Friday, November 18, 2011

TUANZE MAPUNZIKO AU MWISHO WA JUMA NA HII TASWIRA MWANANA KATIKA UFUKWE WA MBAMBA BAY!!!

Picha na maelezo toka blogu ya Profesa J. Mbele.
Mbamba Bay ni mji mdogo, kando kando ya Ziwa Nyasa, upande wa Tanzania. Ingawa umaarufu wa mji huu tangu zamani ni bandari, hapo ni mahali pazuri kwa mapumziko.Picha hii ilipigwa mwanzoni mwa Agosti, mwaka huu.Unaweza kusogea hapo ufukweni, ukawa unapunga upepo na kuangalia shughuli za wavuvi, wauzaji wa samaki, akina mama wakifua nguo, na watoto wakicheza majini. Kama unajua kuogelea, mahali hapo utafafurahia. Ukija siku ambapo meli inakuja, utajionea ujio wa meli na kuondoka kwake.


IJUMAA NJEMA KWA WOTE....

5 comments:

Simon Kitururu said...

Picha nguli hii!

Na nshaona mpaka mtumbwi ufaao kigesti bubu haja za kizinzi zikizidi kisiri giza likiingia:-(


Ijumaa njema kwako pia Da Yasinta!

Goodman Manyanya Phiri said...

Meli ikija kukukuta pale Bamba Bay, Panda tu! Na utasikia utamu wa safari ya meli bila kichefuchefu kile cha kawaida melini za Bahari ya Hindi, Atlantic na kadhaika!

ray njau said...

Kila kuendako hisani hakurudi nuksani bali shukrani.Asante sana binti yetu Yasinta kwa kuonyesha kuwa ukipanda ngazi usiwasahau wale uliowaacha chini maana ukirudi utakutana nao au uking'ang'ania huko wanaweza wakaondoa ngazi.Nami nawakumbuka wazee wangu wa kijiji cha Ras ya Nungwi mkoani Unguja Kaskazini.Usemi wao ni huu:-
"OMO NA TEZI MAREJEO NGAMANI[MWENDA OMO NA TEZI HUREJEA NGAMANI]
==================================
Swali kwa hadhira:
--------------------
Hii rasilimani ina athari gani za kiuchumi kwa wakazi wa eneo hili?

ray njau said...

CHEMSHA BONGO NA MAISHA:-
Katika hii mitumbwi unayoiona kwenye picha ni sehemu ipi inatajwa kwa jina la:
1.Omo?
2.Tezi?
3.Ngamani?
--------------------------------
*Na wazee wa Ras Nungwi waliposema omo na tezi marejeo ngamani walikuwa wanapeleka ujumbe gani kwa jamii yao?

Yasinta Ngonyani said...

Simon, Kaka mkubwa Phiri na kaka Ray yaani hapo nimejikuta kama nipo tena kachiki na nipo hapo maana hiyo ndiyo mitaa niliyozaliwa mwanadada mimi. Muwe na Amani.