Wednesday, January 19, 2011

NAJIVUNIA NA NAIPENDA NCHI YANGU TANZANIA YENYE SIFA ZOTE!!!

Sijui kama wenzangu mmewahi kujisikia hivi, mwenzenu leo nimeamuaka na kujiona ya kwamba:- Ninaringa kwa kuwa mTanzania nchi yangu yenye sifa zote za ustaarabu.

Ninaringia rangi yangu nyeusi, macho meupe, ngozi yangu nyororo, ninapendeza na nywele zangu nyeusi na kiswahili ni lugha yangu.

Ninajivunia nchi yangu ya Tanzania yenye miji ya kuvutia iliyojengeka. Angalia Dar es salaam, Mwanza nayo Dodoma bila kusahau kwenye marashi mji wetu Zanzibar. Halafu ukienda Arusha, Tanga, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa na Songea.

Mnajua kuna vivutio vingi ndani ya Tanzania vinavyotufanya sote tujivunie kwa mfano kuna bahari fahari ya Taifa, Ziwa nyasa, viktoria, Tanganyika pia mlima mkubwa barani afrika Kilimanjaro. Bila kusahau mbuga za wanyama Serengeti, Ngorongoro, Tarangire, Mikumi n.k

10 comments:

Anonymous said...

Je ushawahi kujiuliza hivyo vyooote ulivyotaja vinamnufaishaje huyo mtanzania kama wewe, au ni rahisi tu kusema.Mimi naona nchi yetu ni kama mahindi yaliyofungwa kwenye box ambalo ndani yake kuna panya,sasa unategemea nini hapo. Hongera Dada,hata hivyo huwezi kuacha kujivunia maana ndo kwenu utaenda wapi.

EDNA said...

Hongera mdada....mimi pia najivunia kuwa mtanzania tena MNYALU original....hahahaaa

Fadhy Mtanga said...

alaaaaah....hivi mimi ni nani hasa? Mimi ni Mtanzania kabisa kabisa...hata kama babu yangu alihamia lakini baba yangu kazaliwa hapa...mie nimezaliwa hapa hapa...mimi ni Mtanzania....

Da Yasinta anajivunia Utanzania...mimi je? Mimi natamani kujivunia...lakini je, najivunia? Sina hakika sana kwa sasa...ila zamani wakati nikiwa chipukizi kabambe nikivaa suruali nyeusi, shati la kijani, kofia nyeusi na skafu yanye mchanganyiko wa rangi nyeusi, bluu, manjano na kijani.....

Mimi Mtanzania napata wakati mgumu kujivunia kitu kisichonifaidisha vile istahilivo...mimi huyo...kuna wakati najiuliza endapo kuna madaraja ya uraia nami nijijue nipo daraja gani...mimi huyu huyu....kusema ukweli natamani sana kujivunia Utanzania wenye thamani nayoistahili.....

Nautamani sana Utanzania ambao ule wimbo wetu wa taifa unasema 'Wabariki Viongozi Wake' mahali fulani....najiuliza...je, nijivunie viongozi wabovu...najiuliza...nijivunia usanii uliopelekea wajomba hawa Dowans kupata uhalali wa kututoboa mifuko? Sijui nakosea hapa kujieleza miye.....?

Ama tuseme nastahili kujivunia mikataba mibovu ya rasilimali za nchi? Ama tuseme mfumuko wa bei sijui nini....na Sumatra weshasema mwisho wa mwezi huu watatangaza nauli mpya za magari ya abiria....uwiii...lelo Ntanzania une!

Mbombo jilipo...halafu ngoja tu ije katiba mpya...sijui lini lakini....ila kusema cha ukweli....yataka moyo!

Kila mtu hujisikia raha kujivunia utaifa wake.

Nami najivunia Utanzania japo.........

Simon Kitururu said...

Hivi Tanzannia si ni ileile yenye kusifika kwa kuua Maalibino?

Na Tanzania si ni ileile yenye UDINI ambao uko tu chini kidogo tu ya SURFACE hasa ukichokonoa tu siasa zake?

Tanzania si ndio ile yenye RUSHWA kama kitu tu cha kawaida ?

NDIO ,..
.... sijivuniii kila kitu ambacho siku hizi ndio chawakilisha WATANZANIA ingawa ningependa yale bora yaendelee kudumu TANZANIA kwa kuwa naipenda TANZANIA!


Mungu ibariki Tanzania!

Goodman Manyanya Phiri said...

Mtaa gani tena huo unaotoka jijini Dar es-Salaam kwelekea sehemu za Manzese, Ubungo na kadhalika? Basi, mtaa huohuo, kabla ya kufika kituo cha "FIRE", nadhani bado ipo shule ya jina "Azania" na haiko mbali na shule ya "Shaaban Robert" ambapo niliwahi (kama "Mwalimu Alphonse Mpili" miaka ya 1988) kusomesha Hesabu!


Nilitafakari mara nyingi kwanini shule iitwe "Azania". Nafikiri waliyoanzisha shule walijua waziwazi kwamba Tanzania ndipo huko zamani ya kale (labda hata kabla yaMzungu, Mwarabu na kabila zote kutoka Afrika, kupoteza MELANIN kwenye ngozi, nywele, macho, hata kwenye ubongo, na kuchubuka ngozi zao za Kiswahili kuwa weupe)uustarabu wabinadamu yote ulikoanzia.

Inasemekana Tanzania, hasaa eneo la Mto Rufiji, ndiko makao makuu yalipokuwepo ya nchi yetu ya zamani za kale yenye jina "Zion" au "Azania" (mababu zetu walitamka kama walivyopenda kwa sababu herufi a,e,i,o,u hawakutumia kabisa bali waliandika jina la nchi hiyo "Zn").


Jina hilo la "Zion" ndilo sasa limeibiwa Afrika kupelekwa naWaingereza huko ng'ambo ila kuwakandamiza waPalestina nchini mwao lakini chimbuko la Myahudi, kama binadamu yoyote yule, liko Afrika na eneo laTanzania ndilo limeleta ustaarabu unaojulikana katika maandishi takatifu yaBiblia na misingi yote ya ustaarabu unaotumiwa na binadamu duniani kote.

Sasa hivi sisi Waafrika Kusini tumepata uhuru wetu (1994) kutokana na mchango waWatanzania kuliko... tena samahani... nchi zozote zile ziliotoa michango kwasababu Tanzania, sikama zile nchi zingine ulimwenguni zenye nia ya kuwagawa Waafrika , haikuwa na ubaguzi wa kusema "wewe ni chama cha ukombozi cha African National Congress of South Africa mwenye Kiongozi Ndugu Oliver Tambo au wewe ni chama Pan Africanist Congress of Azania mwenye Kiongozi Ndugu Johnson Mlambo", wala!

Kutokana na mchango waTanzania kuleta hali jinsi ilivyokuwa shwari leo toka Zimbabwe kwenda Namibia hadi Afrika Kusini kwenyewe, siku moja karibuni tutaunganisha tena nchi zetu toka Cape Town mpaka, angalau, huko Kinshasa na Dodoma tupate Azania yetu "kama kawa"!


Kifupi na kwa kufungia mchango wangu mrefu kwako Dada Yasinta: Kwa Tanzania yako, huna budi la kujigamba (ustaarabu wa binadamu yote ulianzia eneo hilo hilo laTanzania hata ukimwuliza Profesa Mazrui!) tena nafurahi sana kukuona wewe Mwanamama hujapoteza mizizi yako ya Uafrika.


Lakini, ukiwa Mwafrika chunga sana! Usiwabague Wazungu, Waarabu au makabila mengine! Sisi binadamu damu yetu ni moja tu na hakuna binadamu aliyekamilika kuliko mwengine... na kama Mzungu unamwona ni dhaifu ni kwasababu wewe Mwafrika mwenyewe ni dhaifu... MTOTO WASIMBA NI SIMBA NA MTOTO WA NYOKA, NYOKA TU! (soma zaidi, kwa mfano http://en.wikipedia.org/wiki/Rufiji_River)

Rachel Siwa said...

Mtu kwao da Yasinta!!!!!!!!

Penina Simon said...

Aisee umependeza sana, unajua sijawahi kukuona ukiwa na nywele umetimua, so nice.

Born 2 Suffer said...

Wote tunaipenda Tanzania sana.

Matha Malima said...

Umependeza sana dada yangu kwanza nywele mimi ndio umenimaliza nitumiemafuta unayo tumia ili na mimi ziwe kama zako. nakutakia ijumaa njeama wewe pamoja na familia yako. NKUPENDA SANA DADA YANGU

Anonymous said...

Mi nilidhani mwanaume....