Sunday, November 27, 2011

NAWATAKIENI JUMAPILI HII YA KWANZA YA MAJILIO PIA YA MWISHO KWA MWEZI HUU PIA NAPENDA KUWASHUKURUNI KWA USHIRIKIANO WENU KWA SALA YA FAMILIA PAMOJA

Milango imefungwa, Ea Bwana.Yule mtoto mchanga amelala, tunajisikia salama.Tuna raha ya ndani, kwani tumeshiba, chakula kilikuwa kizuri, kinatuletea faraja.
Huu nio wakati wa kukugeukia , mwishoni mwa siku hii ya leo, kama familia-familia yako, ambapo Kristu anaishi.
Kwa ajili yetu, kila moja wetu Bwana, tunakushukuru. Kwa ajili ya siku hii ya leo, iliyojaa mambo mengi, mema na yasiyo mema sana. Kwa yote tunakushukuru.
Tunapoangalia nyuma, mara nyingine, ni rahisi kuona kwamba ingaliwezekana kuwa vizuri zaidi. Hapa na pale, tumeshindwa kukupendeza, kwa neno la hasira. Na lile ambalo hatukulitimiza.
Tunasikitika, Bwana tusamehe. Kwani tunahitaji upendo wako. Tunakuhitaji wewe, ukae nasi, ili utulinde, utubariki, kwani wewe ndiwe kuta za kweli na paa za nyumba yetu.
Utubariki tulalapo, utujalie ndoto zetu ziwe za faraha. Na utujalie tuamke kesho tukiwa na uzima mpya tele. Nguvu mpya na starehe mpya. Ili tuweze kuishi tena siku nyingine.

Baada ya hapa napenda kuwashukuruni wote kwa upendo wenu, ushirikiano wenu kwa kushirikiana nami kwa Wiki hii inayokwisha leo kwa maombolezo ya mdogo wetu Asifiwe. AHSANTENI SANA. PIA NAWATAKIENI JUMAPILI HII YA KWANZA YA MAJILIO IWE NJEMA NA MBARIKIWE SANA WOTE MTAKAOPITA KATKA BLOG HII YA MAISHA NA MAFANIKIO. AMINA

5 comments:

Simon Kitururu said...

Jumapili njema Yasinta! Halafu wee mzuri kweli!

Anonymous said...

kuanzia leo ntakuwa natembelea its ma 1st time today

Rachel Siwa said...

Amina da'Yasinta,iwe njema kwako na wote wapitao hapa!

Nampangala said...

Jumapili njema pia kwako na familia yako mlongo. Ubarikiwe

ray njau said...

Mathayo 5:1-16

1 Alipouona umati akapanda mlimani; na baada ya kuketi wanafunzi wake wakamjia; 2 naye akafungua kinywa chake na kuanza kuwafundisha, akisema:

3 “Wenye furaha ni wale wanaotambua uhitaji wao wa kiroho, kwa kuwa ufalme wa mbinguni ni wao.

4 “Wenye furaha ni wale wanaoomboleza, kwa kuwa watafarijiwa.

5 “Wenye furaha ni wale walio na tabia-pole, kwa kuwa watairithi dunia.

6 “Wenye furaha ni wale walio na njaa na walio na kiu kwa ajili ya uadilifu, kwa kuwa watashibishwa.

7 “Wenye furaha ni wale walio na rehema, kwa kuwa wataonyeshwa rehema.

8 “Wenye furaha ni wale walio safi moyoni, kwa kuwa watamwona Mungu.

9 “Wenye furaha ni wale wanaofanya amani, kwa kuwa wataitwa ‘wana wa Mungu.’

10 “Wenye furaha ni wale ambao wameteswa kwa ajili ya uadilifu, kwa kuwa ufalme wa mbinguni ni wao.

11 “Wenye furaha ni ninyi wakati watu wanapowashutumu na kuwatesa na kusema kwa uwongo kila namna ya jambo baya juu yenu kwa ajili yangu. 12 Shangilieni na kuruka kwa shangwe, kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana hivyo ndivyo walivyowatesa manabii waliokuwa kabla yenu.

13 “Ninyi ndio chumvi ya dunia; lakini chumvi ikipoteza nguvu zake, ladha yake itarudishwaje? Haitumiki tena kwa kitu chochote bali ni ya kutupwa nje ili ikanyagwe-kanyagwe na watu.

14 “Ninyi ndio nuru ya ulimwengu. Jiji haliwezi kufichwa likiwa limesimama juu ya mlima. 15 Watu huwasha taa na kuiweka, si chini ya kikapu cha kupimia, bali juu ya kinara cha taa, nayo huangazia watu wote waliomo ndani ya nyumba. 16 Vivyo hivyo acheni nuru yenu iangaze mbele ya watu, ili wapate kuona matendo yenu mazuri na kumpa utukufu Baba yenu aliye mbinguni.