Tuesday, November 15, 2011

KUOLEWA NA WANAUME WAWILI!!

Baada ya kusoma habari hii nimekuwa nikijiuliza ya kwamba kwanini kujipa taabu hasa pale asipojua kama uzauzito huu ni wa nani? Kwa sababu inaonekana, hata kama anawawekea zamu hata hivyo imekuwa ngumu kujua nani na baba. Katika jamii yetu "tumezoa" kuona wanaume ndo wanaoa wake 2-4 na anawawekea zamu na hata wakiwa wazawazito inajulikana ni yeye mume/bwana ndiyo baba. Kama mke hajawa mjanja na kutoka nje kwa kushindwa kusubiri zamu yake.. Sasa hii ya kuolewa na wanaume wawili kaaazii kwelikweli. Palipo na wengi haliharibiki nenoo. Naamini mtanisaidia kuelewa jambo hili!!!

5 comments:

Anonymous said...

kwa mtazamo wangu mie naona hapo kutakuwa na mmoja mwanaume jina na mmoja mwanaume wa vitendo nasema hivyo yawezekana mmoja ni hanithi yaani hana uwezo wa nguvu za kiume na mwingine ni lijari kwa maana ndie aliye mwanaume kamili wa kumlizisha mama - mdau Richie wa ughaibuni

ray njau said...

Hapa ni utata mtupu na ni suala la maofisa kutoka wizara ya afya na ustawi kuingilia kati na kutoa ushauri nasaha kwa wahusika na pale inapowezekana sheria za nchi zichukue mkondo wake.Katika suala hili hakuna kutabasamu wala kucheka.

ray njau said...

Hii ni taswira katika jamii yetu inayotokana na kila mtu kutumia uhuru wake wa kimaadili kama anavyoona inafaa machoni pake mwenyewe.Huenda mtu mwingine akaona haifai kabisa wanaume wawili kuishi na mwanamke mmoja lakini wengine wahoji kwanini wanaume wengine wanaoa zaidi ya mke mmoja na sheria ikatoa baraka zake?Hapa sasa ule usawa wa kijinsia kati ya mwanamke na mwanaume uko wapi?Je wanawake nao si vema wakapewa nafasi kisheria ya kuolewa na zaidi ya mwanaume mmoja?Hizi ndizo changamoto za mwanamke katika harakati za maisha na mafanikio.

Yasinta Ngonyani said...

Richie wa ughaibuni! kwanza ahsante kwa kuwa nasi hapa Maisha na Mafanikio na karibu tena na tena. Pili inawezekana kama ulivyosema ila ni jambo la ajabu na inawezekana hii ni ndoa ya kwanza ya namna hii.

Kaka Ray! hakika ni utata haswa kwa sababu kweli inawezekana mwanamume mmoja akae bila....wakati mwingine anampa uzauzito?

Goodman Manyanya Phiri said...

Ulazima wa kujuwa "ubaba" wamtoto haupo, kwani mtu anaekulea ndiye baba yako, na anayekulea silazima awe mwenye yai kama vile hatambuiki kama baba halisi aliyeacha yai lake kisha kumtoroka mtoto na mamae!.


Kusema ukweli, haya mambo yakutaka kuhakikisha "yai" ni la yupi hayaambatani na maadili ya Mungu na fundisho la "Msamaria Mwema".


Yule mwanamama katika picha yako Kapulya tena ni bora zaidi kuliko dada zetu wenye kutembelea SPERM BANKS, kwani yeye anao uhakika mmoja katika hao wawili lazima ndie "Mbayolojia" wake mtoto). Kwa hiyo tusihukumu mara tuwaite watu wasenge kwakutolea hadharani mambo zaidi ya nusu wanamama ulimwenguni wanayoyafanya kisirisiri huku wakiwa ndani ya ndoa ya bwana mmoja!


Hata kisayansi, tukumbuke kwamba familia ya mtu mmoja na mke wake ni kitu cha juzijuzi tu. Mwanzoni kabisa ndoa yoyote haikuwepo kabisa; lakini watu walikuwa Wachamungu hivyohivyo na magonjwa yakisasa na unafiki wetu karne hii (kama kaswende, kisonono au ukimwi) haya kuwepo.

Kifupi famila ya mtu mmoja na mke mmoja ni ishara kubwa kuliko zote za ubepari nao uliyokuja juzijuzi tu (pamoja na ubaguzi wa rangi dhidhi ya Waswahili na ubaguzi wa kijinsia dhidhi ya wanawake), mara tu binadamu alipoacha uungwana wa ujamaa wa kugawana matamu ya matunda tuliopewa sote kwa usawa na Mungu wetu mmoja!