtu. Kwa mfano unaweza ukampenda mtu na hata huyo unayempenda asione kuwa unampenda, kwasababu hujafanya vitu vitakavyodhirisha aonavyo yeye kuwa ni upendo.
Sasa ni vipi upendo uguse hisia ya mtu, ni vigumu kutambua hilo, na wengi watatamka tu mdomoni `nakupenda' huenda ikawa imetosha, lakini wengine wakaenda zaidi kwa kutoa zawadi nk...lakini kweli huo ndio upendo, au kweli wanpenda hivyo mpendwa anavyotaka! Sijui kwakeli, naomba tusaidiane kwa hilo.
Dada Yasinta tunakupenda dada yetu usiwe na shaka, labda utuambie tufanyeje ili ujue kuwa tunakupenda!
Nakupenda sana da Yasinta,hii ni kutoka moyoni.
Asante kwa ujumbe wa upendo
Asante kwa ujumbe mzuri
Ni kwreli kuna kupendwa,kutamani na nk,lakini tunatakiwa kufahamu kuwa wote tunawqajibu wa kupenda na siyo kupendwa maana suala la kupendwa ni la mtu mwingine na hatuna uwezo wa kumlazimisha mwingine kutupenda.
Upendo wa kweli na kufanya matendo mema hupelekea kutrosaulika na hivyo kutokufa hata pale mwili unaacha dunia
Haya ndiyo mambo waliyafanya mitume yesu na mohamed na baadhio ya watu waliojitoia muhanga kwa ajili ya wengine,Mahatan gadhi,mwalimu Nyerere,mama thereza bila ya kumsahau edward moringe sokoine.
Tukifahamu kuwa tunatakiwa kutosahulika katika dunia hii hata mara baada ya kufa kwetu tutaifanya dunia kuwa sehemu nzuriu na salama kuishi
Kila la kheri na shukrani kwa ujumbe wenye changamoto ya aina yake.
Post a Comment