Tuesday, November 1, 2011

AHSANTE BABA!!!

Hapa Mwenyewe Mzee Ngonyani

Unajua/mnajua kama kumbukumbu nyingine zinakuja wakati ukisikiliza mziki? Basi mimi leo nilikuwa nasikiliza mziki na mara nikakumbuka kisa hiki ambacho kilinipata. Nikiwa nikiishi kijiji cha Kingoli. Nakumbuka nilikuwa darasa la tano. Kwanza nianze na KUMSHUKURU BABA kwa tabia yake aliyokuwa nayo ya kila usiku kupita na kuangalia watoto wamelala? Kwani siku hii aliokoa Maisha yangu. Siku hiyo kama kawaida, nilikuwa na homework , basi baada ya chakula cha jioni nikachukua koroboi yangu na kuanza kusoma. Nilikuwa nimejilaza kitandani na nikaweka karoboi kifuani huku nikisoma. Muda ukapita, nikapitiwa na usingizi. Si mnajua huwezi kulala tu bila kugeuka. Nikawa nimegeuka bila kufikiri ya kwamba koroboi bado inawaka. Halafu mbaya zaidi nilikuwa nimejifunika blanketi. Kama baba angechelewa kidogo tu basi leo nisingekuwa hapa. AHSANTE BABA.

Huu hapa ndio wimbo ambao umenikumbusha kisa hiki.....

15 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

alipaswa kukupa viboko kadhaa

ray njau said...

Mlee mvulana kulingana na njia inayomfaa; hata atakapozeeka hatageuka kando na kuiacha[Methali 22:6]

Ujinga umefungwa pamoja na moyo wa mvulana; fimbo ya nidhamu ndiyo itakayouondolea mbali[Methali 22:15]

Usimnyime mvulana nidhamu. Ukimpiga kwa fimbo, hatakufa.Inakupasa wewe mwenyewe umpige kwa fimbo, upate kuikomboa nafsi yake na Kaburi[Methali 23:13,14]

Msikilize baba yako aliyekuzaa, wala usimdharau mama yako kwa sababu tu amezeeka.Nunua kweli wala usiiuze​—​hekima na nidhamu na uelewaji.Baba ya mtu mwadilifu hakika atakuwa na shangwe; na mtu anayekuwa baba ya mwenye hekima atamshangilia pia.Baba yako na mama yako watashangilia, naye mama aliyekuzaa atakuwa na shangwe[Methali 23:22-25]

Yasinta Ngonyani said...

Kamala! kwanini nilipaswa kuapata viboko?
Kaka Ray! Ahsante nimekuelewa.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

pole sana.....yaani leo Erik na Camila wasingekuwepo!! Dah

chib said...

Duh!
Lakini... uliwezaje kusoma umejifunika na koroboi ikakaa kifuani? Ulikuwa na hatari wewe!
Elimu ni bahari na haina mwisho.

Unknown said...

na ashukuriwe baba yetu...

ray njau said...

Kumbukumbu la Torati 6:4-9
---------------------------------
4 “Sikiliza, Ee Israeli: Yehova Mungu wetu ni Yehova mmoja. 5 Nawe lazima umpende Yehova Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote na kwa nguvu zako zote. 6 Na maneno haya ninayokuamuru leo lazima yawe moyoni mwako; 7 nawe uyakazie kwa mwana wako na kuyasema unapoketi katika nyumba yako na unapotembea barabarani na unapolala na unapoamka. 8 Nawe uyafunge kama ishara kwenye mkono wako, na yawe kama utepe wa kipaji katikati ya macho yako; 9 nawe uyaandike juu ya miimo ya mlango wa nyumba yako na juu ya malango yako.

Rachel Siwa said...

Duuhhh nijambo la kumshukuru sana Mungu, leo hii mzee Ngonyani angeweka kumbukumbu ya kumpoteza mwanawe kama Siwema.

Simon Kitururu said...

DUH!

Kweli uliponeachupuchupu!
Kwa wenye imani za MIUNGU wanaweza kudai ilikuwa ni mipango tu ya MIUNGU au kamalaika fulani kalifanya taimingi nzuri kabla hujazurika!

Mie nashukuru upo lakini na mwenye uwezo wa kucheza sindimba kwechukwechu!

Swali: Hivi hapa ni BABA au MUNGU ashukuriwe!!!?,.....
... kwa kuwa hata wenye imani wangedai kuwa ni mipango yake kama ungeungua.

Na BABA kushukuriwa kuna watakaodai machale yake hayakuwa ni kwa uwezo wake tu wakupata machale kibinadamu.

Naongea tu pekeyangu kwa sauti!:-(

Anonymous said...

mwaitege aliimba maaama mama mama! uwezo wa kukulipa sinaa!! sasa inabidi tuugeuze uwe Baaaba baba baba uwezo wa kukulipa sina!

bye!

Yasinta Ngonyani said...

Chacha AHSANTE! yaani kabisa wasingekuwepo kwa vile mimi nisingekuwepo.

Chib!Sikujifunika blanketi wakati nasoma isipokuwa lilikuwa kitandani kwa ajili ya kujifunika ila nilisahau kujifunika tena ndilo lililoanza kuungua. Kweli elimu kuipata ni kazi...

kaka Mrope! yaani na ashukuriwe mno.

Kaka Raynjau! Ahsante tena kwa kutukumbusha hilo.

Rachel! We acha tu yaani hatungejuana hii leo:-(

Kaka yangu Simon! mmmmhh, ulichosema ni kweli kabisa. labda nianze na kusema ilibidi nisema AHSANTE MUNGU KWA KUMWONGOZA BABA YANGU JIONI ILE NA KUWEZA KUJA CHUMBANI KWANGU LA SIVYO...kwani inawezekana jioni ile baba asingekuwa nyumbani lakini labda pia ni Mungu alimwongoza awe nyumbani na akaa macho hadi muda ule....Nimecheka hapo uliposema "Mie nashukuru upo lakini na mwenye uwezo wa kucheza sindimba kwechukwechu!" maana nilipokuwa mdogo nilikuwa napenda sana kuigiza sindimba kwechukwechu ngoma ya wamakonde. Si wengi mnakumbuka usiku wa mbalamwezi....samahani kwa kuwa nje ya mada:-)
Na nwe kaka Goodluck! Hakika umesema kwani mara nyingi naona huwa tunawasahau kuwashukuru akina baba. Ahsante kwa ushauri wako wa kuanza kuimba hivyo ....

Mija Shija Sayi said...

Mtoto una hatari wewe!!

Kaka Ray ufafanuzi please...

Asante baba kwa kuokoa Janga kubwa.

God bless..

ray njau said...

@Mija:-
Katika hii historia ya maisha ya Yasinta baba yake mzazi alitibitisha kuwa ni mzazi anayejali familia yake na kuisimamia kwa mujibu wa maandiko matakatifu.Hii ni changomoto kwa maisha na mafanikio ya familia zetu ndani ya mikikimikiki ya maisha.

ray njau said...

BABA YASINTA ALITHIBITISHA KWA MATENDO YAKE KUWA NI BABA MWEMA.

[AHSANTE SANA BABA YASINTA]

Anonymous said...

kama alivyosema kamala ulitakiwa ule mboko,mimi hapa sikumoja mwana kaenda kulala alikuwa ananyosha nguo usingizi sijui ulimpitia akaacha pasi kwenye umeme basi ndo hivyo mimi machale ya kimizimu ikanicheza nikakuta nguo imeisha ungua linaenderea godoro we nilimtandika na waya wa hiyo pasi,basi eti mamake agombelezea wacha nayy umlambe maana kila siku ninasema nyoosha nguo mapema hasikii ni hatari kama umechoka zima kibatari lala