Saturday, January 1, 2011

UJUMBE/WOSIA KUTOKA KWA BABA YANGU WA KWA MWAKA MPYA 2011

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda toka mwaka jana mpaka mwaka huu mpya. Bado ninawaza kama nilivyowaza nilipokuwa mwaka mmoja . Kwa nini hakubadiliki rangi kama ni mwaka mpya?
Nachotaka kusema ni kwamba: Nina ujumbe ambao nimepewa na baba yangu leo katika kuuanza mwaka huu 2011. Kwanza aliniuliza Kama najua Mungu ameiumba kwa kusudi gani?
Nikashindwa kumjibu na yeye akasema atanisaidfia kujubu.na majibu yaka ni haya:-
1. Kujua yeye ni muumba wetu.
2. Tumpende kuliko vitu vyote.
3. Tumtumikie kadiri ya wito wetu.
4. Na mwisho ni kwamba ili tuweze kufuka mbinguni.

Halafu akaendelea kunieleza ni kwamba Mungu anajua kama unamtendea kama unamtendea wema na si lazima uende kanisani ndo kumtendea Mungu mema hapana . Ni kwamba unaweza kumtendea jirani yako kitu na hapa ndipo utakuwa umetenda jema, kumwona mtu kama alivyoo, kumwalika/tembela mtu asiye na uwezo.nk nk. maneno haya yamenipa tafakari sana na nimeona niweka hapa ili mnisaidie kutafakari ujumbe huu.

4 comments:

Mija Shija Sayi said...

Safi sana, Roho yangu inaniambia Mungu alitaka kusema nasi wanablogu na wote tunaopitia mablogu kila siku kwa kutumia kinywa cha baba yetu Mzee Ngonyani kwamba tujitahidi kumpenda kwa vitendo na sio kwa maneno pekee.

Heri ya Mwaka mpya tena kwa wote.

John Mwaipopo said...

na mimi naungana na Mija Shija Sayi kuwa kauli ya baba yako hakika inaufikia uma wa wanablogu watembeleao kijiwe hiki

mumyhery said...

Ubarikiwe Mzee Ngonyani

Jacob Malihoja said...

dada Yasinta,

Ujumbe wa baba ni muhimu sasa, lakini blogers chakufanya ni kukazana kuandika kuwatetea wanaoonewa, kuwatetea wanaodhulumiwa lakini mbali na maneno hatua zaidi za vitendo zinahitajika .. kila mtu alipo kwa nafasi yake ukioacha kuandika anapaswa kuchukua hatua ya vitendo vya ziada kufanikisha mawazo yake.
Malombi yamenikumbusha mbaliiii! halafu ndio kipindi chake hiki jamani!