Wednesday, November 9, 2011

TABASAMU!!!

Kama kawaida ni ile JUMATANO YA KIPENGELE CHA MARUDIO na leo Kapulya ameona tuangalia hili neno TABASAMU na nimeikuta hii mada hapa. KARIBUNI.

Tabasamu ni njia rahisi isiyo na gharama ya kubadilisha mwonekano wako.Tabasamu ni kitu gani? Tabasamu ni dirisha linaloonesha nini kilichopo ndani ya moyo wa mtu, ni kitu kinachonyoosha kila kitu kuwa katika mstari ulioonyoka. Ukiwa mtu wa kutabasamu unakuwa na marafiki wengi na ukiwa mtu wa ndita watu huanza kukukwepa.

Kila unapotabasamu kwa mtu yeyote ni ishara ya upendo, ni zawadi kwa yule mtu ni kitu kizuri. Tabasamu ni kusema karibu, tabasamu ni uwezo ambao unaweza kuifanya siku ya giza kuwa siku ya nuru, huweza kufanya pasipo na upendo kuwa na upendo. Inagharimu misuli 17 tu kutabasamu na inakugharimu misuli 43 kuwa na ndita kwa nini ujizeeshe mapema? Amani huanza kwa tabasamu!
Huwezi kuvaa ukapendeza bila kuvaa tabasamu, huwezi kuwa mrembo bila kuvaa tabasamu huwezi kuitwa beautiful one kama hujavaa tabasamu huwezi kuitwa handsome kama hujavaa tabasamu period! Tafiti zinaonesha mtu anayetabasamu huwezi kuongeza miaka mingi katika maisha yake. Hata hivyo watoto hujifunza kutabasamu kutoka kwa wazazi wao.
Umemaliza kusoma hapa, sasa zamu yako kutabasamu halafu kicheko!
AHSANTENI SANA NA TUONANE TENA PANAPO MAJALIWA JUMATANO IJAYO!!

6 comments:

emu-three said...

Tabasamu hilo `cheupe' dawa!

Goodman Manyanya Phiri said...

Weeee, Mtoto!!!


Hapo basi!!!!

ray njau said...

Moyo mtulivu ni uzima wa mwili wenye nyama, lakini wivu hufanya mifupa iwe na ubovu._Methali 14:30

ray njau said...

Jambo kuu hapa ni tabasamu asilia kutoka katika papachi za moyo na siyo ya kuchakachua.
Binadamu ana uwezo kuvaa uwakilishi wa pande mbili kwa muonekano mwema wa usoni lakini moyoni ni tofauti kabisa.Kwa hiyo acha tabasamu zetu zipambwe na matendo mema yaliyosheheni fadhili-upendo.

Mbele said...

Hilo ni tabasamu la kufa mtu :-)

bath towels clearance said...

Tabasamu ni njia rahisi isiyo na gharama ya kubadilisha mwonekano wako.Tabasamu ni kitu gani? Tabasamu ni dirisha linaloonesha nini kilichopo ndani ya moyo wa mtu, ni kitu kinachonyoosha kila kitu kuwa katika mstari ulioonyoka. Ukiwa mtu wa kutabasamu unakuwa na marafiki wengi na ukiwa mtu wa ndita watu huanza kukukwepa.
stitching orders ,
bulk shirt stitching cost ,