Monday, November 21, 2011

NI WIKI YA PEKEE KWANGU/KWETU-ITAKUWA NI WIKI YA KUMKUMBUKA ASIFIWE!!!

Natumaini wote mu-wazima wa afya njema, na mwisho wa juma umekuwa safi.
Ni hivi blog ya MAISHA NA MAFANIKIO inapenda kuwaambia kwamba wiki hii haitakuwa kama kawaida. Nitawaambia kwa nini, ila kwa kifupi ni kwamba itakuwa wiki ya kumuenzi mdogo wangu marehemu Asifiwe. Kwa namna nyingine haitakuwa kama kawaida hapa kibarazani. NINA IMANI TUTAKUWA PAMOJA /MTAKUWA PAMOJA NAMI NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI. KAPULYA.

12 comments:

Nampangala said...

Pole sana mlongo ni vizuri kuwakumbuka wenzetu waliotutangulia. Ndio tutakuwa pamoja nawe. barikiwe

Mija Shija Sayi said...

Pamoja sana Yasinta.

Siku njema.

Rachel Siwa said...

Mungu akutie nguvu kwa wiki hii ya kumbukumbu ya mdogo wetu Asifiwe na Wapendwa wote waliopoteza wapendwa wao, wakipita hapa wakute faraja,MUNGU NI PENDO APENDA WATU!!!Pamoja dada Yasinta.

sam mbogo said...

Yasinta,mshukuru mungu,kwa kutangulia kipenzi mdogo wako. mungu anamakusudio yake,kumbukumbu njema.kaka s.

ray njau said...

Wadau wako tumesoma,wadau wako tunajali na wadau wako tunasema poleni sana.

chib said...

Tutakusaidia katika maombi

Yasinta Ngonyani said...

Nampangala mlongo! Nashukuru kwa kuwa pamoja nami. Ubarikiwe nawe pia.

Ahsante Mija!

Rachel! kuwa nanyi pamoja hivi tayari naona nimetiwa nguvu. Na nimependa jinsi ulivyosema nami nasema wapendwa wote waliopoteza wapendwa wao muwe na faraja mkipita hapa.
Kaka Sam! nitafuata ushauri wako. Ahsante kwa kuwa nami.
kaka Ray! nawe ahsante kwa kuwa nami katika maombolezi haya.

Kaka Chib! Nashukuru kwani ukizingatia sisi wote ni ndugu na watoto wa baba mmoja.
Mbarikiwe sana wote mliopita hapa na mlioacha chochote. Ahsanteni.

ISSACK CHE JIAH said...

Tupo pamoja najuwa kila kitu ni maombi yatakusaidi nasi tutazidisha maombi kia wakati na muda wote kuwa na AMANI jipe MOYO mlongowangu

CHe Jiah

ray njau said...

Asante dada Yasinta kwa kuvunja ukimya na kutoa shukrani kwa wadau wako kila mtu kwa jina lake.
=====================================
Wachaga wanasema:'UPFU WICHO KO MOMRASA'[MSIBA USIKIE KWA JIRANI YAKO].Hapa tunasoma na kutoa maneno ya faraja lakini kamwe si rahisi kufahamu kihalisi maumivu ya moyoni ya wanakaya wako dada Yasinta.
Kwa kuwa kifo ni sehemu ya mikikimikiki ya maisha hatuna kubwa zaidi kuliko kufarijiana kila mtu kwa nafasi yake.
===================================POLENI SANA WANAKAYA WA DADA YASINTA.
================================

Yasinta Ngonyani said...

Mlongo Che Jiah! Usengili mlongo wangu.

Kaka Ray! Naamini kuwa ukaribu tulionao na ushirikiano umetufanya tuwe ndugu sio wale wa kufanana bali wa kufaana ambao ni wa baba mmoja. Na asante ni kweli kila mtu ana maumivu kivyake.

ray njau said...

Asante sana dada Yasinta;
Japo machungu yamehanikiza moyo wako lakini mikononi una nguvu na ujumbe unazidi kutuma.
Kwa kuwa kila mtu kapate maumbile tofauti na mwenzake nazo hisi mwenzi zatofautiana kwa maili lukuki.Awazavyo yule si sawa na mwingine na kilio cha yule siyo huyu.
Uchagani wanasema:'SAMU CHI KITARASA PFO'[DAMU SIYO KITARASA-BLOOD IS BLOOD AND BLOOD IS NOT KITARASA].Kitarasa ni ndizi yenye utomvu mwekundu ambao unafanana na damu.Lakini wahenga na mababu wa kichaga wakasema:'KAMWE UTOMVU WA KITARASA HAUWEZI KUFANANISHWA NA DAMU YA BINADAMU'.Hitimisho la madokezo yangu ni:'UCHUNGU WA NDUGU WA DAMU NI KWA NDUGU WA DAMU'.

Ausal said...

Pole sana Yasinta wala usijal tupo pamoja katika maombolezo yako kwani ss wote ni wapitaji katika ulimwengu huu, inalilah wahnailah rajihun