Tuesday, January 18, 2011

JUMANNE YA LEO EBU TUMSIKILIZE DADA HUYU NA STORY YAKE!!


Maisha haya jamani......zaidi bonyeza hapa china kwa pkupata habari yote nzima.
http://www.youtube.com/watch?v=QZ8vRS_FTWM

8 comments:

emu-three said...

NI UJUMBE MURUA DADA YETU, TUNASHUKURU KWA KUTUPA HILI, NA SWALI LIMEULIZWAJE: `Kama ingeambiwa `UNAO' ungefanyaje?

Yasinta Ngonyani said...

em3! ni kweli ni ujumbe mzuri na wa kuelimisha. "kama ingeambiwa UNAO ungefanyaje? kwa kweli ni swali ngumu kidogo kwani kama unao basi unao cha kufanya ni kuendelea kuishi hata kama unajua siku yoyote utakufa.

Unknown said...

Kuishi kwa matumaini... ndilo jibu sahihi. Muda wa kuishi ni mrefu kama ukijitunza vema na kuzingatia masharti ya afya. Anyway, all in all, tujitunze jamani kwani kinga ni bora zaidi... Siku njema nyote

chib said...

Jumanne njema kwako

ADELA KAVISHE said...

asante mpendwa ujumbe unaelimisha sana pamoja kama kawaida

Goodman Manyanya Phiri said...

Asante kwako, Yasinta Ngonyani Dada Mpendwa, kwa kutupa fursa hii tuongelee suala la kuambukizwa na virusi vya ukimwi kwani hakuna hata mmoja wetu duniani “aliyenusurika” na “WE ARE ALL OF US AFFECTED IF NOT INFECTED!”

Kama panakasoro yoyote tu katika maelezo yake yule binti ni pale ambapo anamlaumu baba yake.


Sasa kama anataka kukamilika kabisa katika safari yake ya maisha amwache baba yake alivyo na aanze KUJISAMEHE mwenyewe maana yake baba yake kamwe atoe kauli "Nenda mitaani kajiuze Binti yangu", huo ulikuwa ni uamuzi wake mwenyewe.


Kwahiyo itamsaidia sana kila anapoamka asubuhi ataamke kama kifungulio/INTRODUCTION kwenye saala yake "Nampenda baba yangu mzazi".


Hiyo itamsaidia KWANZA kutiimiza neno laMungu [tupendane hata na wale tunayofikiri ni maadui zetu].PILI itamsaidia SUBCONSCIOUSLY kumjengea upendo yeye mwenyewe katika dunia na siku moja anaweza akayafuta yale machozi yake yaliyonihuzunisha, anaweza akajikuta kwanjia hiyo yuko huko Merikani Umoja Wamataifa kwendeleza ujumbe wake mzuri kuhusu ukimwi. Lakini hataenda mbali kuliko uwanja wampira huo anaocheza kama anaendelea kuwalaumu wengine juu ya makosa yake binafsi!

Kifupi nimeupenda sana ujumbe wake na angekuwa hapa Afrika Kusini tungenufaika sana na ule ujumbe kwani hesabu za stastiki (STATISTICS) zamwaka huu 2011 zaonyesha uambukizaji umeongezeka hapa kwetu kwa asilimia kama kumi na tano (15%).

Hayo yote Afrika Kusini ni kutokana na ujinga tuliyonao nchini humu na kukosa wanadada kama yeye wakutupa ujumbe "TUPIME".

Maelezo zaidi juu ya hiyo hali huku guuni la Afrika kupitia Waziri Wa Mambo Ya Afya Afrika Kusini Dr Aaron Motsoaledi, soma gazeti la “Sowetan” kama ifwatavyo http://www.sowetanlive.co.za/news/2010/12/22/aids-hitting-life-expectancy-warns-motsoaledi

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mrope! nakubaliana nawe ni lazima kuishi kwa matumaini. Lakini kuna wakati mtu unakata matumaini je itakuwaje?
Ka`Chib! ahsante

Adela pamoja daima.
Goodman Manyanya Phiri!! Umenena wanatakiwa wadada au watu kama hawa wengi ambao wanahamasisha. Kwa kweli ni jambo la kusikitisha kwani utakuta mtu ana huu ugonjwa na anajua kabisa lakini anaendelea kueneza kisa eti tufe wengi sasa hii kweli ni akili au ni uungwana kweli?

Goodman Manyanya Phiri said...

Kukujibu, Mdogo wangu Yasinta, "Tufe wote" ni wajinga wa kupindukia. Utajuwaje kama huyo unayetaka kufa naye naye pia kashaambukizwa ukimwi na badala ya kukabiliana na aina moja ya virusi vya ukimwi unajikuta umebeba aina mbili hata zaidi nakufa kabla ya hiyo miezi sita wanaozungumzia? Hata Merikani inaelekea wako wengi akinaTufe-Wote Soma http://www.google.com/hostednews/afp/article/ALeqM5hj6RA8jW4yvcmLmLZRi882oO9EeQ?docId=CNG.cf3f9df69d3ee50f7a0a62316dbb5b65.641