Thursday, January 6, 2011

MAKABILA YETU NCHINI TANZANIA

Ndugu zangu wapendwa leo nataka kusema kitu ambacho kimekuwa kikinikera sana. Ni kuhusu makabila yetu, mnajua ya kwamba nchi yetu Tanzania ni nchi pekee yenye makabila 129-130? Nasikitika sana kuona/kusikia baadhi ya watu huwa wanayakana makabila yao.

Kwa mfano utasikia mtu anasema mimi si mngoni, mimi siwezi kingoni kwanini kukataa uwewe? Uasili wako? KWANINI???

Nawaambia ukweli binafsi najivuna sana kuwa MNGONI na nilipenda kabila langu pia mila zake. Nachukua nafasi hii kumshukuru kaka Matondo kwa utundu wake ingia hapa ufaidi uhundo kwa wale/yule ambaye hajajua na pia wale waliojua si mbaya kujikumbusha. Mimi binafsi nimefaidi na ninaendelea kufaidi kwa mfano gonga hapa yaaani mpaka raha!!!!

3 comments:

emu-three said...

Kuna usemi usemao mkataa kwao ni `mtumwa'. Kwani unakuwa mtumwa wa `mila na desturi' za wengine.
Ukabila ni tunu ya asili, na inatakuwa mtu ujivunie nawo, ndio asili yako, ndipo ulipotokea, huko kwingine na kwa hawo wenye kabila hilo.
ILA ukabila usitumike vibaya, hasa sehemu za kazi, watu wengine wanabaguana kutokana na ukabila. Hii sio maana ya ukabila. Ukabila ni kulinda zile heshima za kabila lako na ukikutana na mwenzako wa kabila jingine ni rafiki yako, na huenda akawa ndugu yako pia!
Ni hayo tu dada yetu

Salehe Msanda said...

Dada yasinta
Hilo ni tatizo la kutojipenda na kujikubali ndio maana inatokea watu kuyakana makabila yao.
Kingine ni upofu wa kudahni kuwa kabila fulani ni bora zaid ya kabila lingine wakati kinachatufanya wote tujidai ni huo ubinaadamu wetu na si wewe unatoka katika kabila gani.
Maana hata kamautajidai kulikana kabila lako haitakuongezea kitu chochote zaidi ya kujiweka katika hali ya kuishi kwa mashaka na kukosa mani,furaha.
Tunatakiwa kufahamu kuwa kabila ni moja ya utambulisho wetu na tunatakiwa kujivunia na zaidi kwa sisi watanzania kutembea kifua mbele maana pamoja na kuwa na makabila mengio lakini tunaishi kama ndugu na kufanya kuwa mfano wa kuigwa na mataifa mengi ambao wanatuone gere.
Kila la kheri

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Asante dada Yasinta kwa ujumbe huu.