Monday, November 28, 2011

ULIJUA KAMA SONGEA KUNA HIFADHI /MBUGAYA WANYAMA?


Nimeishi miaka mingi Songea nilikuwa sina habari kama kuna mbuga ya wanyama. Mbuga hii ipo nje kidogo ya Msamala . Kwa hiyo nasi tulipata bahati na kuingia hapa kwa msaada ya mwenyeji wetu ndugu Sunday Hebuka.


Hili ni jengo/au niseme ni ofisi ndipo ambapo unalipa....Na pia unaona magari kwa ajili ya watalii........


Ila sisi tuliona ni vizuri kutembea kama unavyoona tupo katika msululu hapo...kusaka wanyama....

Msafara unaendelea hapa ni kadaraja...
Na hapa ni mto Ruhila kwa ubunifu wao wameweka mawe ni kama daraja vile. Ila inabidi uwe shupavu kwani kulikuwa na utelezi. Hapa ni lazima kuvua viatu pia...Siku hii tulifurahi sana kuwa katika eneo hili ambalo hatukujua kama lipo...Ushauri ukifika Songea usikose kuchungulia hapaa.



8 comments:

ray njau said...

Asante sana Yasinta kwa kutufungua macho kuhusiana na maeneo ya yaliyohifadhiwa kiasili.Maeneo hayatangazwi sana kutokana na mamlaka za mikoa na wilaya kushindwa kuwekeza katika utangazaji wa maeneo yaliyopo chini ya mamlaka zao.
====================================
'Mtembea bure siyo sawa na mkaa bure maana hupata...................!!!
=====================================

Anonymous said...

inamaana Yasinta uko hapa Tanganyika?

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray ni kwelikabisa hii hifadhi inabidi itangazwe maana ipo sehemu ambayo ni fichu sana na naahidi nitafanya matangazo na wote watajua. hiyo methali mbona hujamalizia.....?

Usiye na jina! Mimi nipo kila mahali...Tanzania na sehemu nyingine...

ray njau said...

Mtembea bure siyo sawa na mkaa bure maana hupata vya bure!

ray njau said...

Hitimisho la Jumanne ya Novemba 29,2011 bila kujua kinachoendelea kwenye familia ya mama maisha.Huenda afya za wanafamilia hazipo sawa na kuifanya siku ya leo kuwa siku ya 'maisha bila mafanikio'.
Kwa mdau yoyote mwenye taarifa zilizoibua ukimya wa leo aweke hapa kibarazani ili wadau waonyeshe fadhili-upendo.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Ray! Ahsante kwa upendo wako ni kweli afya zetu hazipo sawa ila si mbaya sana Mwenyezi Mungu anasaidia.

Anslaus Komba said...

Hata mimi sikujua kama Songea kuna kitu kama hiki, japo nimezaliwa na kukulia Peramiho! Nashukuru kwa kutujulisha, hope next time nikiwa likizo nitapitia hapo kujionea neema tuliyoipata kwa MUNGU! Thanxs for information!

Nampangala said...

Mlongo mbona haibu hata mim mwenzi nilikuwa sijuwi kama tunambuga ya wanyama uko kunyumba. haa itabidi nipitie uko nikienda. ni vizuri ulienda kujionea mwenyewe.