Tuesday, November 22, 2011

ASIFIWE NGONYANI (1989- 2011). Kioo kingine cha maisha yetu, kwa maisha yetu na wenzetu

Kama jana jumatatu nilivyosema ni wiki ya kumkumbuka mdogo wangu Asifiwe Kwa hiyo nimeona si mbaya kama tukimkumbuka Asifiwe kwa mada hii iliyoandikwa na Mzee wa changamoto.

"..see you in ZION, holding hands together standing by MY FATHER'S SIDE. Meet you in ZION singing songs together....." LUCIANONi mwaka mmoja na siku 24 tangu ilipobandikwa MAKALA HII YA KUMSHUKURU MUNGU KWA KUFANIKISHA UPAUSAJI WA Dada Mdogo Asifiwe Ngonyani. Leo hii NAMSHUKURU MUNGU kwa maisha na mapumziko ya Dada Asifiwe, ambaye aliaga dunia Machi 23 na kuzikwa Machi 26.Dada wa Asifiwe, ni Da Yasinta Ngonyani. Sio bloga mwenzangu tu, bali ndiye anayewasiliana na familia yangu kuliko bloga yeyote. Twawasiliana kwenye chat, kwenye simu na hata skype ambapo huwa tunaongea mara kwa mara.Mara nyingi tumezungumza kuhusu Asifiwe.Na kila mara alikuwa akitujulisha maendeleo yake. Na kwa kila wakati ambao afya ya Da Asifiwe ilikuwa ikihitaji msaada wa uangalizi wa watabibu, Da Yasinta alikuwa mnyonge. Na nakumbuka siku ambayo alisema hakuweza kuweka bandiko kwenye blogu yake kwa kuwa hakuwa na furaha. Baadae tukawasiliana kuwa ameweza kuongea na Asifiwe na alikuwa na furaha kusika maendeleo yake ni mema.Lakini juma hili, taarifa zimefika kuwa ASIFIWE HATUNAYE. Binafsi niliumia sana. Nilikuwa sijapata kuonana na Asifiwe, lakini mazungumzo juu yake kutoka kwa Dadake na Da Koero yalinifanya kuwa karibu naye kwa namna ya pekee.Lakini kwa wote hawa (Yasinta na Koero), nililogundua ni namna ambavyo FURAHA ZAO ZILIATHIRIWA NA HALI YA ASIFIWE. Kwa maongezi nao, niligundua juu ya maisha yake ambayo ndicho kilikuwa kivutio kikubwa kwa ndugu zangu hawa ambacho ni TABIA. Da Yasinta hakuwa tu akimzungumzia Asifiwe kama ndugu yake ambaye ni wao wawili pekee wa kike katika familia, lakini alikuwa akimzungumzia kama RAFIKI.NA HILI NDILO NILILOJIFUNZA NA NINALOJIFUNA.Ninapomuwaza ASIFIWE, nikimuwaza Dada Yasinta na dugu, jamaa na marafiki wakimlilia, naona AKISI YA MAISHA YA ASIFIWE. Naona jambo ambalo sisi sote twatakiwa kujifunza kutoka kwa Asifiwe, kisha kuona maisha yetu na ya wali walio kwetu yakibadilika.KILIO cha kumlilia Asifiwe ni ishara nyingine kuwa alipendwa, na licha ya kuwa ni KAZI YA MUNGU kumpumzisha baada ya kuyagusa maisha yetu kwa namna alivyoyagusa, bado tungependa kuendelea kuwa naye.Nakumbuka Juni mosi mwaka 2009, NILIBANDIKA MAKALA HAYA KUHUSU KILIO CHANGU KWA MJOMBA WANGU, ambaye nililia kwa kuwa nilimlilia, na katika makala hiyo, niliandika kuhusu kilio cangu kwa mjomba kuwa "nililia kwa kuwa kwa tafsiri yangu, kulia ni kutokubali kuwa wakati wa mjomba kupumzika ulikuwa umefika na hakika alistahili kupumzika baada ya kutenda mema mengi tena kwa mapambano ya hali ya juu. Mjomba alikuwa mtu mwema kwangu na kwa wengi..." Mtu wa kwanza kutoa maoni kwenye bandiko hilo (kama ilivyo kwa mabandiko mengi kwenye blogu nyingi) ni Dada yangu Yasinta ambaye alisema "Mzee wa Changamoto pole sana tena sana. Nalia pamoja nawe kwani nakuelewa kabisa. Na nakushauri lia sana kwani kulia ni moja ya kutoa uchungu wako. Natumanini Mjomba wako yupo nawe kila siku amini. Astarehe kwa amani."Leo hii nami namkumbuka Asifiwe, na licha ya kuwa NAMLILIA, bado nakumbuka kuwa ALISTAHILI KUPUMZIKA na kuwa aligusa maisha ya waliohusiana na kuishi naye na yetu tuliomfahamu kupitia ndugu na marafiki.Lililo kubwa kwetu tuliobaki, ni kuishi maisha sahihi na maisha yaliyo mema. Kama ambavyo aliishi ASIFIWE NGONYANI....Na ndio maana (kama kisemavyo kichwa cha post) namuona "ASIFIWE NGONYANI kama Kioo kingine cha maisha yetu, kwa maisha yetu na wenzetu"Chris Rice anasema....COME THOU FOUNT

AHSANTE MZEE WA CHANGAMOTO/KAKA MUBELWA BANDIO!!!

6 comments:

ISSACK CHE JIAH said...

NASEMA TUPO PAMOJA KWA MAOMBOLEZI,
POLENI WANGONYANI WOTE, LAZIMA TUKUBALI KUWA KAZI YAKE HAINA MAKOSA SIKU ZOTE HATUJUWI KAMPA KAZI GANI TENA MUHIMU KULE ALIKOTANGULIA ,HUWENDA YEYE NDIYO MWANDALIZI WA TUTAKAPOFIKIA SISI TUTAKAPO MFUATA KWA MUJIBU WAKE HAKUNA ATAKAE KWEPA MSALABA HUU WALA KIKOMBE HIKI HAKIEPUKIKI HIVYO TUWE WAVUMILIVU NA TUAMINI KUWA HAKUNA KOSA KATIKA HILO ALILOLITENDA
AMEN
CHe Jiah

Unknown said...

Bwana alitoa. Bwana ametwaa. Lihimidiwe jina lake... Bwana na akutangulieni katika muda huu mwafaka wa kumkumbuka mdogo wetu. Amen

Rachel Siwa said...

Maneno aliyotumia baba P Kaka Mubelwa si Upendo tuu bali kwangu ni Chemchem na bubujiko la faraja,utu wa Kufikiri na thamani kwa wengine,Ubarkiwe sana kaka yangu Mubelwa!

Nami nitaimba hii TENZI YA 101,TWONANE MILELE!!!

MUNGU AZIDI KUTUBARIKI SOTE TUNAKAOPITA HAPA!

POLE DA YASINYA POLE FAMILIA YA NGONYANI POLE WOTE WALIOPOTEZA WAPENDWA WAO,MUNGU NI PENDO!!!!

emuthree said...

Poleni sana familia ya Ngoyani, kilichobakia ni kumuombea mwenzetu aliyetangulia mbele za haki

ISSACK CHE JIAH said...

LEO Siku rasmi ya kumwenzi dada ASIFIWE mungu ametenda kile alichukusudia sisi tulimpenda lakini yeye kampenda zaidi tuwe na subira na wavumilivu kwa kipindi hiki kigumu sisi wapendwa na ndugu wote tuwe makini kwa kila tutendalo muda huu wa maombolezi.Pole sana Dada yangu mpendwa YASINTA na Familia yako najuwa vigumu kusahau lakini ukiuzunika sana una mkosoa mungu kuwa alichotenda si sahihi
Mimi kwa niamba ya Familia yangu nawapa pole familia Ya Ngonyani na wana blog hii MAISHA NA MAFANIKIO
(MUBABIKIWE NA BWANA)
MIMI
ISSACK JIAH
CHE JIAH
AMINA

Yasinta Ngonyani said...

Nawashukuruni wote kwa kuwa nasi katika wiki hii na tuendelee kuwa pamoja. Na Mwenyezi Mungu awabariki wote mnaopita hapa Maisha na Mafanikio.Pia hapa si kwamba tunahuzunika ila tunamkumbuka tu. Kwani ni muhimu kuwakumbuka wenzetu waliotutangulia. Ahsanteni na ni ruksa kuendelea kusema kitu.