Thursday, November 17, 2011

UJUMBE WA LEO NI HUU:- MAISHA NI ZAWADI!!

Leo kabla ya kusema neno baya, mfikiria mtu ambaye hanaweza kusema.
Kabla ya kulalamika kuhusu ladha ya chakula, fikiria mtu ambaye hana kitu cha kula. Kabla ya kulalamika kuhusu mume wako au mke wako, fikiria mtu amnbaye amliliaye Mungu kwa ajili ampe rafiki. Leo kabla ya kulalamika kuhusu maisha. Fikiria mtu ambaye alikwenda mbinguni mapema mnoamekufa mapema mno. Kabla ya kunung'unika kuhusu umbali gani unaendfesha garilako, fikiria mtu ambaye anatembea umbali huo kwa miguu yake. Na wakati wewe ni uchovu na ulalamikapo kuhusu kazi yako, fikiria wale wasio na ajira, walemavu, na wale ambao wanataka wangekuwa na kazi kama yako yako. Na wakati mawazo yanakutawala na kukufanya uwe na huzuni, tabasamu na ufikiri. Wewe ni hai na bado upo.
TUWE NA UHAKIKA NA TUFIKIRI/TUWAZE KWA UHAKIKA!!!! 

17 comments:

ISSACK CHE JIAH said...

Nikweli nami niwe mtu wakwnza kuchangia kweli maisha ni zawadi usije ukaona mtu yule anaishi vile nawe ukaiga kuishi kama mwenzio au tuseme nduguyo ukamwona mr sam analala pazuri au anakunywa kila siku nawe ukageza huyo kapewa zawadi na hana mpinzani, ili uishi vizuri ishi kama upendavyo si kama wapendavyo hapo maisha yatakuendea vizuri na hutayumba kwani kila mtu kapewa riziki kwa namna yake si kwa namna ya mtu mwingine kipaji ni kile alichokupangia mwenye enzi si ulazimishe ,fanya mipango yako kutokana na wigo wa uwezo wako usiige kwa mtu jitahidi kukubali matokeo fanya busara kuwa mtulivu katikamipango yako ya maisha kweli
NDUGU YANGU MAISHA NI ZAWADINA MAISHA NI MAISHA KUBALI MATOKEO ILA WEKA JUHUDI KATIKA KUTAFUTA MAISHA USIKATE TAMAA
CHe Jiah

Goodman Manyanya Phiri said...

["...na kabla ya kunung'unika eti umekosa vyatu, wafikirie wasiekuwa na miguu."]

sam mbogo said...

Katika ujumbe wa leo,nimeukubali kiaina. najaribu kuichambua zawadi,jinsi inavyo patikana,au mchakato wake mzima unao kuja kuitwa baadae zawadi.maisha nizawadi kutoka kwa nani,mungu,au wazazi,au dakitari aliye kuwa mstari wa mbele kumsaidia mama mjamzito kujifungua salama,na hatimaye kumpata mtoto ambaye nimimi nawewe.maisha ninini,ni pumzi au kuwa na elimu,kazi nzuri,ndo maisha.maisha nikuishi kama ndivyo nani mwenye mamlaka ya kuishi kwetu hapa duniani.wengine husema maisha nisafari ndefu? na labda wengi watakumbuka katika msemo huohuo wa maisha nisafari ndefu,ambayo mwisho wake nikifo! ,je tuna uhakika na hilo.mtoa ujumbe umeniwazisha sana,maisha nizawadi,hivyo waweza kuiomba kama mtu akikuuliza ? au kwasababu mtoa zawadi hiyo ni mungu? basi hatuna muda wakusema mimi nataka zawadi hi ? kumbe kuishi ni zawadi ukiichezea waweza kunyang'anywa? nanani? asante da Yasinta kwa ujumbe, nikipata muda nitarudi tena,ngoja nisikilize wengine wana semaje. kaka s

EDNA said...

Asante kwa ujumbe murua da Yasinta.

Rachel Siwa said...

Umenena da'Yasinta yaani umekugusa nyanja nyingi sana,ASANTE MUNGU KWA YOTE!!

Mija Shija Sayi said...

Asante kwa neno la leo mama Camilla..

Simon Kitururu said...

Ujumbe kibonge huu! Asante kwa hii!

ray njau said...

nnnnnnnnnnnnnnnnnn

ray njau said...

Msemo:Maisha ni mchezo na dunia ni jukwaa na kila mtu anacheza anavyoweza.
-------------------------------------
"WEWE UKIOMBA VIATU MWENZIO ANAOMBA MIGUU"
-------------------------------------
NINI HASA KUSUDI LA MAISHA?
---------------------------------

Simon Kitururu said...

@Mkuu Njau:Si nasikia kusudi la maisha lingejulikana kwa uhakika kama sie BINADAMU tungeomba kuzaliwa?
Kwa hiyo labda kusudi la MAISHA ni jinsi tu mtu ajitafsiriavyo kwanini yuko hai. Na kuna watakao msingizia MUNGU na watakao singizia tuko MAISHANI ili tuzae... mpaka watakaodai kusudi la kuwa MAISHANI ni KULA!


AU?

Salehe Msanda said...

Ni kweli maisha ni zawadi na ni tunu ambayo tunatakiwa kuitumia kwa kutenda mema ili kudumisha umuhimu wa tunu tuliyopewa na mwenyezi mungu.
Ili kuienzi vyema tunu hiyo tunatakiwa kupunguza choyo ya kujipenda kupindukia bali tuongeze upendo kwa wengine
Kila la kheri.

Unknown said...

tumezoea kulalamika sana bila kuwaza vizuri,ukiyafikira sana unaona maneno yalivyojaa ukweli,si kila wakati ni wakatai wa kulalamika na kusononeka.

ray njau said...

@Mtani wangu Kitururu;
Mada bado inashika kasi na sasa nikuulize hivi:JE KUSUDI NI KUZALIWA,KUISHI NDANI YA CHANGAMOTO NA HITIMISHO LA KIFO?

Simon Kitururu said...

@Mtani wangu MANGI Njau: Wala sina jibu aisee katika swali hilo lako Mkuu!

Mtani swali gumu hilo!


Ila nikikaa mkao fulani naweza kusema BINADAMU aanzaye kudadisi sana mpaka maana ya MAISHA ,.....labda huyo ana MUDA zaidi mapaka ana muda mpaka wa kufikiria.

Kwa kuwa katika kibado kikumbukwacho ni KIBADO hata kama hicho ni kipengele tu kwenye maisha ya MTU.:-(


Swali:
Si wakati hakuna muda vifikiriwavyo zaidi ni vichukuavyo muda?

ray njau said...

Kitururu:-Endelea kufikiria zaidi na huenda ukavuka hilo daraja.
--------------------------------
Suala la muda na wakati kila mtu anajipangia mwenyewe na hapa hakuna fomula.

Yasinta Ngonyani said...

Nachukua nafasi hii na kuwashukuruni kwa ushirikiano wenu maana bila ninyi nadhani MAISHA NA MAFANIKIO ISINGEFIKIA HAPA ILIPO. MNAPENDWA WOTE.

obat penggugur said...

obat telat bulan i think your blog very informative cytotec thanks for sharing obat cytotec