Friday, January 7, 2011

SHUKRANI ZANGU KWA DA´MIJA NA WENGINE WOTE!!!

Sijui nianze vipi? Ngoja nianze hivi AHSANTE sana kwa kunipa heshima hii kubwa katika blog yako na kwa vile macho yangu kwa sasa yamejaa machozi ya furaha basi sitasema mengi. AHSANTENI, Ah nimeipenda HESHIMA hii na napenda iwe moja ya kumbukumbu ambazp sitasahau maishani mwangu ndio maana nimeona niiweka hapa MAISHA NA MAFANIKIO ili iwe karibu nami. Kwa mara nyingine tena AHSANTENI SANA!!!!


Ninachomheshimia Da Yasinta..


Wadau jana mwanablogu mwenzetu Yasinta Ngonyani alisherehekea siku yake ya kuzaliwa. Nilifikiria nizawadie nini nikaona ni bora nimpe tuzo ya kuwa mwanamke wa shoka wa wiki hapa bloguni. Haikuishia hapo nikawa nimetoa changamoto kwamba kuna sababu nyingine iliyonifanya nimchague kama mwanamke wa shoka, nashukuru wadau mliochangia kwani hii ni njia bora ya kutiana moyo pia.
Sasa ngoja nami niseme kinachonifanya nimuheshimu huyu dada.

Kwanza kabisa, ni uwezo wake wa kuhakikisha karibu kila siku anabandika kitu bloguni kwake tena chenye ubunifu, Yasinta kwa hilo nakupa hongera sana.
Pili, ni hili ambalo kaka M-3 pia amelisema, ni uwezo wake wa kutembelea blogu nyingi na kutoa maoni, kuna wakati huwa nakutana na blogu mpya kabisa nikizifungua nakuta Yasinta alishapita tena siku nyiiingi. Kubwa zaidi mtu ukipotea bloguni ni lazima akuulizie na akiona kimya Yasinta hurusha e-mail...! Yasinta hii inaonyesha jinsi ulivyo na moyo wa utu kwa wengine...
Kwa kweli kwa hayo na mengine waliyoyasema wachangiaji waliopita, sina budi kusema YASINTA WE SALUTE YOU!!! UNA MOYO WA UPENDO KWELIKWELI UNAOTAKIWA KUIGWA.
UBARIKIWE SANA.


Hapo chini ni wachangiaji walivyomuelezea Yasinta..

mimi nafikiri ume mbandika kwenye blog yako,kutokana namichango yake katika blog mabilimbali.pia nayeye kama mwanamke, mtanzania kwa kiasi fulani ameonyesha nia ya kuwakomboa wanawake wenzie hasa kwa misimamo yake,hisia zake, nahata uwazi kwa upande mwingine.pia ni mdada ambaye anajiwakilisha yeye kama yeye katika blog kwa kuamini kile akiandikacho,ambacho uhodari huo wa kuthubutu ni njia moja wapo ya mwanamke kujitambua, kuwa yeye ninani,nahtimaye kujikomboa, kimawazo,fikra na vitendo.ingawa nikimwangalia Yasinta,alikotoka ni mbali sana nahata kufikia hapo alipo umejitahidi.ombi kwako,unajuwa mchezo wa KOMBOLELA unavyo chezwa,butuua......uwakomowe wenzako. kaka sam

emu-three said...
MIMI NAMHESHIMU SANA HUYU DADA. Nasema namheshimu kwa sababu ya `ucheshi wake' udadisi wake na ni mtu wa watu, kama angekuwa Tanzania ningemshauri agombee ubunge.
Siku moja nilisema ngoje niwe wa kwanza kuwatembelea wenzangu kwenye blog zao, cha ajabu kila nilipopita nilimkuta keshafika...ana upendo na watu na anajali sana kazi za wenzake, ndio maana lazima aache ujumbe kukupa moyo.
Mimi nimshukuru sana kwani alinipa moyo kwenye `kijiwe' changu, nilikuwa nimekata tamaa kabisa, unaandika watu hawafiki hawachangii, lakini akanipa moyo na hata kunisaidia kunitangaza. NAMSHUKURU SANA NDIO MAANA NASEMA NEMHESHIMU KAMA DADA YANGU!
Ahsante na Da mija na wewe ni miongoni mwao!

Swahili na Waswahili said...
Mimi namkubali sana kwa mengi nikiandika hapa unaweza kunistopisha!
kifupi amejaaliwa upendo,utuwema,busara,

Anastahili kuwa mwanamke wa wiki na zaidi!na mengi ya kuigwa kutoka kwake!

Nakupenda dada Mkubwa Yasinta binti wa Ngonyani!!!!!!!!!.

John Mwaipopo said...
naona utufumbulie fumbo wewe mwenyewe

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...
si mwanamke! anasuka harafu ana blogu! mimi kule kwetu naowaona wengi wanaopaswa kuwa wa wiki ila hawana blogu! ila yasinta si anaishi ulaya?
Makala hii imeandikwa na Da mija ukitaka kumsoma daidi gonga hapa

7 comments:

ADELA KAVISHE said...

ni kweli kabisa Yasinta ni mwanamke wa kipekee hongera sana my dear be blessed for everything

EDNA said...

Ashukuriwe Da Mija kwa kuthamini mchango wako na kukupa hadhi ya MWANAMKE WA SHOKA,ni kweli unastahili,hongera sana Da Yasinta.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Da Yasinta. Na wewe mwenyewe unajitathminije? Misifa yote hii uliyomwagiwa ni ya kweli au watu tunakupaka mafuta mgongo wa chupa tu(kumbuka sie "Waswahili"?). Mbona hakuna aliyejitokeza na kusema japo jambo moja baya?

Hapana, nakuchokoza tu dadangu. Wewe ni mmoja kati ya wanablogu mahiri wa kike kutoka Tanzania. Ninavutiwa sana na unavyojivunia Uafrika na Ungoni wako pamoja na kwamba "ulishaibwa" na kupelekwa huko mbali na nyumbani. Wewe si limbukeni mwenye kusahau utamaduni wa kwao kama tunavyoshuhudia kwa wengi ambao hata mwaka hauishi lakini tayari hata Kiswahili chao kinakuwa kimeshabadilika! Kwa kuwa mtu asiye na utamaduni wake mwenyewe ni "yatima" hapa duniani, hili kwangu ni jambo la muhimu sana + mengine yaliyotajwa na wadau wengine.

Usibadilike! Natumaini kwamba utakimaliza na kukichapisha kile kitabu chetu mwaka huu wa 2011. Kila la heri!

Mija Shija Sayi said...

Asante Yasinta kwa kushukuru.

Kaka Matondo umesema kweli kuhusu kuongelea mabaya, nami nimelikumbuka moja kwa Yasinta. Yasinta anasema ana hasira sana, sasa hili kama ni kweli naomba alifanyie kazi kwani hasira si nzuri.

Haya dada kazi kwako.

emu-three said...

Mhh wanasema `hakuna aliyemkamilifu, sote tunakasoro fulani licha ya kuwa tu wema, kama binadamu. Kwahiyo kibinadamu ni vyema tukasifiana, na kama kuna ubaya wa mtu mwenyewe basi vyema tukaombeana heri kuwa hilo baya litoweke, au sio.
Ni hayo tu wakuu, na wapendwa zangu

Penina Simon said...

Yeah, Yasinta Upo juu sana, nakukubali na unakubalika.

Unknown said...

asante sana nimependa pia hii naomba mungu amjarie pia awajarie heri wote mungu awajaze moyo wa huruma daima