Wednesday, November 2, 2011

WADAU MNAKUMBUKA VITANDA HIVI NA MAGODORO YA SUFI?

Kitanda cha ngozi ya ngómbe au mbuzi wengi huita "teremka tukaze". Kinakukumbusha nini? Mimi nimekumbuka sana leo enzi hizo yaani kitanda kama hiki ........
......na godoro la sufi au Maranda ya mbao. Swali langu ni kwamba je?kuna wangapi nao wamepitia hili?

9 comments:

Anonymous said...

ok now nimeelewa kuwa ulipita hapo.watanzania wengi tumepita hapo dada wala hakuna swali.

emu-three said...

Ndio maisha yetu hayo, tumepitia huko, ...teremka tukaze!

ray njau said...

Ya kale dhahabu na mavi ya kale hayanuki lakini watu huuliza njia wakati wa kwenda na siyo wakati wa kurudi.
"UKIPANDA NGAZI USIWASAHAU WALE ULIOAWAACHA CHINI MAANA UKIRUDI UTAKUTANA NAO."

ISSACK CHE JIAH said...

Na kweli leo nimeamini kapulya na udadisi wake umekamilika kwetu ni kwetu bwana bado vipo hivi mwaka wa jana tuu nimeviona na kulalia nilikwenda kwenye msiba bado vipo Dada eeeeeeeeee tena olijino kule kwetu sitaki niseme wapi ila wewe unajuwa ni kule kwetu mpandangindo
samahani maana huko ndio kwetu niliogopa kusema kule masasi kwani ni kwa wakwe wanawza ninyanganya MDALA wao
Che Jiah

Jiniaaz! Popkorn said...

Vinanikumbsha kunguni. Walikuwa wakiweka doti doti (nukta) hasa kwenye kona za magodoro. Ilikuwa ni maumiiv makali kweli.

Hivyo vitanda havitatoweka kamwe. Hivi sasa vimeshaanza hata kutumiwa katika zahanati, kwa hiyo kuna maendeleo - na vinakubalika.

Justine Magotti said...

Kweli tumetoka mbali,na ndiyo maana tunasema miaka hamsini ya uhuru,'Tumedhubutu tumeweza na tunasonga mbele'na ndiyo maana magodoro ya sufi na hivyo vitanda ni nadra sana kuviona kwa sasa.Ndiyo maana ya hiyo miaka hamsini.

Yasinta Ngonyani said...

Goodluck! nimekuelewa nilichotaka hapa ni kwamba tusisahau tulikotoka....Ila nimekuelewa kakangu..

em-3! haswa tena hata bila godoro au?

Ray! Ulichosema ni kweli maana siku hizi kila kitu cha kale kinarudi tena. Unajua vitu vya zamani vilikuwa vikidumu sana kuliko sasa.

Che Jiah! umenivunja mbavu wewe:-)

Jiniaaz! Kwanza karibu sana Maisha na Mafanikio:-) Duh! hao wadudu, kunguni si mchezo maana wakibana kwenye kitanda basi hakuna kulala hata kama umechoka vipi..Ahsante kwa kunikumbusha KUNGUNI/NGUNGUNI.

Justine nawe karibu sana Maisha na Mafanikio. Hakika ulichosema ni kweli kabisa ni nadra kupatikana ni kama vile viti vya mkalio wa nyani...

Jiniaaz! Popkorn said...

Usengwili Nangonyani. Ni vyema kuwa nanyi nyote tukishirikishana uzoefu wetu wa past lyf!

Jiniaaz! Popkorn said...

Usengwili Nangonyani. Ni vyema kuwa nanyi nyote tukishirikishana uzoefu wetu wa past lyf!