Wednesday, November 9, 2011

NIMEKAA HAPA NIKAKUMBUKA HII NGOMA YA CHIYODA/KIHODA!!!



Ni siku nyingi sijaweka ngoma zetu za asili hapa leo nimekumbuka shule ya msingi pia maisha ya kitamaduni kwa ujumla nimeona tuselebuke na ngoma hii ya CHIYODA ambayo kwa kawaida inachezwa na watoto wa kike/wasichana na akina mama tu. Nimeicheza enzi zake:-). JIONI NJEMA KWA WOTE!!

8 comments:

Rachel Siwa said...

Duuhh Asante da'Yasinta kwa ngoma hii, umenikumbusha nyumbani, kwenye Kipaimara ya wa Nyasa.

Yasinta Ngonyani said...

Rachel! Yaani mwenzio hapa nanengua ungekuwa hapa ungeniunga mkono...Je unaweza kuicheza?

sam mbogo said...

Hakika utamu wa ngoma ya chiyoda/kihoda, ni kiuno! inaonekana ninyi wadada kwa kuicheza ngoma hii mko poa sana.nakumbuka wakati niko chuo nilikuwa naipenda ngoma ya lizombe,lakini si kucheza. ina viuno vingi tuuu,japo niliicheza kutokana na kuwa moja katika somo.safi sana . rachel twanga wanakuja vipi kisgino kitasiginwa!!? kaka s

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Sam! Yaani ww ni kiuno tu kinachokuvutia? Umeifanya jioni yangu iwe ya kucheka cheka...:-)Nawaza ni jinsi gani nawe siku hizo wakati unachezo lizombe ...ningependa kukuona kwa kweli...

Rachel Siwa said...

Pangechimbika da'Yasinta si mzuri sana lakini nayarudiii,kuna wimbo mmoja wlimba siku ya kipaira; Nani anawezaax2 Nanianaweza kulea watoto wakiwaeeeee!!!Duhh leo umenikumbusha sana hiyo Familia,FAMILIA PUTAPUTA POPOTE WALIPOOOOO!!.

@Kaka Sam kwikwikwi duuh Wangoni kwa Viuno kama Wamerogwaaaa kwenye lizombe kakaS ulikatikaje hahahhaa!!

Kisigino mimi thiwezi labda Uniletee za KITAMADUNI kaka yangu mbona utanisahau!!

ray njau said...

7 Nenda, ukale chakula chako kwa kushangilia na kunywa divai yako kwa moyo mchangamfu, kwa sababu tayari Mungu wa kweli amependezwa na kazi zako. 8 Katika kila pindi, mavazi yako na yawe meupe, wala kichwa chako kisikose mafuta. 9 Furahia maisha pamoja na mke unayempenda siku zote za maisha yako yaliyo ya ubatili ambayo umepewa na Yeye chini ya jua, siku zote za hali yako iliyo ya ubatili, kwa maana hilo ndilo fungu lako maishani na katika kazi yako ngumu unayoifanya kwa bidii chini ya jua. 10 Yote ambayo mkono wako unapata kufanya, yafanye kwa nguvu zako zote, kwa maana hakuna kazi, wala utungaji wala ujuzi wala hekima katika Kaburi, mahali unapokwenda._Mhubiri 9:7-10

ray njau said...

Taswira ya mwanablogu inaonyesha kuwa ngoma ni sehemu muhimu katika kudumisha utamaduni wa jamii zetu.Kwa ujumla mashairi yanayotumika kwenye ngoma za makabila yetu yalenga kuhamasisha maadili mema kwa wanajamii na siyo kuwapotosha.Je wanamuziki wa muziki wa kemo[bongo fleva] hawawezi kuyabeba mashairi haya na kuyaweka katika mfumo wa kisasa na ujumbe ukaifikia jamii?

Rachel Siwa said...

Kaka wa Maisha na Mikiki, nafikiri wale wapo kwa kuuza zaidi si kufundisha baadhi yao kama si wote, maana kama hakuweka mapenzi hawajaimba, ni nadra sana kusikia wanaimba kuhusu ukimwi,malezi na mengine.Ngoma za asili hata mimi nazipenda sana mengi kuhusu malezi,heshima yaani zaidi zinalenga jamii.

Huu ni mtazamo wangu mimi.