Monday, November 7, 2011

TUIANZE JUMATATU HII KWA KUMBUKUMBU HII/JE? WEWE UNAIKUMBUKA HII:-SIZITAKI MBICHI HIZI !!






Hadithi inayokuja, ni ya Sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia


Siku ile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia.


Sungura karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua Sungura nakuambia.


Mtazame hapo juu Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.


Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho Wave akachoka, kachoka hata mk-Ia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Subgura nakuambia.


“Sizitaki mbichi hizi” Sungura akagumia,
“Naona nafanya kazi, bila faida kujua”,
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.


Sio kama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.


Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikta,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi.

17 comments:

ray njau said...

Mtaka cha uvunguni...bindua tanda?
Kila ndege...ruka eyapoti yake menewe?
Bandundu....dugu ake Somji iko Mumbai?
Simba mwenda pole ......tofungwa na..?
Usipoziba ufa....miji tochugulia dani?
----------------------------------
"NO SWEET WITHOUT SWEAT"
==================================

ray njau said...

Hii ni hadithi iliyoandikwa kwa mtindo wa sanaa za maonyesho ikizingatia tasnia ya nyimbo na mashairi.
Mtunzi hapa anatumia lugha ya mficho ili msomaji anunue wakatika katika kufanya tafakari itayomuonyesha kuwa huwezi kufikia maisha na mafanikio kwa kukwepa mikikimikiki.
Kamwe katika maisha na mafanikio hakuna kususa bali kuikabili mikikimikiki.
Ni hayo tu kwa sasa wadau wa kibaraza cha maisha na mafanikio.Hadi wakati ufaao siku zijazo asante na kwaherini kwa sasa.

sam mbogo said...

Doh!!,Yaani wewe leo umewekelea kanyau. niko nyumbani leo siku itakuwa poa sana hasa kipengere cha sizitaki mbichi hizi. lilikuwa soma tosha enzi zetu,mpaka sasa hivi bado wengi ni akina sizitaki mbichi hizi!!..? weweweee. sungura huyoo.
safi sana ,Dada,mpendwa,mtukufu,kingunge,ndugu,kapulya,Yasinta. kaka S.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray! haswa ulichosema pia nachukua nafasi hii na kusema AHSANTE kwa kutochoka kupita hapa na kuacha kitu.

Kaka S! una vituko wewe yaani basi si Ahsante kwa wasifa wako. Ndiyo leo nimeweka hii nimekumbuka darasa la tano au sijui la nne? mmh hapana litakuwa la tano. Una bahati kuwa nyumbani wengine tunahenya tu:-)

ray njau said...

Maisha na mafanikio ni mtoni usipoenda kuteka maji utaenda kufua au kuoga!
===================================
"YA KALE NI DHAHABU NA KINYESI CHA KALE HAKINUKI AU KINANUKIA?

Bennet said...

Hivi mgomba ni mti maana huyu sungura mtini akasogea

Fadhy Mtanga said...

unajua mie ni mgonjwa sana wa mashairi. ahsante sana kwa shairi hili. limenikumbusha zamani sana.

Rachel Siwa said...

Dada'ke umetukumbusha mbaliiii sana, Asante sana mwayego!

ray njau said...

shukrani za wadau ni njema sana lakini ni vema tuweke kibarazani kile jamii yetu inachoweza kunufaika nacho kupitia utunzi huu wa enzi za Mwalimu.Je taaluma hii inapotea au imeadimika?
@Swahili binti Waswahili chambua mada kwa kina chake!

John Mwaipopo said...

what a nostalgic piece.

bennet katika ushairi kuna kitu kinaitwa 'poetic licence' kinakuruhusu kuvunja misingi fulani ili ufanikiwe katika vina na mizani. lakini hata katika kizungu mgomba waitwa banana 'tree'

Anonymous said...

Yasinta umenikumbusha mbali!! acha tu. Ubarikiwe

Jacob Malihoja said...

Umenikumbusha mbali sana Yasinta .. unanikumbusha mchaka mchaka .. kabla ya kuingia darasani asubuhi na mapema.. kuanza vipindi.

"mchaka mchaka Chinja, Aliselema hadija"

"mchaka mchaka Chinja, Aliselema hadija"

au ile Nyimbo ya "Bomaa standasta .. Bomaa nalolilee .. Bomaaa standastaa .. alo .. alo aloo"

"Bomaa standasta .. Boma Bomaa nalolilee .. Bomaaa standastaa .. alo .. alo aloo"

Nakumbuka katka moja ya mchaka mchaka nilijikwa na kucha ya dole gumba la mguu wa kulia likabanduka na kukaa mithili ya bonet ya gari ifunguliwavyo .. ngoma ikawa kuliondoa...we acha tu..

Kwa kweli imepita miaka zaidi ya 25 sasa tangu niimbe nyimbo hizo na kwa kweli sikumbuki na hata sasa sielewi maana ya nyimbo hizo ambazo nakumbuke vipande vifupi tu.

sam mbogo said...

Jacob, huo wimbo wa mchakamchaka,ni lugha ya watu, aliselema alija na siyo adija. nikinyamwezi hicho ndugu yangu. kaka s

Justine Magotti said...

du kweli sizipendfi hizi mbichi

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua fursa hii kwa kuwa nami katika KUMBUKUMBU hii na karibuni tena na tena na ruksa kuendelea na kukumbuka kumbukumbu hii.

Jacob Malihoja said...

Asante da Yasinta kwa kuweko mada hii, Maana kwa kweli leo ndio nimejua angalao si kwa sana kuwa Nyimbo fulani nilikuwa nikiipenda ni ya ki lugha .. kinyamwezi! asante sana Samu Mbogo kwa kunifunulia .. na nimeweza kujua kuwa nilikuwa nakosea .. na nafikiri wengi tumekuwa tukikosea.

Anonymous said...

nimecheka kweli asante Yasinta