Wednesday, November 2, 2011

HOT NEWZ...............UNYAMA UNYAMA MZEE WA MIAKA 60 LUDEWA ACHOMWA MOTO KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

Katika kipengele chetu cha JUMATANO YA MARUDIO mbalimbali leo Kapulya amefika mpaka mkoani Njombe na kukutana na habari hii ya kusikitisha ambayo imeniliza na nimeona tulie pamoja. Habari hii nimeikuta kwa kaka Francis. Kweli binadamu tuna roho za namna ya pekee yaani.....

Mwili wa marehemu mzee Laurance Nkwera

Umati wa Wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo wakiwa wamemshikilia dada wa marehemu aliyekuwa akilia huku akimlaumu marehemu kaka yake kwa kujihisisha na uchawi na kukataa ushauri wake.

MTU MMOJA aitwaye Laurance Nkwera 60 mkazi wa Kijiji cha Ibani Ludewa katika Mkoa mpya wa Njombe amekufa kwa kuchomwa moto na kuungua vibaya kwa imani za kishirikina, huku nyumba yake ikiteketea, na familia yake kunusulika kifo kwa kutoboa nyumba.

Mwandishi wa mtandao huu kutoka Ludewa Basil Makungu anaripoti kuwa tukio hilo limetokea usiku wa octoba 01 mwaka huu majira ya saa nane alfajili baada ya mlango wa Nyumba yake kufungwa nje na watu wasiojulika kutokana na mvutano uliotokea kati yake na wauaji kabla ya wauaji hao kumzidi nguvu na hatimaye kuchoma nyumba yake.

Akizungumza katika eneo la tukio Cesilia Haule ambaye ni mke wa marehemu Laurance alisema kuwa yeye na mumewe walikuwa wamelala chumbani na watoto wao wawili wakiwa wamelala sebuleni na kwamba ilipofika saa nane za usiku watu wasiojulikana waligonga mlango na kutoa masharti ya kutokutoka nje.

Ester Nkwera ni mtoto wa marehemu na Mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Kimbila anasema yeye alikuwemo ndani wakati Nyumba ikiunguzwa moto na kwamba yeye na mama yake walifanikiwa kujiokoa kwa kutoboa nyumba yao ya miti lakini Baba yake alibaki pamoja na mdogo wake Laurance.

Laurance ni mtoto wa marehemu mwenye miaka mitano tu, yeye alinusurika kifo kwa kupita katika mikono ya wauaji ambao walikuwa wamezingira nyumba hiyo ya miti huku wakiwa wamesimama pembeni kuhakikisha Nyumba na vyote vilivyomo vinateketea.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Ibani Philipo Haule, Afisa Mtendaji Kata Onesmo Haule wamesema kuwa marehemu pamoja na watu wengine wanne ni muda mrefu walikuwa wakituhumiwa kujihusisha na kuwatesa watu kwa uchawi ikiwemo kubaka wake za watu kiuchawi, kuua watu na kuwafanyisha kazi usiku kwa uchawi.

Wakizungumza kwa masharti ya kutoandika majina kwa kuhofia usalama wao wakazi wa kitongoji cha Ibani Ludewa walisema wamechoshwa na udhalilishwaji unaofanywa na wachawi ikiwemo kuwabaka wake zao kiuchawi,kuwauwa na kuwatumikisha kazi usiku na kwamba watahakikisha wanaikomesha tabia hiyo kwa kila anayehusika kwa kuwa wananfahamika.

Aidha Monica Mchiro Diwani wa Kata ya Ludewa alikiri kufanyika kwa mkutano wa hadhara octoba 11 mwaka huu unaowahusu watu watano wanaotuhumiwa na Wananchi kuwatesa kwa nguvu za uchawi hata hivyo watuhumiwa akiwemo marehemu walikana kuhusika na matukio hayo.

Bi Monica aliwataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake watoe taarifa polisi na ofisi za vijiji na Kata kuhusu uhalifu wowote uanotokea katika maeneo yao.

Kufuatia tukio hilo,Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Bi Georgina Bundala amemwagiza mkuu wa polisi wilaya kuhakikisha wale wote waliohusika na ukatili huo wanakamatwa haraka na kupelekwa mahakamani ili sheria iweze kufuata mkondo wake.

Aidha Bundala amekemea vikali tabia hiyo na kusema kuwa kwa jamii iliyoelimika haiwezi kufanya mambo kama hayo, na kuongeza kuwa kuna haja ya kutoa elimu kwa wananchi ili kuwajengea uelewa namna ya kukabiliana na matukio kama hayo kwa kufuata sheria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi wa polisi Evarist Mangala alikiri kutokea kwa mauaji hayo na kwamba taarifa kamili atatoa baada ya kupata taarifa kamili ingawa alikiri kuwa chanzo cha mauaji ni imani za kishirikina

Blog ya Maisha na Mafanikio inatoa pole kwa wafiwa wote kwa janga hili. Pia inapenda kutoa ushauri kuwa ingekuwa jambo la busara au ni jambo la busara kutumia vyombo vya sheria. Swali langu ni kwamba hao wanaosema Mzee Nkwera alikuwa na tabia hii wanajuaje kama wao nao wanahusika?
TUONANE TENA JUMATANO IJAYO MPAKA HAPO MUWE NA WAKATI MZURI!!

5 comments:

ray njau said...

Siku zote ni muhimu busara itawale maamuzi yetu.
-----------------------------------
Mwanzo 9:1-7
-----------------------
1 Naye Mungu akambariki Noa na wanawe, akawaambia: “Zaeni, muwe wengi, mjaze dunia. 2 Kila kiumbe hai cha dunia na kila kiumbe kinachoruka cha mbinguni kitawahofu na kuwaogopa ninyi, na pia kila kitu kinachotembea juu ya nchi, na samaki wote wa baharini. Vimetiwa mkononi mwenu. 3 Kila mnyama anayetembea ambaye yuko hai anaweza kuwa chakula chenu. Kama nilivyowapa mimea ya majani, nawapeni hao wote. 4 Isipokuwa tu nyama pamoja na nafsi yake—damu yake—msile. 5 Na, tena, damu ya nafsi zenu nitaitaka. Kwa mkono wa kila kiumbe kilicho hai nitaitaka; na kwa mkono wa mwanadamu, kwa mkono wa kila mmoja ambaye ni ndugu yake, nitaitaka nafsi ya mwanadamu. 6 Yeyote anayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake nayo itamwagwa na mwanadamu, kwa maana kwa mfano wa Mungu alimfanya mwanadamu. 7 Nanyi, zaeni na kuwa wengi, mjaze dunia na kuwa wengi ndani yake.”

ISSACK CHE JIAH said...

Hii ni kali sana kwani mshahara wa dhambi ndio huo si umeona wale wasihusika wote wamenusurika safi saaana kama alijifanya mtemi wa nguvu za giza watu wana nguvu ukatili na unyama
poleni sana wafiwa hii ni fundisho kwa hao wenzake wajiandae vinginevyo waanze yaani wahame fasta

ISSACK CHE JIAH said...

Hii ni kali sana kwani mshahara wa dhambi ndio huo si umeona wale wasihusika wote wamenusurika safi saaana kama alijifanya mtemi wa nguvu za giza watu wana nguvu ukatili na unyama
poleni sana wafiwa hii ni fundisho kwa hao wenzake wajiandae vinginevyo waanze yaani wahame fasta

Mija Shija Sayi said...

Kaaazi kwel kwel!!!

emu-three said...

Swali kubwa ni je ni kweli alikuwa hivyo, au ni hisia tu, na kama tunaamini kuwa kweli alikuwa hivyo, ina maana tunaamini uchawi! Najiuliza tu!