Tuesday, January 25, 2011

UNAKUMBUKA MICHEZO KAMA HII?

Nimekumbuka michezo kama hii nilipokuwa mdogo, maana katika familia yetu watoto wa kiume ni wengi zaidi kwa hiyo tulikuwa hawanibagui katika michezo....haya wewe je uliwahi kusafiri na gari kama hili????:-) brrrrrrrrrrrrrrr kanyonyonyooooooo twendeeee....

15 comments:

EDNA said...

Hahaaaa,mimi nilicheza MDAKO na KOMBOLELA sijui unaijuaaaa!

Yasinta Ngonyani said...

Edna! kweli unafikiri nisijue michezo kama hiyo nimeicheza sana tu na pia kuruka kamba si unajua mdako unamaana ule wa "rede" au kurusha jiwe moja juu na kukusanya mawe mengine kimpangilio?

Goodman Manyanya Phiri said...

Asanteni sana lakini labda nitawakwaza wengi lakini mimi naona bora nisiogope kuuliza juu ya michezo hii ya pale utotoni.


Niliwahi kusikia unapojaza fomu yoyote ile unaweza kuulizwa maswali ya kukaribiana sana lakini tofauti

1. SEX (yako, yaani)
2. GENDER (yako hivyohivyo)


Sasa naambiwa maswali hayo ni tofauti kabisa. "SEX" unajichunguza mwenyewe kimaumbile wakati "GENDER" ni jinsi wewe unavyotaka ulimwengu ukutambue.

Kwa mfano. Naweza nikawa mwanaume kama vile ninavyoweza kuwasaidia akinadada kupata watoto nami niwe baba ya watoto hao (kwa hiyo: SEX=MALE). Papo hapo, naweza nikawa sipendi kabisa kuchukuliwa kama mwanaume lisha kwamba mimi ni baba ya mimba. Badala yake napenda kuchukuliwa kama mwanamama na ningependa kuwa na mpenzi wa mwanaume mwenzangu...maana yake kwangu GENDER=FEMALE.


Sasa swali kwa Dada Yasinta (ninayempenda sana pamoja na wasaidizi wake au wafuasi):


JE HII MICHEZO YA KUCHANG'ANYA WAVULANA KWA WASICHANA SIYO MOJA YA SABABU YA KUFANYA HAYA MAMBO YA KUMCHANG'ANYA MTOTO ANAPOKUWA ASIJIJUWE ANATAKA UVULANA AU USICHANA?

Yasinta Ngonyani said...

Kucheza na wavulana si kuchanganya usijue wewe ni nina kwa sababu tayari unajua wewe ni nani. Kama utajiona upo tafauti basi itakuwa hivyo lakini sidhani sababu kubwa itakuwa kwasababu ya kucheza au kuchanganywa na wavulana HAPANA. Haya ni mawazo/mtizamo yangu. Inawezekana ni kweli lakini mimi sikubalini nawe.

Koero Mkundi said...

Dada una visa wewe..... unanikumbusha zamani kidogo

emu-three said...

Hiyo michezo ya kitoto kila mtu kapitia, kama sikosei, labda inatofautiana kimazingira, mjini, wana yao kijijini wana yao lakini `mtizamo' ni ule ule. Gari, kujificha, mdako, nk
Ama kwa swali la mpiganaji mwenzetu kuhusiana na hoja ya SEX and GENDER...Labda kwa mtizamo wangu ulikuwa na ajenda ya kuthibitisha `uchunguzi wako' kuwa huenda `michezo ya kuchanganyikana kati ya waume na wake' inaweza ikaathiri `saikolojia ya mtoto'
Kwa mafano kuna watoto wa kike wanapenda sana kucheza na wanaume, labda hii inaweza ikamuathiri akawa na tabia ya kidumedume...!
HAPANA...Mimi hili nalipinga kwa msisitizo, kuwa `tabia' za maumbile `uke au uume' ni asilia. Watu wenyewe kwa `tamaa zao' au `ushawishi ambata' kama mapicha, kuchezewa...nk ndivyo vinaweza kuja kumuathiri mtu pale anapoviweka akilini, kama atajishirikisha kwa hilo pale anapofikisha umri wa kutambua...!
Hawa wanaojifanya mashoga, sijui nani hawa...waulize vizuri watakuambia, aliyenisababishia hivii ni mjomba, au binamu au jamaa wa karibu, ..nk.
Michezo ya utotoni, haibadilishi kabisa `uuke au uume ' wa mtu..kitabia! `UTOTONI..TOFAUTISHA HILO, UTOTONI NA UJANANI..
Ni wazo tu labda tupate wataalamu watujuze hili zaidi!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

duh!

Unknown said...

Ole wangu mimi, maana nimekuwa mwepesi wa kuchota dhambi, lakini nashindwa kuzimwaga.

Ni nani atakayeniokoa na haya?

Namshukuru YESU Kristo, Baba wa Neema, maana Neema yake yatufundisha kuachana na madhambi.

Asante YESU kwa ajili ya Maisha ya tangu utoto hadi sasa ukubwani.

Usinisahau katika Ufalme wako.

Simon Kitururu said...

Mie nimependa huo mlio wa gari katika maandishi yako Yasinta!:-)

Mija Shija Sayi said...

Dah!! Sijui hilo gari ni kazi ya mikono ya nani? Usikute ni watoto hao hao...

Kazi nzuri yasinta.

Yasinta Ngonyani said...

Koero! nafurahi kama umekumbuka zamani na pia nafurahi upo nasi.

em3! Nakubaliana na ulichoandika mtoto hawezi kubadilika kwa kucheza michezo ya jinsia ngingine. Ahsante kwa hilo
Kaka Chacha! duh!

Mcharia! nawe ahsante kwa mchango wako ila nina wasiwaasi kama nimekuelewa.
Mtakatifu Simon! sijui kama ungeusikia kwa ukweli ungependa:-)

Mija! Ahsante, mimi naamini ni kazi ya mikono yao kabisa. Maana si unajua utundu wa watoto ulivyo.

Anonymous said...

Mcharia ni kati ya wale WALOKOLE waliochanganyikiwa ambao bila kujali mada ya mazungumzo wala kinacheondelea basi wanarukia mahubiri ya Yesu wao. Hapa kuna watu wa imani mbalimbali na usifikiri kwamba kila mtu anaamini huyo Yesu wako.

Kinachoudhi zaidi utakuta watu vimbelembele kama hawa ndiyo wanafanya dhambi kisirisiri. Maisha gani haya ya kipumbavu?

---Mimi nilicheza michezo hii sana pale Mkuranga. Nilipenda sana ile ya kujificha na wasichana na kulaliana. We acha.

Mcharia ; Bwana Asifiwe!!!!

Goodman Manyanya Phiri said...

Burudhani ya kimawazo juu ya hii posti sijawahi kuona...na tumbo linaniuma sasa kwa vicheko. Labda Dada Yasinta utuletee tena hili swala la utoto na uzee, hasa mambo ya ROLE PLAYING ("???uigizaji wa mitindo ya maisha"??)vilevile na ROLE MODELS ("??mifano ya kuigwa maishani??")ambao tunaambiwa na wanasayansi ROLE MODELS hao ndio wanaotusadia kuwa waume na wake wazuri hapo baadaye.


Asanteni nyote kwa kumpitia Dada Yasinta!

Mrekebisha tabia said...

Na wewe Goodman Manyanya Phiri tafadhali punguza moto. Naona umekuja na moto kweli kweli...Sijui uhusiano wako na Yasinta lakini napenda kuuliza, unamaanisha nini unaposema...

"Asanteni nyote kwa kumpitia Dada Yasinta!?"

Mbona mimi sijawahi kumpitia? Punguza mcheche wa kuandika andika hovyo bila ya kufikiri. Yasinta ni mwanamke anayejiheshimu na siyo wa kupitiwa na kila mtu, ala!!!

Na unatushukuru kwa kumpitia Yasita kama nani????

Goodman Manyanya Phiri said...

Duh! Sijui nimekosea Kiswahili gani hapo mpaka "nirekebishwe tabia" kumradhi kama nimetukana.

Mwenzio mimi naishi hapa Pretoria na Kiswahili sio lugha yangu. Kumradhi kama nimeshindwa kujieleza lakini Dada yasinta nili"mpitia" kwamaana ndie mwenye blogi hii. Labda kwaKiswahil chaMrekebisha Tabia heshima hamna (au "kumpitia mtu" inamaana ileyile moja anayoelewa yeye tu), lakini kwa lugha nilezowea (Kiingereza) ilikuwa lazima nionyeshe PROTOCOL kwa mwenyeBlogi hii (Dada Yasinta)na hiyo ilikuwa maana yangu ya "kumpitia"

Asante kwa kunirekebisa tabia; bali si tabia ni "kukosea lugha tu". Kumradhi kwako nawengine wanaofikiri kama wewe!